0:00:00.000,0:00:06.766 Kila ndoa ina migongano, lakini si kila mgongano hujenga ndoa. 0:00:06.766,0:00:12.266 Kutoelewana ni sehemu ya muungano wowote wa kiungu. 0:00:12.266,0:00:15.833 Lakini kutoelewana kunapaswa kusababisha maelewano zaidi. 0:00:15.833,0:00:20.600 Kutokuelewana kunapaswa kuzalisha uelewa zaidi. 0:00:20.600,0:00:27.700 Tukitumia vibaya kutokuelewana kwetu, 0:00:27.700,0:00:34.500 badala ya kujifunza kutoka huko, tunaishia kurudia kosa. 0:00:34.500,0:00:44.166 Na hiyo ni sababu ya kawaida ya upendo kupoa - kwa sababu tunaishi maisha ya zamani. 0:00:44.166,0:00:48.233 Unamkumbusha mume wako ya zamani. 0:00:48.233,0:00:52.900 Unamkumbusha mke wako mambo ya nyuma pale migogoro inapokuja 0:00:52.900,0:00:55.600 na kwa hivyo unaishia kurudia yale yale, 0:00:55.600,0:00:59.666 badala ya kujifunza kutoka kwa hayo, badala ya kukua kupitia hayo. 0:00:59.666,0:01:01.833 Kutokuelewana lazima kutakuja. 0:01:01.833,0:01:03.633 Kutokubaliana lazima kutakuja. 0:01:03.633,0:01:05.366 Migogoro lazima ije. 0:01:05.366,0:01:10.000 Lakini kama Wakristo wanaoelewa kwamba yaliyopita yamekwisha, 0:01:10.000,0:01:14.400 tunapaswa kujifunza kutoka kwayo, kukua kupitia hayo. 0:01:14.400,0:01:18.966 Kuna tofauti kati ya uzoefu wa maisha na mafunzo ya maisha.