Tuseme tuna namba 5 na tumeulizwa,
ni namba gani tukijumlisha na namba 5 tunapata 0?
Unaweza ukawa umeshafahamu, ila nitachora.
Tunamstari wa namba hapa.
Na 0 imekaa hapo.
Na tayari tupo hapa kwenye 5.
Hivyo kutoka kwenye 5 mpaka 0, inatakiwa twende nafasi 5 kushoto.
Na kama tunaenda nafasi 5 kushoto,
Inamaanisha tunajumlisha hasi 5.
Tukiongeza hasi 5 hapa,
hii itaturudisha kwenye 0.
hii itaturudisha hapa kwenye 0.
Pengine ulikuwa umeshajua.
Nafikiri hii hapa inaingia akilini.
Ila tunaweza kuita kinyume cha
kujumlisha.
Na zakujumlisha-- ninaiandika.
nafikiri inachanganya
kutoa jina gumu kwenye jambo rahisi--
kinyume cha kujumlisha.
Na ni wazo kwamba kama una namba
na ujumlishe kinyume cha hiyo namba, ambayo
watu wengi wanaita hasi ya namba --
ukijumlisha hasi ya namba kwenye namba yako
utapata 0 kwa sababu
zinalingana, unaweza kuona hivyo.
Zote zina ukubwa wa 5, ila hii inaongeza tano
kulia na kisha unapunguza tano kwa kwenda kushoto.
Ni sawa, na kama ukianza kwenye- ngoja nichore mstari mwingine wa namba
hapa-- kama ukianza kwenye hasi 3.
Kama ukianza hapa kwenye hasi 3,
utakuwa umeshasogea nafasi tatu kwenda kushoto,
mmoja kasema, ninatakiwa kuongeza ngapi kwenye hasi 3
ili nirudi kwenye 0?
Itatakiwa nisogee nafasi tatu kwenda kulia.
Na nafasi tatu kwenda kulia ni upande chanya.
Hivyo natakiwa kuongeza chanya 3.
Hivyo kama nimejumlisha chanya 3 kwenye hasi 3 ninapata 0.
Kwa ujumla, kama nina namba yeyote-- kama nina 1,725,314
na nikajiuliza natakiwa nijumlishe ngapi ili nirudi kwenye 0?
Nitatakiwa kwenda uelekeo kinyume.
Nitakwenda kwenye uelekeo wa kushoto.
Hivyo natakiwa kutoa kiasi kilekile.
Au ninaweza kusema ninajumlisha namba kinyume,
au ninajumlisha kinyume cha hiyo namba.
Hivyo hii itakuwa ni sawa na kujumlisha
hasi 1,725,314 na hapa nitapata 0.
Ni sawa na nikisema, ni namba gani natakiwa nijumlishe na hasi 7
nipate 0?
Kama tayari niko kwenye hasi 7, natakiwa niende mara saba kulia
hivyo ninaongeza chanya 7.
Na hii itakuwa sawa na 0.
Na hii inatokana na uelewa wa jumla
5 jumlisha hasi 5,
au 5 jumlisha kinyume cha 5,
unaweza kusema ni namna nyingine ya kusema 5 toa 5.
Na kama una 5 ya kitu,
na ukaondoa tano, umejifunza miaka mingi iliyopita
kwamba hiyo itakuwa ni sawa na 0.