Dhambi siku zote hupitiliza ukaribisho. Inakupa kidogo sana kuliko unavyotamani na inachukua zaidi ya vile unavyofikiria. Dhambi ni kama moto wa nyikani ambao hauwezi kuzuilika mara moja unapowashwa. Hakuna jitihada za kibinadamu za kuizuia zitafanikiwa bila toba. Dhambi itakupeleka mbali zaidi kuliko ulivyo jiandaa kupotea, itakushikilia kwa muda mrefu kuliko vile unavyotaka kukaa, na itakugharimu zaidi ya ulivyo tayari kulipa.