Hawa ni minyoo.
Si minyoo ambayo utaiona ikitambaa kwenye uchafu
Hivi ni vimelea vya minyookuru.
Wanaishi ndani utumbo wa mwanadamu.
Kila mmoja wa minyoo hii huweza kukua hadi urefu wa inchi 12,
na wapo 200 katika kopo hili kwa sababu fulani,
kwa sababu hiyo ni idadi ambayo kwa kawaida utawakuta
ndani ya tumbo la mtoto anayeugua.
Maambukizi ya minyoo yamekuwapo kwa takribani ya maelfu ya miaka.
Yamechangia katika matokeo ya baada ya vita,
na kukinzana na afya ya mwanadamu kwa muda sana.
minyookuru, safura,
minyoo-mjeledi, kichocho:
maambukizi kutoka katika vijidudu hivi husababisha maumivu na kukosa raha.
Huiba virutubisho na kunyong'onyeza mwili.
Hudumaza ukuaji wa kimwili na kiakili.
Katika matukio mbalimbali, minyoo hawa huwa si wenye madhara makubwa,
lakini cha kushangaza, hiyo ndiyo sababu mojawapo ya tatizo.
Inamaanisha kwamba nchi nyingi
hazihitajika kuweza kutoa kipaumbele cha matibabu yake.
Na kuna madhara kwa jamii kutokana na hilo:
watoto ambao hawapati huduma za dawa za kuua minyoo
wana mahudhurio ya chini shuleni.
Watu wazima ambao hukua bila kutumia dawa za kuua minyoo
hawawezi fanya kazi kwa juhudi na huwa na kipato duni.
Kitu ambacho minyoo hufanya, kihalisia,
ni kuweka kikwazo cha uwezo wa uchapakazi.
Hadi sasa, kuna watu bilioni 1.7 duniani walio katika hatari ya minyoo hii.
Milioni mia sita kati yao wanaishi Afrika.
Kwa kila dola inayowekezwa katika kupambana na kuondokana na minyoo,
Afrika inapata hadi dola 42 katika faidiko la kiuchumi.
Habari njema ni kwamba matibabu ya kuua minyoo ni rahisi mno.
Kuanzia kidonge kimoja hadi vitatu vikitolewa mara moja au mbili kwa mwaka
hutosha kabisa kumfanya mtoto kutoka kuwa na minyoo 200 hadi kutokuwa na mnyoo hata mmoja
na kuwalinda na maambukizi yajayo.
Katika jamii ambazo kuna uwepo mkubwa wa minyoo,
matibabu yanaweza fanyika shuleni.
Mchakato huu ni rahisi na wa haraka.
Nchini Ethiopia, kwa mfano, hii inafanyika kwa watoto milioni 20
ndani ya wiki chache tu.
Dunia imetoka mbali
katika kuwapatia dawa za minyoo watu wanaozihitaji,
na serikali za nchi za Afrika zinataka kupata msukumo.
Ni wakati sasa wa kuendana na malengo yao.
Mradi wa END utashirikiana na serikali
kuandaa mpango madhubuti wa kupunguza mzigo wa magonjwa yanayosababishwa na minyoo.
Watafanya kazi pamoja kuhakikisha programu za kinga na tiba
zinaweza kumpa huduma kila mtu.
Mradi wa END una wazo lenye uthubutu:
wanaamini kwamba sisi ni kizazi ambacho kitakomesha magonjwa yatokanayo na minyoo milele.
Mpango si tu kuunda programu mpya kuanzia mwanzo,
lakini kuzipa muamko zaidi juhudi za programu ambazo tayari zinaleta mabadiliko.
Kwa kutathmini tatizo la namna gani minyoo husambaza magonjwa,
mradi wa END umegundua sehemu tano muhimu ambazo wanaweza fanyia maboresho.
Namba moja: matibabu yaliyo nafuu.
Makampuni mengi ya kutengeneza madawa hutoa dawa za minyoo bure,
hivyo mradi wa END unafanya kazi na washirika sahihi
kusimamia utoaji wa dawa.
Wataendelea kusimamia utoaji wa dawa
katika jamii ambazo zipo katika hatari.
Sasa wanaweza kufanya kwa chini ya zaidi ya senti 25 kwa mtoto katika mwaka mmoja.
Namba mbili: kutazamia katika kinga.
Mradi wa END unahamasisha washirika sahihi ili kuelimisha jamii
katika usafi wa mazingira na usafi binafsi
ili kuweza kubadili mienendo kama kuosha mikono
na matumizi ya msalani,
kuhakikisha kwamba watu hawapati tena maambukizi.
Namba tatu: kuwekeza katika ubunifu.
Mradi wa END umechangia katika kutokomeza minyoo
kwa kuleta namna za kibunifu ambazo zinawalenga watu na kuwatibu.
Watajaribu namna mpya za utoaji huduma,
kulenga mazingira ambayo vimelea huweza kuishi
na kushawishi mabadiliko ya mienendo.
Namba nne: kusimamia na kufanya tathmini.
Mradi wa END hukusanya taarifa za programu zote mara kwa mara
ili kuweza kuboresha programu zaidi na zaidi kadiri muda unavyokwenda.
Namba tano: kuongeza umilikishaji katika jamii.
Katika hatua zote za mchakato,
mradi wa END unafanya kazi na serikali na wadau katika jamii
ili kuweza kuchangia michango ya kifedha kwa pamoja ili kuunga mkono juhudi za kuondokana na minyoo.
Wamefanya kazi wa wahisani kutoka Afrika
na viongozi wa makampuni katika juhudi hizi.
Kuna fursa kubwa sana ya kufanya kazi pamoja kutengeneza namna mpya
ya kuondoa ugonjwa kwa muongo unaofata na zaidi.
Kiasi cha fedha ambacho mradi wa END unahitaji
kitakwenda moja kwa moja katika utoaji wa matibabu ya minyoo
kwa jamii ambazo zina uhitaji
na kiasi kingine kitaenda katika uwezeshaji wa miradi
kwa umilikishaji wa jamii.
Kwa pamoja, hizi juhudi zitatengeneza programu za kukinga na kutibu
ambazo zitakuwa madhubuti hadi miaka ijayo.
Kama mradi huu utawezeshwa kifedha kwa miaka sita ijayo,
makumi ya mamilioni ya watu wataweza pata matibabu ya minyoo.
Kwa hilo, nchi zitaweza kuuondoa mzunguko wa maambukizi ya ugonjwa
katika ngazi zote,
na lililo muhimu zaidi, watu wataweza kuimarika zaidi
katika afya ya kiakili, kimwili na mahusiano ya kijamii.
Hebu fikiria uwezo utakao kuwepo
pale watu wanapokoma kupata wasiwasi wa jambo hili
na kuweka nguvu zao katika mambo kama haya.
(Wanafunzi wakipaza sauti)
(Wakipiga makofi na kuimba)
(Wakishangilia)