0:00:00.482,0:00:02.065 Hawa ni minyoo. 0:00:02.089,0:00:04.675 Si minyoo ambayo utaiona ikitambaa kwenye uchafu 0:00:04.699,0:00:06.853 Hivi ni vimelea vya minyookuru. 0:00:06.877,0:00:09.312 Wanaishi ndani utumbo wa mwanadamu. 0:00:09.336,0:00:12.092 Kila mmoja wa minyoo hii huweza kukua hadi urefu wa inchi 12, 0:00:12.116,0:00:14.497 na wapo 200 katika kopo hili kwa sababu fulani, 0:00:14.521,0:00:16.903 kwa sababu hiyo ni idadi ambayo kwa kawaida utawakuta 0:00:16.927,0:00:19.371 ndani ya tumbo la mtoto anayeugua. 0:00:19.395,0:00:22.055 Maambukizi ya minyoo yamekuwapo kwa takribani ya maelfu ya miaka. 0:00:22.079,0:00:24.079 Yamechangia katika matokeo ya baada ya vita, 0:00:24.103,0:00:26.016 na kukinzana na afya ya mwanadamu kwa muda sana. 0:00:26.040,0:00:27.627 minyookuru, safura, 0:00:27.651,0:00:29.674 minyoo-mjeledi, kichocho: 0:00:29.698,0:00:32.810 maambukizi kutoka katika vijidudu hivi husababisha maumivu na kukosa raha. 0:00:32.834,0:00:34.927 Huiba virutubisho na kunyong'onyeza mwili. 0:00:34.951,0:00:37.425 Hudumaza ukuaji wa kimwili na kiakili. 0:00:37.449,0:00:40.171 Katika matukio mbalimbali, minyoo hawa huwa si wenye madhara makubwa, 0:00:40.195,0:00:42.374 lakini cha kushangaza, hiyo ndiyo sababu mojawapo ya tatizo. 0:00:42.398,0:00:43.938 Inamaanisha kwamba nchi nyingi 0:00:43.962,0:00:46.694 hazihitajika kuweza kutoa kipaumbele cha matibabu yake. 0:00:46.718,0:00:48.335 Na kuna madhara kwa jamii kutokana na hilo: 0:00:48.359,0:00:50.551 watoto ambao hawapati huduma za dawa za kuua minyoo 0:00:50.575,0:00:52.618 wana mahudhurio ya chini shuleni. 0:00:52.642,0:00:54.754 Watu wazima ambao hukua bila kutumia dawa za kuua minyoo 0:00:54.778,0:00:57.578 hawawezi fanya kazi kwa juhudi na huwa na kipato duni. 0:00:57.602,0:00:59.714 Kitu ambacho minyoo hufanya, kihalisia, 0:00:59.738,0:01:01.165 ni kuweka kikwazo cha uwezo wa uchapakazi. 0:01:01.189,0:01:05.408 Hadi sasa, kuna watu bilioni 1.7 duniani walio katika hatari ya minyoo hii. 0:01:05.432,0:01:07.878 Milioni mia sita kati yao wanaishi Afrika. 0:01:07.902,0:01:11.028 Kwa kila dola inayowekezwa katika kupambana na kuondokana na minyoo, 0:01:11.052,0:01:15.203 Afrika inapata hadi dola 42 katika faidiko la kiuchumi. 0:01:15.227,0:01:18.271 Habari njema ni kwamba matibabu ya kuua minyoo ni rahisi mno. 0:01:18.295,0:01:20.540 Kuanzia kidonge kimoja hadi vitatu vikitolewa mara moja au mbili kwa mwaka 0:01:20.564,0:01:23.604 hutosha kabisa kumfanya mtoto kutoka kuwa na minyoo 200 hadi kutokuwa na mnyoo hata mmoja 0:01:23.628,0:01:26.051 na kuwalinda na maambukizi yajayo. 0:01:26.075,0:01:28.695 Katika jamii ambazo kuna uwepo mkubwa wa minyoo, 0:01:28.719,0:01:30.542 matibabu yanaweza fanyika shuleni. 0:01:30.855,0:01:33.188 Mchakato huu ni rahisi na wa haraka. 0:01:33.212,0:01:36.338 Nchini Ethiopia, kwa mfano, hii inafanyika kwa watoto milioni 20 0:01:36.362,0:01:38.148 ndani ya wiki chache tu. 0:01:38.172,0:01:39.800 Dunia imetoka mbali 0:01:39.824,0:01:42.649 katika kuwapatia dawa za minyoo watu wanaozihitaji, 0:01:42.673,0:01:45.213 na serikali za nchi za Afrika zinataka kupata msukumo. 0:01:45.237,0:01:47.346 Ni wakati sasa wa kuendana na malengo yao. 0:01:47.729,0:01:49.674 Mradi wa END utashirikiana na serikali 0:01:49.698,0:01:54.417 kuandaa mpango madhubuti wa kupunguza mzigo wa magonjwa yanayosababishwa na minyoo. 0:01:54.441,0:01:57.579 Watafanya kazi pamoja kuhakikisha programu za kinga na tiba 0:01:57.603,0:01:58.897 zinaweza kumpa huduma kila mtu. 0:01:58.921,0:02:01.100 Mradi wa END una wazo lenye uthubutu: 0:02:01.124,0:02:05.504 wanaamini kwamba sisi ni kizazi ambacho kitakomesha magonjwa yatokanayo na minyoo milele. 0:02:05.528,0:02:08.723 Mpango si tu kuunda programu mpya kuanzia mwanzo, 0:02:08.747,0:02:12.389 lakini kuzipa muamko zaidi juhudi za programu ambazo tayari zinaleta mabadiliko. 0:02:12.413,0:02:15.525 Kwa kutathmini tatizo la namna gani minyoo husambaza magonjwa, 0:02:15.549,0:02:19.469 mradi wa END umegundua sehemu tano muhimu ambazo wanaweza fanyia maboresho. 0:02:20.017,0:02:22.460 Namba moja: matibabu yaliyo nafuu. 0:02:22.484,0:02:25.533 Makampuni mengi ya kutengeneza madawa hutoa dawa za minyoo bure, 0:02:25.557,0:02:27.700 hivyo mradi wa END unafanya kazi na washirika sahihi 0:02:27.724,0:02:29.291 kusimamia utoaji wa dawa. 0:02:29.315,0:02:31.735 Wataendelea kusimamia utoaji wa dawa 0:02:31.759,0:02:34.396 katika jamii ambazo zipo katika hatari. 0:02:34.982,0:02:38.760 Sasa wanaweza kufanya kwa chini ya zaidi ya senti 25 kwa mtoto katika mwaka mmoja. 0:02:39.120,0:02:41.550 Namba mbili: kutazamia katika kinga. 0:02:41.574,0:02:44.576 Mradi wa END unahamasisha washirika sahihi ili kuelimisha jamii 0:02:44.600,0:02:46.169 katika usafi wa mazingira na usafi binafsi 0:02:46.193,0:02:49.035 ili kuweza kubadili mienendo kama kuosha mikono 0:02:49.059,0:02:50.210 na matumizi ya msalani, 0:02:50.234,0:02:52.927 kuhakikisha kwamba watu hawapati tena maambukizi. 0:02:52.951,0:02:55.660 Namba tatu: kuwekeza katika ubunifu. 0:02:55.684,0:02:57.759 Mradi wa END umechangia katika kutokomeza minyoo 0:02:57.783,0:03:02.023 kwa kuleta namna za kibunifu ambazo zinawalenga watu na kuwatibu. 0:03:02.047,0:03:03.815 Watajaribu namna mpya za utoaji huduma, 0:03:03.839,0:03:06.031 kulenga mazingira ambayo vimelea huweza kuishi 0:03:06.055,0:03:07.766 na kushawishi mabadiliko ya mienendo. 0:03:07.790,0:03:10.503 Namba nne: kusimamia na kufanya tathmini. 0:03:10.527,0:03:14.322 Mradi wa END hukusanya taarifa za programu zote mara kwa mara 0:03:14.346,0:03:17.058 ili kuweza kuboresha programu zaidi na zaidi kadiri muda unavyokwenda. 0:03:17.082,0:03:19.924 Namba tano: kuongeza umilikishaji katika jamii. 0:03:19.948,0:03:21.567 Katika hatua zote za mchakato, 0:03:21.591,0:03:24.758 mradi wa END unafanya kazi na serikali na wadau katika jamii 0:03:24.782,0:03:28.560 ili kuweza kuchangia michango ya kifedha kwa pamoja ili kuunga mkono juhudi za kuondokana na minyoo. 0:03:28.584,0:03:30.760 Wamefanya kazi wa wahisani kutoka Afrika 0:03:30.784,0:03:33.631 na viongozi wa makampuni katika juhudi hizi. 0:03:33.655,0:03:37.377 Kuna fursa kubwa sana ya kufanya kazi pamoja kutengeneza namna mpya 0:03:37.401,0:03:40.623 ya kuondoa ugonjwa kwa muongo unaofata na zaidi. 0:03:40.647,0:03:42.402 Kiasi cha fedha ambacho mradi wa END unahitaji 0:03:42.426,0:03:45.027 kitakwenda moja kwa moja katika utoaji wa matibabu ya minyoo 0:03:45.051,0:03:46.449 kwa jamii ambazo zina uhitaji 0:03:46.473,0:03:49.894 na kiasi kingine kitaenda katika uwezeshaji wa miradi 0:03:49.918,0:03:51.219 kwa umilikishaji wa jamii. 0:03:51.243,0:03:54.704 Kwa pamoja, hizi juhudi zitatengeneza programu za kukinga na kutibu 0:03:54.728,0:03:57.314 ambazo zitakuwa madhubuti hadi miaka ijayo. 0:03:57.338,0:04:00.830 Kama mradi huu utawezeshwa kifedha kwa miaka sita ijayo, 0:04:00.854,0:04:04.511 makumi ya mamilioni ya watu wataweza pata matibabu ya minyoo. 0:04:04.883,0:04:08.605 Kwa hilo, nchi zitaweza kuuondoa mzunguko wa maambukizi ya ugonjwa 0:04:08.629,0:04:09.800 katika ngazi zote, 0:04:09.824,0:04:13.677 na lililo muhimu zaidi, watu wataweza kuimarika zaidi 0:04:13.701,0:04:16.652 katika afya ya kiakili, kimwili na mahusiano ya kijamii. 0:04:16.676,0:04:19.194 Hebu fikiria uwezo utakao kuwepo 0:04:19.218,0:04:21.637 pale watu wanapokoma kupata wasiwasi wa jambo hili 0:04:21.661,0:04:24.510 na kuweka nguvu zao katika mambo kama haya. 0:04:25.331,0:04:27.050 (Wanafunzi wakipaza sauti) 0:04:27.074,0:04:30.257 (Wakipiga makofi na kuimba) 0:04:30.281,0:04:33.121 (Wakishangilia)