1 00:00:00,482 --> 00:00:02,065 Hawa ni minyoo. 2 00:00:02,089 --> 00:00:04,675 Si minyoo ambayo utaiona ikitambaa kwenye uchafu 3 00:00:04,699 --> 00:00:06,853 Hivi ni vimelea vya minyookuru. 4 00:00:06,877 --> 00:00:09,312 Wanaishi ndani utumbo wa mwanadamu. 5 00:00:09,336 --> 00:00:12,092 Kila mmoja wa minyoo hii huweza kukua hadi urefu wa inchi 12, 6 00:00:12,116 --> 00:00:14,497 na wapo 200 katika kopo hili kwa sababu fulani, 7 00:00:14,521 --> 00:00:16,903 kwa sababu hiyo ni idadi ambayo kwa kawaida utawakuta 8 00:00:16,927 --> 00:00:19,371 ndani ya tumbo la mtoto anayeugua. 9 00:00:19,395 --> 00:00:22,055 Maambukizi ya minyoo yamekuwapo kwa takribani ya maelfu ya miaka. 10 00:00:22,079 --> 00:00:24,079 Yamechangia katika matokeo ya baada ya vita, 11 00:00:24,103 --> 00:00:26,016 na kukinzana na afya ya mwanadamu kwa muda sana. 12 00:00:26,040 --> 00:00:27,627 minyookuru, safura, 13 00:00:27,651 --> 00:00:29,674 minyoo-mjeledi, kichocho: 14 00:00:29,698 --> 00:00:32,810 maambukizi kutoka katika vijidudu hivi husababisha maumivu na kukosa raha. 15 00:00:32,834 --> 00:00:34,927 Huiba virutubisho na kunyong'onyeza mwili. 16 00:00:34,951 --> 00:00:37,425 Hudumaza ukuaji wa kimwili na kiakili. 17 00:00:37,449 --> 00:00:40,171 Katika matukio mbalimbali, minyoo hawa huwa si wenye madhara makubwa, 18 00:00:40,195 --> 00:00:42,374 lakini cha kushangaza, hiyo ndiyo sababu mojawapo ya tatizo. 19 00:00:42,398 --> 00:00:43,938 Inamaanisha kwamba nchi nyingi 20 00:00:43,962 --> 00:00:46,694 hazihitajika kuweza kutoa kipaumbele cha matibabu yake. 21 00:00:46,718 --> 00:00:48,335 Na kuna madhara kwa jamii kutokana na hilo: 22 00:00:48,359 --> 00:00:50,551 watoto ambao hawapati huduma za dawa za kuua minyoo 23 00:00:50,575 --> 00:00:52,618 wana mahudhurio ya chini shuleni. 24 00:00:52,642 --> 00:00:54,754 Watu wazima ambao hukua bila kutumia dawa za kuua minyoo 25 00:00:54,778 --> 00:00:57,578 hawawezi fanya kazi kwa juhudi na huwa na kipato duni. 26 00:00:57,602 --> 00:00:59,714 Kitu ambacho minyoo hufanya, kihalisia, 27 00:00:59,738 --> 00:01:01,165 ni kuweka kikwazo cha uwezo wa uchapakazi. 28 00:01:01,189 --> 00:01:05,408 Hadi sasa, kuna watu bilioni 1.7 duniani walio katika hatari ya minyoo hii. 29 00:01:05,432 --> 00:01:07,878 Milioni mia sita kati yao wanaishi Afrika. 30 00:01:07,902 --> 00:01:11,028 Kwa kila dola inayowekezwa katika kupambana na kuondokana na minyoo, 31 00:01:11,052 --> 00:01:15,203 Afrika inapata hadi dola 42 katika faidiko la kiuchumi. 32 00:01:15,227 --> 00:01:18,271 Habari njema ni kwamba matibabu ya kuua minyoo ni rahisi mno. 33 00:01:18,295 --> 00:01:20,540 Kuanzia kidonge kimoja hadi vitatu vikitolewa mara moja au mbili kwa mwaka 34 00:01:20,564 --> 00:01:23,604 hutosha kabisa kumfanya mtoto kutoka kuwa na minyoo 200 hadi kutokuwa na mnyoo hata mmoja 35 00:01:23,628 --> 00:01:26,051 na kuwalinda na maambukizi yajayo. 36 00:01:26,075 --> 00:01:28,695 Katika jamii ambazo kuna uwepo mkubwa wa minyoo, 37 00:01:28,719 --> 00:01:30,542 matibabu yanaweza fanyika shuleni. 38 00:01:30,855 --> 00:01:33,188 Mchakato huu ni rahisi na wa haraka. 39 00:01:33,212 --> 00:01:36,338 Nchini Ethiopia, kwa mfano, hii inafanyika kwa watoto milioni 20 40 00:01:36,362 --> 00:01:38,148 ndani ya wiki chache tu. 41 00:01:38,172 --> 00:01:39,800 Dunia imetoka mbali 42 00:01:39,824 --> 00:01:42,649 katika kuwapatia dawa za minyoo watu wanaozihitaji, 43 00:01:42,673 --> 00:01:45,213 na serikali za nchi za Afrika zinataka kupata msukumo. 44 00:01:45,237 --> 00:01:47,346 Ni wakati sasa wa kuendana na malengo yao. 45 00:01:47,729 --> 00:01:49,674 Mradi wa END utashirikiana na serikali 46 00:01:49,698 --> 00:01:54,417 kuandaa mpango madhubuti wa kupunguza mzigo wa magonjwa yanayosababishwa na minyoo. 47 00:01:54,441 --> 00:01:57,579 Watafanya kazi pamoja kuhakikisha programu za kinga na tiba 48 00:01:57,603 --> 00:01:58,897 zinaweza kumpa huduma kila mtu. 49 00:01:58,921 --> 00:02:01,100 Mradi wa END una wazo lenye uthubutu: 50 00:02:01,124 --> 00:02:05,504 wanaamini kwamba sisi ni kizazi ambacho kitakomesha magonjwa yatokanayo na minyoo milele. 51 00:02:05,528 --> 00:02:08,723 Mpango si tu kuunda programu mpya kuanzia mwanzo, 52 00:02:08,747 --> 00:02:12,389 lakini kuzipa muamko zaidi juhudi za programu ambazo tayari zinaleta mabadiliko. 53 00:02:12,413 --> 00:02:15,525 Kwa kutathmini tatizo la namna gani minyoo husambaza magonjwa, 54 00:02:15,549 --> 00:02:19,469 mradi wa END umegundua sehemu tano muhimu ambazo wanaweza fanyia maboresho. 55 00:02:20,017 --> 00:02:22,460 Namba moja: matibabu yaliyo nafuu. 56 00:02:22,484 --> 00:02:25,533 Makampuni mengi ya kutengeneza madawa hutoa dawa za minyoo bure, 57 00:02:25,557 --> 00:02:27,700 hivyo mradi wa END unafanya kazi na washirika sahihi 58 00:02:27,724 --> 00:02:29,291 kusimamia utoaji wa dawa. 59 00:02:29,315 --> 00:02:31,735 Wataendelea kusimamia utoaji wa dawa 60 00:02:31,759 --> 00:02:34,396 katika jamii ambazo zipo katika hatari. 61 00:02:34,982 --> 00:02:38,760 Sasa wanaweza kufanya kwa chini ya zaidi ya senti 25 kwa mtoto katika mwaka mmoja. 62 00:02:39,120 --> 00:02:41,550 Namba mbili: kutazamia katika kinga. 63 00:02:41,574 --> 00:02:44,576 Mradi wa END unahamasisha washirika sahihi ili kuelimisha jamii 64 00:02:44,600 --> 00:02:46,169 katika usafi wa mazingira na usafi binafsi 65 00:02:46,193 --> 00:02:49,035 ili kuweza kubadili mienendo kama kuosha mikono 66 00:02:49,059 --> 00:02:50,210 na matumizi ya msalani, 67 00:02:50,234 --> 00:02:52,927 kuhakikisha kwamba watu hawapati tena maambukizi. 68 00:02:52,951 --> 00:02:55,660 Namba tatu: kuwekeza katika ubunifu. 69 00:02:55,684 --> 00:02:57,759 Mradi wa END umechangia katika kutokomeza minyoo 70 00:02:57,783 --> 00:03:02,023 kwa kuleta namna za kibunifu ambazo zinawalenga watu na kuwatibu. 71 00:03:02,047 --> 00:03:03,815 Watajaribu namna mpya za utoaji huduma, 72 00:03:03,839 --> 00:03:06,031 kulenga mazingira ambayo vimelea huweza kuishi 73 00:03:06,055 --> 00:03:07,766 na kushawishi mabadiliko ya mienendo. 74 00:03:07,790 --> 00:03:10,503 Namba nne: kusimamia na kufanya tathmini. 75 00:03:10,527 --> 00:03:14,322 Mradi wa END hukusanya taarifa za programu zote mara kwa mara 76 00:03:14,346 --> 00:03:17,058 ili kuweza kuboresha programu zaidi na zaidi kadiri muda unavyokwenda. 77 00:03:17,082 --> 00:03:19,924 Namba tano: kuongeza umilikishaji katika jamii. 78 00:03:19,948 --> 00:03:21,567 Katika hatua zote za mchakato, 79 00:03:21,591 --> 00:03:24,758 mradi wa END unafanya kazi na serikali na wadau katika jamii 80 00:03:24,782 --> 00:03:28,560 ili kuweza kuchangia michango ya kifedha kwa pamoja ili kuunga mkono juhudi za kuondokana na minyoo. 81 00:03:28,584 --> 00:03:30,760 Wamefanya kazi wa wahisani kutoka Afrika 82 00:03:30,784 --> 00:03:33,631 na viongozi wa makampuni katika juhudi hizi. 83 00:03:33,655 --> 00:03:37,377 Kuna fursa kubwa sana ya kufanya kazi pamoja kutengeneza namna mpya 84 00:03:37,401 --> 00:03:40,623 ya kuondoa ugonjwa kwa muongo unaofata na zaidi. 85 00:03:40,647 --> 00:03:42,402 Kiasi cha fedha ambacho mradi wa END unahitaji 86 00:03:42,426 --> 00:03:45,027 kitakwenda moja kwa moja katika utoaji wa matibabu ya minyoo 87 00:03:45,051 --> 00:03:46,449 kwa jamii ambazo zina uhitaji 88 00:03:46,473 --> 00:03:49,894 na kiasi kingine kitaenda katika uwezeshaji wa miradi 89 00:03:49,918 --> 00:03:51,219 kwa umilikishaji wa jamii. 90 00:03:51,243 --> 00:03:54,704 Kwa pamoja, hizi juhudi zitatengeneza programu za kukinga na kutibu 91 00:03:54,728 --> 00:03:57,314 ambazo zitakuwa madhubuti hadi miaka ijayo. 92 00:03:57,338 --> 00:04:00,830 Kama mradi huu utawezeshwa kifedha kwa miaka sita ijayo, 93 00:04:00,854 --> 00:04:04,511 makumi ya mamilioni ya watu wataweza pata matibabu ya minyoo. 94 00:04:04,883 --> 00:04:08,605 Kwa hilo, nchi zitaweza kuuondoa mzunguko wa maambukizi ya ugonjwa 95 00:04:08,629 --> 00:04:09,800 katika ngazi zote, 96 00:04:09,824 --> 00:04:13,677 na lililo muhimu zaidi, watu wataweza kuimarika zaidi 97 00:04:13,701 --> 00:04:16,652 katika afya ya kiakili, kimwili na mahusiano ya kijamii. 98 00:04:16,676 --> 00:04:19,194 Hebu fikiria uwezo utakao kuwepo 99 00:04:19,218 --> 00:04:21,637 pale watu wanapokoma kupata wasiwasi wa jambo hili 100 00:04:21,661 --> 00:04:24,510 na kuweka nguvu zao katika mambo kama haya. 101 00:04:25,331 --> 00:04:27,050 (Wanafunzi wakipaza sauti) 102 00:04:27,074 --> 00:04:30,257 (Wakipiga makofi na kuimba) 103 00:04:30,281 --> 00:04:33,121 (Wakishangilia)