WEBVTT 00:00:00.482 --> 00:00:02.065 Hawa ni minyoo. 00:00:02.089 --> 00:00:04.675 Si minyoo ambayo utaiona ikitambaa kwenye uchafu 00:00:04.699 --> 00:00:06.853 Hivi ni vimelea vya minyookuru. 00:00:06.877 --> 00:00:09.312 Wanaishi ndani utumbo wa mwanadamu. 00:00:09.336 --> 00:00:12.092 Kila mmoja wa minyoo hii huweza kukua hadi urefu wa inchi 12, 00:00:12.116 --> 00:00:14.497 na wapo 200 katika kopo hili kwa sababu fulani, 00:00:14.521 --> 00:00:16.903 kwa sababu hiyo ni idadi ambayo kwa kawaida utawakuta 00:00:16.927 --> 00:00:19.371 ndani ya tumbo la mtoto anayeugua. NOTE Paragraph 00:00:19.395 --> 00:00:22.055 Maambukizi ya minyoo yamekuwapo kwa takribani ya maelfu ya miaka. 00:00:22.079 --> 00:00:24.079 Yamechangia katika matokeo ya baada ya vita, 00:00:24.103 --> 00:00:26.016 na kukinzana na afya ya mwanadamu kwa muda sana. 00:00:26.040 --> 00:00:27.627 minyookuru, safura, 00:00:27.651 --> 00:00:29.674 minyoo-mjeledi, kichocho: 00:00:29.698 --> 00:00:32.810 maambukizi kutoka katika vijidudu hivi husababisha maumivu na kukosa raha. 00:00:32.834 --> 00:00:34.927 Huiba virutubisho na kunyong'onyeza mwili. 00:00:34.951 --> 00:00:37.425 Hudumaza ukuaji wa kimwili na kiakili. NOTE Paragraph 00:00:37.449 --> 00:00:40.171 Katika matukio mbalimbali, minyoo hawa huwa si wenye madhara makubwa, 00:00:40.195 --> 00:00:42.374 lakini cha kushangaza, hiyo ndiyo sababu mojawapo ya tatizo. 00:00:42.398 --> 00:00:43.938 Inamaanisha kwamba nchi nyingi 00:00:43.962 --> 00:00:46.694 hazihitajika kuweza kutoa kipaumbele cha matibabu yake. 00:00:46.718 --> 00:00:48.335 Na kuna madhara kwa jamii kutokana na hilo: 00:00:48.359 --> 00:00:50.551 watoto ambao hawapati huduma za dawa za kuua minyoo 00:00:50.575 --> 00:00:52.618 wana mahudhurio ya chini shuleni. 00:00:52.642 --> 00:00:54.754 Watu wazima ambao hukua bila kutumia dawa za kuua minyoo 00:00:54.778 --> 00:00:57.578 hawawezi fanya kazi kwa juhudi na huwa na kipato duni. 00:00:57.602 --> 00:00:59.714 Kitu ambacho minyoo hufanya, kihalisia, 00:00:59.738 --> 00:01:01.165 ni kuweka kikwazo cha uwezo wa uchapakazi. NOTE Paragraph 00:01:01.189 --> 00:01:05.408 Hadi sasa, kuna watu bilioni 1.7 duniani walio katika hatari ya minyoo hii. 00:01:05.432 --> 00:01:07.878 Milioni mia sita kati yao wanaishi Afrika. 00:01:07.902 --> 00:01:11.028 Kwa kila dola inayowekezwa katika kupambana na kuondokana na minyoo, 00:01:11.052 --> 00:01:15.203 Afrika inapata hadi dola 42 katika faidiko la kiuchumi. NOTE Paragraph 00:01:15.227 --> 00:01:18.271 Habari njema ni kwamba matibabu ya kuua minyoo ni rahisi mno. 00:01:18.295 --> 00:01:20.540 Kuanzia kidonge kimoja hadi vitatu vikitolewa mara moja au mbili kwa mwaka 00:01:20.564 --> 00:01:23.604 hutosha kabisa kumfanya mtoto kutoka kuwa na minyoo 200 hadi kutokuwa na mnyoo hata mmoja 00:01:23.628 --> 00:01:26.051 na kuwalinda na maambukizi yajayo. 00:01:26.075 --> 00:01:28.695 Katika jamii ambazo kuna uwepo mkubwa wa minyoo, 00:01:28.719 --> 00:01:30.542 matibabu yanaweza fanyika shuleni. 00:01:30.855 --> 00:01:33.188 Mchakato huu ni rahisi na wa haraka. 00:01:33.212 --> 00:01:36.338 Nchini Ethiopia, kwa mfano, hii inafanyika kwa watoto milioni 20 00:01:36.362 --> 00:01:38.148 ndani ya wiki chache tu. NOTE Paragraph 00:01:38.172 --> 00:01:39.800 Dunia imetoka mbali 00:01:39.824 --> 00:01:42.649 katika kuwapatia dawa za minyoo watu wanaozihitaji, 00:01:42.673 --> 00:01:45.213 na serikali za nchi za Afrika zinataka kupata msukumo. 00:01:45.237 --> 00:01:47.346 Ni wakati sasa wa kuendana na malengo yao. NOTE Paragraph 00:01:47.729 --> 00:01:49.674 Mradi wa END utashirikiana na serikali 00:01:49.698 --> 00:01:54.417 kuandaa mpango madhubuti wa kupunguza mzigo wa magonjwa yanayosababishwa na minyoo. 00:01:54.441 --> 00:01:57.579 Watafanya kazi pamoja kuhakikisha programu za kinga na tiba 00:01:57.603 --> 00:01:58.897 zinaweza kumpa huduma kila mtu. 00:01:58.921 --> 00:02:01.100 Mradi wa END una wazo lenye uthubutu: 00:02:01.124 --> 00:02:05.504 wanaamini kwamba sisi ni kizazi ambacho kitakomesha magonjwa yatokanayo na minyoo milele. 00:02:05.528 --> 00:02:08.723 Mpango si tu kuunda programu mpya kuanzia mwanzo, 00:02:08.747 --> 00:02:12.389 lakini kuzipa muamko zaidi juhudi za programu ambazo tayari zinaleta mabadiliko. 00:02:12.413 --> 00:02:15.525 Kwa kutathmini tatizo la namna gani minyoo husambaza magonjwa, 00:02:15.549 --> 00:02:19.469 mradi wa END umegundua sehemu tano muhimu ambazo wanaweza fanyia maboresho. NOTE Paragraph 00:02:20.017 --> 00:02:22.460 Namba moja: matibabu yaliyo nafuu. 00:02:22.484 --> 00:02:25.533 Makampuni mengi ya kutengeneza madawa hutoa dawa za minyoo bure, 00:02:25.557 --> 00:02:27.700 hivyo mradi wa END unafanya kazi na washirika sahihi 00:02:27.724 --> 00:02:29.291 kusimamia utoaji wa dawa. 00:02:29.315 --> 00:02:31.735 Wataendelea kusimamia utoaji wa dawa 00:02:31.759 --> 00:02:34.396 katika jamii ambazo zipo katika hatari. 00:02:34.982 --> 00:02:38.760 Sasa wanaweza kufanya kwa chini ya zaidi ya senti 25 kwa mtoto katika mwaka mmoja. NOTE Paragraph 00:02:39.120 --> 00:02:41.550 Namba mbili: kutazamia katika kinga. 00:02:41.574 --> 00:02:44.576 Mradi wa END unahamasisha washirika sahihi ili kuelimisha jamii 00:02:44.600 --> 00:02:46.169 katika usafi wa mazingira na usafi binafsi 00:02:46.193 --> 00:02:49.035 ili kuweza kubadili mienendo kama kuosha mikono 00:02:49.059 --> 00:02:50.210 na matumizi ya msalani, 00:02:50.234 --> 00:02:52.927 kuhakikisha kwamba watu hawapati tena maambukizi. NOTE Paragraph 00:02:52.951 --> 00:02:55.660 Namba tatu: kuwekeza katika ubunifu. 00:02:55.684 --> 00:02:57.759 Mradi wa END umechangia katika kutokomeza minyoo 00:02:57.783 --> 00:03:02.023 kwa kuleta namna za kibunifu ambazo zinawalenga watu na kuwatibu. 00:03:02.047 --> 00:03:03.815 Watajaribu namna mpya za utoaji huduma, 00:03:03.839 --> 00:03:06.031 kulenga mazingira ambayo vimelea huweza kuishi 00:03:06.055 --> 00:03:07.766 na kushawishi mabadiliko ya mienendo. NOTE Paragraph 00:03:07.790 --> 00:03:10.503 Namba nne: kusimamia na kufanya tathmini. 00:03:10.527 --> 00:03:14.322 Mradi wa END hukusanya taarifa za programu zote mara kwa mara 00:03:14.346 --> 00:03:17.058 ili kuweza kuboresha programu zaidi na zaidi kadiri muda unavyokwenda. NOTE Paragraph 00:03:17.082 --> 00:03:19.924 Namba tano: kuongeza umilikishaji katika jamii. 00:03:19.948 --> 00:03:21.567 Katika hatua zote za mchakato, 00:03:21.591 --> 00:03:24.758 mradi wa END unafanya kazi na serikali na wadau katika jamii 00:03:24.782 --> 00:03:28.560 ili kuweza kuchangia michango ya kifedha kwa pamoja ili kuunga mkono juhudi za kuondokana na minyoo. 00:03:28.584 --> 00:03:30.760 Wamefanya kazi wa wahisani kutoka Afrika 00:03:30.784 --> 00:03:33.631 na viongozi wa makampuni katika juhudi hizi. NOTE Paragraph 00:03:33.655 --> 00:03:37.377 Kuna fursa kubwa sana ya kufanya kazi pamoja kutengeneza namna mpya 00:03:37.401 --> 00:03:40.623 ya kuondoa ugonjwa kwa muongo unaofata na zaidi. 00:03:40.647 --> 00:03:42.402 Kiasi cha fedha ambacho mradi wa END unahitaji 00:03:42.426 --> 00:03:45.027 kitakwenda moja kwa moja katika utoaji wa matibabu ya minyoo 00:03:45.051 --> 00:03:46.449 kwa jamii ambazo zina uhitaji 00:03:46.473 --> 00:03:49.894 na kiasi kingine kitaenda katika uwezeshaji wa miradi 00:03:49.918 --> 00:03:51.219 kwa umilikishaji wa jamii. 00:03:51.243 --> 00:03:54.704 Kwa pamoja, hizi juhudi zitatengeneza programu za kukinga na kutibu 00:03:54.728 --> 00:03:57.314 ambazo zitakuwa madhubuti hadi miaka ijayo. 00:03:57.338 --> 00:04:00.830 Kama mradi huu utawezeshwa kifedha kwa miaka sita ijayo, 00:04:00.854 --> 00:04:04.511 makumi ya mamilioni ya watu wataweza pata matibabu ya minyoo. 00:04:04.883 --> 00:04:08.605 Kwa hilo, nchi zitaweza kuuondoa mzunguko wa maambukizi ya ugonjwa 00:04:08.629 --> 00:04:09.800 katika ngazi zote, 00:04:09.824 --> 00:04:13.677 na lililo muhimu zaidi, watu wataweza kuimarika zaidi 00:04:13.701 --> 00:04:16.652 katika afya ya kiakili, kimwili na mahusiano ya kijamii. NOTE Paragraph 00:04:16.676 --> 00:04:19.194 Hebu fikiria uwezo utakao kuwepo 00:04:19.218 --> 00:04:21.637 pale watu wanapokoma kupata wasiwasi wa jambo hili 00:04:21.661 --> 00:04:24.510 na kuweka nguvu zao katika mambo kama haya. NOTE Paragraph 00:04:25.331 --> 00:04:27.050 (Wanafunzi wakipaza sauti) NOTE Paragraph 00:04:27.074 --> 00:04:30.257 (Wakipiga makofi na kuimba) NOTE Paragraph 00:04:30.281 --> 00:04:33.121 (Wakishangilia)