0:00:00.000,0:00:08.480 Ikiwa jumbe unazosikia zinaonekana tu kuonyesha upendo wa Mungu kwa wenye dhambi 0:00:08.480,0:00:12.840 lakini si chuki ya Mungu juu ya dhambi, kuwa makini. 0:00:12.840,0:00:20.000 Ikiwa mafundisho unayopokea yanalenga zaidi ustawi wa mali 0:00:20.000,0:00:25.200 kuliko mafanikio ya kiroho, kuwa mwangalifu. 0:00:25.200,0:00:35.680 Ikiwa mahubiri yanayohubiriwa yanazingatia sana ahadi za Mungu 0:00:35.680,0:00:43.120 bila kuzungumzia juu ya utii wako, kuwa mwangalifu. 0:00:43.120,0:00:47.280 Baadhi yenu mnaweza kushangaa na ninachosema, 0:00:47.280,0:00:51.320 'Ndugu Chris, unazungumza kuhusu mafanikio - injili ya mafanikio. 0:00:51.320,0:00:59.080 Je, unasema kwamba Mungu hataki nifanikiwe, nibarikiwe, nisitawi, nifanye vizuri?' 0:00:59.080,0:01:02.440 Hapana, usininukuu vibaya. 0:01:02.440,0:01:06.280 Sisemi Mungu hawezi kukufanikisha. 0:01:06.280,0:01:11.400 Ninasema lengo letu lisiwe kwenye ustawi wa mali 0:01:11.400,0:01:14.360 kwa gharama ya ustawi wa kiroho. 0:01:14.360,0:01:25.600 Zingatia jambo hili – ahadi ya Mungu ya utele si kibali cha kufanya ubadhirifu. 0:01:25.600,0:01:33.760 Ahadi ya Mungu ya utele si leseni ya umbea. 0:01:33.760,0:01:38.800 Wacha tuzungumze juu ya utoaji wa kupita kiasi, sio maisha ya kupita kiasi. 0:01:38.800,0:01:43.760 Mungu akikufanikisha, amekuandaa kuwabariki wengine. 0:01:43.760,0:01:46.560 Tuwe makini watu wa Mungu. 0:01:46.560,0:01:53.240 Matarajio yasiyofaa hutuweka tayari kwa kukatishwa tamaa. 0:01:53.240,0:01:56.280 Ukimjia Mungu kwa matarajio 0:01:56.280,0:02:01.160 ambayo yanalenga tu ustawi wa mali, 0:02:01.160,0:02:06.760 utajiweka tayari kwa kukata tamaa. 0:02:06.760,0:02:11.680 Kwa sababu hata kama ustawi wa mali unakuja, 0:02:11.680,0:02:16.760 matakwa ya mwanadamu hayana kikomo. 0:02:16.760,0:02:21.040 Mungu ameahidi kukutana nasi kulingana na mahitaji yetu, si matakwa yetu. 0:02:21.040,0:02:24.680 Hakuna kikomo kwa kile mwanadamu anataka. 0:02:24.680,0:02:28.040 Kila hatua unayofikia katika mafanikio ya kimwili, 0:02:28.040,0:02:30.760 daima kuna kiwango cha juu zaidi cha kufikia. 0:02:30.760,0:02:36.560 Ikiwa huo ndio msingi wa mtazamo wako juu ya maisha, hutaridhika kamwe. 0:02:36.560,0:02:42.080 Sisemi Mungu hawezi kukufanikisha, akubariki sana. 0:02:42.080,0:02:45.640 Sio leseni ya ubadhirifu. 0:02:45.640,0:02:50.520 Hapana! Ni leseni ya utoaji wa kupita kiasi, sio maisha ya ubadhirifu.