0:00:00.400,0:00:08.040 Ukishindwa kumuingiza Mungu katika mipango yako,[br]unapanga kushindwa. 0:00:09.760,0:00:14.960 Karibuni tena nyote kwenye[br]Ibada hii ya Maombi Shirikishi. 0:00:14.960,0:00:21.520 Kabla ya jambo lolote, tuombe pamoja. 0:00:21.520,0:00:31.520 Ninaomba sasa hivi kwa kila moyo[br]ulioungana na huduma hii 0:00:31.520,0:00:46.040 kwamba wakutane na uhalisia wa uwezo wako, upendo, wema wako katika maisha yao. 0:00:46.040,0:00:54.960 Katika jina kuu la Yesu Kristo tunaomba. 0:00:54.960,0:00:59.120 Na watu wa Mungu wakasema, Amina! 0:00:59.120,0:01:10.000 Kwanza kabisa, wacha niwasalimie nyote[br]Heri ya Mwaka Mpya 2025. 0:01:10.000,0:01:15.160 Nina neno la kutia moyo[br]la kukushirikisha leo. 0:01:15.160,0:01:20.600 Ni kawaida katika kipindi hiki - tunapoondoka mwaka mmoja na kuingia mwaka mpya - 0:01:20.600,0:01:25.240 ni kawaida sana kwetu kuwa na muda wa kutafakari yaliyo mbele. 0:01:25.240,0:01:28.840 Je, nina mipango gani[br]kwa mwaka huu unaokuja? 0:01:28.840,0:01:34.400 Inaweza kuwa katika maisha yako ya kibinafsi,[br]maisha yako ya kitaaluma. 0:01:34.400,0:01:37.680 Inaweza kuwa katika taaluma yako -[br]'Nataka kupanua biashara hapa.' 0:01:37.680,0:01:42.640 Labda mahusiano - 'Mwaka huu,[br]nataka kuolewa!' 0:01:42.640,0:01:46.160 'Mwaka huu, tunataka kupata watoto pamoja' - waume na wake. 0:01:46.160,0:01:47.840 Huu ni wakati ambao tunapanga mipango. 0:01:47.840,0:01:51.520 Tunafikiria mwaka ujao,[br]mwaka ujao. Nzuri! 0:01:51.520,0:01:56.640 Ni vizuri kupanga mipango lakini 0:01:56.640,0:02:08.960 usiingie kwenye makosa ya kupanga mipango ya kesho kana kwamba wewe ndiye mmiliki wake. 0:02:08.960,0:02:13.720 Fikirini juu ya hilo enyi watu wa Mungu. 0:02:13.720,0:02:27.400 Usiingie kwenye mtego wa kupanga mipango ya siku zijazo kana kwamba ni yako. 0:02:27.400,0:02:30.800 Sisemi ni makosa kupanga mipango. 0:02:30.800,0:02:34.080 Sisemi ni makosa kuangalia mbele. 0:02:34.080,0:02:40.280 Ninasema unapofanya[br]mipango kama Mkristo - 0:02:40.280,0:02:44.440 'Nini kinachofuata mnamo 2025? Kipi kilicho mbele? 0:02:44.440,0:02:45.640 Je! ninataka kuzingatia nini? 0:02:45.640,0:02:51.440 Ninataka kufikia nini katika kazi yangu, maisha ya kibinafsi, biashara, fedha? 0:02:51.440,0:02:52.880 Ninataka kufanya nini?' 0:02:52.880,0:03:00.800 Unapopanga mipango, lazima ufanye hivyo[br]kwa utambuzi wa mambo matatu. 0:03:00.800,0:03:03.600 Na mimi nataka uandike.[br]Tafadhali andika hii. 0:03:03.600,0:03:07.240 Ujumbe huu utakusaidia kwa mwaka huu. 0:03:07.240,0:03:16.160 1. Maisha hayana uhakika 0:03:16.160,0:03:26.880 2. Mungu ni mwenye enzi kuu 0:03:26.880,0:03:36.160 3. Kila siku ina riziki yake 0:03:36.160,0:03:38.840 Nitawaambia tena, watu wa Mungu. 0:03:38.840,0:03:43.800 Unapopanga mipango, unapopanga juu ya siku zijazo, 0:03:43.800,0:03:50.320 lazima ufanye hivyo ukiwa na utambuzi huu,[br]ufahamu huu - 0:03:50.320,0:03:55.880 1. Maisha hayana uhakika 0:03:55.880,0:04:04.040 Wakati fulani tutakabili hali[br]zilizo nje ya uwezo wetu. 0:04:04.040,0:04:10.480 Kwa nini unapanga mipango[br]kana kwamba unaudhibiti? 0:04:10.480,0:04:22.640 Wakati mwingine kama mtoto wa Mungu, unaweza[br]kukutana na matukio yasiyobadilika - 0:04:22.640,0:04:33.640 hakuna kiasi cha maombi, kufunga au[br]kukomaa kiroho kutabadili. 0:04:33.640,0:04:38.840 Maisha hayana uhakika. 0:04:38.840,0:04:44.800 2. Mungu ni mwenye enzi kuu 0:04:44.800,0:04:53.320 Maisha kukosa uhakika hakubadili[br]enzi kuu ya Mungu. 0:04:53.320,0:04:56.240 Ndiyo, maisha yamejawa na kutokuwa na uhakika. 0:04:56.240,0:05:06.640 Lakini jambo moja unaweza kuwa na uhakika nalo - wema wa Mungu, nguvu za Mungu, upendo wa Mungu. 0:05:06.640,0:05:12.600 Hata katikati ya[br]wazimu wa dunia hii, 0:05:12.600,0:05:17.400 tunaweza kuwa na uhakika juu ya[br]wema wa Mungu. 0:05:17.400,0:05:19.320 Yeye ni mwenye enzi. 0:05:19.320,0:05:33.360 Na kama Wakristo, lazima tutambue maisha yetu, nyakati zetu ziko mikononi mwake. 0:05:33.360,0:05:34.960 Mungu ni mwenye enzi. 0:05:34.960,0:05:40.120 3. Kila siku ina riziki yake 0:05:40.120,0:05:45.880 Utupe leo mkate wetu wa kila siku. 0:05:45.880,0:05:49.320 Mana kwa hitaji la wakati huu. 0:05:49.320,0:05:58.280 Kila siku ina riziki yake -[br]Mungu hutoa neema kwa kila siku. 0:05:58.280,0:06:04.520 Ujumbe ninaopaswa kushiriki[br]nawe, kwa ufupi ni huu: 0:06:04.520,0:06:10.360 'Mipango yako Mikononi mwa Mungu'. 0:06:10.360,0:06:15.360 Unaweza kusema hivyo sasa hivi. Ikiwa uko na mtu nyumbani, mwambie tu, 0:06:15.360,0:06:20.840 "Mipango yako mikononi mwa Mungu." 0:06:20.840,0:06:25.520 Ikiwa uko peke yako, unaweza kujiambia[br]au unaweza kuniambia, 0:06:25.520,0:06:31.680 "Mipango yangu iko mikononi mwa Mungu." 0:06:31.680,0:06:37.000 Mwanadamu hupanga; Mungu hutekeleza. 0:06:37.000,0:06:43.680 Mwanadamu anapendekeza; Mungu huamuru. 0:06:43.680,0:06:49.840 Kama Mkristo, tazama, sikwambii tena kwamba usifanye mpango, 0:06:49.840,0:06:57.960 bali panga mipango huku ukifahamu[br]kuwa maisha yako yako mikononi mwa Mungu. 0:06:57.960,0:07:07.680 Fanya mipango kutoka katika nafasi ya[br]kujitiisha kwa Mpangaji Mkuu 0:07:07.680,0:07:15.640 ambaye njia zake ni za juu kuliko zetu,[br]ambaye mipango yake ni mikubwa kuliko yetu. 0:07:15.640,0:07:25.800 Wale wanaoshindwa kuweka[br]mipango yao mikononi mwa Mungu 0:07:25.800,0:07:31.560 wanajiweka kwenye[br]njia ya kushindwa. 0:07:31.560,0:07:35.240 Hata nitarahisisha. Nitasema hivi - 0:07:35.240,0:07:45.840 ukishindwa kumjumuisha Mungu katika mipango yako,[br]unapanga kushindwa. 0:07:45.840,0:07:52.240 Hebu tuyaangazie Maandiko makini katika Yakobo 4. 0:07:52.240,0:07:58.960 Ninataka kuangazia ukweli huu ili wakati tunapanga mipango ya kesho, 0:07:58.960,0:08:06.840 tunafanya hivyo tukiwa na ufahamu sahihi wa[br]nafasi ya Mungu na nafasi yetu. 0:08:06.840,0:08:13.000 Unapopanga juu ya siku zijazo,[br]kumbuka ni nani aliye Mkuu. 0:08:13.000,0:08:19.600 Hebu tusome pamoja - Yakobo 4:13. 0:08:19.600,0:08:28.600 “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutakwenda katika mji fulani; 0:08:28.600,0:08:33.560 tutakaa huko mwaka mzima, tutanunua na kuuza[br]na kujipatia faida...” 0:08:33.560,0:08:39.920 'Mnamo 2025, nitaenda huko.[br]Nitafanya hivi katika biashara yangu. 0:08:39.920,0:08:44.120 Hakika hili litatokea.' 0:08:44.120,0:08:52.960 “... kumbe hujui kitakachotokea kesho. Kwani maisha yako ni nini? 0:08:52.960,0:09:08.160 Bali ni mvuke unaoonekana kwa muda mfupi na kisha kutoweka. 0:09:08.160,0:09:20.120 Badala yake mnapaswa kusema, Bwana akipenda, tutaishi na kufanya hili au lile. 0:09:20.120,0:09:25.400 "Bwana akipenda, hili litatokea mwaka wa 2025. 0:09:25.400,0:09:32.840 Bwana akipenda, mpango huu utatimia.' 0:09:32.840,0:09:44.480 Yakobo 4:16 BHN - Lakini sasa mnajivunia majivuno yenu. Majivuno yote kama hayo ni mabaya.” 0:09:44.480,0:09:51.880 Maandiko hapa, nataka kusisitiza,[br]hayasemi kamwe usifanye mpango, 0:09:51.880,0:09:59.960 lakini yanakuonya usiichukue nafasi ya Mungu inapokuja kwenye mpango wako. 0:09:59.960,0:10:08.360 Kama nilivyosema hapo awali, unapotazama mbele, kumbuka ni nani aliye Kichwa - Yesu. 0:10:08.360,0:10:15.360 Hakuna kitu hatari zaidi kama kuchukua nafasi ya Mungu katika mpango wako. 0:10:15.360,0:10:28.360 Kuchukua nafasi ya Mungu katika mpango wako ndiyo njia ya uhakika ya kuanguka kwa mpango huo - hatimaye. 0:10:28.360,0:10:31.360 Sasa, unaweza kunitazama na kusema,[br]'Unasema nini Ndugu Chris? 0:10:31.360,0:10:38.600 Sichukui nafasi ya Mungu katika mpango wangu. Ningewezaje kuwa Mungu? Mimi si Mungu!' 0:10:38.600,0:10:45.680 Lakini wengi wetu, kwa jinsi tunavofanya[br]mipango yetu ya kesho, 0:10:45.680,0:10:51.560 tunafanya hivyo kwa njia inayochukua[br]umiliki wa kesho. 0:10:51.560,0:10:55.040 Na unajua hatari ya hii? 0:10:55.040,0:10:58.680 Unapochukua umiliki wa kesho, 0:10:58.680,0:11:02.240 unabeba uzito ambao hukukusudiwa[br]kubeba, 0:11:02.240,0:11:10.840 ndiyo maana bila shaka huishia[br]katika wasiwasi, woga na mashaka. 0:11:10.840,0:11:15.320 'Nini kitatokea? Itakuwaje juu ya hiki?[br]Vipi kuhusu lile?' 0:11:15.320,0:11:20.080 Wasiwasi ni mwizi wa furaha. 0:11:20.080,0:11:24.840 Wasiwasi ni mwizi wa amani. 0:11:24.840,0:11:30.000 Wasiwasi ni mwizi wa hukumu halali, 0:11:30.000,0:11:35.600 ambayo ni muhimu katika kuwa msimamizi mzuri[br]wa kile kilicho mikononi mwako leo. 0:11:35.600,0:11:47.200 Ngoja nikukumbushe maneno mazuri ya Bwana wetu Yesu Kristo katika Mathayo 6:34. 0:11:47.200,0:11:53.760 Yesu alisema, “Basi, msisumbukie[br]ya kesho; 0:11:53.760,0:12:02.200 maana kesho itajisumbukia na mambo yake. Yatosha kwa siku taabu yake yenyewe.” 0:12:02.200,0:12:04.800 Kila siku ina riziki yake. 0:12:04.800,0:12:06.600 Kila siku ina baraka zake. 0:12:06.600,0:12:08.440 Kila siku ina shida zake. 0:12:08.440,0:12:10.080 Tazama Yesu anachosema hapa. 0:12:10.080,0:12:17.880 Lakini kwa nini ni jambo la kawaida kwetu leo ​​kuanguka katika mtego wa kuhangaikia kesho? 0:12:17.880,0:12:22.840 Kwa sababu tunaanguka katika mtego[br]wa kujivunia kesho, 0:12:22.840,0:12:32.000 Tunafanya kana kwamba kesho ni yetu,[br]ilihali leo tu ndio yetu. 0:12:32.000,0:12:33.680 Kesho ni ya Mungu. 0:12:33.680,0:12:39.000 Sasa ni yako; kinachofuata ni cha Mungu. 0:12:39.000,0:12:44.560 Ngoja nisome Andiko lingine[br]kutoka Mithali 27, 0:12:44.560,0:12:48.720 tukirudia maneno ya[br]Yakobo ambayo tumesoma hivi punde. 0:12:48.720,0:12:53.280 Katika Mithali 27:1, mwenye hekima anasema hivi, 0:12:53.280,0:13:12.160 "Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa maana hujui yatakayoletwa na siku moja." 0:13:12.160,0:13:16.720 Ninasisitiza nini kwa kunukuu Maandiko haya, watu wa Mungu, 0:13:16.720,0:13:19.880 kuzungumza juu ya mada hii?[br]Kwa sababu ni mwaka mpya. 0:13:19.880,0:13:23.040 Ni wakati tunafikiria mbele, tunapanga mipango. 0:13:23.040,0:13:24.880 Lengo ni lipi? Tutafanya nini? 0:13:24.880,0:13:27.720 Sipingani na mipango hiyo, narudia. 0:13:27.720,0:13:32.760 Mimi sihimizi uvivu.[br]Mimi sihimizi uzembe. 0:13:32.760,0:13:36.160 Sikuhimii[br]kukaa tu, kukunja mikono yako 0:13:36.160,0:13:38.680 na kutarajia mambo kushuka kutoka[br]Mbinguni hadi mapajani mwako. 0:13:38.680,0:13:51.360 Ni vizuri kufanya mipango, lakini ni lazima tufanye hivyo kwa kutambua nafasi ya Mungu. 0:13:51.360,0:14:00.040 Ikiwa sivyo, unaweza kuanguka katika mtego wa kuwa na wasiwasi juu ya kesho au kujisifu kuhusu kesho. 0:14:00.040,0:14:02.160 Unaweza hata usijue, 0:14:02.160,0:14:09.080 lakini jinsi unavyoitikia[br]mpango wako unapokatizwa itaonyesha hivyo. 0:14:09.080,0:14:12.760 Hii ni hatua ya kujichunguza,[br]watu wa Mungu. 0:14:12.760,0:14:18.480 Umefanya mpango - 'Nataka kwenda hapa wakati huu; Nataka kufanya hivi katika biashara yangu.' 0:14:18.480,0:14:24.160 Je, unaitikiaje[br]mpango huo unapokatizwa? 0:14:24.160,0:14:33.760 Mwitikio wako kwa kukatizwa kwa mpango wako unaonyesha ni mpango wa yupi unauamini hakika. 0:14:33.760,0:14:37.120 Je, unaanguka pale mipango yako inapoanguka? 0:14:37.120,0:14:42.880 Unaanza kunung'unika, kulalamika,[br]kujilinganisha na wengine 0:14:42.880,0:14:46.880 na kujipima kwa[br]viwango vilivyotengenezwa na mwanadamu. 0:14:46.880,0:14:52.080 Je, furaha yako huanguka pale[br]mipango yako inapovunjika? 0:14:52.080,0:14:57.480 Je, amani yako husambaratika[br]pale mpango wako unaposambaratika? 0:14:57.480,0:15:01.360 Inaonyesha hujaweka[br]mpango wako mikononi mwa Mungu. 0:15:01.360,0:15:05.800 Kwa sababu kile unachokiona kama[br]usumbufu katika mpango wako 0:15:05.800,0:15:10.840 kinaweza kuwa hatua kuelekea[br]utimilifu wa mpango wa Mungu. 0:15:10.840,0:15:15.480 Mungu ni mkuu! 0:15:15.480,0:15:19.080 Anawatunza watoto wake. 0:15:19.080,0:15:26.960 Wakati mwingine kile unachokiona kama usumbufu kinaweza kuwa uingiliaji kati wa Mungu 0:15:26.960,0:15:36.120 kukuhifadhi, kukutayarisha, kukuimarisha, kukurekebisha, kukujenga kiroho. 0:15:36.120,0:15:40.400 Unachokiona kama[br]usumbufu katika mpango wako 0:15:40.400,0:15:45.880 kinaweza kuwa hatua ya kutimiza mpango wa Mungu. 0:15:45.880,0:15:55.560 Lakini mara nyingi, mipango yetu inapoingiliwa, inapodukizwa, 0:15:55.560,0:16:01.040 tunaitikiaje? Je, tunajibuje? 0:16:01.040,0:16:04.960 Unajibu kwa imani au hofu? 0:16:04.960,0:16:09.840 Je, unajibu kwa[br]utulivu au kulalamika? 0:16:09.840,0:16:13.600 Je, unatendaje[br]mpango wako unapoingiliwa? 0:16:13.600,0:16:16.440 Umefanya kila[br]linalowezekana kibinadamu. 0:16:16.440,0:16:20.440 Umetekeleza sehemu yako, lakini[br]mambo yaliyo nje ya uwezo wako 0:16:20.440,0:16:24.840 yakaja na kuusambaratisha huo mpango.[br]Je, unaitikiaje? 0:16:24.840,0:16:31.640 Ndiyo maana nilisema watu wa Mungu,[br]mnapopanga mipango ya kesho, 0:16:31.640,0:16:42.280 fanya hivyo ukitambua maisha hayana uhakika, Mungu ni mwenye enzi na kila siku ina riziki yake. 0:16:42.280,0:16:48.760 Unapaswa kufanya nini?[br]Zingatia neema ya leo. 0:16:48.760,0:16:55.080 Wengine tunahangaika sana kuhusu kesho, tunajishughulisha sana kufikiria kesho 0:16:55.080,0:17:02.960 kiasi kwamba hatusimamii ipasavyo, kukifanyia kazi kile kilicho mikononi mwetu leo. 0:17:02.960,0:17:07.800 Usitarajie tu 0:17:07.800,0:17:13.080 kwamba neema uliyo nayo leo itapatikana kwako kesho. 0:17:13.080,0:17:24.080 Usifikirie kuwa unachoweza kufikia leo, utaweza kukifikia kesho. 0:17:24.080,0:17:28.520 Mungu hutupa neema kwa kila siku. 0:17:28.520,0:17:33.000 Ndiyo maana ni lazima umwamini Yeye kila siku. 0:17:33.000,0:17:36.880 Ndiyo maana unahitaji kuwa na[br]uhusiano naye. 0:17:36.880,0:17:41.520 Ndio, unapanga mipango yako. Ndiyo, unafanya kazi kwa bidii kuelekea utimizo huo. 0:17:41.520,0:17:46.520 Ndio, unatoa ubora wako kwa[br]ufahamu: 0:17:46.520,0:17:52.040 Nani mwenye kauli ya mwisho?[br]Yehova ndiye mwenye uamuzi wa mwisho. 0:17:52.040,0:17:54.000 Unakumbuka wimbo huo! 0:17:54.000,0:18:03.080 Nani mwenye usemi wa mwisho[br]Yehova ndiye mwenye usemi wa mwisho 0:18:03.080,0:18:06.480 Mungu ndiye mwenye neno la mwisho katika maisha yetu. 0:18:06.480,0:18:09.800 Mipango yetu si kuchukua nafasi yake. 0:18:09.800,0:18:16.080 Ukifanya mpango, uweke mikononi Mwake. 0:18:16.080,0:18:20.680 Hili ni neno langu la kutia moyo[br]kwenu leo ​​watu wa Mungu. 0:18:20.680,0:18:24.200 Narudia, sikukatishi tamaa[br]kufanya mpango huo. 0:18:24.200,0:18:26.480 Kwa kweli, ninahimiza! 0:18:26.480,0:18:31.160 Ukiwa Mkristo, tafakari kwa makini na kwa sala mwaka ujao. 0:18:31.160,0:18:35.960 Fanya mpango. Utafuteni uso wa Mungu kwa ajili yake. Ni nzuri! 0:18:35.960,0:18:38.960 Wakati mwingine watu huenda[br]mbali sana kwa njia nyingine. 0:18:38.960,0:18:43.760 Wanasema, ‘Vema, kama Mungu[br]ameniahidi hilo, basi 0:18:43.760,0:18:47.680 Yeye ndiye atakayeileta[br]kwangu.' - kama hivyo. 0:18:47.680,0:18:49.040 Wacha niiweke kama hii: 0:18:49.040,0:18:55.680 Kumngoja Bwana si kisingizio[br]cha kutokufanya sehemu yako. 0:18:55.680,0:18:58.760 'Namngoja Bwana kwa baraka hii. 0:18:58.760,0:19:00.720 Namngoja Bwana[br]kwa ajili ya mafanikio hayo. 0:19:00.720,0:19:04.760 Ninamngojea Bwana[br]ahadi hiyo itimie.' Nzuri! 0:19:04.760,0:19:07.080 Je, unamngojeaje Bwana kwa ufanisi? 0:19:07.080,0:19:09.800 Unatumia kile kilicho[br]mikononi mwako leo. 0:19:09.800,0:19:12.480 Kumngoja Bwana si[br]kisingizio cha uvivu. 0:19:12.480,0:19:16.240 Wacha tusiwe na usimamizi mbaya wa kiroho. 0:19:16.240,0:19:24.640 Mungu hatabariki uwakili usiowajibika kwa mafanikio. 0:19:24.640,0:19:27.960 Unaomba, 'Mungu, ibariki biashara yangu' 0:19:27.960,0:19:31.880 lakini unasimamia vibaya kile[br]kilicho mikononi mwako leo. 0:19:31.880,0:19:34.720 Sala hiyo inawezaje kutimia? 0:19:34.720,0:19:37.840 Natumaini mtafuata ninachosema[br], watu wa Mungu. 0:19:37.840,0:19:43.440 Tumia kile kilicho mikononi mwako leo[br]kwa neema ya leo. 0:19:43.440,0:19:44.640 Wacha niiweke kama hii: 0:19:44.640,0:19:50.920 Changanya kazi ngumu na[br]imani tulivu kwa Mungu kwa siku zijazo. 0:19:50.920,0:19:56.280 Fanya bidii kuelekea ndoto yako. Ndoto yako haitafanya kazi kwako. 0:19:56.280,0:20:03.400 Fanya bidii kuelekea mpango wako. Mpango wako[br]hautapanda mbegu kwa ajili yako. 0:20:03.400,0:20:10.000 Lakini unapofanya kazi kwa bidii, unapotoa bora yako, unafanya hivyo kwa ufahamu - 0:20:10.000,0:20:16.400 maisha yangu yako mikononi mwa Mungu;[br]nyakati zangu ziko mikononi mwa Mungu. 0:20:16.400,0:20:22.080 Acha nikusomee methali moja zaidi,[br]wakati huu kutoka Mithali 16. 0:20:22.080,0:20:28.560 Mwenye hekima anaiweka wazi.[br]Mithali 16:9 inasema hivi, 0:20:28.560,0:20:35.520 "Moyo wa mtu huifikiri njia yake,[br]bali Bwana huziongoza hatua zake." 0:20:35.520,0:20:42.040 Mipango yako mikononi mwa Mungu. 0:20:42.040,0:20:48.680 Wana wa Mungu, liwekeni neno hili moyoni. 0:20:48.680,0:20:57.040 Unapoweka kila kitu mikononi mwa Mungu, 0:20:57.040,0:21:03.480 hivi karibuni utaona[br]mikono ya Mungu katika kila kitu. 0:21:03.480,0:21:10.760 Lazima uamini kwamba mkono Wake unafanya kazi 0:21:10.760,0:21:18.640 hata wakati huwezi[br]kufuatilia maandishi ya mkono Wake. 0:21:18.640,0:21:26.000 Labda sijui mwisho wa hadithi, 0:21:26.000,0:21:31.800 Lakini ninamwamini Mwandishi wa hadithi. 0:21:31.800,0:21:37.480 Labda nisione picha kamili. 0:21:37.480,0:21:41.080 Lakini ninamwamini Mpangaji Mkuu. 0:21:41.080,0:21:44.280 Labda nisione bidhaa iliyokamilishwa. 0:21:44.280,0:21:48.560 Lakini ninamwamini Mbuni wa Kimungu. 0:21:48.560,0:21:53.360 Huu ndio msimamo wetu kama Wakristo. 0:21:53.360,0:21:57.880 Ngoja ninukuu kitu[br]alichosema Nabii TB Joshua 0:21:57.880,0:22:00.840 kufikisha ujumbe huu kwenye hitimisho. 0:22:00.840,0:22:09.000 Baada ya lazima uwe umefanya[br]kila linalowezekana kibinadamu, 0:22:09.000,0:22:15.440 mwachie Mungu suala hilo ili atie alama kazi yako. 0:22:15.440,0:22:21.240 Hivi ndivyo unavyoweka[br]mipango yako mikononi mwa Mungu. 0:22:21.240,0:22:27.200 Shetani anataka tukazie fikira kile ambacho hatuna, na kukazia fikira kile ambacho hatujui. 0:22:27.200,0:22:32.600 Kwa sababu hii husababisha wasiwasi,[br]malalamiko, usimamizi mbaya. 0:22:32.600,0:22:37.480 Lakini kama Mkristo, unajua nini?[br]Mungu ni mwenye enzi. Mungu ni mwema. 0:22:37.480,0:22:40.640 Anaona picha kubwa zaidi. 0:22:40.640,0:22:44.080 Una nini? Neema kwa leo. 0:22:44.080,0:22:53.240 Tumia kile kilicho mikononi mwako leo na acha kila kitu mikononi mwake kwa ajili ya kesho. 0:22:53.240,0:23:01.240 Mungu abariki neno hili la kutia moyo katikati ya mioyo yetu.