0:00:00.400,0:00:08.040
Ukishindwa kumuingiza Mungu katika mipango yako,[br]unapanga kushindwa.
0:00:09.760,0:00:14.960
Karibuni tena nyote kwenye[br]Ibada hii ya Maombi Shirikishi.
0:00:14.960,0:00:21.520
Kabla ya jambo lolote, tuombe pamoja.
0:00:21.520,0:00:31.520
Ninaomba sasa hivi kwa kila moyo[br]ulioungana na huduma hii
0:00:31.520,0:00:46.040
kwamba wakutane na uhalisia wa uwezo wako, upendo, wema wako katika maisha yao.
0:00:46.040,0:00:54.960
Katika jina kuu la Yesu Kristo tunaomba.
0:00:54.960,0:00:59.120
Na watu wa Mungu wakasema, Amina!
0:00:59.120,0:01:10.000
Kwanza kabisa, wacha niwasalimie nyote[br]Heri ya Mwaka Mpya 2025.
0:01:10.000,0:01:15.160
Nina neno la kutia moyo[br]la kukushirikisha leo.
0:01:15.160,0:01:20.600
Ni kawaida katika kipindi hiki - tunapoondoka mwaka mmoja na kuingia mwaka mpya -
0:01:20.600,0:01:25.240
ni kawaida sana kwetu kuwa na muda wa kutafakari yaliyo mbele.
0:01:25.240,0:01:28.840
Je, nina mipango gani[br]kwa mwaka huu unaokuja?
0:01:28.840,0:01:34.400
Inaweza kuwa katika maisha yako ya kibinafsi,[br]maisha yako ya kitaaluma.
0:01:34.400,0:01:37.680
Inaweza kuwa katika taaluma yako -[br]'Nataka kupanua biashara hapa.'
0:01:37.680,0:01:42.640
Labda mahusiano - 'Mwaka huu,[br]nataka kuolewa!'
0:01:42.640,0:01:46.160
'Mwaka huu, tunataka kupata watoto pamoja' - waume na wake.
0:01:46.160,0:01:47.840
Huu ni wakati ambao tunapanga mipango.
0:01:47.840,0:01:51.520
Tunafikiria mwaka ujao,[br]mwaka ujao. Nzuri!
0:01:51.520,0:01:56.640
Ni vizuri kupanga mipango lakini
0:01:56.640,0:02:08.960
usiingie kwenye makosa ya kupanga mipango ya kesho kana kwamba wewe ndiye mmiliki wake.
0:02:08.960,0:02:13.720
Fikirini juu ya hilo enyi watu wa Mungu.
0:02:13.720,0:02:27.400
Usiingie kwenye mtego wa kupanga mipango ya siku zijazo kana kwamba ni yako.
0:02:27.400,0:02:30.800
Sisemi ni makosa kupanga mipango.
0:02:30.800,0:02:34.080
Sisemi ni makosa kuangalia mbele.
0:02:34.080,0:02:40.280
Ninasema unapofanya[br]mipango kama Mkristo -
0:02:40.280,0:02:44.440
'Nini kinachofuata mnamo 2025? Kipi kilicho mbele?
0:02:44.440,0:02:45.640
Je! ninataka kuzingatia nini?
0:02:45.640,0:02:51.440
Ninataka kufikia nini katika kazi yangu, maisha ya kibinafsi, biashara, fedha?
0:02:51.440,0:02:52.880
Ninataka kufanya nini?'
0:02:52.880,0:03:00.800
Unapopanga mipango, lazima ufanye hivyo[br]kwa utambuzi wa mambo matatu.
0:03:00.800,0:03:03.600
Na mimi nataka uandike.[br]Tafadhali andika hii.
0:03:03.600,0:03:07.240
Ujumbe huu utakusaidia kwa mwaka huu.
0:03:07.240,0:03:16.160
1. Maisha hayana uhakika
0:03:16.160,0:03:26.880
2. Mungu ni mwenye enzi kuu
0:03:26.880,0:03:36.160
3. Kila siku ina riziki yake
0:03:36.160,0:03:38.840
Nitawaambia tena, watu wa Mungu.
0:03:38.840,0:03:43.800
Unapopanga mipango, unapopanga juu ya siku zijazo,
0:03:43.800,0:03:50.320
lazima ufanye hivyo ukiwa na utambuzi huu,[br]ufahamu huu -
0:03:50.320,0:03:55.880
1. Maisha hayana uhakika
0:03:55.880,0:04:04.040
Wakati fulani tutakabili hali[br]zilizo nje ya uwezo wetu.
0:04:04.040,0:04:10.480
Kwa nini unapanga mipango[br]kana kwamba unaudhibiti?
0:04:10.480,0:04:22.640
Wakati mwingine kama mtoto wa Mungu, unaweza[br]kukutana na matukio yasiyobadilika -
0:04:22.640,0:04:33.640
hakuna kiasi cha maombi, kufunga au[br]kukomaa kiroho kutabadili.
0:04:33.640,0:04:38.840
Maisha hayana uhakika.
0:04:38.840,0:04:44.800
2. Mungu ni mwenye enzi kuu
0:04:44.800,0:04:53.320
Maisha kukosa uhakika hakubadili[br]enzi kuu ya Mungu.
0:04:53.320,0:04:56.240
Ndiyo, maisha yamejawa na kutokuwa na uhakika.
0:04:56.240,0:05:06.640
Lakini jambo moja unaweza kuwa na uhakika nalo - wema wa Mungu, nguvu za Mungu, upendo wa Mungu.
0:05:06.640,0:05:12.600
Hata katikati ya[br]wazimu wa dunia hii,
0:05:12.600,0:05:17.400
tunaweza kuwa na uhakika juu ya[br]wema wa Mungu.
0:05:17.400,0:05:19.320
Yeye ni mwenye enzi.
0:05:19.320,0:05:33.360
Na kama Wakristo, lazima tutambue maisha yetu, nyakati zetu ziko mikononi mwake.
0:05:33.360,0:05:34.960
Mungu ni mwenye enzi.
0:05:34.960,0:05:40.120
3. Kila siku ina riziki yake
0:05:40.120,0:05:45.880
Utupe leo mkate wetu wa kila siku.
0:05:45.880,0:05:49.320
Mana kwa hitaji la wakati huu.
0:05:49.320,0:05:58.280
Kila siku ina riziki yake -[br]Mungu hutoa neema kwa kila siku.
0:05:58.280,0:06:04.520
Ujumbe ninaopaswa kushiriki[br]nawe, kwa ufupi ni huu:
0:06:04.520,0:06:10.360
'Mipango yako Mikononi mwa Mungu'.
0:06:10.360,0:06:15.360
Unaweza kusema hivyo sasa hivi. Ikiwa uko na mtu nyumbani, mwambie tu,
0:06:15.360,0:06:20.840
"Mipango yako mikononi mwa Mungu."
0:06:20.840,0:06:25.520
Ikiwa uko peke yako, unaweza kujiambia[br]au unaweza kuniambia,
0:06:25.520,0:06:31.680
"Mipango yangu iko mikononi mwa Mungu."
0:06:31.680,0:06:37.000
Mwanadamu hupanga; Mungu hutekeleza.
0:06:37.000,0:06:43.680
Mwanadamu anapendekeza; Mungu huamuru.
0:06:43.680,0:06:49.840
Kama Mkristo, tazama, sikwambii tena kwamba usifanye mpango,
0:06:49.840,0:06:57.960
bali panga mipango huku ukifahamu[br]kuwa maisha yako yako mikononi mwa Mungu.
0:06:57.960,0:07:07.680
Fanya mipango kutoka katika nafasi ya[br]kujitiisha kwa Mpangaji Mkuu
0:07:07.680,0:07:15.640
ambaye njia zake ni za juu kuliko zetu,[br]ambaye mipango yake ni mikubwa kuliko yetu.
0:07:15.640,0:07:25.800
Wale wanaoshindwa kuweka[br]mipango yao mikononi mwa Mungu
0:07:25.800,0:07:31.560
wanajiweka kwenye[br]njia ya kushindwa.
0:07:31.560,0:07:35.240
Hata nitarahisisha. Nitasema hivi -
0:07:35.240,0:07:45.840
ukishindwa kumjumuisha Mungu katika mipango yako,[br]unapanga kushindwa.
0:07:45.840,0:07:52.240
Hebu tuyaangazie Maandiko makini katika Yakobo 4.
0:07:52.240,0:07:58.960
Ninataka kuangazia ukweli huu ili wakati tunapanga mipango ya kesho,
0:07:58.960,0:08:06.840
tunafanya hivyo tukiwa na ufahamu sahihi wa[br]nafasi ya Mungu na nafasi yetu.
0:08:06.840,0:08:13.000
Unapopanga juu ya siku zijazo,[br]kumbuka ni nani aliye Mkuu.
0:08:13.000,0:08:19.600
Hebu tusome pamoja - Yakobo 4:13.
0:08:19.600,0:08:28.600
“Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutakwenda katika mji fulani;
0:08:28.600,0:08:33.560
tutakaa huko mwaka mzima, tutanunua na kuuza[br]na kujipatia faida...”
0:08:33.560,0:08:39.920
'Mnamo 2025, nitaenda huko.[br]Nitafanya hivi katika biashara yangu.
0:08:39.920,0:08:44.120
Hakika hili litatokea.'
0:08:44.120,0:08:52.960
“... kumbe hujui kitakachotokea kesho. Kwani maisha yako ni nini?
0:08:52.960,0:09:08.160
Bali ni mvuke unaoonekana kwa muda mfupi na kisha kutoweka.
0:09:08.160,0:09:20.120
Badala yake mnapaswa kusema, Bwana akipenda, tutaishi na kufanya hili au lile.
0:09:20.120,0:09:25.400
"Bwana akipenda, hili litatokea mwaka wa 2025.
0:09:25.400,0:09:32.840
Bwana akipenda, mpango huu utatimia.'
0:09:32.840,0:09:44.480
Yakobo 4:16 BHN - Lakini sasa mnajivunia majivuno yenu. Majivuno yote kama hayo ni mabaya.”
0:09:44.480,0:09:51.880
Maandiko hapa, nataka kusisitiza,[br]hayasemi kamwe usifanye mpango,
0:09:51.880,0:09:59.960
lakini yanakuonya usiichukue nafasi ya Mungu inapokuja kwenye mpango wako.
0:09:59.960,0:10:08.360
Kama nilivyosema hapo awali, unapotazama mbele, kumbuka ni nani aliye Kichwa - Yesu.
0:10:08.360,0:10:15.360
Hakuna kitu hatari zaidi kama kuchukua nafasi ya Mungu katika mpango wako.
0:10:15.360,0:10:28.360
Kuchukua nafasi ya Mungu katika mpango wako ndiyo njia ya uhakika ya kuanguka kwa mpango huo - hatimaye.
0:10:28.360,0:10:31.360
Sasa, unaweza kunitazama na kusema,[br]'Unasema nini Ndugu Chris?
0:10:31.360,0:10:38.600
Sichukui nafasi ya Mungu katika mpango wangu. Ningewezaje kuwa Mungu? Mimi si Mungu!'
0:10:38.600,0:10:45.680
Lakini wengi wetu, kwa jinsi tunavofanya[br]mipango yetu ya kesho,
0:10:45.680,0:10:51.560
tunafanya hivyo kwa njia inayochukua[br]umiliki wa kesho.
0:10:51.560,0:10:55.040
Na unajua hatari ya hii?
0:10:55.040,0:10:58.680
Unapochukua umiliki wa kesho,
0:10:58.680,0:11:02.240
unabeba uzito ambao hukukusudiwa[br]kubeba,
0:11:02.240,0:11:10.840
ndiyo maana bila shaka huishia[br]katika wasiwasi, woga na mashaka.
0:11:10.840,0:11:15.320
'Nini kitatokea? Itakuwaje juu ya hiki?[br]Vipi kuhusu lile?'
0:11:15.320,0:11:20.080
Wasiwasi ni mwizi wa furaha.
0:11:20.080,0:11:24.840
Wasiwasi ni mwizi wa amani.
0:11:24.840,0:11:30.000
Wasiwasi ni mwizi wa hukumu halali,
0:11:30.000,0:11:35.600
ambayo ni muhimu katika kuwa msimamizi mzuri[br]wa kile kilicho mikononi mwako leo.
0:11:35.600,0:11:47.200
Ngoja nikukumbushe maneno mazuri ya Bwana wetu Yesu Kristo katika Mathayo 6:34.
0:11:47.200,0:11:53.760
Yesu alisema, “Basi, msisumbukie[br]ya kesho;
0:11:53.760,0:12:02.200
maana kesho itajisumbukia na mambo yake. Yatosha kwa siku taabu yake yenyewe.”
0:12:02.200,0:12:04.800
Kila siku ina riziki yake.
0:12:04.800,0:12:06.600
Kila siku ina baraka zake.
0:12:06.600,0:12:08.440
Kila siku ina shida zake.
0:12:08.440,0:12:10.080
Tazama Yesu anachosema hapa.
0:12:10.080,0:12:17.880
Lakini kwa nini ni jambo la kawaida kwetu leo kuanguka katika mtego wa kuhangaikia kesho?
0:12:17.880,0:12:22.840
Kwa sababu tunaanguka katika mtego[br]wa kujivunia kesho,
0:12:22.840,0:12:32.000
Tunafanya kana kwamba kesho ni yetu,[br]ilihali leo tu ndio yetu.
0:12:32.000,0:12:33.680
Kesho ni ya Mungu.
0:12:33.680,0:12:39.000
Sasa ni yako; kinachofuata ni cha Mungu.
0:12:39.000,0:12:44.560
Ngoja nisome Andiko lingine[br]kutoka Mithali 27,
0:12:44.560,0:12:48.720
tukirudia maneno ya[br]Yakobo ambayo tumesoma hivi punde.
0:12:48.720,0:12:53.280
Katika Mithali 27:1, mwenye hekima anasema hivi,
0:12:53.280,0:13:12.160
"Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa maana hujui yatakayoletwa na siku moja."
0:13:12.160,0:13:16.720
Ninasisitiza nini kwa kunukuu Maandiko haya, watu wa Mungu,
0:13:16.720,0:13:19.880
kuzungumza juu ya mada hii?[br]Kwa sababu ni mwaka mpya.
0:13:19.880,0:13:23.040
Ni wakati tunafikiria mbele, tunapanga mipango.
0:13:23.040,0:13:24.880
Lengo ni lipi? Tutafanya nini?
0:13:24.880,0:13:27.720
Sipingani na mipango hiyo, narudia.
0:13:27.720,0:13:32.760
Mimi sihimizi uvivu.[br]Mimi sihimizi uzembe.
0:13:32.760,0:13:36.160
Sikuhimii[br]kukaa tu, kukunja mikono yako
0:13:36.160,0:13:38.680
na kutarajia mambo kushuka kutoka[br]Mbinguni hadi mapajani mwako.
0:13:38.680,0:13:51.360
Ni vizuri kufanya mipango, lakini ni lazima tufanye hivyo kwa kutambua nafasi ya Mungu.
0:13:51.360,0:14:00.040
Ikiwa sivyo, unaweza kuanguka katika mtego wa kuwa na wasiwasi juu ya kesho au kujisifu kuhusu kesho.
0:14:00.040,0:14:02.160
Unaweza hata usijue,
0:14:02.160,0:14:09.080
lakini jinsi unavyoitikia[br]mpango wako unapokatizwa itaonyesha hivyo.
0:14:09.080,0:14:12.760
Hii ni hatua ya kujichunguza,[br]watu wa Mungu.
0:14:12.760,0:14:18.480
Umefanya mpango - 'Nataka kwenda hapa wakati huu; Nataka kufanya hivi katika biashara yangu.'
0:14:18.480,0:14:24.160
Je, unaitikiaje[br]mpango huo unapokatizwa?
0:14:24.160,0:14:33.760
Mwitikio wako kwa kukatizwa kwa mpango wako unaonyesha ni mpango wa yupi unauamini hakika.
0:14:33.760,0:14:37.120
Je, unaanguka pale mipango yako inapoanguka?
0:14:37.120,0:14:42.880
Unaanza kunung'unika, kulalamika,[br]kujilinganisha na wengine
0:14:42.880,0:14:46.880
na kujipima kwa[br]viwango vilivyotengenezwa na mwanadamu.
0:14:46.880,0:14:52.080
Je, furaha yako huanguka pale[br]mipango yako inapovunjika?
0:14:52.080,0:14:57.480
Je, amani yako husambaratika[br]pale mpango wako unaposambaratika?
0:14:57.480,0:15:01.360
Inaonyesha hujaweka[br]mpango wako mikononi mwa Mungu.
0:15:01.360,0:15:05.800
Kwa sababu kile unachokiona kama[br]usumbufu katika mpango wako
0:15:05.800,0:15:10.840
kinaweza kuwa hatua kuelekea[br]utimilifu wa mpango wa Mungu.
0:15:10.840,0:15:15.480
Mungu ni mkuu!
0:15:15.480,0:15:19.080
Anawatunza watoto wake.
0:15:19.080,0:15:26.960
Wakati mwingine kile unachokiona kama usumbufu kinaweza kuwa uingiliaji kati wa Mungu
0:15:26.960,0:15:36.120
kukuhifadhi, kukutayarisha, kukuimarisha, kukurekebisha, kukujenga kiroho.
0:15:36.120,0:15:40.400
Unachokiona kama[br]usumbufu katika mpango wako
0:15:40.400,0:15:45.880
kinaweza kuwa hatua ya kutimiza mpango wa Mungu.
0:15:45.880,0:15:55.560
Lakini mara nyingi, mipango yetu inapoingiliwa, inapodukizwa,
0:15:55.560,0:16:01.040
tunaitikiaje? Je, tunajibuje?
0:16:01.040,0:16:04.960
Unajibu kwa imani au hofu?
0:16:04.960,0:16:09.840
Je, unajibu kwa[br]utulivu au kulalamika?
0:16:09.840,0:16:13.600
Je, unatendaje[br]mpango wako unapoingiliwa?
0:16:13.600,0:16:16.440
Umefanya kila[br]linalowezekana kibinadamu.
0:16:16.440,0:16:20.440
Umetekeleza sehemu yako, lakini[br]mambo yaliyo nje ya uwezo wako
0:16:20.440,0:16:24.840
yakaja na kuusambaratisha huo mpango.[br]Je, unaitikiaje?
0:16:24.840,0:16:31.640
Ndiyo maana nilisema watu wa Mungu,[br]mnapopanga mipango ya kesho,
0:16:31.640,0:16:42.280
fanya hivyo ukitambua maisha hayana uhakika, Mungu ni mwenye enzi na kila siku ina riziki yake.
0:16:42.280,0:16:48.760
Unapaswa kufanya nini?[br]Zingatia neema ya leo.
0:16:48.760,0:16:55.080
Wengine tunahangaika sana kuhusu kesho, tunajishughulisha sana kufikiria kesho
0:16:55.080,0:17:02.960
kiasi kwamba hatusimamii ipasavyo, kukifanyia kazi kile kilicho mikononi mwetu leo.
0:17:02.960,0:17:07.800
Usitarajie tu
0:17:07.800,0:17:13.080
kwamba neema uliyo nayo leo itapatikana kwako kesho.
0:17:13.080,0:17:24.080
Usifikirie kuwa unachoweza kufikia leo, utaweza kukifikia kesho.
0:17:24.080,0:17:28.520
Mungu hutupa neema kwa kila siku.
0:17:28.520,0:17:33.000
Ndiyo maana ni lazima umwamini Yeye kila siku.
0:17:33.000,0:17:36.880
Ndiyo maana unahitaji kuwa na[br]uhusiano naye.
0:17:36.880,0:17:41.520
Ndio, unapanga mipango yako. Ndiyo, unafanya kazi kwa bidii kuelekea utimizo huo.
0:17:41.520,0:17:46.520
Ndio, unatoa ubora wako ukiwa na[br]ufahamu:
0:17:46.520,0:17:52.040
Nani mwenye kauli ya mwisho?[br]Yehova ndiye mwenye uamuzi wa mwisho.
0:17:52.040,0:17:54.000
Unakumbuka wimbo huo!
0:17:54.000,0:18:03.080
Nani mwenye usemi wa mwisho[br]Yehova ndiye mwenye usemi wa mwisho
0:18:03.080,0:18:06.480
Mungu ndiye mwenye neno la mwisho katika maisha yetu.
0:18:06.480,0:18:09.800
Mipango yetu si kuchukua nafasi yake.
0:18:09.800,0:18:16.080
Ukifanya mpango, uweke mikononi Mwake.
0:18:16.080,0:18:20.680
Hili ni neno langu la kutia moyo[br]kwenu leo watu wa Mungu.
0:18:20.680,0:18:24.200
Narudia, sikukatishi tamaa[br]kufanya mpango huo.
0:18:24.200,0:18:26.480
Kwa kweli, ninahimiza!
0:18:26.480,0:18:31.160
Ukiwa Mkristo, tafakari kwa makini na kwa sala mwaka ujao.
0:18:31.160,0:18:35.960
Fanya mpango. Utafuteni uso wa Mungu kwa ajili yake. Ni nzuri!
0:18:35.960,0:18:38.960
Wakati mwingine watu huenda[br]mbali sana kwa njia nyingine.
0:18:38.960,0:18:43.760
Wanasema, ‘Vema, kama Mungu[br]ameniahidi hilo, basi
0:18:43.760,0:18:47.680
Yeye ndiye atakayeileta[br]kwangu.' - kama hivyo.
0:18:47.680,0:18:49.040
Wacha niiweke kama hii:
0:18:49.040,0:18:55.680
Kumngoja Bwana si kisingizio[br]cha kutokufanya sehemu yako.
0:18:55.680,0:18:58.760
'Namngoja Bwana kwa baraka hii.
0:18:58.760,0:19:00.720
Namngoja Bwana[br]kwa ajili ya mafanikio hayo.
0:19:00.720,0:19:04.760
Ninamngojea Bwana[br]ahadi hiyo itimie.' Nzuri!
0:19:04.760,0:19:07.080
Je, unamngojeaje Bwana kwa ufanisi?
0:19:07.080,0:19:09.800
Unatumia kile kilicho[br]mikononi mwako leo.
0:19:09.800,0:19:12.480
Kumngoja Bwana si[br]kisingizio cha uvivu.
0:19:12.480,0:19:16.240
Wacha tusiwe na usimamizi mbaya wa kiroho.
0:19:16.240,0:19:24.640
Mungu hatabariki uwakili usiowajibika kwa mafanikio.
0:19:24.640,0:19:27.960
Unaomba, 'Mungu, ibariki biashara yangu'
0:19:27.960,0:19:31.880
lakini unasimamia vibaya kile[br]kilicho mikononi mwako leo.
0:19:31.880,0:19:34.720
Sala hiyo inawezaje kutimia?
0:19:34.720,0:19:37.840
Natumaini mtafuata ninachosema[br], watu wa Mungu.
0:19:37.840,0:19:43.440
Tumia kile kilicho mikononi mwako leo[br]kwa neema ya leo.
0:19:43.440,0:19:44.640
Wacha niiweke kama hii:
0:19:44.640,0:19:50.920
Changanya kazi ngumu na[br]imani tulivu kwa Mungu kwa siku zijazo.
0:19:50.920,0:19:56.280
Fanya bidii kuelekea ndoto yako. Ndoto yako haitafanya kazi kwako.
0:19:56.280,0:20:03.400
Fanya bidii kuelekea mpango wako. Mpango wako[br]hautapanda mbegu kwa ajili yako.
0:20:03.400,0:20:10.000
Lakini unapofanya kazi kwa bidii, unapotoa bora yako, unafanya hivyo kwa ufahamu -
0:20:10.000,0:20:16.400
maisha yangu yako mikononi mwa Mungu;[br]nyakati zangu ziko mikononi mwa Mungu.
0:20:16.400,0:20:22.080
Acha nikusomee methali moja zaidi,[br]wakati huu kutoka Mithali 16.
0:20:22.080,0:20:28.560
Mwenye hekima anaiweka wazi.[br]Mithali 16:9 inasema hivi,
0:20:28.560,0:20:35.520
"Moyo wa mtu huifikiri njia yake,[br]bali Bwana huziongoza hatua zake."
0:20:35.520,0:20:42.040
Mipango yako mikononi mwa Mungu.
0:20:42.040,0:20:48.680
Wana wa Mungu, liwekeni neno hili moyoni.
0:20:48.680,0:20:57.040
Unapoweka kila kitu mikononi mwa Mungu,
0:20:57.040,0:21:03.480
hivi karibuni utaona[br]mikono ya Mungu katika kila kitu.
0:21:03.480,0:21:10.760
Lazima uamini kwamba mkono Wake unafanya kazi
0:21:10.760,0:21:18.640
hata wakati huwezi[br]kufuatilia maandishi ya mkono Wake.
0:21:18.640,0:21:26.000
Labda sijui mwisho wa hadithi,
0:21:26.000,0:21:31.800
Lakini ninamwamini Mwandishi wa hadithi.
0:21:31.800,0:21:37.480
Labda nisione picha kamili.
0:21:37.480,0:21:41.080
Lakini ninamwamini Mpangaji Mkuu.
0:21:41.080,0:21:44.280
Labda nisione bidhaa iliyokamilishwa.
0:21:44.280,0:21:48.560
Lakini ninamwamini Mbuni wa Kimungu.
0:21:48.560,0:21:53.360
Huu ndio msimamo wetu kama Wakristo.
0:21:53.360,0:21:57.880
Ngoja ninukuu kitu[br]alichosema Nabii TB Joshua
0:21:57.880,0:22:00.840
kufikisha ujumbe huu kwenye hitimisho.
0:22:00.840,0:22:09.000
Baada ya lazima uwe umefanya[br]kila linalowezekana kibinadamu,
0:22:09.000,0:22:15.440
mwachie Mungu suala hilo ili atie alama kazi yako.
0:22:15.440,0:22:21.240
Hivi ndivyo unavyoweka[br]mipango yako mikononi mwa Mungu.
0:22:21.240,0:22:27.200
Shetani anataka tukazie fikira kile ambacho hatuna, na kukazia fikira kile ambacho hatujui.
0:22:27.200,0:22:32.600
Kwa sababu hii husababisha wasiwasi,[br]malalamiko, usimamizi mbaya.
0:22:32.600,0:22:37.480
Lakini kama Mkristo, unajua nini?[br]Mungu ni mwenye enzi. Mungu ni mwema.
0:22:37.480,0:22:40.640
Anaona picha kubwa zaidi.
0:22:40.640,0:22:44.080
Una nini? Neema kwa leo.
0:22:44.080,0:22:53.240
Tumia kile kilicho mikononi mwako leo na acha kila kitu mikononi mwake kwa ajili ya kesho.
0:22:53.240,0:23:01.240
Mungu abariki neno hili la kutia moyo katikati ya mioyo yetu.