0:00:00.000,0:00:03.800 Ingawa bado niliipata ofa ya kazi hiyo,[br]bado nilimtafuta Mungu. 0:00:03.800,0:00:08.880 Kwa sababu nilielewa Alikuwa amenipa ndoto kuhusu kampuni ya awali, Kampuni A. 0:00:08.880,0:00:12.720 Na sasa fursa hii na[br]Kampuni B ilikuwa imepatikana. 0:00:12.720,0:00:15.800 Kwa hiyo wakati huo nilitafuta uso wa Mungu. 0:00:15.800,0:00:21.680 USHUHUDA [br]YV YA MOYO WA MUNGU 0:00:22.520,0:00:32.920 Ndiyo, watu wa Mungu, sasa hivi,[br]ninazungumza na kila eneo la maisha yenu 0:00:32.920,0:00:38.680 ambapo umekuwa ukipata msongo wa mawazo. 0:00:38.680,0:00:46.560 Sasa hivi, pokea pumziko la Kimbingu[br]kwa jina la Yesu Kristo! 0:00:46.560,0:00:53.080 Pumzika katika kazi yako! Pumzika katika biashara yako! Pumzika kwenye ndoa yako! Pumzika katika familia yako! 0:00:53.080,0:00:56.280 Pokea pumziko kutoka juu leo! 0:00:57.640,0:01:00.520 Jina langu ni Dumisani kutoka Zambia. 0:01:00.520,0:01:05.400 Ushuhuda wangu unahusu mafanikio ya kazi mwaka huu, 2024. 0:01:05.400,0:01:12.160 Yote ilianza 2022 nilipomaliza shule, na wakati huo nilikuwa nikitafuta kazi. 0:01:12.160,0:01:17.760 Nilikuwa nimehitimu kutoka China. Nimekuwa nikisoma nje ya nchi kwa zaidi ya miaka minne. 0:01:17.760,0:01:22.920 Na nilipokea digrii yangu ya kwanza[br]kufikia mwisho wa mwaka wa 2022. 0:01:22.920,0:01:26.200 Kwa hiyo nilikuwa nimerudi Zambia,[br]na kipindi hicho, 0:01:26.200,0:01:30.760 baada ya shahada yangu ndipo nilipolazimika[br]kuanza kutafuta kazi. 0:01:30.760,0:01:37.920 Na katika hali hiyo, haikuwa rahisi hata kidogo kwa sababu ya ushindani wa soko la ajira. 0:01:37.920,0:01:44.960 Tunao wahitimu wengi ambao wana uwezo wa kupata kazi yoyote ile. 0:01:44.960,0:01:48.960 Lakini kwa upande wangu, nilikuwa pia nikijaribu kushindana katika soko hilohilo la ajira. 0:01:48.960,0:01:52.120 Nilisomea uhandisi wa umeme na elektroniki nchini China. 0:01:52.120,0:02:02.520 Ilinibidi nichukue hatua hiyo mbele ili kupata kazi inayolingana na taaluma yangu 0:02:02.520,0:02:04.400 na katika kisa hiki, ilikuwa ngumu sana. 0:02:04.400,0:02:11.280 Kufikia wakati huo, sikujua ni kazi gani ningeweza hata kuomba - iwe mafunzo au kujishikiza. 0:02:11.280,0:02:15.200 Kwa sababu wakati wa kukaa kwangu nchini Uchina,[br]ambao ulikuwa wakati wa COVID, 0:02:15.200,0:02:21.160 ilikuwa ngumu sana kwangu kuwa na[br]aina yoyote ya kujishikiza kikazi 0:02:21.160,0:02:28.840 au kupata uzoefu wowote wakati wa masomo yangu ambao unaweza kutumika katika kutuma maombi ya kazi kwa urahisi zaidi. 0:02:28.840,0:02:32.560 Kwanza kabisa, sina budi kusema kwamba[br]Mungu amenisaidia sana. 0:02:32.560,0:02:37.440 Wakati huo nilikuwa nimeomba na kumtafuta Mungu juu ya kazi gani naweza kuomba. 0:02:37.440,0:02:41.000 Naweza kufanya nini? Je, ni aina gani ya nafasi ya kazi ninayopaswa kutafuta? 0:02:41.000,0:02:43.160 Na katika hali hiyo, Mungu aliniongoza kweli, 0:02:43.160,0:02:49.360 na kwa usadikisho huo, ilinisaidia kuanza kuangalia nafasi ya mwanafunzi aliyehitimu. 0:02:49.360,0:02:54.560 Na wakati huo, iligusa sana[br]moyo wangu na kunihukumu. 0:02:54.560,0:02:59.160 Nilikuwa nimemshirikisha wazo mama yangu,[br]na hivyo ndivyo nilianza kufanya utafiti zaidi. 0:02:59.160,0:03:03.440 Niliomba kwa Mungu na kutafuta mwongozo wake kwa sababu ya usadikisho huo huo - 0:03:03.440,0:03:05.560 kujua nini cha kufanya baadaye. 0:03:05.560,0:03:11.840 Kwa hiyo, wakati huo, nilijaribu kutuma ombi kwenye kampuni fulani ya uchimbaji madini katika nchi yangu. 0:03:11.840,0:03:16.320 Sikujua hata kuandika CV. 0:03:16.320,0:03:23.040 Sikujua jinsi ya kuangazia uzoefu niliokuwa nao nchini Uchina na mara nyingi, 0:03:23.040,0:03:27.640 watu wangeniambia ninahitaji uzoefu kupitia kujishikiza au aina fulani ya uzoefu wa kazi 0:03:27.640,0:03:31.600 ili upate kazi kwa urahisi. 0:03:31.600,0:03:38.880 Kwa hivyo nilihisi kukatishwa tamaa na ilionekana kana kwamba hakuna tumaini kwangu. 0:03:38.880,0:03:43.160 Lakini nilitiwa moyo na usadikisho huo wa kufuata mafunzo ya wahitimu. 0:03:43.160,0:03:47.920 Wakati huo, mama yangu alikuwa amenitia moyo kujaribu kutuma ombi mahali tofauti. 0:03:47.920,0:03:51.880 Nilisema ningejaribu ingawa[br]nilikuwa nikihisi kukata tamaa. 0:03:51.880,0:03:59.240 Nilikuwa nikimfuata Ndugu Chris[br]tangu mapema mwaka wa 2022. 0:03:59.240,0:04:03.760 Kwa sababu wakati huo, alikuwa ameonekana[br]kwenye muhtasari wa taarifa zangu kwenye Facebook. 0:04:03.760,0:04:08.760 Na kisha nikatiwa moyo na maneno yake katika mahubiri fulani niliyotazama. 0:04:08.760,0:04:14.760 Nilitiwa moyo kuanza kumfuata na kusikiliza mahubiri yake. 0:04:14.760,0:04:20.120 Na kwa neema ya Mungu, nilianza kufuatilia kwa jumbe 0:04:20.120,0:04:22.960 na klipu fupi za kutia moyo[br]hapa na pale. 0:04:22.960,0:04:27.960 Kwa hivyo wakati huo, nilipokuwa nikituma maombi,[br]mama yangu aliota ndoto 0:04:27.960,0:04:35.200 ambapo alipewa jina la 'Nishati'. 0:04:35.200,0:04:37.200 Nikasema, ‘Nishati. Unamaanisha nini?' 0:04:37.200,0:04:43.920 Alisema, 'Dumisani, nimeota jambo hili, na wewe ndiye pekee katika familia yetu 0:04:43.920,0:04:49.040 ambaye najua amefanya jambo linalohusiana na uhandisi, kwa hiyo inapaswa kuwa yako.' 0:04:49.040,0:04:54.240 Nilifikiri, 'Sawa, nishati. Ni kampuni gani[br]inayohusiana na nishati?' Nami nikaitazama. 0:04:54.240,0:04:59.640 Kwa hivyo nilikuwa na imani ya kutafiti[br]zaidi kuhusu kampuni hii. 0:04:59.640,0:05:06.400 Nilikuwa nimetafuta maoni ya Mungu kwa sababu kama si Yeye, hata nisingeweza 0:05:06.400,0:05:11.560 kujua la kufanya, jinsi ya kuandika wasifu wa kazi(curriculum vitae) au kitu kama hicho. 0:05:11.560,0:05:20.280 Wakati wa utafiti, niligundua kuwa walikuwa na programu ya mafunzo kwa wahitimu. 0:05:20.280,0:05:31.560 Ili kutoa muktadha zaidi, mara tu nilipoanza kufikiria zaidi juu ya mafunzo kwa wahitimu, 0:05:31.560,0:05:35.880 pia kulikuwa na fursa ambayo[br]ilikuja katika kampuni nyingine. 0:05:35.880,0:05:38.760 Kwa hivyo katika kisa hiki, sina budi kuelezea[br]kampuni hizi mbili 0:05:38.760,0:05:42.120 kama Kampuni A na Kampuni B,[br]kwa ajili ya uwazi. 0:05:42.120,0:05:45.120 Kwa hivyo Kampuni A ndiyo ambayo[br]mama yangu aliniambia kuihusu, 0:05:45.120,0:05:49.320 basi Kampuni B ilikuwa fursa hii ya baadaye ambayo ilikuwa imetokea. 0:05:49.320,0:05:53.240 Kwa hivyo kufikia wakati huo nilisema, 'Hey, nitajaribu tu[br]na kutuma maombi.' 0:05:53.240,0:05:58.920 Na kwa neema ya Mungu, niliitwa kwenye mahojiano ambayo nilihudhuria. 0:05:58.920,0:06:02.960 Niliwaza, 'Acha nijiweke pale na niende kwenye mahojiano haya.' 0:06:02.960,0:06:09.480 Sikufikiri kwamba nilifanya vyema[br]katika mahojiano na Kampuni B. 0:06:09.480,0:06:14.120 Lakini kwa neema ya Mungu, nilihojiwa[br]na niliitwa kwa ajili ya ofa ya kazi. 0:06:14.120,0:06:19.560 Kwa hiyo, ingawa bado nilipokea kazi hiyo, bado nilimtafuta Mungu. 0:06:19.560,0:06:24.680 Kwa sababu nilielewa Alikuwa amenipa ndoto kuhusu Kampuni A. 0:06:24.680,0:06:28.520 Na sasa fursa hii na[br]Kampuni B ilikuwa imepatikana. 0:06:28.520,0:06:31.920 Kwa hiyo wakati huo nilitafuta uso wa Mungu. 0:06:31.920,0:06:36.560 Na kwa neema ya Mungu, alikuwa amempa mama yangu ndoto tena. 0:06:36.560,0:06:40.680 Alikuwa ameniona katika ndoto yake[br]nikisaini mikataba miwili. 0:06:40.680,0:06:44.200 Kwa hiyo kulikuwa na karatasi ndogo na kisha kulikuwa na karatasi kubwa zaidi. 0:06:44.200,0:06:52.440 Karatasi ndogo iliwakilisha ofa ya kazi niliyokuwa nimepata kwanza, ambayo aliniona nikitia sahihi. 0:06:52.440,0:06:55.960 Baada ya kuzinduka kutoka kwenye ndoto hiyo, alinitia moyo, 0:06:55.960,0:06:58.600 'Utapata kazi hii na Kampuni B - ifanyie kazi. 0:06:58.600,0:07:06.360 Lakini baadaye, utajiunga na Kampuni A - kampuni ile ile niliyokuambia juu yake hapo awali.' 0:07:06.360,0:07:10.320 Kwa hiyo, kwa neema ya Mungu, nilianza[br]kufanya kazi katika Kampuni B 0:07:10.320,0:07:16.080 lakini bado nilikuwa nikitafuta mwongozo na uwazi kwa Kampuni A, kujua wakati wa Mungu ndio bora zaidi. 0:07:16.080,0:07:22.320 Kwa hivyo, mapema mwaka huu, kulikuwa na fursa ambayo ilikuja na Kampuni A 0:07:22.320,0:07:26.200 chini ya nafasi hiyo hiyo ya mkufunzi wa wahitimu, na nilisitasita kidogo 0:07:26.200,0:07:31.280 kwa sababu ya ndoto hizo hizo na sikutaka kumwasi Mungu kwa njia yoyote ile. 0:07:31.280,0:07:40.240 Kwa hiyo mnamo Februari 2024, Ndugu Chris alikuwa na Huduma ya Maombi ya Pamoja. 0:07:40.240,0:07:44.040 Kufikia wakati huo, nilikuwa nikiitazama kwenye[br]YouTube na nilisali naye. 0:07:44.040,0:07:46.920 Na kwa usadikisho uliokuja[br]moyoni mwangu wakati wa sala, 0:07:46.920,0:07:52.440 Niliamua kuweka ombi[br]la kazi katika Kampuni A. 0:07:52.440,0:07:57.240 Maombi yalifunguliwa Januari,[br]lakini nilipata fursa tu 0:07:57.240,0:08:00.880 kufanya mtihani wa kupima uwezo(aptitude test) mwezi Mei. 0:08:00.880,0:08:07.880 Kufikia wakati huo, watu wengi pia walikuwa wametuma maombi, wakijaribu kupata fursa hiyo pia. 0:08:07.880,0:08:12.840 Lakini kwa neema ya Mungu, katika mwezi wa[br]Agosti 2024, nilipokea simu 0:08:12.840,0:08:15.920 kusema nihudhurie mahojiano. 0:08:15.920,0:08:22.720 Kufikia wakati huo, nilikuwa nimeomba. Na kati ya mwezi wa Februari na Agosti, 0:08:22.720,0:08:31.040 Nilikuwa bado nikiomba pamoja na Ndugu Chris kuhusu usadikisho wangu na fursa hii. 0:08:31.040,0:08:37.640 Na kwa usadikisho huo, nilisikia sauti ya Mungu moyoni mwangu - ni vizuri! 0:08:37.640,0:08:41.840 Nilijua nilihitaji tu kuendelea kumtegemea, kujua wakati wa Mungu ndio bora zaidi. 0:08:41.840,0:08:46.640 Kwa hiyo Agosti ilikuja na nilikuwa[br]nimehudhuria mahojiano hayo. 0:08:46.640,0:08:51.120 Ninahitaji kuelezea kuwa[br]haikuwa wakati rahisi 0:08:51.120,0:08:54.080 kwa sababu wakati huo, nilikuwa nikivunjika moyo pia. 0:08:54.080,0:08:58.680 Watu walikuwa wakisema, 'Hapana, kampuni hii ni ngumu sana kuingia. 0:08:58.680,0:09:00.400 Labda unahitaji kujuana na mtu 0:09:00.400,0:09:03.760 ili upate fursa hapo ya kupata kazi hiyo.' 0:09:03.760,0:09:06.360 Na watu pia walikuwa wakitoa malalamiko. 0:09:06.360,0:09:08.720 Lakini kwa ujumbe kutoka kwa Ndugu Chris, 0:09:08.720,0:09:14.200 Nilitiwa moyo kuendelea kudumisha imani yangu[br]na kumtumaini Mungu, nikijua hilo 0:09:14.200,0:09:19.800 Alikuwa ametoa ndoto na mwongozo kwamba[br]ningeenda kwenye kampuni hii, 0:09:19.800,0:09:22.080 na kwamba kwa wakati Wake mwenyewe, ningeenda huko. 0:09:22.080,0:09:26.840 Kwa hiyo, ingawa nyakati za kuvunjika moyo zilikuwa zimefika, Neno la Mungu lilikuwa likinitia moyo 0:09:26.840,0:09:30.960 na pia jumbe na Huduma shirikishi za Maombi pamoja na Ndugu Chris. 0:09:30.960,0:09:33.800 Zilikuwa zikinitia moyo sana[br]kwa kila namna. 0:09:33.800,0:09:38.760 Kwa hivyo baada ya mahojiano mnamo Agosti,[br]nilisubiri hadi Oktoba 0:09:38.760,0:09:44.400 na kwa neema ya Mungu, nilipokea simu kwamba nimepata ofa ya kazi katika Kampuni A, 0:09:44.400,0:09:46.800 kampuni ambayo ninafanya kazi kwa sasa. 0:09:46.800,0:09:50.120 Na unaionaje[br]kazi hapo kwenye jukumu hilo jipya? 0:09:50.120,0:09:54.120 Inasisimua kabisa.[br]Ninafurahia sana kazi hiyo. 0:09:54.120,0:09:56.880 Kwa sababu ni kitu ambacho[br]siku zote nilitaka kufanya. 0:09:56.880,0:10:00.920 Kwa neema ya Mungu nikifaulu vizuri[br]kupandishwa cheo (promotion) kupo mezani. 0:10:00.920,0:10:03.760 Neno langu la ushauri naloweza kumpa mtu yeyote, 0:10:03.760,0:10:09.120 awe kijana au mtu yeyote ambaye bado yuko shuleni na labda anatazamia kupata kazi, 0:10:09.120,0:10:12.000 ni kwamba tunapaswa daima kumtafuta Mungu kwanza. 0:10:12.000,0:10:14.360 Tunapaswa kuanza naye[br]na kumaliza naye. 0:10:14.360,0:10:17.800 Yeye ndiye Mwanzilishi na Mkamilishaji wa imani yetu. 0:10:17.800,0:10:21.400 Naye yuko pale akitutunza[br]katika kila eneo. 0:10:21.400,0:10:24.280 Tunaanza maisha yetu naye na tunapaswa kuhitimisha maisha yetu pamoja Naye. 0:10:24.280,0:10:29.280 Wakati huo, hatupaswi kukatishwa tamaa, haswa na sauti zilizo nje. 0:10:29.280,0:10:32.880 Na pia tunapaswa kuweka mioyo yetu[br]sambamba na Neno la Mungu. 0:10:32.880,0:10:41.480 Kama vile inavyosema katika Kitabu cha Yeremia 29:11 kuhusu mipango yake ya ajabu kwa ajili yetu. 0:10:41.480,0:10:44.200 kutufanikisha, tufanikiwe,[br]na sio kutuangamiza. 0:10:44.200,0:10:47.840 Kwa njia hiyo hiyo, tunapaswa pia kuweka mioyo yetu sambamba na Neno hilo, 0:10:47.840,0:10:52.040 na pia kwa maneno mengi ya hekima yaliyomo katika Biblia, 0:10:52.040,0:10:57.840 ili tusipoteze mwelekeo wetu na kuchukuliwa na matamanio ya muda mfupi - 0:10:57.840,0:11:00.360 'Hapana, nahitaji pesa tu, hiki na kile...' 0:11:00.360,0:11:04.880 Kwa sababu zaidi ya yote, tunapaswa kutafuta kumtukuza Mungu katika kila jambo tunalofanya, 0:11:04.880,0:11:08.960 ikiwa ni pamoja na kazi au kazi[br]ambazo tunaomba au kuingia. 0:11:08.960,0:11:13.480 Hivyo nakushauri usikate tamaa, endelea kutuma maombi lakini umtumaini Mungu kwa kila jambo. 0:11:13.480,0:11:16.080 badala ya kuingia katika uasi.