Hebu tufanye maswali ya kukokotoa milinganyo. Tuchukulie tuna mlinganyo huu, 1/3 jumlisha A ni sawa na 5/3. Je, thamani ya A ni ngapi kwenye mlinganyo? Kama nina 1/3 jumlisha A, je A inatakiwa kuwa ngapi ili tukiijumlisha kwa 1/3 iwe sawa na 5/3? Kuna njia nyingi za kufanya hii, na hiki ni kitu cha kufurahisha kuhusu mlinganyo na hakuna njia moja ya kukokotoa. Hivyo ngoja nifikirie, njia nyepesi ya kutumia. Na kabla sijafanya chochote, unaweza kusubirisha video, na ufanye mwenyewe. Hivyo nachotakiwa ni kuwa na A upande mmoja wa mlinganyo. Kwa kuwa A ipo tayari upande wa kushoto, tuone kama nitaweza kuendelea kuiweka upande wa kushoto, hivyo naiondoa 1/3. Vizuri, njia rahisi ya kuiondoa hii 1/3 ni kutoa 1/3 kutoka upande wa kushoto wa mlinganyo. Siwezi kutoa upande wa kushoto wa mlinganyo peke yake. Kama 1/3 jumlisha A ni sawa na 5/3, na kama nikitoa 1/3 kutoka upande wa kushoto tu, hivyo haiwezi kuwa sawa. Hivyo upande huu utakuwa pungufu ya 1/3, endapo upande huu hautobadilika. Hivyo basi upande wa kushoto utakuwa pungufu ya 5/3. Kwa hiyo ili kupata usawa, nitakachokifanya upande wa kushoto nitakifanya upande wa kulia pia. Hivyo nitatoa 1/3 pande zote. Na kama nikifanya hivyo, upande wa kushoto, 1/3 toa 1/3, ndiyo maana nimetoa 1/3 ili kuondoa 1/3, na nimebakiwa na A ni sawa na 5/3 toa 1/3, 5/3 toa 1/3, toa 1/3 , tutapata ngapi? Nina tano ya kitu hapa, kwenye hili swali nina 5/3, ninatoa kwa 1/3. Hivyo nitabakiwa na 4/3. Hivyo nitaandika A ni sawa na 4/3. Unaweza kuhakikisha kama ni sahihi. 1/3 jumlisha 4/3 ni sawa na 5/3. Hebu tufanye mfano mwingine. Tuchukulie tuna mlinganyo huu, K toa nane ni sawa na 11.8. Kwa mara nyingine, natafuta thamani ya K. Nina K upande wa kushoto. Sihitaji kuwa na hii, toa nane hapa. Hivyo ili kuondoa hii nane, hivyo tuongeze nane upande wa kushoto. Hivyo, kama nafanya hivi upande wa kushoto, nitafanya hivyohivyo upande wa kulia. Hivyo tunaongeza nane pande zote. Upande wa kushoto, unatoa nane na pia unajumlisha nane. Hii inaisha, na unabakiwa na K. Na upande wa kulia, 11.8 jumlisha nane. Vizuri, 11 jumlisha nane ni 19, itakuwa 19.8. Na tumemaliza, Unaweza kuhakikisha kama umepata jibu sahihi. 19.8 toa nane ni 11.8. Hebu tufanye nyingine, hii inavutia. Sawa, tuchukulie nina 5/13 ni sawa na T toa 6/13. Vizuri, hii inavutia kwa sababu sasa nina mtajo upande wa kulia. Hivyo naiacha hapa. Tuone kama tunaweza kutafuta thamani ya T kwa kuondoa namba yoyote upande wa kulia. Na kama tulivyofanya awali, kama natoa 6/13, kwa nini nisiijumlishe? Kwa nini nisijumlishe 6/13? Siwezi kufanya hivyo upande wa kushoto. Hizi pande mbili hazitakuwa sawa, nitafanya hivyo upande wa kulia kama ninataka kupata usawa. Hivyo nini kitatokea? Nini kitatokea? Upande wa kushoto nina ngoja niache nafasi kidogo, nina 5/13 jumlisha 6/13, jumlisha 6/13 ni sawa na , ni sawa na Nilitoa 6/13, sasa najumlisha 6/13. Hizi zitatupatia sifuri. 6/13 toa 6/13 inabaki sifuri, hivyo umebakiwa na T. Hivyo T ni sawa na hii. Kama nina 5/13 na najumlisha na hii 6/13, Nitapata 11/13. Hivyo hii itakuwa 11/13 ni sawa na T, au naweza kuiandika kwa njia nyingine. Naandika T ni sawa na 11/13.