Logo hii inakufanania nini?
Pengine haiwezi ashiria mengi kwa mtazamo wa kwanza
lakini ilizua vurugu mtandaoni.
Logo hii ilipatikana pembeni mwa lori ya kupimia UVIKO-19.
Picha na pia logo ni halisi.
mchango uliotamba Facebook unadai kuwa logo hii inaashiria Anubis,
mojawapo ya miungu ya Misri wa mauti na kuzimu.
Uvumi ulisambaa katika makundi yanayohusishwa na QAnon,
ambayo ilikuwa kikundi asi cha dhana ya majungu na sasa imejipenyeza katika dhana kuu.
Wanachama wa QAnon walisema kuwa logo hiyo ilifunua njama ya vingungwe wa dola dhidi ya Wamarekani.
Walielezea hofu kuwa lori hizi za kupimia chanjo zina nia mbaya.
Ilidhihirika kuwa logo hiyo ni ya Advaki.
Advaki?
Ndio. Advaki, ambaye niligundua kuwa,
ni mnyama wa kiafrika anayependa kutokea usiku na hula mende.
Sarah Spencer, mwanahabari wa mtandao wa factchecker.org ,
alitafiti kwa kina kung'amua chanzo cha logo hiyo
na jinsi ilivyohushishwa na miungu ya mauti ya Misri.
Mwanzoni, kikaragosi hiki kiliwasilishwa kwetu mtandaoni Facebook.
Kwa nini kituo cha kupimia UVIKO-19 una logo ya Anubis, mungu wa mauti?
Hatua ya kwanza itakuwa ya kutafiti picha kinyume.
inaweza kupa chanzo
na ikupe hisia ya jiinsi kitu hiki kimeenea.
Unaweza ona dhahiri ambapo anayeweka hiki kikaragosi anaashiria,
kuainisha kwa rangi nyekundu, kuonyesha kile wanachodhani ni cha kusisimua kulihusu.
Hiyo itapotosha utafiti wa picha
lakini pia unaweza bonyeza na kuyeyusha,
na kuiweka katika programu yoyote ya uhariri wa picha
katika picha kama hii, Ningeikata hivyo,
ili upate sehemu hiyo halisi ya picha.
halafu unaweza ziba hiyo picha
ndani ya utafiti wako wa kiwangogezi cha picha.
hapa TinEye, unaweza kuchagua aina yako ulioikata.
Kwa TinEye, tofauti na Google,
Unaweza ainisha kuanzia mpya hadi zee.
kwa muktadha huu, ilitumika katika jarida la biashara la Philadelphia-
habari kuhusu biashara ya eneo hili iliyoanza kuunda upya lori zao
ili kutumiwa kama vitengo vya kupimia vya kusongasonga wakati wa UVIKO-19
Wakatambua jina la kampuni kama Aardvark Mobile.
Kwa hivyo kutafiti rahisi mtandaoni,
matokeo dhahiri ni tovuti ya kampuni ya ziara ya Aardvark Mobile
iliyo na logo sawa na unayoiona kwenye lori.
Wapo na kitengo cha huduma ya afya ya kusonga.
Hiyo inafanana sana.
Ni mipangilio pacha
Kitu ambacho TinEye ipo hodari ni kutafuta
pale ambapo picha zilichipuka kwanza mtandaoni.
rudio la kwanza ilionekana kwa 8KUN,
ambayo ni bodi za ujumbe za dhana za majungu
Ni mahali ambapo dhana za majungu huendelezwa na kudhihirika
kabla hazijachipuka katika mitandao ya Facebook na Twitter.
Kwa hivyo dokezo lako kwa msomi wa kawaida-
wakiona picha ambazo zina madai sawa na hizi,
Ni nini wanafaa kudhania?
Ni nini wanafaa kufikiria?
Unapopitia katika mitandao ya kijamii, uone jambo
linalokuzungumzia na linaonekana sawa.
na unafikiri, ndio hiyo, inadhihirisha ninachokidhani.
Hiyo inafaa kuwa onyo kwako kuwa inaweza kuwa na shaka.
Mara si haba utapata kuwa mambo yanayojumuishwa kwa vikaragosi mtandaoni
ambazo zinaonekana kuwa sahihi, ni za uwongo.
Ulimwengu unaogopa sasa hivi
na kesho ipo katika sintofahamu.
Kusoma kitu mtandaoni na kudhania mabaya mno,
inaonekana kuwa na mantiki.
Lakini kama vile Sarah alivyosema, inapoonekana kuwa sawa,
itakubidi kuchunguza kwanza.
Na kama kitu kinahitaji maelezo ya kina,
pengine kuna jibu rahisi.
Mara nyingine, logo ni logo tu.
Mara nyingine Advaki ni advaki tu.
Na kwa nini kampuni hii kupewa jina la Advaki?
Mmiliki wa Aardvark Tours alichagua jina Aardvark
kwa sababu inatangulizwa na AA
na mbeleni kulikokuwa na mfumo wa yellow pages katika orodha za nambari za simu.
Hakika tulikuwa na AA carpet cleaning, AAA carpet cleaning.
Na aardvark ipo na A mbili mwanzoni.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Hadi wakati mwingine.
Usisambaze habari za uwongo. Dumisha ukweli.
Mimi ni Hari Sreenivasan na hii ni Take on Fake.
Asante kwa kutizama.
Unahitaji vidokezo na ujanja za kuweza kuwa mchunguzi bora wa ukweli?
Jiunge na idhaa yetu na utujuze unachokifikiria kwa michango hapa chini.