Asimilia tisaini ya ubongo wa mtoto hukua kabla afike umri wa miaka mitano. Afikapo miaka mitatu, uunganisho wa ubongo wake huwa umefikia kiwango cha kwadrilioni. Kwa sababu ya uharaka huo, wakati huu unaonekana kuwa bora zaidi wa kukuza ujuzi wa watoto utakaowasaidia katika usomaji wa vitabu.