Asimilia tisaini ya ubongo wa mtoto
hukua kabla afike umri wa miaka mitano.
Afikapo miaka mitatu,
uunganisho wa ubongo wake
huwa umefikia kiwango
cha kwadrilioni tatu.
Kwa sababu ya uharaka huo,
wakati huu unaonekana
kuwa bora zaidi wa
kukuza ujuzi wa watoto
utakaowasaidia katika usomaji wa vitabu.
Walezi wanaeza wasaidia watoto
kwa kutumia hizi mbinu tano
zilizobuniwa na wataalamu
wa masomo ya watoto.
Ya kwanza, kusoma.
Akademia ya Madaktari ya Watoto
inashauri kuwa watoto wasomewe
vitabu kwa dakika ishirini kila siku.
Ya pili, kuimba.
Sababu nyimbo huleta hisia za furaha,
inashauriwa watoto waimbiwe
sababu itawasaidia kujifunza
kutamka maneno tofauti.
Ya tatu, kuongea.
Mazungumzo na watoto
ukizingatia ishara pia
huwasaidia kujifunza
kuongea na kujieleza.
Ya nne, kucheza.
Kucheza na watoto hukuza ubunifu
na kufikiria kwa watoto.
Ya tano, kuandika.
Kuandika hukuza uwezo
wa kushika na kushikilia vitu tofauti
kama vile vyombo vya jikoni.
Tafuta wakati katika siku na ujaribu
kutumia mbinu hizi tano na wanao
kama vile wakati wa kulala,
kuoga, kuvaa nguo na kadhalika.
Dakika kadhaa kila siku
zitawasaidia wanao kuwa tayari kusoma.
Tembelea Herrick.dl/EarlyLiteracy
kwa maelezo zaidi ya mbinu hizi tano.