Asimilia tisaini ya ubongo wa mtoto hukua kabla afike umri wa miaka mitano. Afikapo miaka mitatu, uunganisho wa ubongo wake huwa umefikia kiwango cha kwadrilioni tatu. Kwa sababu ya uharaka huo, wakati huu unaonekana kuwa bora zaidi wa kukuza ujuzi wa watoto utakaowasaidia katika usomaji wa vitabu. Walezi wanaeza wasaidia watoto kwa kutumia hizi mbinu tano zilizobuniwa na wataalamu wa masomo ya watoto. Ya kwanza, kusoma. Akademia ya Madaktari ya Watoto inashauri kuwa watoto wasomewe vitabu kwa dakika ishirini kila siku. Ya pili, kuimba. Sababu nyimbo huleta hisia za furaha, inashauriwa watoto waimbiwe sababu itawasaidia kujifunza kutamka maneno tofauti. Ya tatu, kuongea. Mazungumzo na watoto ukizingatia ishara pia huwasaidia kujifunza kuongea na kujieleza. Ya nne, kucheza. Kucheza na watoto hukuza ubunifu na kufikiria kwa watoto. Ya tano, kuandika. Kuandika hukuza uwezo wa kushika na kushikilia vitu tofauti kama vile vyombo vya jikoni. Tafuta wakati katika siku na ujaribu kutumia mbinu hizi tano na wanao kama vile wakati wa kulala, kuoga, kuvaa nguo na kadhalika. Dakika kadhaa kila siku zitawasaidia wanao kuwa tayari kusoma. Tembelea Herrick.dl/EarlyLiteracy kwa maelezo zaidi ya mbinu hizi tano.