1 00:00:00,000 --> 00:00:07,040 Nilitarajia. Nilijiambia, 'Kisa hiki kimekaidi maarifa ya matibabu 2 00:00:07,040 --> 00:00:11,200 na hakitapinga uwezo wa Mungu.' 3 00:00:17,920 --> 00:00:25,480 Ikiwa bado kuna maumivu katika sehemu yoyote ya mwili wako, weka mkono wako hapo. 4 00:00:25,480 --> 00:00:33,680 Popote pale maumivu hayo yalipo, katika jina la Yesu Kristo, 5 00:00:33,680 --> 00:00:37,440 upako wa Roho Mtakatifu uko hapa kuponya. 6 00:00:37,440 --> 00:00:46,600 Upone kwa jina la Yesu! 7 00:00:48,280 --> 00:00:55,200 Jina langu ni Ivan na ninaishi hapa Norway. 8 00:00:55,200 --> 00:00:58,520 Kwa asili, mimi ni natokea Uganda. 9 00:00:58,520 --> 00:01:06,680 Nilikuwa na maradhi ambayo yalinitoa kwenye nafasi yangu. 10 00:01:06,680 --> 00:01:10,400 Ilibidi hata nichukue wakati wa kupumzika kazini. 11 00:01:10,400 --> 00:01:17,280 Na ugonjwa huo ulisababisha maumivu kwenye kifua changu, 12 00:01:17,280 --> 00:01:22,760 ambapo nilipata maumivu makali. 13 00:01:22,760 --> 00:01:26,440 Sikuweza kueleza yalikuwa yanatoka wapi. 14 00:01:26,440 --> 00:01:32,600 yalikuwa makali sana kiasi kwamba sikuweza kufanya chochote. 15 00:01:32,600 --> 00:01:36,880 Karibu miaka 15 iliyopita, nilikuwa na homa ya mapafu kali (acute pneumonia), 16 00:01:36,880 --> 00:01:41,480 nikiwa bado nyumbani Uganda kabla sijahamia Norway. 17 00:01:41,480 --> 00:01:51,960 Na ugonjwa huu ulikuwa mkali sana kwamba sehemu ya ganda la kushoto la pafu langu iliharibika 18 00:01:51,960 --> 00:01:56,320 Nililazwa hospitalini kwa mwezi mmoja. 19 00:01:56,320 --> 00:01:58,760 Na hata nilipotoka hospitalini, 20 00:01:58,760 --> 00:02:05,120 Ilinibidi niwe na kipindi cha kusubiri kupona kidigo kidogo kwa takriban mwezi mmoja. Ilikuwa mbaya sana. 21 00:02:05,120 --> 00:02:10,960 Kwa hivyo nilipopata maumivu hayo, nilianza kiyahusisha na kisa hicho, 22 00:02:10,960 --> 00:02:17,240 kwamba pengine inaweza kuwa nimonia ilikuwa inajidhihirisha tena. 23 00:02:17,240 --> 00:02:20,720 Wakati maumivu yalipoendelea, niliamua ... 24 00:02:20,720 --> 00:02:25,920 Kumbuka, wakati huo nilikuwa nimeacha kufanya kazi kwa sababu sikuweza kugeuka. 25 00:02:25,920 --> 00:02:34,440 Hata lilipokuja suala la kutembea, kupiga hatua, nilihisi maumivu makali ndani. 26 00:02:34,440 --> 00:02:40,000 Hata wakati wowote nilipokuwa nimelala, nikigeuka kutoka upande mmoja hadi mwingine, 27 00:02:40,000 --> 00:02:44,040 ilikuwa shida, ilikuwa tatizo. 28 00:02:44,040 --> 00:02:48,240 Kwa hiyo niliamua kuwasiliana na daktari wangu. 29 00:02:48,240 --> 00:02:53,320 Alipokuwa akinichunguza, alijaribu kugusa eneo hilo 30 00:02:53,320 --> 00:02:57,840 kwa sababu nilimwambia kuwa maumivu yalikuwa ndani ya kifua changu. 31 00:02:57,840 --> 00:02:59,440 Yalikuwa makali sana. 32 00:02:59,440 --> 00:03:03,480 Hata sikujua jinsi ya kumweleza maumivu yangu. 33 00:03:03,480 --> 00:03:08,880 Kwa hivyo kisa hicho, nadhani, kikawa kingumu sana kwake. 34 00:03:08,880 --> 00:03:16,200 Na kisha akaamua kunielekeza kwenye hospitali kubwa zaidi kwa huduma za ushauri. 35 00:03:16,200 --> 00:03:23,320 Nikaenda na kufika pale wakanipa mapokeo ya dharura. 36 00:03:23,320 --> 00:03:27,960 Kwa hiyo nilipata timu ya madaktari na wauguzi. Walikuja na kunichunguza. 37 00:03:27,960 --> 00:03:31,280 Walinihoji na nikawaambia kila kitu. 38 00:03:31,280 --> 00:03:39,040 Na kisha wakasema wataenda kuchukua X-ray na kisha kufanya uchunguzi(scan) wa moyo wangu. 39 00:03:39,040 --> 00:03:45,600 Kwa hiyo walikuja na kunichukua ndani na kuchukua X-ray mbili za sehemu ya kifua changu. 40 00:03:45,600 --> 00:03:51,720 Walichukua sampuli za damu kutoka kwangu, kwa kweli sampuli nyingi za damu, 41 00:03:51,720 --> 00:03:54,800 kwa sababu walilazimika kufanya majaribio kadhaa. 42 00:03:54,800 --> 00:04:01,920 Kilichonishangaza ni, baada ya kuchunguza mfululizo wa majaribio hayo yote waliyofanya, 43 00:04:01,920 --> 00:04:10,480 waligundua kuwa hakuna kitu - kila kitu kiligeuka kuwa hasi. 44 00:04:10,480 --> 00:04:14,240 Jumamosi ijayo tungekuwa na 45 00:04:14,240 --> 00:04:19,240 tukio la mhadhara la 'Acha Mioyo Iamke' nchini Uingereza. 46 00:04:19,240 --> 00:04:24,440 Nilikuwa na bahati ya kupokea kiungo ili nijiunge mtandaoni, 47 00:04:24,440 --> 00:04:27,320 kwa hivyo nilikuwa nikitarajia. 48 00:04:27,320 --> 00:04:31,280 Na moyoni mwangu nilikuwa na imani. 49 00:04:31,280 --> 00:04:38,960 Nilifikiria, kama kisa hiki kimekuwa, 50 00:04:38,960 --> 00:04:44,760 kigumu sana kwa mwanadamu kufasiri, nitakileta mbele za Mungu. 51 00:04:44,760 --> 00:04:48,160 Najua lisilowezekana kwa mwanadamu linawezekana kwa Mungu. 52 00:04:48,160 --> 00:04:52,560 Jumamosi ilifika na nikajiunga. Nilitarajia. 53 00:04:52,560 --> 00:05:02,640 Nilijua kisa hiki kimekaidi maarifa ya matibabu na hakitakaidi uwezo wa Mungu. 54 00:05:02,640 --> 00:05:08,760 Kwa hiyo maombi yakaanza na tukasikiliza shuhuda. 55 00:05:08,760 --> 00:05:14,960 Kisha mtu wa Mungu alipokuja, alipokuwa akiwaombea watu, 56 00:05:14,960 --> 00:05:20,360 Nilianza kuona nguvu za Mungu zikiwagusa watu. 57 00:05:20,360 --> 00:05:22,280 Watu walikuwa wakijidhihirisha. 58 00:05:22,280 --> 00:05:27,160 Kweli Mungu alikuwa anatembea kwa nguvu pale ukumbini. 59 00:05:27,160 --> 00:05:31,560 Na alipokuwa akiwaombea watu, maombi yangu yalikuwa moja tu. 60 00:05:31,560 --> 00:05:38,040 Niliendelea kusema moyoni mwangu, 'Bwana, unapowagusa wengine, usinipite. 61 00:05:38,040 --> 00:05:42,680 Unapowatembelea wengine, tafadhali Bwana, usinipite. 62 00:05:42,680 --> 00:05:50,720 niko hapa. Najua umbali sio kizuizi kwa nguvu zako. Unaweza kunigusa.' 63 00:05:50,720 --> 00:05:56,480 Lakini mnajua, watu wa Mungu, nilichogundua ni 64 00:05:56,480 --> 00:06:01,880 kwamba hata kabla ibada haijafikia hatua 65 00:06:01,880 --> 00:06:08,200 ambapo mtu wa Mungu alijitokeza kuwaombea watazamaji waliokuwa wameunganishwa mtandaoni, 66 00:06:08,200 --> 00:06:13,560 Niligundua kuwa maumivu yalikuwa yametoweka yenyewe. 67 00:06:13,560 --> 00:06:16,320 Ndugu Chris alipokuja kuwaombea watazamaji, 68 00:06:16,320 --> 00:06:21,400 na akasema kwamba watu wanapaswa kugusa sehemu hizo 69 00:06:21,400 --> 00:06:28,640 ambapo walikuwa na maumivu au usumbufu, wakati huo kulikuwa na maumivu kidogo sana 70 00:06:28,640 --> 00:06:35,160 nami nikagusa na nadhani hiyo ilitia muhuri uponyaji wote kwa ajili yangu. 71 00:06:35,160 --> 00:06:41,800 Na baada ya hapo, nilihisi vizuri. Usiku huo, nililala vizuri. 72 00:06:41,800 --> 00:06:44,720 Siku iliyofuata ningeweza kufanya mambo ambayo sikuweza kufanya. 73 00:06:44,720 --> 00:06:48,680 Ningeweza kuinama. Ningeweza kugeuka. 74 00:06:48,680 --> 00:06:53,000 Siku ya Jumatatu, nilirudi kazini na nilikuwa sawa. 75 00:06:53,000 --> 00:07:00,120 Nilirejeshwa kikamilifu. Utukufu ni kwa Mungu. Sasa niko huru kabisa! 76 00:07:00,120 --> 00:07:04,560 Kama unavyoona, sikuweza kusonga kama hii. 77 00:07:04,560 --> 00:07:07,040 Sikuweza kufanya hivi kwa sababu 78 00:07:07,040 --> 00:07:11,440 maumivu yangekuwa makali sana na kupenya hadi kifuani mwangu. 79 00:07:11,440 --> 00:07:13,800 Sikuweza kusimama. 80 00:07:13,800 --> 00:07:17,840 Sasa naweza kuruka. 81 00:07:17,840 --> 00:07:22,280 Kwa hiyo niko huru kabisa kwa utukufu wa Mungu! 82 00:07:22,280 --> 00:07:25,360 Je, ulisikia maumivu yoyote wakati wa kufanya mazoezi? 83 00:07:25,360 --> 00:07:30,200 Hapana, hata kidogo. Niko huru kwa utukufu wa Mungu. 84 00:07:30,200 --> 00:07:34,560 Tafadhali, sasa endelea na ushirikishe neno lako zuri la ushauri kwa watazamaji. 85 00:07:34,560 --> 00:07:41,560 Tunahitaji kumtegemea Mungu, na tunahitaji kutambua 86 00:07:41,560 --> 00:07:45,840 ya kwamba yasiyowezekana kwa mwanadamu yanawezekana kwa Mungu. 87 00:07:45,840 --> 00:07:51,320 Hali yoyote ambayo inaweza kukujia, usivunjike moyo. 88 00:07:51,320 --> 00:07:55,040 Jua kuwa lililo gumu kwako, 89 00:07:55,040 --> 00:08:00,040 lisilowezekana kwa mwanadamu, kwa Mungu linawezekana. 90 00:08:00,040 --> 00:08:06,960 Mungu anapendezwa nasi kumkazia macho, kumaanisha kumtumaini. 91 00:08:06,960 --> 00:08:12,520 Kwa maana Maandiko Matakatifu yasemavyo: 'Bila imani hatuwezi kumpendeza Mungu.' 92 00:08:12,520 --> 00:08:18,880 Mungu anaheshimiwa tunapomtegemea , tunapomtumaini. 93 00:08:18,880 --> 00:08:24,880 Kwa hivyo ushauri wangu ni, bila kujali hali, haijalishi mazingira, 94 00:08:24,880 --> 00:08:26,960 hakuna lisilowezekana kwa Mungu. 95 00:08:26,960 --> 00:08:30,480 Tumtegemee Mungu. Tumtumaini Yeye. 96 00:08:30,480 --> 00:08:35,600 Na tunapomtumaini Yeye, atatujia. 97 00:08:35,600 --> 00:08:41,000 Atatugusa, Atagusa hali zetu na tutafanywa kuwa wakamilifu.