Nilitarajia. Nilijiambia, 'Kisa hiki kimekaidi maarifa ya matibabu na hakitapinga uwezo wa Mungu.' Ikiwa bado kuna maumivu katika sehemu yoyote ya mwili wako, weka mkono wako hapo. Popote pale maumivu hayo yalipo, katika jina la Yesu Kristo, upako wa Roho Mtakatifu uko hapa kuponya. Upone kwa jina la Yesu! Jina langu ni Ivan na ninaishi hapa Norway. Kwa asili, mimi ni natokea Uganda. Nilikuwa na maradhi ambayo yalinitoa kwenye nafasi yangu. Ilibidi hata nichukue wakati wa kupumzika kazini. Na ugonjwa huo ulisababisha maumivu kwenye kifua changu, ambapo nilipata maumivu makali. Sikuweza kueleza yalikuwa yanatoka wapi. yalikuwa makali sana kiasi kwamba sikuweza kufanya chochote. Karibu miaka 15 iliyopita, nilikuwa na homa ya mapafu kali (acute pneumonia), nikiwa bado nyumbani Uganda kabla sijahamia Norway. Na ugonjwa huu ulikuwa mkali sana kwamba sehemu ya ganda la kushoto la pafu langu iliharibika Nililazwa hospitalini kwa mwezi mmoja. Na hata nilipotoka hospitalini, Ilinibidi niwe na kipindi cha kusubiri kupona kidigo kidogo kwa takriban mwezi mmoja. Ilikuwa mbaya sana. Kwa hivyo nilipopata maumivu hayo, nilianza kiyahusisha na kisa hicho, kwamba pengine inaweza kuwa nimonia ilikuwa inajidhihirisha tena. Wakati maumivu yalipoendelea, niliamua ... Kumbuka, wakati huo nilikuwa nimeacha kufanya kazi kwa sababu sikuweza kugeuka. Hata lilipokuja suala la kutembea, kupiga hatua, nilihisi maumivu makali ndani. Hata wakati wowote nilipokuwa nimelala, nikigeuka kutoka upande mmoja hadi mwingine, ilikuwa shida, ilikuwa tatizo. Kwa hiyo niliamua kuwasiliana na daktari wangu. Alipokuwa akinichunguza, alijaribu kugusa eneo hilo kwa sababu nilimwambia kuwa maumivu yalikuwa ndani ya kifua changu. Yalikuwa makali sana. Hata sikujua jinsi ya kumweleza maumivu yangu. Kwa hivyo kisa hicho, nadhani, kikawa kingumu sana kwake. Na kisha akaamua kunielekeza kwenye hospitali kubwa zaidi kwa huduma za ushauri. Nikaenda na kufika pale wakanipa mapokeo ya dharura. Kwa hiyo nilipata timu ya madaktari na wauguzi. Walikuja na kunichunguza. Walinihoji na nikawaambia kila kitu. Na kisha wakasema wataenda kuchukua X-ray na kisha kufanya uchunguzi(scan) wa moyo wangu. Kwa hiyo walikuja na kunichukua ndani na kuchukua X-ray mbili za sehemu ya kifua changu. Walichukua sampuli za damu kutoka kwangu, kwa kweli sampuli nyingi za damu, kwa sababu walilazimika kufanya majaribio kadhaa. Kilichonishangaza ni, baada ya kuchunguza mfululizo wa majaribio hayo yote waliyofanya, waligundua kuwa hakuna kitu - kila kitu kiligeuka kuwa hasi. Jumamosi ijayo tungekuwa na tukio la mhadhara la 'Acha Mioyo Iamke' nchini Uingereza. Nilikuwa na bahati ya kupokea kiungo ili nijiunge mtandaoni, kwa hivyo nilikuwa nikitarajia. Na moyoni mwangu nilikuwa na imani. Nilifikiria, kama kisa hiki kimekuwa, kigumu sana kwa mwanadamu kufasiri, nitakileta mbele za Mungu. Najua lisilowezekana kwa mwanadamu linawezekana kwa Mungu. Jumamosi ilifika na nikajiunga. Nilitarajia. Nilijua kisa hiki kimekaidi maarifa ya matibabu na hakitakaidi uwezo wa Mungu. Kwa hiyo maombi yakaanza na tukasikiliza shuhuda. Kisha mtu wa Mungu alipokuja, alipokuwa akiwaombea watu, Nilianza kuona nguvu za Mungu zikiwagusa watu. Watu walikuwa wakijidhihirisha. Kweli Mungu alikuwa anatembea kwa nguvu pale ukumbini. Na alipokuwa akiwaombea watu, maombi yangu yalikuwa moja tu. Niliendelea kusema moyoni mwangu, 'Bwana, unapowagusa wengine, usinipite. Unapowatembelea wengine, tafadhali Bwana, usinipite. niko hapa. Najua umbali sio kizuizi kwa nguvu zako. Unaweza kunigusa.' Lakini mnajua, watu wa Mungu, nilichogundua ni kwamba hata kabla ibada haijafikia hatua ambapo mtu wa Mungu alijitokeza kuwaombea watazamaji waliokuwa wameunganishwa mtandaoni, Niligundua kuwa maumivu yalikuwa yametoweka yenyewe. Ndugu Chris alipokuja kuwaombea watazamaji, na akasema kwamba watu wanapaswa kugusa sehemu hizo ambapo walikuwa na maumivu au usumbufu, wakati huo kulikuwa na maumivu kidogo sana nami nikagusa na nadhani hiyo ilitia muhuri uponyaji wote kwa ajili yangu. Na baada ya hapo, nilihisi vizuri. Usiku huo, nililala vizuri. Siku iliyofuata ningeweza kufanya mambo ambayo sikuweza kufanya. Ningeweza kuinama. Ningeweza kugeuka. Siku ya Jumatatu, nilirudi kazini na nilikuwa sawa. Nilirejeshwa kikamilifu. Utukufu ni kwa Mungu. Sasa niko huru kabisa! Kama unavyoona, sikuweza kusonga kama hii. Sikuweza kufanya hivi kwa sababu maumivu yangekuwa makali sana na kupenya hadi kifuani mwangu. Sikuweza kusimama. Sasa naweza kuruka. Kwa hiyo niko huru kabisa kwa utukufu wa Mungu! Je, ulisikia maumivu yoyote wakati wa kufanya mazoezi? Hapana, hata kidogo. Niko huru kwa utukufu wa Mungu. Tafadhali, sasa endelea na ushirikishe neno lako zuri la ushauri kwa watazamaji. Tunahitaji kumtegemea Mungu, na tunahitaji kutambua ya kwamba yasiyowezekana kwa mwanadamu yanawezekana kwa Mungu. Hali yoyote ambayo inaweza kukujia, usivunjike moyo. Jua kuwa lililo gumu kwako, lisilowezekana kwa mwanadamu, kwa Mungu linawezekana. Mungu anapendezwa nasi kumkazia macho, kumaanisha kumtumaini. Kwa maana Maandiko Matakatifu yasemavyo: 'Bila imani hatuwezi kumpendeza Mungu.' Mungu anaheshimiwa tunapomtegemea , tunapomtumaini. Kwa hivyo ushauri wangu ni, bila kujali hali, haijalishi mazingira, hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Tumtegemee Mungu. Tumtumaini Yeye. Na tunapomtumaini Yeye, atatujia. Atatugusa, Atagusa hali zetu na tutafanywa kuwa wakamilifu.