Hebu tuseme kwamba
tuna sehemu 9/10,
na mimi nataka kuongeza sehemu 1/6.
Hii itakuwa sawa na nini?
Hivyo wakati unaangalia hii, unaweza kusema,
"Oh, nina asili tofauti hapa.
Siyo kawaida kufanya hesabu kama hizi. "
Na njia sahihi ya kufanya hii ni
kuanza kwa kutafuta kigawe cha shirika,
kubadili sehemu zote hizi mbili kuwa
sehemu zenye asili sawa.
Hivyo ni jinsi gani unaweza kupata asili ya shirika?
Naam, asili ya shirika itakuwa ni
kigawe cha shirika cha asili 10 na 6.
Hivyo kigawe cha shirika cha 10 na 6 ni kipi?
Na ni rahisi kutafuta kigawe kidogo cha shirika,
na njia nzuri ya kufanya hii ni kuanza na
asili kubwa, 10, na ujiulize, je 10 inagawanyika kwa 6?
Hapana. Je 20 inagawanyika kwa 6?
Hapana. Je 30 inagawanyika kwa 6?
Hapa tulikuwa tunaangalia vigawe vya 10
na ni kigawe gani kidogo cha 10
ambacho kinagawanyika kwa 6? Na hiko kitakuwa ni 30.
Hivyo naweza kuziandika upya hizi sehemu
kama namba fulani juu ya 30.
Hivyo 9 juu ya 10. Nitaandika vipi hiyo
kama kitu fulani juu ya 30? Nitazidisha
asili kwa 3.
Hivyo nimezidisha asili kwa 3.
Kwa hiyo kama sihitaji kubadili thamani ya sehemu ,
ninatakiwa kufanya vivyo hivyo kwa kiasi.
Nitazidisha kiasi kwa tatu
kwa sababu nilizidisha kiasi kwa tatu
na asili kwa tatu, na hiyo haitabadili
thamani ya sehemu.
Hivyo sita mara tatu ni 27.
Na hivyo, 9/10 na 27/30
zinawakilisha kitu sawa.
Nimeandika hii ikiwa na asili 30,
na pia naweza kuandika 1/6
ikiwa na asili 30. Hebu tufanye hiyo.
Hivyo 1/6 ni nini juu ya 30?
Nakushauri usimamishe hii video
na ujaribu kufanya hiyo.
Hivyo tutafanya nini kutoka 6 mpaka 30?
Tunatakiwa kuzidisha kwa tano.
hivyo kama tukizidisha asili kwa tano,
pia tunatakiwa kuzidisha kiasi kwa tano,
hivyo moja mara tano ni tano.
Hivyo 9/10 ni sawa na 27/30,
na 1/6 ni sawa na 5/30.
Na sasa tunaweza kujumlisha
na iko wazi.
Tuna namba fulani juu ya 30,
na tunajumlisha namba fulani juu ya 30,
hivyo 27/30 + 5/30, hiyo itakuwa sawa na
27 jumlisha 5,
27 + 5,
ambayo
itakuwa sawa na 32/30.
32 juu ya 30, na
kama tukitaka, tunaweza kurahisisha hii sehemu.
Tuna kigawo cha 32 na 30,
zote zinagawanyika kwa 2.
Hivyo kama tukigawanya kiasi na asili kwa 2,
kiasi gawa kwa mbili ni 16,
asili gawa kwa 2 ni 15.
Hivyo, hii ni sawa na 16/15, na kama tukitaka
kuandika hii kama namba mchanganyiko, 15 inaingia mara moja katika 16
na baki moja.
Hivyo hii ni sawa na 1 1/15.
Hebu tufanye hesabu nyingine.
Hebu tuseme tunahitaji kujumlisha
1/2 na
11/12.
Nakushauri usimamishe video
na ujaribu kufanya hii.
Kama tulivyoona mwanzo, tunatakiwa kutafuta
kigawe cha shirika.
Kama hizi zina asili sawa,
tunaweza kuzijumlisha moja kwa moja,
lakini tunatakiwa kutafuta asili ya shirika
kwa sababu haziko sawa.
Tunachotakiwa kutafuta ni rahisi,
kigawe cha shirika cha 2 na12,
na ni vizuri kutafuta kigawe kidogo cha shirika cha 2 na 12,
na kama tulivyofanya mwanzoni, hebu tuanze na kubwa
kati ya hizi mbili, ambayo ni 12.
Na sasa tunachukua 12 mara moja ambayo ni 12,
na hivyo tunaweza kuona kuwa ni kigawe kidogo cha 12.
Na je hiyo inagawanyika kwa mbili? Ndiyo, hakika.
12 inagawanyika kwa mbili.
Hivyo 12 ni kigawe kidogo cha shirika cha mbili na 12,
tunaweza kuandika hizi sehemu mbili
kama kitu fulani juu ya 12.
Hiyo 1/2 ni nini juu ya 12?
Kutoka mbili mpaka 12, utazidisha kwa sita,
pia tutazidisha kiasi kwa sita.
Sasa tunaona 1/2, na 6/12, hizi ni kitu sawa.
Moja ni nusu ya mbili, sita ni nusu ya 12.
Na tutaandikaje 11/12 kama kitu fulani juu ya 12?
Hii tayari imekwisha andikwa juu ya 12,
11/12 tayari ina 12 kama asili,
hivyo hatuna sababu ya kubadili hiyo.
11/12, sasa tuko tayari kujumlisha.
Hivyo hii itakuwa sawa na sita,
hii itakuwa sawa na sita jumlisha 11,
sita jumlisha 11 juu ya 12.
Tuna 6/12 jumlisha 11/12,
itakuwa sita jumlisha 11 juu ya 12,
ambayo itakuwa sawa, na sita jumlisha 11 ni 17/12.
Kama tukitaka kuandika hii kama namba mchanganyiko,
12 inaingia mara moja katika 17
na baki tano, hivyo ni 1 5/12.
Hebu tufanye nyingine kama hii.
Hii ni tofauti kidogo.
Hebu tuseme tunataka kujumlisha,
3/4 na,
1/5.
Na moja juu ya tano.
Hii itakuwa sawa na nini?
Na kwa mara nyingine tena, simamisha hii video na
ujaribu kufanya mwenyewe.
Tuna asili tofauti,
na tunataka kuandika hizi
zikiwa na asili sawa,
hivyo tunatakiwa kutafuta kigawe cha shirika,
ni vizuri kiwe kigawe kidogo cha shirika.
Je, kipi ni kigawe kidogo cha shirika cha nne na tano?
Hebu tuanze na namba kubwa,
na tuangalie vigawe vyake
mpaka tutakapopata kigawe kitakacho gawanyika kwa nne.
Hivyo tano haigawanyiki kwa nne.
10 haigawanyiki kwa nne, bila kubaki
ndio kitu tunachoangalia zaidi.
15 haigawanyiki kwa nne bila kubaki.
20 inagawanyika kwa nne, hiyo ni sawa na tano mara nne.
Kigawe ni 20. Hivyo tunachotakiwa kufanya ni kuandika
sehemu zote mbili zikiwa na asili 20,
au 20 kama asili.
Hivyo tunaweza kuandika 3/4 kama kitu fulani juu ya 20.
Hivyo kutoka nne mpaka 20 katika asili,
tunazidisha kwa tano.
Pia tutazidisha katika kiasi .
Tunazidisha tatu mara tano kupata 15.
Tulichofanya ili kupata 20 ni kuzidisha kwa tano.
Pia tunatakiwa kufanya sawa kwa kiasi,
tatu mara tano ni 15.
3/4 ni sawa na 15/20.
1/5. Itakuwa sawa na nini juu ya 20?
Hivyo kutoka tano mpaka 20, unatakiwa kuzidisha kwa nne.
Pia tunatakiwa kufanya sawa na kwa kiasi.
Tunatakiwa kuzidisha kiasi kwa nne ili kupata 4/20.
Hivyo nimeandika hii badala ya 3/4 jumlisha 1/5,
sasa tumeandika 15/20 jumlisha 4/20.
Na hiyo itakuwa sawa na nini?
Hiyo itakuwa sawa na 15 jumlisha nne ambayo ni 19/20.
19/20, na tumemaliza.