1 00:00:00,000 --> 00:00:07,300 [muziki] 2 00:00:08,000 --> 00:00:12,000 Je! unajua kuwa wewe ni kazi ya sanaa? 3 00:00:12,000 --> 00:00:14,035 Mwanadamu ndiye zao kuu la Mungu. 4 00:00:14,035 --> 00:00:20,000 Ninamaanisha, mtu aliyeumbwa kufikiria, kuzungumza na kutenda pamoja na Mungu. 5 00:00:20,000 --> 00:00:22,000 Je, unaishi sambamba na Mungu? 6 00:00:22,000 --> 00:00:25,000 Je, hali yako ikoje mbele za Mungu leo? 7 00:00:25,000 --> 00:00:28,210 Bila neema ya Roho Mtakatifu inayokaa ndani yake, 8 00:00:28,210 --> 00:00:33,000 mwanadamu ni kivuli tu cha yule aliyeumbwa na Mungu! 9 00:00:33,000 --> 00:00:34,860 Mwanadamu ambaye Mungu alimuumba 10 00:00:34,860 --> 00:00:37,346 hakuwa mtu wa kimwili tu 11 00:00:37,346 --> 00:00:39,940 anayetawaliwa na hisi zake 12 00:00:39,940 --> 00:00:45,000 bali ni mjumbe kati ya ulimwengu unaoonekana na usioonekana. 13 00:00:45,000 --> 00:00:50,000 Mungu na mwanadamu walikuwa wakizungumza pamoja kama marafiki. 14 00:00:50,000 --> 00:00:55,660 Lakini siku moja, mwanadamu alivunja uhusiano kwa kutokutii 15 00:00:55,660 --> 00:00:59,960 na akaenda mbali na Mungu. Kisha akaenda mbali zaidi, 16 00:00:59,960 --> 00:01:03,280 hadi mwishowe akaondoka nyumbani. 17 00:01:03,280 --> 00:01:06,740 Aliiacha nchi yake ya asili, Edeni, ambako aliishi na Mungu. 18 00:01:06,740 --> 00:01:12,000 Alihama kutoka kwenye uwepo wa Mungu. 19 00:01:12,000 --> 00:01:15,770 Tangu wakati huo, Mungu amekuwa na shauku ya kuweza kuzungumza tena 20 00:01:15,770 --> 00:01:18,810 na rafiki yake wa zamani 21 00:01:18,810 --> 00:01:20,100 lakini mwanadamu, 22 00:01:20,100 --> 00:01:22,620 kwa kuondoka katika uwepo wa Muumba wake, 23 00:01:22,620 --> 00:01:25,000 alipoteza lugha yake mama. 24 00:01:25,000 --> 00:01:29,000 Namaanisha, alipoteza lugha yake ya asili na Mungu. 25 00:01:29,000 --> 00:01:34,000 Na akawa hawezi kuwasiliana na Muumba wake katika roho na kweli. 26 00:01:34,000 --> 00:01:38,230 Mwanadamu wa kawaida hawezi kusikia au kuzungumza na Mungu; 27 00:01:38,230 --> 00:01:42,780 hii ndiyo changamoto tunayokabiliana nayo leo. 28 00:01:42,780 --> 00:01:45,990 Ingawa Mungu huzungumza tena na tena, 29 00:01:45,990 --> 00:01:49,000 wengi sana hawapo makini kusikia kile Anachosema (Ayubu 33:14). 30 00:01:49,000 --> 00:01:52,000 Ukimya ni mgumu kwa Mungu. 31 00:01:52,000 --> 00:01:55,700 Kama vile baba wa mwana mpotevu 32 00:01:55,700 --> 00:01:58,480 alivyokuwa na shauku ya kumwona mwanawe akirudi nyumbani, 33 00:01:58,480 --> 00:02:02,400 Mungu ana shauku ya kuwa na uhusiano wa karibu tena na mwanadamu, 34 00:02:02,400 --> 00:02:04,420 Rafiki yake wa zamani. 35 00:02:04,420 --> 00:02:06,820 Ndiyo maana ilimbidi achague lugha 36 00:02:06,820 --> 00:02:08,520 ambayo mwanadamu angeelewa. 37 00:02:08,520 --> 00:02:13,230 Kwa hivyo alimtuma Mwanawe, Yesu Kristo duniani kumrudisha mwanadamu, 38 00:02:13,230 --> 00:02:18,000 Rafiki Yake wa zamani, arudi Kwake tena. 39 00:02:18,000 --> 00:02:22,270 Mungu aliheshimu lugha ya mwanadamu kwa kumwita Yesu Neno. 40 00:02:22,270 --> 00:02:25,850 Neno alifanyika mwili na akaingia ulimwenguni. 41 00:02:25,850 --> 00:02:29,270 Yesu ni Mungu akijieleza Mwenyewe 42 00:02:29,270 --> 00:02:33,070 kwa lugha ambayo mwanadamu anaweza kuelewa, 43 00:02:33,070 --> 00:02:36,000 lugha ya roho na uzima (Yohana 6:63). 44 00:02:36,000 --> 00:02:38,540 Je, ni kwa muda gani tutaendelea kuwaza, 45 00:02:38,540 --> 00:02:41,380 kuzungumza na kuishi katika hali ya kimwili 46 00:02:41,380 --> 00:02:45,465 ilihali Yesu anakungoja katika mahala pa Roho Wake? 47 00:02:45,465 --> 00:02:48,335 Ni wasaa wa kurudi tena katika chuo cha Mungu 48 00:02:48,335 --> 00:02:51,545 Na kuanza kumtafuta Roho. 49 00:02:51,545 --> 00:02:55,650 Kutoka kwenye miaka mingi ya kujifunza chini ya, na kutembea 50 00:02:55,650 --> 00:02:58,540 pamoja na Jenerali wa Mungu, Nabii TB Joshua, 51 00:02:58,540 --> 00:03:01,090 hadi alipoitwa Nyumbani Mbinguni, 52 00:03:01,090 --> 00:03:06,887 shauku imewaka mioyoni mwetu kutoa hazina tuliyopewa na Mungu; 53 00:03:06,887 --> 00:03:10,360 Neno lililo hai katika nguvu za Roho Mtakatifu! 54 00:03:10,360 --> 00:03:12,310 Maandishi ya Neno hayawezi kusonga, 55 00:03:12,310 --> 00:03:14,880 hayawezi kufanya kazi bila uhai wa Mungu (Yohana 6:63). 56 00:03:14,880 --> 00:03:18,210 Kila Neno la Mungu ni Roho na uzima. 57 00:03:18,210 --> 00:03:20,130 Na ni uzima halisi wa Mungu 58 00:03:20,130 --> 00:03:24,000 katika Neno hilo unaotia nguvu, nishati katika Neno. 59 00:03:24,000 --> 00:03:27,110 Hili ndilo Neno linaloponya, kuokoa, kukomboa 60 00:03:27,110 --> 00:03:30,000 na kumwezesha mwamini kuishi maisha ya ushindi katika Kristo. 61 00:03:30,000 --> 00:03:34,600 Kama vile Simoni Petro katika Yohana 6:68, 62 00:03:34,600 --> 00:03:38,260 tumegundua kwamba hakuna mbadala wa Yesu 63 00:03:38,260 --> 00:03:42,000 kwa sababu Yeye peke yake ndiye mwenye Maneno ya uzima wa milele. 64 00:03:42,000 --> 00:03:46,900 Baada ya mshauri wetu kuitwa Nyumbani tarehe 5 Juni 2021, 65 00:03:46,900 --> 00:03:51,000 kama wanafunzi wa zamani, Yesu alipopaa Mbinguni, 66 00:03:51,000 --> 00:03:54,802 tumekuwa tukingoja katika imani. 67 00:03:54,802 --> 00:03:59,920 Na katika tarehe 8 ya Desemba 2021, nilipokea ufunuo toka kwa Mungu. 68 00:03:59,920 --> 00:04:05,050 Na nikapewa jina la 'Chuo Kikuu Cha Mungu'. 69 00:04:05,105 --> 00:04:15,550 [muziki] 70 00:04:15,550 --> 00:04:19,560 Nilijikuata katika chumba cha glasi ndani ya pango 71 00:04:19,560 --> 00:04:23,000 lisilokuwa na sehemu ya kutokea 72 00:04:23,000 --> 00:04:28,000 Ghafla mwamba wenye nguvu ukaja kutoka Mbinguni 73 00:04:28,000 --> 00:04:31,000 na kugonga mlima wa mawe. 74 00:04:31,000 --> 00:04:33,000 ulitoboa lile pango. 75 00:04:33,000 --> 00:04:38,000 Mlima ulitikisika, lakini nilibaki thabiti ndani ya chumba cha kioo. 76 00:04:38,000 --> 00:04:48,000 Jiwe lilitoboa kwenye mlima wa mawe. 77 00:04:48,000 --> 00:04:52,000 Niliangalia. 78 00:04:52,000 --> 00:04:54,000 Kisha nikatoka na kutembea. 79 00:04:54,000 --> 00:04:58,000 Nilisimama na kushtuka pale nilipoona 80 00:04:58,000 --> 00:05:06,000 mwamba ulikuwa umechimba handaki zuri kabisa iliyotengenezwa kwa dhahabu! 81 00:05:06,000 --> 00:05:12,000 Nilijiambia, lazima kuwe na maji mwishoni mwa handaki hili. 82 00:05:12,000 --> 00:05:14,000 Nilianza kutembea. 83 00:05:14,000 --> 00:05:18,000 Ghafla sauti ikasikika kutoka juu: 84 00:05:18,000 --> 00:05:25,000 “Baki hapo ulipo. Usiingie! Maji yanakujia.” 85 00:05:25,000 --> 00:05:29,000 Nilisimama na kubaki pale nilipokuwa. 86 00:05:29,000 --> 00:05:33,290 Niliposimama tuli, ghafla niliona maji 87 00:05:33,290 --> 00:05:36,000 yakitiririka kutoka mwishoni mwa handaki kuelekea kwangu. 88 00:05:36,000 --> 00:05:40,000 Maji yalikuwa safi, yakimeta kwa uhai. 89 00:05:40,000 --> 00:05:43,000 Yalitiririka karibu zaidi 90 00:05:43,000 --> 00:05:45,000 mpaka yakafika kwenye vidole vyangu 91 00:05:45,000 --> 00:05:53,000 na kunawisha miguu yangu kama wimbi kwenye ufuo wa bahari. 92 00:05:53,000 --> 00:05:55,600 Nilipokuwa nikitafakari juu ya ono hilo, 93 00:05:55,600 --> 00:06:02,583 moyo wangu ulinisukuma kwenye Kitabu cha Danieli 2:44. Nitasoma; 94 00:06:02,583 --> 00:06:07,943 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme 95 00:06:07,943 --> 00:06:13,299 ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; 96 00:06:13,299 --> 00:06:18,363 bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuzikomesha, 97 00:06:18,363 --> 00:06:22,357 nao utasimama milele na milele. 98 00:06:22,357 --> 00:06:28,557 Hii ndiyo maana ya maono ya mwamba uliochongwa kutoka mlimani, 99 00:06:28,557 --> 00:06:32,212 lakini si kwa mikono ya binadamu — mwamba uliovunja 100 00:06:32,212 --> 00:06:40,818 chuma, shaba, udongo, fedha na dhahabu vipande vipande. 101 00:06:41,090 --> 00:06:44,280 Kusudi la mwamba ni nini? 102 00:06:44,410 --> 00:06:49,230 Kama inavyosema katika kitabu cha Yeremia 1:10, nitasoma; 103 00:06:49,465 --> 00:06:56,615 angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, 104 00:06:56,787 --> 00:07:01,927 na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda. 105 00:07:03,000 --> 00:07:10,350 Kusudi la mwamba ni kuondoa kizuizi kati ya mioyo yetu na Mungu. 106 00:07:10,350 --> 00:07:16,000 Muda ambapo mtu anapokabidhi moyo wake kwa Roho Mtakatifu, pazia huondolewa. 107 00:07:16,000 --> 00:07:19,750 Neno la Mungu ni mbegu ya maisha ya kiungu 108 00:07:19,750 --> 00:07:25,000 ambayo huja ndani ya mioyo yetu na kusababisha imani kukua. 109 00:07:25,000 --> 00:07:31,000 Maono hayo ni kwa wakati ulioamriwa (Habakuki 2:3). 110 00:07:31,000 --> 00:07:33,810 Sasa, muda umewadia 111 00:07:33,810 --> 00:07:37,900 Maono ni kwa ajiri kumuunganisha mwanadamu kwa Mungu tena. 112 00:07:37,900 --> 00:07:44,000 kupitia Neno Lake, kwa Roho Wake, ili kuujenga Mwili wa Kristo. 113 00:07:44,000 --> 00:07:49,000 na kushirikiana na mtandao wa makanisa kote ulimwenguni. 114 00:07:49,000 --> 00:07:54,000 Maono haya yanaendana na wito na zawadi ya Mungu katika maisha yetu. 115 00:07:54,000 --> 00:07:59,000 Mwamba ulioanguka kutoka Mbinguni ni Neno la Ufalme 116 00:07:59,000 --> 00:08:04,050 kama Yesu alivyosema katika Mathayo 13:19. 117 00:08:04,050 --> 00:08:07,240 Maono yetu ni kusaidia kuingiza Neno katika mioyo ya watu - 118 00:08:07,240 --> 00:08:10,590 kwa sababu ni pale tu ndipo linafanya kazi kwa ufanisi. 119 00:08:10,590 --> 00:08:16,290 Kama Biblia inavyosema Katika kitabu cha 2 Wakorintho 3:3 - Wacha nikusomee; 120 00:08:17,480 --> 00:08:20,540 Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua iliyoandikwa na Kristo, 121 00:08:20,540 --> 00:08:22,490 matokeo ya kazi yetu. 122 00:08:22,490 --> 00:08:26,390 Barua hii haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai, 123 00:08:26,390 --> 00:08:31,795 si juu ya vibao vya mawe, bali juu ya vibao vya mioyo ya wanadamu. 124 00:08:32,000 --> 00:08:36,000 Katika miongo miwili iliyopita chini ya ushauri wa Nabii TB Joshua, 125 00:08:36,000 --> 00:08:40,000 mwingiliano wetu na maelfu ya waumini na viongozi wa makanisa ulimwenguni kote 126 00:08:40,000 --> 00:08:44,410 na maswali ya mara kwa mara yaliyoulizwa na wengi wakati wa mihadhara 127 00:08:44,410 --> 00:08:48,000 yamevuta mtazamo wetu kwenye upande wa vitendo wa Ukristo, 128 00:08:48,000 --> 00:08:52,670 Namaanisha, matembezi yetu ya kila siku na Roho Mtakatifu: 129 00:08:52,670 --> 00:08:57,080 jinsi ya kukuza ufahamu wa kiroho, jinsi ya kusikia kutoka kwa Mungu, 130 00:08:57,080 --> 00:09:01,000 jinsi ya kujenga imani ya mtu katika hali ya kutokuwa na uhakika wa maisha. 131 00:09:01,000 --> 00:09:04,220 Masuala haya ya msingi na mengine yatashughulikiwa 132 00:09:04,220 --> 00:09:06,000 chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu 133 00:09:06,000 --> 00:09:11,310 kupitia vipindi vya ufundishaji wa kina na muda wa maswali shirikishi na majibu. 134 00:09:11,310 --> 00:09:16,000 Maono yetu pia yanakumbatia makanisa ya mtaani. 135 00:09:16,000 --> 00:09:21,020 Tunataka kushirikiana na mtandao wa huduma mbalimbali 136 00:09:21,020 --> 00:09:28,000 ili kutoa ujuzi wetu, uzoefu, na karama za kiroho kama Roho anavyoongoza. 137 00:09:28,000 --> 00:09:35,000 Hadi kanisa la leo linatambua kwamba roho ya mwanadamu ni chemchemi ya imani, 138 00:09:35,000 --> 00:09:39,000 hapo ndipo Roho Mtakatifu atakapohusika katika mambo yetu. 139 00:09:39,000 --> 00:09:41,870 Jiunge nasi katika Chuo Kikuu cha Mungu 140 00:09:41,870 --> 00:09:45,530 Maarifa ya kimwili hukoma, mara ufunuo unapowadia. 141 00:09:45,530 --> 00:09:48,000 Kama mshauri wetu, Nabii TB Joshua alitufundisha, 142 00:09:48,000 --> 00:09:54,830 “Katika Chuo Kikuu cha Mungu, hata uwe na kipaji gani, hutapandishwa maradufu, 143 00:09:55,140 --> 00:10:00,000 lazima usome kila kozi kwani kila kozi ina kusudi lake.” 144 00:10:00,000 --> 00:10:02,000 Kwa hiyo, unahitaji nini? 145 00:10:02,000 --> 00:10:04,000 Moyo wazi. 146 00:10:04,000 --> 00:10:08,700 Ni nyenzo gani zinazohitajika kuchukua kila kozi - kutokukata tamaa, 147 00:10:08,700 --> 00:10:11,190 kutafuta njia mbadala au kukata tamaa 148 00:10:11,190 --> 00:10:13,600 kwa vipigo vya kikatili vya maisha vya mara kwa mara? 149 00:10:13,600 --> 00:10:23,000 Unyenyekevu, imani, uvumilivu, saburi, msamaha na upendo bila kutarajia. 150 00:10:23,000 --> 00:10:25,000 Nani anasahihisha kazi zetu? 151 00:10:25,000 --> 00:10:27,480 Roho Mtakatifu. 152 00:10:27,480 --> 00:10:34,070 Mungu anakungojea mahala pa Roho wake.