Je! Uanajua kuwa wewe ni kazi ya sa Mwanadamu ndiye zao kuu la Mungu. Ninamaanisha,mtu aliyeumbwa kufikiria, kuzungumza na kutenda pamoja na Mungu. Je, unaishi sambamba na Mungu? Je, hali yako ikoje mbele za Mungu leo/ Bila neema ya Roho Mtakatifu inayokaa ndani yake, mwanadamu ni kama kivuli cha yule aliyemuumba kwanza. Mwanadamu Mungu aliyemuumba hakuwa mtu wa kutawaliwa na hisia za kimwili tu, bali ni mjumbe kati ya ulimwengu unaoonekana na usioonekana. Mungu na mwanadamu walizoea kuongea pamoja kama marafiki. Lakini siku moja mwanadamu alivunja uhusiano huo kwa kutotii na kwenda mbali na Mungu. Yeye basi akaenda mbali na hatimaye akaondoka nyumbani. Aliiacha nchi yake ya asili, Edeni, mahali alipoishi na Mungu. Alihama kutoka kwenye uwepo wa Mungu. Tangu hapo, Mungu amekuwa na shauku ya kutaka kuongea na rafiki yake wa zamani, lakini mwanadamu katika kuondoka mbele ya muumba wake alipoteza lugha mama. nina maana, aliipoteza lugha ya asili aliyoitumia kuongea na Mungu. na akawa hawezi kuwasiliana na muumba wake katika roho na ukweli. Mwanadamu wa kawaida hawezi kusikia au kuongea na Mungu; hii ni changamoto inayotukabili leo. Ingawa Mungu anaongea tena na tena, walio wengi hawatilii maanani Anayoyasema [Ayubu 33:14]. Ukimya huu ni mgumu kwa Mungu. Kama ilivyokuwa hamu ya baba wa mwana mpotevu kumuona mwanae akirudi nyumbani, Mungu anayo hamu ya kuwa na ukaibu tena na mwanadamu, rafiki yake wa zamani. Ndiyo maana Amelazimika kuchagua kuchagua lugha ambayo mwanadamu ataielewa. Hivyo,Alimtuma mwanae wa pekee, Yesu Kristohapa duniani kumrudisha kwake mwanadamu, rafiki wake wa zamani. Mungu aliiheshimu lugha ya mwanadamu na kumuita Yesu NENO. NENO akawa mwili na na kuingia ulimwenguni. Ingawa Mungu huzungumza tena na tena, wengi sana hawapo makini kusikia kile Anachosema (Ayubu 33:14). Ukimya ni mgumu kwa Mungu. Kama vile baba wa mwana mpotevu alivyokuwa na shauku ya kumwona mwanawe akirudi nyumbani, Mungu ana shauku ya kuwa na uhusiano wa karibu tena na mwanadamu, Rafiki yake wa zamani. Ndiyo maana ilimbidi achague lugha ambayo mwanadamu angeelewa. Kwa hivyo alimtuma Mwanawe, Yesu Kristo duniani kumrudisha mwanadamu, Rafiki Yake wa zamani, arudi Kwake tena. Mungu aliheshimu lugha ya mwanadamu kwa kumwita Yesu Neno. Neno alifanyika mwili na akaingia ulimwenguni. Yesu ni Mungu akijieleza Mwenyewe kwa lugha ambayo mwanadamu anaweza kuelewa, lugha ya roho na uzima (Yohana 6:63). Je, ni kwa muda gani tutaendelea kuwaza, kuzungumza na kuishi katika hali ya kimwili ilihali Yesu anakungoja katika mahala pa Roho Wake? Ni wasaa wa kurudi tena katika chuo cha Mungu Na kuanza kumtafuta Roho. Kutoka kwenye miaka mingi ya kujifunza chini ya, na kutembea pamoja na Jenerali wa Mungu, Nabii TB Joshua, hadi alipoitwa Nyumbani Mbinguni, shauku imewaka mioyoni mwetu kutoa hazina tuliyopewa na Mungu; Neno lililo hai katika nguvu za Roho Mtakatifu! Maandishi ya Neno hayawezi kusonga, hayawezi kufanya kazi bila uhai wa Mungu (Yohana 6:63). Kila Neno la Mungu ni Roho na uzima. Na ni uzima halisi wa Mungu katika Neno hilo unaotia nguvu, nishati katika Neno. Hili ndilo Neno linaloponya, kuokoa, kukomboa na kumwezesha mwamini kuishi maisha ya ushindi katika Kristo. Kama vile Simoni Petro katika Yohana 6:68, tumegundua kwamba hakuna mbadala wa Yesu kwa sababu Yeye peke yake ndiye mwenye Maneno ya uzima wa milele. Baada ya mshauri wetu kuitwa Nyumbani tarehe 5 Juni 2021, kama wanafunzi wa zamani, Yesu alipopaa Mbinguni, tumekuwa tukingoja katika imani. Na katika tarehe 8 ya Desemba 2021, nilipokea ufunuo toka kwa Mungu. Na nikapewa jina la 'Chuo Kikuu Cha Mungu'. [muziki] Nilijikuata katika chumba cha glasi ndani ya pango lisilokuwa na sehemu ya kutokea Ghafla mwamba wenye nguvu ukaja kutoka Mbinguni na kugonga mlima wa mawe. ulitoboa lile pango. Mlima ulitikisika, lakini nilibaki thabiti ndani ya chumba cha kioo. Jiwe lilitoboa kwenye mlima wa mawe. Niliangalia. Kisha nikatoka na kutembea. Nilisimama na kushtuka pale nilipoona mwamba ulikuwa umechimba handaki zuri kabisa iliyotengenezwa kwa dhahabu! Nilijiambia, lazima kuwe na maji mwishoni mwa handaki hili. Nilianza kutembea. Ghafla sauti ikasikika kutoka juu: “Baki hapo ulipo. Usiingie! Maji yanakujia.” Nilisimama na kubaki pale nilipokuwa. Niliposimama tuli, ghafla niliona maji yakitiririka kutoka mwishoni mwa handaki kuelekea kwangu. Maji yalikuwa safi, yakimeta kwa uhai. Yalitiririka karibu zaidi mpaka yakafika kwenye vidole vyangu na kunawisha miguu yangu kama wimbi kwenye ufuo wa bahari. Nilipokuwa nikitafakari juu ya ono hilo, moyo wangu ulinisukuma kwenye Kitabu cha Danieli 2:44. Nitasoma; Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuzikomesha, nao utasimama milele na milele. Hii ndiyo maana ya maono ya mwamba uliochongwa kutoka mlimani, lakini si kwa mikono ya binadamu — mwamba uliovunja chuma, shaba, udongo, fedha na dhahabu vipande vipande. Kusudi la mwamba ni nini? Kama inavyosema katika kitabu cha Yeremia 1:10, nitasoma; angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda. Kusudi la mwamba ni kuondoa kizuizi kati ya mioyo yetu na Mungu. Muda ambapo mtu anapokabidhi moyo wake kwa Roho Mtakatifu, pazia huondolewa. Neno la Mungu ni mbegu ya maisha ya kiungu ambayo huja ndani ya mioyo yetu na kusababisha imani kukua. Maono hayo ni kwa wakati ulioamriwa (Habakuki 2:3). Sasa, muda umewadia Maono ni kwa ajiri kumuunganisha mwanadamu kwa Mungu tena. kupitia Neno Lake, kwa Roho Wake, ili kuujenga Mwili wa Kristo. na kushirikiana na mtandao wa makanisa kote ulimwenguni. Maono haya yanaendana na wito na zawadi ya Mungu katika maisha yetu. Mwamba ulioanguka kutoka Mbinguni ni Neno la Ufalme kama Yesu alivyosema katika Mathayo 13:19. Maono yetu ni kusaidia kuingiza Neno katika mioyo ya watu - kwa sababu ni pale tu ndipo linafanya kazi kwa ufanisi. Kama Biblia inavyosema Katika kitabu cha 2 Wakorintho 3:3 - Wacha nikusomee; Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua iliyoandikwa na Kristo, matokeo ya kazi yetu. Barua hii haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai, si juu ya vibao vya mawe, bali juu ya vibao vya mioyo ya wanadamu. Katika miongo miwili iliyopita chini ya ushauri wa Nabii TB Joshua, mwingiliano wetu na maelfu ya waumini na viongozi wa makanisa ulimwenguni kote na maswali ya mara kwa mara yaliyoulizwa na wengi wakati wa mihadhara yamevuta mtazamo wetu kwenye upande wa vitendo wa Ukristo, Namaanisha, matembezi yetu ya kila siku na Roho Mtakatifu: jinsi ya kukuza ufahamu wa kiroho, jinsi ya kusikia kutoka kwa Mungu, jinsi ya kujenga imani ya mtu katika hali ya kutokuwa na uhakika wa maisha. Masuala haya ya msingi na mengine yatashughulikiwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu kupitia vipindi vya ufundishaji wa kina na muda wa maswali shirikishi na majibu. Maono yetu pia yanakumbatia makanisa ya mtaani. Tunataka kushirikiana na mtandao wa huduma mbalimbali ili kutoa ujuzi wetu, uzoefu, na karama za kiroho kama Roho anavyoongoza. Hadi kanisa la leo linatambua kwamba roho ya mwanadamu ni chemchemi ya imani, hapo ndipo Roho Mtakatifu atakapohusika katika mambo yetu. Jiunge nasi katika Chuo Kikuu cha Mungu Maarifa ya kimwili hukoma, mara ufunuo unapowadia. Kama mshauri wetu, Nabii TB Joshua alitufundisha, “Katika Chuo Kikuu cha Mungu, hata uwe na kipaji gani, hutapandishwa maradufu, lazima usome kila kozi kwani kila kozi ina kusudi lake.” Kwa hiyo, unahitaji nini? Moyo wazi. Ni nyenzo gani zinazohitajika kuchukua kila kozi - kutokukata tamaa, kutafuta njia mbadala au kukata tamaa kwa vipigo vya kikatili vya maisha vya mara kwa mara? Unyenyekevu, imani, uvumilivu, saburi, msamaha na upendo bila kutarajia. Nani anasahihisha kazi zetu? Roho Mtakatifu. Mungu anakungojea mahala pa Roho wake.