[Script Info] Title: [Events] Format: Layer, Start, End, Style, Name, MarginL, MarginR, MarginV, Effect, Text Dialogue: 0,0:00:08.00,0:00:12.00,Default,,0000,0000,0000,,Je! unajua kuwa wewe ni kazi ya sanaa? Dialogue: 0,0:00:12.00,0:00:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Mwanadamu ndiye bidhaa kuu ya Mungu. Dialogue: 0,0:00:14.00,0:00:20.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninamaanisha, mtu aliyeundwa kufikiria, kuzungumza na kutenda na Mungu. Dialogue: 0,0:00:20.00,0:00:22.00,Default,,0000,0000,0000,,Je, unaishi pamoja na Mungu? Dialogue: 0,0:00:22.00,0:00:25.00,Default,,0000,0000,0000,,Je, hadhi yako ikoje mbele za Mungu leo? Dialogue: 0,0:00:25.00,0:00:33.00,Default,,0000,0000,0000,,Bila neema ya Roho Mtakatifu inayokaa ndani yake, \Nmwanadamu ni kivuli tu cha yule aliyeumbwa na Mungu! Dialogue: 0,0:00:33.00,0:00:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Mwanadamu ambaye Mungu alimuumba hakuwa mtu wa kimwili tu \Nanayetawaliwa na hisia zake Dialogue: 0,0:00:39.00,0:00:45.00,Default,,0000,0000,0000,,bali ni mjumbe kati ya ulimwengu unaoonekana na usioonekana. Dialogue: 0,0:00:45.00,0:00:50.00,Default,,0000,0000,0000,,Mungu na mwanadamu walikuwa wakizungumza pamoja kama marafiki. Dialogue: 0,0:00:50.00,0:00:57.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini siku moja mwanadamu alivunja uhusiano kwa kutotii \Nna akaenda mbali na Mungu. Dialogue: 0,0:00:57.00,0:01:03.00,Default,,0000,0000,0000,,Kisha akaenda mbali zaidi hadi mwishowe akaondoka nyumbani. Dialogue: 0,0:01:03.00,0:01:06.00,Default,,0000,0000,0000,,Aliiacha nchi yake ya asili, Edeni, ambako aliishi na Mungu. Dialogue: 0,0:01:06.00,0:01:12.00,Default,,0000,0000,0000,,Alihama kutoka kwenye uwepo wa Mungu. Dialogue: 0,0:01:12.00,0:01:18.00,Default,,0000,0000,0000,,Tangu wakati huo, Mungu amekuwa na shauku ya kuweza \Nkuzungumza tena na rafiki yake wa zamani Dialogue: 0,0:01:18.00,0:01:25.00,Default,,0000,0000,0000,,lakini mwanadamu, kwa kuacha uwepo wa Muumba wake, \Nalikuwa amepoteza lugha yake mama. Dialogue: 0,0:01:25.00,0:01:29.00,Default,,0000,0000,0000,,Namaanisha, alipoteza lugha yake ya asili na Mungu Dialogue: 0,0:01:29.00,0:01:34.00,Default,,0000,0000,0000,,na hakuweza kuwasiliana na Muumba wake katika roho na kweli. Dialogue: 0,0:01:34.00,0:01:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Mwanadamu wa kawaida hawezi kusikia au kuzungumza na Mungu; \Nhii ndiyo changamoto tunayokabiliana nayo leo. Dialogue: 0,0:01:42.78,0:01:45.99,Default,,0000,0000,0000,,Ingawa Mungu huzungumza tena na tena, Dialogue: 0,0:01:45.99,0:01:49.00,Default,,0000,0000,0000,,wengi sana hawapo makini kusikia \Nkile Anachosema (Ayubu 33:14). Dialogue: 0,0:01:49.00,0:01:52.00,Default,,0000,0000,0000,,Ukimya ni mgumu kwa Mungu. Dialogue: 0,0:01:52.00,0:01:55.70,Default,,0000,0000,0000,,Kama vile baba wa mwana mpotevu Dialogue: 0,0:01:55.70,0:01:58.48,Default,,0000,0000,0000,,alivyokuwa na shauku ya kumwona\Nmwanawe akirudi nyumbani, Dialogue: 0,0:01:58.48,0:02:02.40,Default,,0000,0000,0000,,Mungu ana shauku ya kuwa na uhusiano\Nwa karibu tena na mwanadamu, Dialogue: 0,0:02:02.40,0:02:04.42,Default,,0000,0000,0000,,Rafiki yake wa zamani. Dialogue: 0,0:02:04.42,0:02:06.82,Default,,0000,0000,0000,,Ndiyo maana ilimbidi achague lugha Dialogue: 0,0:02:06.82,0:02:08.52,Default,,0000,0000,0000,,ambayo mwanadamu angeelewa. Dialogue: 0,0:02:08.52,0:02:13.23,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hivyo alimtuma Mwanawe,\NYesu Kristo duniani kumrudisha mwanadamu, Dialogue: 0,0:02:13.23,0:02:18.00,Default,,0000,0000,0000,,Rafiki Yake wa zamani, arudi Kwake tena. Dialogue: 0,0:02:18.00,0:02:22.27,Default,,0000,0000,0000,,Mungu aliheshimu lugha ya mwanadamu\Nkwa kumwita Yesu Neno. Dialogue: 0,0:02:22.27,0:02:25.85,Default,,0000,0000,0000,,Neno alifanyika mwili na akaingia \Nulimwenguni. Dialogue: 0,0:02:25.85,0:02:29.27,Default,,0000,0000,0000,,Yesu ni Mungu akijieleza Mwenyewe Dialogue: 0,0:02:29.27,0:02:33.07,Default,,0000,0000,0000,,kwa lugha ambayo mwanadamu\Nanaweza kuelewa, Dialogue: 0,0:02:33.07,0:02:36.00,Default,,0000,0000,0000,,lugha ya roho na uzima (Yohana 6:63). Dialogue: 0,0:02:36.00,0:02:38.54,Default,,0000,0000,0000,,Je, ni kwa muda gani tutaendelea kuwaza, Dialogue: 0,0:02:38.54,0:02:41.38,Default,,0000,0000,0000,,kuzungumza na kuishi katika hali \Nya kimwili Dialogue: 0,0:02:41.38,0:02:45.46,Default,,0000,0000,0000,,ilhali Yesu anakungoja katika mahala\Npa Roho Wake? Dialogue: 0,0:02:45.46,0:02:48.34,Default,,0000,0000,0000,,Ni wasaa wa kurudi tena katika Chuo Kikuu \Ncha Mungu Dialogue: 0,0:02:48.34,0:02:51.54,Default,,0000,0000,0000,,Na kuanza kumtafuta Roho. Dialogue: 0,0:02:51.54,0:02:55.65,Default,,0000,0000,0000,,Kutoka kwenye miaka mingi ya kujifunza\Nchini ya, na kutembea Dialogue: 0,0:02:55.65,0:02:58.54,Default,,0000,0000,0000,,pamoja na Jenerali wa Mungu, Nabii\NTB Joshua, Dialogue: 0,0:02:58.54,0:03:01.09,Default,,0000,0000,0000,,hadi alipoitwa Nyumbani Mbinguni, Dialogue: 0,0:03:01.09,0:03:06.89,Default,,0000,0000,0000,,shauku imewaka mioyoni mwetu\Nkutoa hazina tuliyopewa na Mungu; Dialogue: 0,0:03:06.89,0:03:10.36,Default,,0000,0000,0000,,Neno lililo hai katika nguvu za \NRoho Mtakatifu! Dialogue: 0,0:03:10.36,0:03:12.31,Default,,0000,0000,0000,,Maandishi ya Neno hayawezi kusonga, Dialogue: 0,0:03:12.31,0:03:14.88,Default,,0000,0000,0000,,hayawezi kufanya kazi bila \Nuhai wa Mungu (Yohana 6:63). Dialogue: 0,0:03:14.88,0:03:18.21,Default,,0000,0000,0000,,Kila Neno la Mungu ni Roho na uzima. Dialogue: 0,0:03:18.21,0:03:20.13,Default,,0000,0000,0000,,Na ni uzima halisi wa Mungu Dialogue: 0,0:03:20.62,0:03:24.00,Default,,0000,0000,0000,,katika Neno hilo unaotia nguvu,\Nnishati katika Neno. Dialogue: 0,0:03:24.00,0:03:27.11,Default,,0000,0000,0000,,Hili ndilo Neno linaloponya, kuokoa,\Nkukomboa Dialogue: 0,0:03:27.11,0:03:30.00,Default,,0000,0000,0000,,na kumwezesha mwamini kuishi maisha\Nya ushindi katika Kristo. Dialogue: 0,0:03:30.00,0:03:34.60,Default,,0000,0000,0000,,Kama vile Simoni Petro katika Yohana 6:68, Dialogue: 0,0:03:34.60,0:03:38.26,Default,,0000,0000,0000,,tumegundua kwamba hakuna mbadala wa Yesu Dialogue: 0,0:03:38.26,0:03:42.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu Yeye peke yake ndiye mwenye \NManeno ya uzima wa milele. Dialogue: 0,0:03:42.00,0:03:46.90,Default,,0000,0000,0000,,Baada ya mshauri wetu kuitwa Nyumbani\Ntarehe 5 Juni 2021, Dialogue: 0,0:03:46.90,0:03:51.00,Default,,0000,0000,0000,,kama wanafunzi wa zamani,\NYesu alipopaa Mbinguni, Dialogue: 0,0:03:51.00,0:03:54.80,Default,,0000,0000,0000,,tumekuwa tukingoja katika imani. Dialogue: 0,0:03:54.80,0:03:59.92,Default,,0000,0000,0000,,Na tarehe 8 ya Desemba 2021,\Nnilipokea ufunuo toka kwa Mungu. Dialogue: 0,0:03:59.92,0:04:05.05,Default,,0000,0000,0000,,Na nikapewa jina la \N'Chuo Kikuu Cha Mungu'. Dialogue: 0,0:04:05.10,0:04:15.55,Default,,0000,0000,0000,,[muziki] Dialogue: 0,0:04:15.55,0:04:19.56,Default,,0000,0000,0000,,Nilijikuta katika chumba cha glasi\Nndani ya pango Dialogue: 0,0:04:19.56,0:04:23.00,Default,,0000,0000,0000,,lisilokuwa na sehemu ya kutokea Dialogue: 0,0:04:23.00,0:04:28.00,Default,,0000,0000,0000,,Ghafla mwamba wenye nguvu ukaja \Nkutoka Mbinguni Dialogue: 0,0:04:28.00,0:04:31.00,Default,,0000,0000,0000,,na kugonga mlima wa mawe. Dialogue: 0,0:04:31.00,0:04:33.00,Default,,0000,0000,0000,,ulitoboa lile pango. Dialogue: 0,0:04:33.00,0:04:38.00,Default,,0000,0000,0000,,Mlima ulitikisika, lakini nilibaki\Nthabiti ndani ya chumba cha kioo. Dialogue: 0,0:04:38.00,0:04:48.00,Default,,0000,0000,0000,,Jiwe lilitoboa kwenye mlima wa mawe. Dialogue: 0,0:04:48.00,0:04:52.00,Default,,0000,0000,0000,,Niliangalia. Dialogue: 0,0:04:52.00,0:04:54.00,Default,,0000,0000,0000,,Kisha nikatoka na kutembea. Dialogue: 0,0:04:54.00,0:04:58.00,Default,,0000,0000,0000,,Nilisimama na kushtuka pale nilipoona Dialogue: 0,0:04:58.00,0:05:06.00,Default,,0000,0000,0000,,mwamba ulikuwa umechimba handaki zuri kabisa\Niliyotengenezwa kwa dhahabu! Dialogue: 0,0:05:06.00,0:05:12.00,Default,,0000,0000,0000,,Nilijiambia, lazima kuwe na maji\Nmwishoni mwa handaki hili. Dialogue: 0,0:05:12.00,0:05:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Nilianza kutembea. Dialogue: 0,0:05:14.00,0:05:18.00,Default,,0000,0000,0000,,Ghafla sauti ikasikika kutoka juu: Dialogue: 0,0:05:18.00,0:05:25.00,Default,,0000,0000,0000,,“Baki hapo ulipo. Usiingie!\NMaji yanakujia.” Dialogue: 0,0:05:25.00,0:05:29.00,Default,,0000,0000,0000,,Nilisimama na kubaki pale nilipokuwa. Dialogue: 0,0:05:29.00,0:05:33.29,Default,,0000,0000,0000,,Niliposimama tuli, ghafla niliona maji Dialogue: 0,0:05:33.29,0:05:36.00,Default,,0000,0000,0000,,yakitiririka kutoka mwishoni mwa handaki \Nkuelekea kwangu. Dialogue: 0,0:05:36.00,0:05:40.00,Default,,0000,0000,0000,,Maji yalikuwa safi, yakimeta kwa uhai. Dialogue: 0,0:05:40.00,0:05:43.00,Default,,0000,0000,0000,,Yalitiririka karibu zaidi Dialogue: 0,0:05:43.00,0:05:45.00,Default,,0000,0000,0000,,mpaka yakafika kwenye vidole vyangu Dialogue: 0,0:05:45.00,0:05:53.00,Default,,0000,0000,0000,,na kunawisha miguu yangu kama wimbi\Nkwenye ufuo wa bahari. Dialogue: 0,0:05:53.00,0:05:55.60,Default,,0000,0000,0000,,Nilipokuwa nikitafakari juu ya ono hilo, Dialogue: 0,0:05:55.60,0:06:02.58,Default,,0000,0000,0000,,moyo wangu ulinisukuma kwenye \NKitabu cha Danieli 2:44. Nitasoma; Dialogue: 0,0:06:02.58,0:06:07.94,Default,,0000,0000,0000,,Na katika siku za wafalme hao Mungu\Nwa mbinguni atausimamisha ufalme Dialogue: 0,0:06:07.94,0:06:13.30,Default,,0000,0000,0000,,ambao hautaangamizwa milele, wala watu \Nwengine hawataachiwa enzi yake; Dialogue: 0,0:06:13.30,0:06:18.36,Default,,0000,0000,0000,,bali utavunja falme hizi zote \Nvipande vipande na kuzikomesha, Dialogue: 0,0:06:18.36,0:06:22.36,Default,,0000,0000,0000,,nao utasimama milele na milele. Dialogue: 0,0:06:22.36,0:06:28.56,Default,,0000,0000,0000,,Hii ndiyo maana ya maono ya mwamba \Nuliochongwa kutoka mlimani, Dialogue: 0,0:06:28.56,0:06:32.21,Default,,0000,0000,0000,,lakini si kwa mikono ya binadamu\N— mwamba uliovunja Dialogue: 0,0:06:32.21,0:06:40.82,Default,,0000,0000,0000,,chuma, shaba, udongo, fedha na dhahabu \Nvipande vipande. Dialogue: 0,0:06:41.09,0:06:44.28,Default,,0000,0000,0000,,Kusudi la mwamba ni nini? Dialogue: 0,0:06:44.41,0:06:49.23,Default,,0000,0000,0000,,Kama inavyosema katika kitabu cha \NYeremia 1:10, nitasoma; Dialogue: 0,0:06:49.46,0:06:56.62,Default,,0000,0000,0000,,angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa \Nna juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, Dialogue: 0,0:06:56.79,0:07:01.93,Default,,0000,0000,0000,,na kuharibu, na kuangamiza; \Nili kujenga na kupanda. Dialogue: 0,0:07:03.00,0:07:10.35,Default,,0000,0000,0000,,Kusudi la mwamba ni kuondoa kizuizi \Nkati ya mioyo yetu na Mungu. Dialogue: 0,0:07:10.35,0:07:16.00,Default,,0000,0000,0000,,Muda ambapo mtu anapokabidhi moyo wake\Nkwa Roho Mtakatifu, pazia huondolewa. Dialogue: 0,0:07:16.00,0:07:19.75,Default,,0000,0000,0000,,Neno la Mungu ni mbegu ya maisha ya \Nkiungu Dialogue: 0,0:07:19.75,0:07:25.00,Default,,0000,0000,0000,,ambayo huja ndani ya mioyo yetu\Nna kusababisha imani kukua. Dialogue: 0,0:07:25.00,0:07:31.00,Default,,0000,0000,0000,,Maono hayo ni kwa wakati ulioamriwa \N(Habakuki 2:3). Dialogue: 0,0:07:31.00,0:07:33.81,Default,,0000,0000,0000,,Sasa, muda umewadia Dialogue: 0,0:07:33.81,0:07:37.90,Default,,0000,0000,0000,,Maono ni kwa ajili kumuunganisha mwanadamu\Nkwa Mungu tena. Dialogue: 0,0:07:37.90,0:07:44.00,Default,,0000,0000,0000,,kupitia Neno Lake, kwa Roho Wake, \Nili kuujenga Mwili wa Kristo. Dialogue: 0,0:07:44.00,0:07:49.00,Default,,0000,0000,0000,,na kushirikiana na mtandao wa makanisa\Nkote ulimwenguni. Dialogue: 0,0:07:49.00,0:07:54.00,Default,,0000,0000,0000,,Maono haya yanaendana na wito na\Nzawadi ya Mungu katika maisha yetu. Dialogue: 0,0:07:54.00,0:07:59.00,Default,,0000,0000,0000,,Mwamba ulioanguka kutoka Mbinguni \Nni Neno la Ufalme Dialogue: 0,0:07:59.00,0:08:04.05,Default,,0000,0000,0000,,kama Yesu alivyosema katika Mathayo 13:19. Dialogue: 0,0:08:04.05,0:08:07.24,Default,,0000,0000,0000,,Maono yetu ni kusaidia kuingiza Neno\Nkatika mioyo ya watu - Dialogue: 0,0:08:07.24,0:08:10.59,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu ni pale tu ndipo linafanya kazi\Nkwa ufanisi. Dialogue: 0,0:08:10.59,0:08:16.29,Default,,0000,0000,0000,,Kama Biblia inavyosema Katika kitabu cha \N2 Wakorintho 3:3 - Wacha nikusomee; Dialogue: 0,0:08:17.48,0:08:20.54,Default,,0000,0000,0000,,Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua \Niliyoandikwa na Kristo, Dialogue: 0,0:08:20.54,0:08:22.49,Default,,0000,0000,0000,,matokeo ya kazi yetu. Dialogue: 0,0:08:22.49,0:08:26.39,Default,,0000,0000,0000,,Barua hii haikuandikwa kwa wino bali kwa \NRoho wa Mungu aliye hai, Dialogue: 0,0:08:26.39,0:08:31.80,Default,,0000,0000,0000,,si juu ya vibao vya mawe, bali juu ya \Nvibao vya mioyo ya wanadamu. Dialogue: 0,0:08:32.00,0:08:36.00,Default,,0000,0000,0000,,Katika miongo miwili iliyopita chini ya \Nushauri wa Nabii TB Joshua, Dialogue: 0,0:08:36.00,0:08:40.00,Default,,0000,0000,0000,,mwingiliano wetu na maelfu ya waumini na \Nviongozi wa makanisa ulimwenguni kote Dialogue: 0,0:08:40.00,0:08:44.41,Default,,0000,0000,0000,,na maswali ya mara kwa mara yaliyoulizwa\Nna wengi wakati wa mihadhara Dialogue: 0,0:08:44.41,0:08:48.00,Default,,0000,0000,0000,,yamevuta mtazamo wetu kwenye upande\Nwa vitendo wa Ukristo, Dialogue: 0,0:08:48.00,0:08:52.67,Default,,0000,0000,0000,,Namaanisha, matembezi yetu\Nya kila siku na Roho Mtakatifu: Dialogue: 0,0:08:52.67,0:08:57.08,Default,,0000,0000,0000,,jinsi ya kukuza ufahamu wa kiroho, \Njinsi ya kusikia kutoka kwa Mungu, Dialogue: 0,0:08:57.08,0:09:01.00,Default,,0000,0000,0000,,jinsi ya kujenga imani ya mtu katika\Nhali ya kutokuwa na uhakika wa maisha. Dialogue: 0,0:09:01.00,0:09:04.22,Default,,0000,0000,0000,,Masuala haya ya msingi na mengine\Nyatashughulikiwa Dialogue: 0,0:09:04.22,0:09:06.00,Default,,0000,0000,0000,,chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu Dialogue: 0,0:09:06.00,0:09:11.31,Default,,0000,0000,0000,,kupitia vipindi vya ufundishaji wa kina \Nna muda wa maswali shirikishi na majibu. Dialogue: 0,0:09:11.31,0:09:16.00,Default,,0000,0000,0000,,Maono yetu pia yanakumbatia \Nmakanisa ya mtaani. Dialogue: 0,0:09:16.00,0:09:21.02,Default,,0000,0000,0000,,Tunataka kushirikiana na mtandao wa \Nhuduma mbalimbali Dialogue: 0,0:09:21.02,0:09:28.00,Default,,0000,0000,0000,,ili kutoa ujuzi wetu, uzoefu, na karama \Nza kiroho kama Roho anavyoongoza. Dialogue: 0,0:09:28.00,0:09:35.00,Default,,0000,0000,0000,,Hadi kanisa la leo linatambua kwamba \Nroho ya mwanadamu ni chemchemi ya imani, Dialogue: 0,0:09:35.00,0:09:39.00,Default,,0000,0000,0000,,hapo ndipo Roho Mtakatifu atakapohusika\Nkatika mambo yetu. Dialogue: 0,0:09:39.00,0:09:41.87,Default,,0000,0000,0000,,Jiunge nasi katika Chuo Kikuu cha Mungu Dialogue: 0,0:09:41.87,0:09:45.53,Default,,0000,0000,0000,,Maarifa ya kimwili hukoma, \Nmara ufunuo unapowadia. Dialogue: 0,0:09:45.53,0:09:48.00,Default,,0000,0000,0000,,Kama mshauri wetu, Nabii TB Joshua\Nalivyotufundisha, Dialogue: 0,0:09:48.00,0:09:54.83,Default,,0000,0000,0000,,“Katika Chuo Kikuu cha Mungu, hata uwe \Nna kipaji gani, hutapandishwa maradufu, Dialogue: 0,0:09:55.14,0:10:00.00,Default,,0000,0000,0000,,lazima usome kila kozi kwani\Nkila kozi ina kusudi lake.” Dialogue: 0,0:10:00.00,0:10:02.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo, unahitaji nini? Dialogue: 0,0:10:02.00,0:10:04.00,Default,,0000,0000,0000,,Moyo wazi. Dialogue: 0,0:10:04.00,0:10:08.70,Default,,0000,0000,0000,,Ni nyenzo gani zinazohitajika kuchukua \Nkila kozi - kutokukata tamaa, Dialogue: 0,0:10:08.70,0:10:11.19,Default,,0000,0000,0000,,kutafuta njia mbadala au kutokukata tamaa Dialogue: 0,0:10:11.19,0:10:13.60,Default,,0000,0000,0000,,kwa vipigo vya kikatili vya maisha \Nvya mara kwa mara? Dialogue: 0,0:10:13.60,0:10:23.00,Default,,0000,0000,0000,,Unyenyekevu, imani, uvumilivu, saburi,\Nmsamaha na upendo bila kutarajia. Dialogue: 0,0:10:23.00,0:10:25.00,Default,,0000,0000,0000,,Nani anasahihisha kazi zetu? Dialogue: 0,0:10:25.00,0:10:27.48,Default,,0000,0000,0000,,Roho Mtakatifu. Dialogue: 0,0:10:27.48,0:10:34.07,Default,,0000,0000,0000,,Mungu anakungojea mahala pa Roho wake.