Tumeambiwa tutafute kipeuo cha pili cha 100.
Ngoja niichore hii alama kubwa hapa chini ionekane vizuri.
Kwa hiyo kipeuo cha pili ni hii alama kubwa inayoonekana hapa
Kipeuo cha pili cha 100.
Ukiiona kama hii, ina maana
kipeuo cha pili cha namba chanya.
Kama ni mzoefu wa namba hasi, unafahamu
pia kuna kipeuo cha pili cha namba hasi, lakini
ukiona hii alama, ina maana ni kipeuo cha pili cha namba chanya.
Hebu sasa tufanye hili swali.
Tumeambiwa tutafute namba chanya,
ambayo tukiizidisha kwa yenyewe tunapata 100.
Je ni namba gani ambayo nikiizidisha kwa yenyewe ninapata 100?
Hebu tuone, kama nikiizidisha 9 kwa yenyewe
nitapata 81.
kama nikiizidisha 10 kwa yenyewe, napata 100.
Kwa hiyo, hii ni sawa na --ngoja niandike hapa
Kawaida unaweza kuiruka hii hatua.
Lakini unaweza kuiandika kama kipeuo cha pili cha --na
badala ya 100, 100 ni sawa na 10 mara 10.
Sasa umefahamu, kiepuo cha pili cha namba
ukiizidisha kwa yenyewe itakuwa namba fulani
Hii ni sawa na 10.
Kwa hiyo kipeuo cha pili cha 100 ni 10.
Au ungeweza kuiandika,
10 ikizidishwa kwa yenyewe, ambayo ni sawa na 10 mara 10,
ni sawa na 100.