0:00:00.000,0:00:00.540 0:00:00.540,0:00:03.730 Tumeambiwa tutafute kipeuo cha pili cha 100. 0:00:03.730,0:00:05.130 Ngoja niichore hii alama kubwa hapa chini ionekane vizuri. 0:00:05.130,0:00:09.060 Kwa hiyo kipeuo cha pili ni hii alama kubwa inayoonekana hapa 0:00:09.060,0:00:11.880 Kipeuo cha pili cha 100. 0:00:11.880,0:00:13.650 Ukiiona kama hii, ina maana 0:00:13.650,0:00:15.120 kipeuo cha pili cha namba chanya. 0:00:15.120,0:00:16.850 Kama ni mzoefu wa namba hasi, unafahamu 0:00:16.850,0:00:19.490 pia kuna kipeuo cha pili cha namba hasi, lakini 0:00:19.490,0:00:22.700 ukiona hii alama, ina maana ni kipeuo cha pili cha namba chanya. 0:00:22.700,0:00:24.570 Hebu sasa tufanye hili swali. 0:00:24.570,0:00:28.090 Tumeambiwa tutafute namba chanya, 0:00:28.090,0:00:34.350 ambayo tukiizidisha kwa yenyewe tunapata 100. 0:00:34.350,0:00:37.700 Je ni namba gani ambayo nikiizidisha kwa yenyewe ninapata 100? 0:00:37.700,0:00:40.220 Hebu tuone, kama nikiizidisha 9 kwa yenyewe 0:00:40.220,0:00:41.580 nitapata 81. 0:00:41.580,0:00:44.280 kama nikiizidisha 10 kwa yenyewe, napata 100. 0:00:44.280,0:00:46.800 Kwa hiyo, hii ni sawa na --ngoja niandike hapa 0:00:46.800,0:00:48.740 Kawaida unaweza kuiruka hii hatua. 0:00:48.740,0:00:51.470 Lakini unaweza kuiandika kama kipeuo cha pili cha --na 0:00:51.470,0:00:56.610 badala ya 100, 100 ni sawa na 10 mara 10. 0:00:56.610,0:00:58.960 Sasa umefahamu, kiepuo cha pili cha namba 0:00:58.960,0:01:00.890 ukiizidisha kwa yenyewe itakuwa namba fulani 0:01:00.890,0:01:03.240 Hii ni sawa na 10. 0:01:03.240,0:01:06.720 Kwa hiyo kipeuo cha pili cha 100 ni 10. 0:01:06.720,0:01:09.330 Au ungeweza kuiandika, 0:01:09.330,0:01:16.520 10 ikizidishwa kwa yenyewe, ambayo ni sawa na 10 mara 10, 0:01:16.520,0:01:20.000 ni sawa na 100. 0:01:20.000,0:01:20.734