Sitasahau kamwe jinsi nilihisi nilipoona bahari na kuingia mashuani kwa mara ya kwanza. Kwa mtoto wa umri wa miaka minne, ilikuwa hisia kuu ya uhuru ambayo ningeweza dhania. Nilihisi, wajua, kutokea umri huo, Ningependa sana kwa njia moja au nyingine, kuenda kwa matanga kote duniani. Unapong'oa nanga kuanzisha safari hizi, wajua, unabeba kila kitu unachohitaji kusalimika. Ulichonacho ndicho chote unacho. lazima utumie vizuri ulicho nacho hadi tone la mwisho la mafuta ya diseli, kifurushi cha mwisho cha chakula. Ni muhimu sana, au hautafanikiwa. Na ghafla nikagundua, "mbona ulimwengu wetu ni tofauti?' Unajua tuna raslimali chache, vinavyopatikana mara moja katika historia ya binadamu. Wajua, vyuma, plastiki na mbolea. Tunachimba vitu hivi vyote ardhini na kuvimaliza. Inawezekanaje kwa muda mrefu? Hakika kuna njia tofauti tungeweza kutumia raslimali kimataifa bila kuzimaliza. Hilo ndilo swali nililolitia maanani, na ikachukua muda mrefu kufika mahali ambapo niligundua kuwa kuna njia mbadala ya kuendesha uchumi, kuna njia mbadala tunaweza kutumia vitu, kutumia vifaa. Na hiyo inaweza kuwa uchumi mzunguko. Jinsi uchumi inavyoendeshwa sana leo hii ni kwa kutoa. Ni finyu. Tunatoa kitu chini ya ardhi, tunatengeneza kitu kwayo, hatimaye mwishoni mwa utumizi ya bidhaa ile, tunaitupa. Haijalishi upo na ufanisi upi na vifaa unavyoleta mfumoni, hata kama umetengeneza hiyo bidhaa kutumia nishati kidogo au vifaa chache, mwishowe utapungukiwa. Ukigeuza hiyo na kuangalia mfano mzunguko, pale ambapo unapobuni bidhaa, unachukua kifaa chini ya ardhi, au kifaa kilicho tengezwa upya, kimsingi, unaingiza hicho ndani ya bidhaa, lakini unabuni bidhaa ndio uweze kurejesha kifaa kwa kubuni, tangia mwanzo. Unabuni kukabiliana na taka na uchafuzi wa mazingira. Kwa nini uunde mojawapo ya haya kwa ulimwengu wa raslimali finyu? Ni kuhusu maelezo fupi ya kubuni. Leo hii ukinunua mashine ya kufulia nguo unalipa ushuru ukinunua, na kumiliki vifaa vyake vyote, na inapoharibika, na lazima ziharibike, unalipa ushuru tena, ushuru wa taka. Katika mfumo mzunguko, hayo yote yanabadilika. Haumiliki mashine yako, unalipa kila unapofua. Itachukuzwa na watengenezaji wa mashine, na watahakikisha mara mashine ile inapofika hatima yake, wanaichukua, wanajua kilicho ndani yake, na wanaweza rudisha vifaa kutoka kwayo. kwa hivyo unabakia kubuni mfumo mzunguko. Tumetafiti kwa upana takwimu zake, wajua, hisabati, na ni wa bei nafuu zaidi. Ni senti 12 za Marekani kinyume na senti 27 za Marekani kwa kila mwosho kwa mashine mzunguko. Tungeishi ndani ya mfumo unaofanya kazi. Hatungekuwa tunazalisha taka. Tungekuwa na huduma bora. Tungepata teknolojia kwa njia rahisi. Kutokana na utafiti wote tuliofanya, kwa sababu hao watengenezaji hawanunui bidhaa zote, waendelea wanaziuza, tungeweza kupata bei bora, kwa sababu wangehakikishiwa mpito wa vifaa kurudi kwa mfumo. Ni na matumaini makubwa kwa sababu unapotizama takwimu, unapotizama hesabu, ina maana kubadili na kutumia uchumi mzunguko. Kuna thamani kubwa kwa uchumi mzunguko kuliko uchumi finyu. Hakika kuna gharama kwa mpito kwa mashirika kubwa, lakini pengine unafaa kujiuliza : Ni nini athari ya mfumo finyu? Kwa sababu kwangu ni rahisi, Kuna athari kubwa kwa mfumo finyu. Haiwezi kuwa kesho, kulingana na uchumi safi. Kwa hivyo, ni wapi unawekeza wakati wako? Ni wapi unawekeza juhudi zako? Wacha tushughulikie ni nini uchumi mzunguko na ujaribu kuchora aina ya mzunguko huo unavyoweza manukuu ni na Mauricio Kakuei Tanaka, Uhakiki na Jenny Lam-Chowdhury ΒΆ tamati