WEBVTT 00:00:01.218 --> 00:00:05.738 Sitasahau kamwe jinsi nilihisi nilipoona bahari 00:00:05.738 --> 00:00:07.923 na kuingia mashuani kwa mara ya kwanza. 00:00:07.923 --> 00:00:09.829 Kwa mtoto wa umri wa miaka minne, 00:00:09.829 --> 00:00:12.781 ilikuwa hisia kuu ya uhuru ambayo ningeweza dhania. 00:00:13.774 --> 00:00:15.698 Nilihisi, wajua, kutokea umri huo, 00:00:15.698 --> 00:00:19.257 Ningependa sana kwa njia moja au nyingine, kuenda kwa matanga kote duniani. 00:00:27.524 --> 00:00:29.196 Unapong'oa nanga kuanzisha safari hizi, 00:00:29.196 --> 00:00:32.615 wajua, unabeba kila kitu unachohitaji kusalimika. 00:00:32.925 --> 00:00:34.680 Ulichonacho ndicho chote unacho. 00:00:34.680 --> 00:00:36.666 lazima utumie vizuri ulicho nacho 00:00:36.666 --> 00:00:39.339 hadi tone la mwisho la mafuta ya diseli, kifurushi cha mwisho cha chakula. 00:00:39.339 --> 00:00:41.677 Ni muhimu sana, au hautafanikiwa. 00:00:41.757 --> 00:00:44.704 Na ghafla nikagundua, "mbona ulimwengu wetu ni tofauti?' 00:00:44.704 --> 00:00:46.732 Unajua tuna raslimali chache, 00:00:46.732 --> 00:00:49.447 vinavyopatikana mara moja katika historia ya binadamu. 00:00:49.785 --> 00:00:52.565 Wajua, vyuma, plastiki na mbolea. 00:00:52.565 --> 00:00:55.852 Tunachimba vitu hivi vyote ardhini na kuvimaliza. 00:00:56.347 --> 00:00:58.366 Inawezekanaje kwa muda mrefu? 00:00:59.154 --> 00:01:02.296 Hakika kuna njia tofauti tungeweza kutumia raslimali kimataifa 00:01:02.296 --> 00:01:04.088 bila kuzimaliza. 00:01:04.088 --> 00:01:05.945 Hilo ndilo swali nililolitia maanani, 00:01:05.945 --> 00:01:07.992 na ikachukua muda mrefu kufika mahali 00:01:07.992 --> 00:01:10.899 ambapo niligundua kuwa kuna njia mbadala ya kuendesha uchumi, 00:01:10.899 --> 00:01:13.632 kuna njia mbadala tunaweza kutumia vitu, kutumia vifaa. 00:01:13.867 --> 00:01:15.795 Na hiyo inaweza kuwa uchumi mzunguko. 00:01:19.539 --> 00:01:23.068 Jinsi uchumi inavyoendeshwa sana leo hii ni kwa kutoa. 00:01:23.068 --> 00:01:24.069 Ni finyu. 00:01:24.069 --> 00:01:27.116 Tunatoa kitu chini ya ardhi, tunatengeneza kitu kwayo, 00:01:27.116 --> 00:01:29.971 hatimaye mwishoni mwa utumizi ya bidhaa ile, tunaitupa. 00:01:30.240 --> 00:01:31.746 Haijalishi upo na ufanisi upi 00:01:31.746 --> 00:01:33.927 na vifaa unavyoleta mfumoni, 00:01:33.927 --> 00:01:35.332 hata kama umetengeneza hiyo bidhaa 00:01:35.332 --> 00:01:38.232 kutumia nishati kidogo au vifaa chache, 00:01:38.232 --> 00:01:40.188 mwishowe utapungukiwa. 00:01:40.460 --> 00:01:43.190 Ukigeuza hiyo na kuangalia mfano mzunguko, 00:01:43.190 --> 00:01:45.100 pale ambapo unapobuni bidhaa, 00:01:45.100 --> 00:01:49.088 unachukua kifaa chini ya ardhi, au kifaa kilicho tengezwa upya, 00:01:49.088 --> 00:01:50.563 kimsingi, unaingiza hicho ndani ya bidhaa, 00:01:50.563 --> 00:01:51.852 lakini unabuni bidhaa 00:01:51.852 --> 00:01:55.358 ndio uweze kurejesha kifaa kwa kubuni, tangia mwanzo. 00:01:55.500 --> 00:01:57.577 Unabuni kukabiliana na taka na uchafuzi wa mazingira. 00:01:57.577 --> 00:02:00.671 Kwa nini uunde mojawapo ya haya kwa ulimwengu wa raslimali finyu? 00:02:00.671 --> 00:02:02.500 Ni kuhusu maelezo fupi ya kubuni. 00:02:03.298 --> 00:02:05.010 Leo hii ukinunua mashine ya kufulia nguo 00:02:05.010 --> 00:02:08.411 unalipa ushuru ukinunua, na kumiliki vifaa vyake vyote, 00:02:08.411 --> 00:02:10.917 na inapoharibika, na lazima ziharibike, 00:02:10.917 --> 00:02:13.292 unalipa ushuru tena, ushuru wa taka. 00:02:13.292 --> 00:02:15.332 Katika mfumo mzunguko, hayo yote yanabadilika. 00:02:15.332 --> 00:02:17.498 Haumiliki mashine yako, unalipa kila unapofua. 00:02:17.498 --> 00:02:20.317 Itachukuzwa na watengenezaji wa mashine, 00:02:20.317 --> 00:02:21.520 na watahakikisha 00:02:21.520 --> 00:02:23.664 mara mashine ile inapofika hatima yake, 00:02:23.664 --> 00:02:25.858 wanaichukua, wanajua kilicho ndani yake, 00:02:25.858 --> 00:02:27.861 na wanaweza rudisha vifaa kutoka kwayo. 00:02:27.861 --> 00:02:30.053 kwa hivyo unabakia kubuni mfumo mzunguko. 00:02:30.053 --> 00:02:32.767 Tumetafiti kwa upana takwimu zake, 00:02:32.767 --> 00:02:34.018 wajua, hisabati, 00:02:34.018 --> 00:02:35.246 na ni wa bei nafuu zaidi. 00:02:35.246 --> 00:02:39.683 Ni senti 12 za Marekani kinyume na senti 27 za Marekani kwa kila mwosho 00:02:39.683 --> 00:02:41.420 kwa mashine mzunguko. 00:02:42.595 --> 00:02:44.773 Tungeishi ndani ya mfumo unaofanya kazi. 00:02:44.773 --> 00:02:47.163 Hatungekuwa tunazalisha taka. 00:02:47.163 --> 00:02:48.637 Tungekuwa na huduma bora. 00:02:48.637 --> 00:02:51.114 Tungepata teknolojia kwa njia rahisi. 00:02:51.114 --> 00:02:52.638 Kutokana na utafiti wote tuliofanya, 00:02:52.638 --> 00:02:55.453 kwa sababu hao watengenezaji hawanunui bidhaa zote, 00:02:55.453 --> 00:02:56.474 waendelea wanaziuza, 00:02:56.474 --> 00:02:57.806 tungeweza kupata bei bora, 00:02:57.806 --> 00:03:00.601 kwa sababu wangehakikishiwa mpito wa vifaa 00:03:00.601 --> 00:03:02.057 kurudi kwa mfumo. 00:03:06.836 --> 00:03:07.942 Ni na matumaini makubwa 00:03:07.942 --> 00:03:09.722 kwa sababu unapotizama takwimu, 00:03:09.722 --> 00:03:11.722 unapotizama hesabu, 00:03:11.722 --> 00:03:14.325 ina maana kubadili na kutumia uchumi mzunguko. 00:03:14.325 --> 00:03:17.658 Kuna thamani kubwa kwa uchumi mzunguko kuliko uchumi finyu. 00:03:17.658 --> 00:03:20.801 Hakika kuna gharama kwa mpito kwa mashirika kubwa, 00:03:20.801 --> 00:03:22.981 lakini pengine unafaa kujiuliza : 00:03:22.981 --> 00:03:24.470 Ni nini athari ya mfumo finyu? 00:03:24.470 --> 00:03:26.138 Kwa sababu kwangu ni rahisi, 00:03:26.138 --> 00:03:27.521 Kuna athari kubwa kwa mfumo finyu. 00:03:27.777 --> 00:03:31.636 Haiwezi kuwa kesho, kulingana na uchumi safi. 00:03:31.636 --> 00:03:33.587 Kwa hivyo, ni wapi unawekeza wakati wako? 00:03:33.587 --> 00:03:34.968 Ni wapi unawekeza juhudi zako? 00:03:34.968 --> 00:03:37.183 Wacha tushughulikie ni nini uchumi mzunguko 00:03:37.183 --> 00:03:39.053 na ujaribu kuchora aina ya mzunguko huo unavyoweza 00:03:39.053 --> 00:03:40.053 manukuu ni na Mauricio Kakuei Tanaka, 00:03:40.053 --> 00:03:41.053 Uhakiki na Jenny Lam-Chowdhury ΒΆ 00:03:41.053 --> 00:03:44.912 tamati