WEBVTT 00:00:00.000 --> 00:00:05.166 Baraka mara nyingi huambatana na vita. 00:00:05.166 --> 00:00:13.000 Ni vita gani kwa mwili huu vinaweza kuwa na manufaa kwa roho yako. 00:00:13.000 --> 00:00:19.233 Kile ambacho ni kigumu kwa mwili mara nyingi ni msaada kwa roho yako. 00:00:19.233 --> 00:00:36.133 Ikiwa unamtumikia Mungu kwa namna iliyo rahisi tu kwako, basi huduma yako itakosa kujitolea. 00:00:36.133 --> 00:00:38.133 Sisemi hakutakuwa na kujitolea kokote. 00:00:38.133 --> 00:00:44.766 Kunaweza kuwa na kujitolea kwa sehemu, sio kujitolea kamili. 00:00:44.766 --> 00:00:47.366 Unajua tatizo hapa? 00:00:47.366 --> 00:00:53.133 Ikiwa kujitolea kwako kwa Mungu ni kwa sehemu - 00:00:53.133 --> 00:00:57.800 unamtumikia Mungu kwa namna iliyo rahisi wako tu - 00:00:57.800 --> 00:01:07.633 na unakabiliwa na hali ambapo imani yako katika Kristo inapingana 00:01:07.633 --> 00:01:11.800 na imani ya jadi, 00:01:11.800 --> 00:01:15.233 na matarajio ya kitamaduni, 00:01:15.233 --> 00:01:19.700 na shinikizo la nafasi, 00:01:19.700 --> 00:01:23.966 na mambo ya dunia hii... 00:01:23.966 --> 00:01:29.966 Ikiwa kujitolea kwako kwa Mungu ni kwa sehemu na unakumbana na mzozo kama huo, 00:01:29.966 --> 00:01:41.033 una uwezekano wa kubaki bila tofauti, kujaribu na kukaa kwenye uzio 00:01:41.033 --> 00:01:49.566 hasa wakati ambapo kushikilia imani yako kunahusisha maumivu fulani, dhabihu fulani. 00:01:49.566 --> 00:02:00.133 Lakini ukijaribu kuepuka maumivu katika mwili, hivi karibuni utakaribisha maumivu katika roho. 00:02:00.133 --> 00:02:09.966 Kwa sababu kile kinachoanza na kuridhika muda si mrefu kitamalizika kwa ukiukwaji wa kanuni. 00:02:09.966 --> 00:02:13.133 Ni suala la muda tu. 00:02:13.133 --> 00:02:22.900 Njia ya kukiuka kanuni haina mwisho na inazidi kupanuka. 00:02:22.900 --> 00:02:29.533 Ndio maana linapokuja swala la mambo ya Mungu, huduma ya Mungu - 00:02:29.533 --> 00:02:33.400 lazima tujitoe kwa moyo wote. 00:02:33.400 --> 00:02:36.233 Ahadi kamili, sio sehemu. 00:02:36.233 --> 00:02:39.600 Hatumtumikii Mungu tu wakati inapotufaa. 00:02:39.600 --> 00:02:43.966 Hatumtumikii Mungu tu nyakati zinapokuwa nzuri. Hapana!