< Return to Video

MAAJABU: Baba Amsamehe Muuaji Aliyemuua Binti Yake!

  • 0:00 - 0:05
    Ulisema kumbukumbu yako, juu ya wanawake wote uliowaua, ilikuwa imetoweka.
  • 0:05 - 0:07
    Kwetu sisi, haijatoweka.
  • 0:07 - 0:11
    Kwa maneno yako, ulisema kwamba hawakuwa na maana yoyote kwako.
  • 0:11 - 0:13
    Lakini alimaanisha kila kitu kwetu.
  • 0:13 - 0:19
    Alikuwa mama. Alikuwa mke. Alikuwa dada. Na tunamkumbuka.
  • 0:19 - 0:26
    Gary Ridgway aliketi pale, akiwa ametazama kwa uso kauzu huku jamaa za waathiriwa wakimlaani na kumdhihaki.
  • 0:26 - 0:32
    Yeye ni mnyama. Natamani awe na kifo , cha mateso ya muda mrefu na cha kikatili.
  • 0:32 - 0:36
    Ataenda kuzimu na huko ndiko anakostahili.
  • 0:36 - 0:39
    Lakini basi
    uso wake kauzu usio na hisia hatimaye ulivunjika
  • 0:39 - 0:43
    pale baba wa mmoja wa wahanga wake alipoonekana kumshangaza.
  • 0:43 - 0:55
    Bwana Ridgway, kuna watu hapa ambao wanakuchukia.
  • 0:55 - 0:58
    Mimi si mmoja wao.
  • 0:58 - 1:06
    Umefanya iwe vigumu kuishi kulingana na kile ninachoamini.
  • 1:06 - 1:10
    Na hivyo ndivyo
    MUNGU anasema tufanye.
  • 1:10 - 1:12
    Na huko ndiko kusamehe.
  • 1:12 - 1:17
    Umesamehewa, bwana.
  • 1:17 - 1:24
    Nguvu ya kusamehe inatokana na kujisalimisha
  • 1:24 - 1:27
    kwa Mwanzilishi wa msamaha.
  • 1:27 - 1:33
    “Baba, wasamehe,”
  • 1:33 - 1:41
    Yesu alisema Msalabani (Luka 23:34).
  • 1:41 - 1:46
    "Baba, wasamehe."
  • 1:46 - 1:56
    Nguvu ya kusamehe inatokana na kujisalimisha kwa Mwanzilishi wa msamaha.
  • 1:56 - 2:02
    Siwezi kupata nguvu ndani yangu ya kusamehe.
  • 2:02 - 2:06
    Nikijisamehe, kutakuwa na masharti.
  • 2:06 - 2:07
    Kutakuwa na kikomo.
  • 2:07 - 2:12
    Kutakuwa na muda ambao
    nitaweka kulingana na uzito wa makosa niliyotendewa.
  • 2:12 - 2:17
    Ikiwa nitasamehe kwa nguvu zangu mwenyewe, bado nitakuwa nikipigana moyoni mwangu
  • 2:17 - 2:20
    hata kama nimeutoa kwa mdomo.
  • 2:20 - 2:25
    Nguvu ya kusamehe kutoka moyoni haipo
    katika mwili huu.
  • 2:25 - 2:27
    Sio katika hisia zako.
  • 2:27 - 2:29
    Si katika nguvu na uwezo wako mwenyewe.
  • 2:29 - 2:32
    Inatokana na kujisalimisha.
  • 2:32 - 2:38
    Ikiwa unapambana na msamaha, acha kupinga kujisalimisha.
Title:
MAAJABU: Baba Amsamehe Muuaji Aliyemuua Binti Yake!
Description:

Huu ndio wakati wa kushangaza baba anapokabiliana na mwanamume aliyepatikana na hatia ya kumuua bintiye, pamoja na wanawake wengine 48…

“Nguvu ya kusamehe huja kwa kujisalimisha kwa Mwanzilishi wa msamaha. “Baba, wasamehe,” Yesu alisema pale Msalabani (Luka 23:34) Siwezi kupata nguvu ndani yangu ili kusamehe. Nikijisamehe, kutakuwa na masharti. Kutakuwa na kikomo. Kutakuwa na muda ambao nitaweka kulingana na uzito wa makosa niliyotendewa. Ikiwa nitasamehe kwa nguvu zangu mwenyewe, bado nitakuwa nikipigana moyoni mwangu hata kama nimeutoa kwa kinywa changu. Nguvu ya kusamehe kutoka moyoni haipo katika mwili huu. Sio katika hisia zako. Si katika nguvu na uwezo wako mwenyewe. Inatokana na kujisalimisha. Ikiwa unapambana na msamaha, acha kupinga kujisalimisha. - Ndugu Chris

Unaweza kutazama ujumbe kamili kwenye God’s Heart Tv ambapo kimetoka kipande hiki kiliochnyeshwa hapa - https://www.youtube.com/watch?v=yvRzWsIir6U

Unaweza kupata picha halisi ya klipu hii, inayoonyesha kesi ya Gary Ridgway mwaka wa 2003, hapa - https://www.youtube.com/watch?v=NmOUAdLgN1A na https://www.youtube.com/watch?v =f2_OOaP763k

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
02:39

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions