-
Mwaka unapokaribia kufika mwisho, mara nyingi tunajitahidi kuona ni sherehe gani tutahudhuria, sivyo?
-
Utasherehekea wapi mwaka huu? Jibu ni wazi: katika uwepo wa Bwana!
-
Ni jambo jema kwetu, kila tarehe 31 Desemba
-
kutumia muda kidogo kutafakari yale tuliyofanikiwa mwaka uliopita.
-
Tunakaribia kuingia mwaka mpya, "Wacha nitazame nyuma. Nimeweza kufanya nini hadi sasa?"
-
"Nimefanikiwa nini maishani mwangu?"
-
"Je, ninaweza kuwa na furaha? Je, ninaweza kujivunia kitu,
-
na kusema kwamba kwa hakika nimefanikiwa mambo kadhaa mwaka huu?"
-
Au je, unapoangalia nyuma, unaona makosa yako tu?
-
Je, unaona maamuzi mabaya uliyoyafanya?
-
Unaona watu uliowaumiza unapotazama nyuma.
-
Kama mtoto wa Mungu, ni hatari kutazama nyuma kwenye maisha yako ya zamani.
-
"Lakini kwa nini, ndugu, umetueleza tuangalie mafanikio yetu ya zamani!"
-
Ndiyo, tunapaswa kutazama nyuma tu kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
-
Kwa nini ni hatari kutazama nyuma kama mtoto wa Mungu?
-
Kwa sababu kutazama maisha yako ya zamani ni mtego wa shetani!
-
Anakujaribu kukumbusha jinsi ulivyokuwa mzuri na kile unachokosa sasa.
-
Anakujaribu kukumbusha muda mzuri uliokuwa nao na marafiki zako, ukifanya chochote ulichotaka,
-
lakini sasa unatumia muda wako na Wakristo.
-
Kisha, unaanza kufikiria ungemalizia wapi kama hungekuwa kwenye uwepo wa Mungu.
-
Kwa maneno haya machache, tutafika kwenye kichwa cha ujumbe wa leo, ambacho ni:
-
"MTIZAMO WAKO KWA MAISHA."
-
Kama mtoto wa Mungu, mtazamo wako kwa maisha lazima uwe tofauti na watu wa kidunia.
-
mtazamo wako kwa maisha ni nini?
-
Mke wa Lutu alilipa kwa uhai wake kwa kutotii Neno la Mungu!
-
Ingawa alijua Neno la Mungu,
-
ingawa alijua maelekezo ya haki yaliyopewa na Mungu,
-
alisisitiza kufanya mambo kwa njia yake mwenyewe, na ikamgharimu uhai wake, kama wengi wetu tunavyofanya leo.
-
Kujua Neno la Mungu hakutakuokoa.
-
Shetani pia anajua Neno la Mungu, hata zaidi yako!
-
Shetani alipoenda kumjaribu Yesu Kristo, alimwambia: "Imeandikwa."
-
Ni ujasiri gani!
-
Adui wa nafsi ya mwanadamu alikwenda kwa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, na kumwambia,
-
"Tazama, imeandikwa! Mungu alisema hivyo, kwa hiyo unapaswa kufanya hivyo!"
-
Alijaribu kutumia maneno ya Mungu kumwelekeza Yesu Kristo afanye nini!
-
Unadhani kwa sababu unajua Neno la Mungu, utaingia mbinguni siku moja!
-
Wengi wetu tunafanya vivyo hivyo. Tuna njia zetu wenyewe.
-
Tunajua Neno la Mungu, tunasoma Biblia, tunajua Neno la Mungu linasema nini,
-
lakini tuna njia zetu!
-
Tunatii kwa njia zetu!
-
Tunafanya kile Neno la Mungu kinasema kwa njia zetu.
-
Mke wa Lutu alitii Neno la Mungu kwa njia yake mwenyewe.
-
Alikuwa akimfuata mumewe. Si hivyo Biblia inavyosema?
-
Inasema kwamba Lutu alikuwa akitembea, na mke wake alikuwa akimfuata.
-
Kama watu wengi leo, mwanaume huenda kanisani na mke hufuata
-
Kuja kwako kanisani ukimfuata mume au mke hakutakuokoa.
-
Kutii Neno la Mungu ndiko kutakuokoa!
-
Yesu Kristo anajua jinsi tusivyostahili neema Yake,
-
ndiyo maana Ameamua kuacha mbali yaliyopita ili kubainisha yajayo!
-
Kumbuka, kutoka kwa Lutu na familia yake kutoka Sodoma na Gomora ni mfano.
-
Inawakilisha kutoka kwako na kwangu kutoka maisha ya dhambi na kuingia maisha ya haki!
-
Kutoka maisha yasiyo ya haki kwenda maisha ya utakatifu.
-
Wengi wetu, ingawa tulifanya uamuzi wa kutembea na Bwana, na Yesu Kristo,
-
katikati ya safari, tunasema: "Kuna nini kibaya na kuvuta sigara moja tu?"
-
Tunapojaribu kutafuta sababu za makosa yetu, tunataja neema.
-
Tunapojaribu kumhukumu mtu, tunasema: "Neno la Mungu linasema hivi na vile
-
kwa nini unafanya hivi?"
-
"Wewe ni mnafiki!"
-
Hakuna neema katika hali hii. Unajua Neno la Mungu na unalitumia katika hali hii!
-
Tumeitwa kumfuata Mungu, kwa njia ya Mungu, si kwa njia yetu!
-
Njia ya Mungu iko hapa, katika Neno Lake.
-
Ukipenda kufanikiwa maishani, lazima ujifunze kutazama mbele,
-
kwenye vita vyako vya kiroho pamoja na Yesu Kristo.
-
Kwa sababu kwa kutazama mbele ndipo unapoona mambo mapya, upeo mpya,
-
na fursa mpya ambazo usingewahi kuota ndoto kuzihusu!
-
Unajua kwa nini Mungu alitupa Neno Lake?
-
Alitupa Neno Lake kutufundisha hekima Yake ili tusije kuwa wahanga wa ujinga wetu.
-
Neno la Mungu linasema:
"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa." (Hosea 4:6)
-
Tunahitaji kutatua matatizo ya leo kwa kutumia maarifa ya jana.
-
Matumizi ya mbinu za jana
-
hakuwezi kusaidia!
-
Ikiwa mbinu za jana zingeweza kutatua matatizo yako, matatizo yako yangekuwa yamekwisha leo!!
-
Kwa wengi wetu, tupo jangwani sasa, tupo kwenye ardhi kavu.
-
Tuko mahali ambapo hakuna njia, bila njia ya kutoka, na tunajihisi tumepotea
-
Neno la Mungu linakuambia leo kwamba ikiwa hutatazama nyuma,
-
ikiwa hutatazama nyuma kwenye yaliyopita, Mungu atafanya jambo jipya maishani mwako.
-
Jambo hili jipya ni kwamba Atakufanyia njia mahali ambapo hakuna njia!
-
[♪ Muziki ♪]