-
Baada ya kuathirika na maambukizi,
-
mfumo wetu wa kingamaradhi
hukumbuka tishio,
-
hasa kwa kuzalisha chembechembe za
kingamwili.
-
Hizi ni protini ambazo huzunguka katika
damu na kote mwilini;
-
huwa zinatambua haraka na kulemaza
maradhi zinapoigusa,
-
na hivyo kuzuia au kupunguza ugonjwa.
-
Hii ndiyo maana hatuwi wagonjwa kwa
kirusi kimoja mara mbili;
-
tuna kingamaradhi.
-
Chanjo huiga mchakato huu,
-
kuhimiza mfumo wa kingamaradhi
kuzalisha kingamwili
-
bila sisi kuwa wagonjwa.
-
Baadhi ya vipengee vikuu vya chanjo ya
SARS-CoV-2
-
ni "chanjo za mRNA,"
-
inayohusu kujumuisha muundo wa kijenetiki
-
wa protini muhimu yenye miiba
kwa umbo la kirusi
-
katika fomyula
-
ambayo wakati itadungwa kwa wanadamu,
-
huagiza seli zetu hai kuzalisha
protini ya miiba.
-
Kisha, mwili huzalisha kingamwili ili
kukabili protini ya miiba,
-
na zinatulinda dhidi ya athari ya virusi.
-
Mkakati huu ni wa haraka zaidi kuliko
mbinu zaidi za kiasili,
-
ambazo kwa sana huhusisha kuzalisha kirusi
hai ambacho kimefanywa hafifu au tuli,
-
au kubuni kiasi cha juu cha
protini ya miiba
-
ili kubaini iwapo zinaweza kuanzisha
shughuli ya kingamwili.
-
Baada ya chanjo inayoweza kutumika
kugunduliwa,
-
kuna shughuli kadhaa za ukaguzi
kabla iweze kutolewa kwa watu.
-
Kwanza ni vipimo visivyo vya watu,
-
vinavyojumuisha majaribio katika
maabara na kwa kutumia wanyama.
-
Sharti wanasayansi wahakikishe
-
kuwa kipengee cha chanjo si tu
kizuri, bali pia ni salama.
-
Kwa mfano, shughuli ya kingamwili
kwa chanjo yenye dosari
-
inaweza, katika hali adimu zaidi,
-
kuishia kuzidisha hatari ya kuathiriwa.
-
Chanjo inapotimiza matokeo yanayofaa
ya vipimo visivyo vya watu,
-
vipimo vya watu vinaweza kuanza
katika kundi dogo.
-
Kadri kipengee cha chanjo kinavyoimarika,
-
kinajaribiwa kwa idadi inayoongezeka
ya watu,
-
huku wanasayansi na madaktrai
-
wakifuatilia kwa karibu usalama, ufaafu
na vipimo vya dawa.
-
Baada ya ukamilishaji wa majaribio kwa
binadamu,
-
lazima chanjo ikaguliwe na kuidhinishwa
-
na mashirika ya udhibiti,
-
kama vile FDA,
-
kabla utengenezaji na usambazaji kwa
kiwango cha juu kuanza
-
na chanjo iliyothibiyishwa kutolewa
kwa wengi.
-
Imenukuliwa na Mauricio Kakuei Tanaka
Imekaguliwa na Carol Wang