Injili ya Mafanikio: Tuzungumzie UTOAJI MKUBWA, na sio MAISHA YA ANASA!
-
0:00 - 0:08Ikiwa jumbe unazosikia zinaonekana tu kuonyesha upendo wa Mungu kwa wenye dhambi
-
0:08 - 0:13lakini si chuki ya Mungu juu ya dhambi, kuwa makini.
-
0:13 - 0:20Ikiwa mafundisho unayopokea yanalenga zaidi ustawi wa mali
-
0:20 - 0:25kuliko mafanikio ya kiroho, kuwa mwangalifu.
-
0:25 - 0:36Ikiwa mahubiri yanayohubiriwa yanazingatia sana ahadi za Mungu
-
0:36 - 0:43bila kuzungumzia juu ya utii wako, kuwa mwangalifu.
-
0:43 - 0:47Baadhi yenu mnaweza kushangaa na ninachosema,
-
0:47 - 0:51'Ndugu Chris, unazungumza kuhusu mafanikio - injili ya mafanikio.
-
0:51 - 0:59Je, unasema kwamba Mungu hataki nifanikiwe, nibarikiwe, nisitawi, nifanye vizuri?'
-
0:59 - 1:02Hapana, usininukuu vibaya.
-
1:02 - 1:06Sisemi Mungu hawezi kukufanikisha.
-
1:06 - 1:11Ninasema lengo letu lisiwe kwenye ustawi wa mali
-
1:11 - 1:14kwa gharama ya ustawi wa kiroho.
-
1:14 - 1:26Zingatia jambo hili – ahadi ya Mungu ya utele si kibali cha kufanya ubadhirifu.
-
1:26 - 1:34Ahadi ya Mungu ya utele si leseni ya umbea.
-
1:34 - 1:39Wacha tuzungumze juu ya utoaji wa kupita kiasi, sio maisha ya kupita kiasi.
-
1:39 - 1:44Mungu akikufanikisha, amekuandaa kuwabariki wengine.
-
1:44 - 1:47Tuwe makini watu wa Mungu.
-
1:47 - 1:53Matarajio yasiyofaa hutuweka tayari kwa kukatishwa tamaa.
-
1:53 - 1:56Ukimjia Mungu kwa matarajio
-
1:56 - 2:01ambayo yanalenga tu ustawi wa mali,
-
2:01 - 2:07utajiweka tayari kwa kukata tamaa.
-
2:07 - 2:12Kwa sababu hata kama ustawi wa mali unakuja,
-
2:12 - 2:17matakwa ya mwanadamu hayana kikomo.
-
2:17 - 2:21Mungu ameahidi kukutana nasi kulingana na mahitaji yetu, si matakwa yetu.
-
2:21 - 2:25Hakuna kikomo kwa kile mwanadamu anataka.
-
2:25 - 2:28Kila hatua unayofikia katika mafanikio ya kimwili,
-
2:28 - 2:31daima kuna kiwango cha juu zaidi cha kufikia.
-
2:31 - 2:37Ikiwa huo ndio msingi wa mtazamo wako juu ya maisha, hutaridhika kamwe.
-
2:37 - 2:42Sisemi Mungu hawezi kukufanikisha, akubariki sana.
-
2:42 - 2:46Sio leseni ya ubadhirifu.
-
2:46 - 2:51Hapana! Ni leseni ya utoaji wa kupita kiasi, sio maisha ya ubadhirifu.
- Title:
- Injili ya Mafanikio: Tuzungumzie UTOAJI MKUBWA, na sio MAISHA YA ANASA!
- Description:
-
Ikiwa jumbe unazosikia zinaonekana kuangazia tu upendo wa Mungu kwa wenye dhambi lakini sio chuki ya Mungu dhidi ya dhambi, kuwa mwangalifu. Ikiwa mafundisho unayopokea yanaangazia zaidi mafanikio ya kimwili kuliko mafanikio ya kiroho, kuwa mwangalifu. Ikiwa mahubiri yanayohubiriwa yanazingatia sana ahadi za Mungu bila kuzungumzia utiifu wako, kuwa mwangalifu. Baadhi yenu mnaweza kushangaa na kile ninachosema, ‘Ndugu Chris, unazungumzia kuhusu mafanikio - injili ya mafanikio. Je, unasema kwamba Mungu hataki nifanikiwe, kubarikiwa, kustawi, kufanya vizuri?’ Hapana, usinukuu vibaya. Sisemi kwamba Mungu hawezi kukufanikisha. Ninasema kwamba lengo letu halipaswi kuwa kwenye mafanikio ya kimwili kwa gharama ya mafanikio ya kiroho. Kumbuka hili - Ahadi ya Mungu ya wingi sio leseni ya ubadhirifu. Ahadi ya Mungu ya wingi sio leseni ya anasa za kupindukia. Hebu tuzungumze kuhusu utoaji ulio mwingi, sio maisha ya ubadhirifu. Mungu akikufanikisha, amekuandaa kuwabariki wengine. Tuwe waangalifu, watu wa Mungu. Matarajio yasiyo sahihi yanatuweka kwenye kukata tamaa. Ukimjia Mungu na matarajio ambayo yanalenga tu mafanikio ya kimwili, utajiweka kwa urahisi kwenye kukata tamaa. Kwa sababu hata mafanikio ya kimwili yakija, mahitaji ya mwanadamu hayana kikomo. Mungu ameahidi kutukutana nasi kulingana na mahitaji yetu, sio tamaa zetu. Hakuna kikomo kwa kile mwanadamu anataka. Kila hatua unayofikia katika mafanikio ya kimwili, daima kuna kiwango cha juu zaidi cha kufikia. Ikiwa huo ndio msingi ambao unayatama maisha, hautaweza kuridhika kamwe. Sisemi kwamba Mungu hawezi kukufanikisha, kukubariki kwa wingi. Sio leseni ya ubadhirifu. Hapana! Ni leseni ya utoaji mkubwa, sio maisha ya ubadhirifu.
Unaweza kutazama mahubiri kamili kutoka kwa Ndugu Chris hapa - [https://www.youtube.com/watch?v=rGcRR2HdONY](https://www.youtube.com/watch?v=rGcRR2HdONY)
- Video Language:
- English
- Team:
- God's Heart TV
- Duration:
- 02:51
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Prosperity Gospel: Let’s talk about EXTRAVAGANT GIVING, not EXTRAVAGANT LIVING! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Prosperity Gospel: Let’s talk about EXTRAVAGANT GIVING, not EXTRAVAGANT LIVING! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Prosperity Gospel: Let’s talk about EXTRAVAGANT GIVING, not EXTRAVAGANT LIVING! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Prosperity Gospel: Let’s talk about EXTRAVAGANT GIVING, not EXTRAVAGANT LIVING! |