< Return to Video

Injili ya Mafanikio: Tuzungumzie UTOAJI MKUBWA, na sio MAISHA YA ANASA!

  • 0:00 - 0:08
    Ikiwa jumbe unazosikia zinaonekana tu kuonyesha upendo wa Mungu kwa wenye dhambi
  • 0:08 - 0:13
    lakini si chuki ya Mungu juu ya dhambi, kuwa makini.
  • 0:13 - 0:20
    Ikiwa mafundisho unayopokea yanalenga zaidi ustawi wa mali
  • 0:20 - 0:25
    kuliko mafanikio ya kiroho, kuwa mwangalifu.
  • 0:25 - 0:36
    Ikiwa mahubiri yanayohubiriwa yanazingatia sana ahadi za Mungu
  • 0:36 - 0:43
    bila kuzungumzia juu ya utii wako, kuwa mwangalifu.
  • 0:43 - 0:47
    Baadhi yenu mnaweza kushangaa na ninachosema,
  • 0:47 - 0:51
    'Ndugu Chris, unazungumza kuhusu mafanikio - injili ya mafanikio.
  • 0:51 - 0:59
    Je, unasema kwamba Mungu hataki nifanikiwe, nibarikiwe, nisitawi, nifanye vizuri?'
  • 0:59 - 1:02
    Hapana, usininukuu vibaya.
  • 1:02 - 1:06
    Sisemi Mungu hawezi kukufanikisha.
  • 1:06 - 1:11
    Ninasema lengo letu lisiwe kwenye ustawi wa mali
  • 1:11 - 1:14
    kwa gharama ya ustawi wa kiroho.
  • 1:14 - 1:26
    Zingatia jambo hili – ahadi ya Mungu ya utele si kibali cha kufanya ubadhirifu.
  • 1:26 - 1:34
    Ahadi ya Mungu ya utele si leseni ya umbea.
  • 1:34 - 1:39
    Wacha tuzungumze juu ya utoaji wa kupita kiasi, sio maisha ya kupita kiasi.
  • 1:39 - 1:44
    Mungu akikufanikisha, amekuandaa kuwabariki wengine.
  • 1:44 - 1:47
    Tuwe makini watu wa Mungu.
  • 1:47 - 1:53
    Matarajio yasiyofaa hutuweka tayari kwa kukatishwa tamaa.
  • 1:53 - 1:56
    Ukimjia Mungu kwa matarajio
  • 1:56 - 2:01
    ambayo yanalenga tu ustawi wa mali,
  • 2:01 - 2:07
    utajiweka tayari kwa kukata tamaa.
  • 2:07 - 2:12
    Kwa sababu hata kama ustawi wa mali unakuja,
  • 2:12 - 2:17
    matakwa ya mwanadamu hayana kikomo.
  • 2:17 - 2:21
    Mungu ameahidi kukutana nasi kulingana na mahitaji yetu, si matakwa yetu.
  • 2:21 - 2:25
    Hakuna kikomo kwa kile mwanadamu anataka.
  • 2:25 - 2:28
    Kila hatua unayofikia katika mafanikio ya kimwili,
  • 2:28 - 2:31
    daima kuna kiwango cha juu zaidi cha kufikia.
  • 2:31 - 2:37
    Ikiwa huo ndio msingi wa mtazamo wako juu ya maisha, hutaridhika kamwe.
  • 2:37 - 2:42
    Sisemi Mungu hawezi kukufanikisha, akubariki sana.
  • 2:42 - 2:46
    Sio leseni ya ubadhirifu.
  • 2:46 - 2:51
    Hapana! Ni leseni ya utoaji wa kupita kiasi, sio maisha ya ubadhirifu.
Title:
Injili ya Mafanikio: Tuzungumzie UTOAJI MKUBWA, na sio MAISHA YA ANASA!
Description:

Ikiwa jumbe unazosikia zinaonekana kuangazia tu upendo wa Mungu kwa wenye dhambi lakini sio chuki ya Mungu dhidi ya dhambi, kuwa mwangalifu. Ikiwa mafundisho unayopokea yanaangazia zaidi mafanikio ya kimwili kuliko mafanikio ya kiroho, kuwa mwangalifu. Ikiwa mahubiri yanayohubiriwa yanazingatia sana ahadi za Mungu bila kuzungumzia utiifu wako, kuwa mwangalifu. Baadhi yenu mnaweza kushangaa na kile ninachosema, ‘Ndugu Chris, unazungumzia kuhusu mafanikio - injili ya mafanikio. Je, unasema kwamba Mungu hataki nifanikiwe, kubarikiwa, kustawi, kufanya vizuri?’ Hapana, usinukuu vibaya. Sisemi kwamba Mungu hawezi kukufanikisha. Ninasema kwamba lengo letu halipaswi kuwa kwenye mafanikio ya kimwili kwa gharama ya mafanikio ya kiroho. Kumbuka hili - Ahadi ya Mungu ya wingi sio leseni ya ubadhirifu. Ahadi ya Mungu ya wingi sio leseni ya anasa za kupindukia. Hebu tuzungumze kuhusu utoaji ulio mwingi, sio maisha ya ubadhirifu. Mungu akikufanikisha, amekuandaa kuwabariki wengine. Tuwe waangalifu, watu wa Mungu. Matarajio yasiyo sahihi yanatuweka kwenye kukata tamaa. Ukimjia Mungu na matarajio ambayo yanalenga tu mafanikio ya kimwili, utajiweka kwa urahisi kwenye kukata tamaa. Kwa sababu hata mafanikio ya kimwili yakija, mahitaji ya mwanadamu hayana kikomo. Mungu ameahidi kutukutana nasi kulingana na mahitaji yetu, sio tamaa zetu. Hakuna kikomo kwa kile mwanadamu anataka. Kila hatua unayofikia katika mafanikio ya kimwili, daima kuna kiwango cha juu zaidi cha kufikia. Ikiwa huo ndio msingi ambao unayatama maisha, hautaweza kuridhika kamwe. Sisemi kwamba Mungu hawezi kukufanikisha, kukubariki kwa wingi. Sio leseni ya ubadhirifu. Hapana! Ni leseni ya utoaji mkubwa, sio maisha ya ubadhirifu.

Unaweza kutazama mahubiri kamili kutoka kwa Ndugu Chris hapa - [https://www.youtube.com/watch?v=rGcRR2HdONY](https://www.youtube.com/watch?v=rGcRR2HdONY)

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
02:51

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions