< Return to Video

MIPANGO YAKO MIKONONI MWA MUNGU! | Mahubiri ya Ndugu Chris

  • 0:00 - 0:08
    Ukishindwa kumuingiza Mungu katika mipango yako,
    unapanga kushindwa.
  • 0:10 - 0:15
    Karibuni tena nyote kwenye
    Ibada hii ya Maombi Shirikishi.
  • 0:15 - 0:22
    Kabla ya jambo lolote, tuombe pamoja.
  • 0:22 - 0:32
    Ninaomba sasa hivi kwa kila moyo
    ulioungana na huduma hii
  • 0:32 - 0:46
    kwamba wakutane na uhalisia wa uwezo wako, upendo, wema wako katika maisha yao.
  • 0:46 - 0:55
    Katika jina kuu la Yesu Kristo tunaomba.
  • 0:55 - 0:59
    Na watu wa Mungu wakasema, Amina!
  • 0:59 - 1:10
    Kwanza kabisa, wacha niwasalimie nyote
    Heri ya Mwaka Mpya 2025.
  • 1:10 - 1:15
    Nina neno la kutia moyo
    la kukushirikisha leo.
  • 1:15 - 1:21
    Ni kawaida katika kipindi hiki - tunapoondoka mwaka mmoja na kuingia mwaka mpya -
  • 1:21 - 1:25
    ni kawaida sana kwetu kuwa na muda wa kutafakari yaliyo mbele.
  • 1:25 - 1:29
    Je, nina mipango gani
    kwa mwaka huu unaokuja?
  • 1:29 - 1:34
    Inaweza kuwa katika maisha yako ya kibinafsi,
    maisha yako ya kitaaluma.
  • 1:34 - 1:38
    Inaweza kuwa katika taaluma yako -
    'Nataka kupanua biashara hapa.'
  • 1:38 - 1:43
    Labda mahusiano - 'Mwaka huu,
    nataka kuolewa!'
  • 1:43 - 1:46
    'Mwaka huu, tunataka kupata watoto pamoja' - waume na wake.
  • 1:46 - 1:48
    Huu ni wakati ambao tunapanga mipango.
  • 1:48 - 1:52
    Tunafikiria mwaka ujao,
    mwaka ujao. Nzuri!
  • 1:52 - 1:57
    Ni vizuri kupanga mipango lakini
  • 1:57 - 2:09
    usiingie kwenye makosa ya kupanga mipango ya kesho kana kwamba wewe ndiye mmiliki wake.
  • 2:09 - 2:14
    Fikirini juu ya hilo enyi watu wa Mungu.
  • 2:14 - 2:27
    Usiingie kwenye mtego wa kupanga mipango ya siku zijazo kana kwamba ni yako.
  • 2:27 - 2:31
    Sisemi ni makosa kupanga mipango.
  • 2:31 - 2:34
    Sisemi ni makosa kuangalia mbele.
  • 2:34 - 2:40
    Ninasema unapofanya
    mipango kama Mkristo -
  • 2:40 - 2:44
    'Nini kinachofuata mnamo 2025? Kipi kilicho mbele?
  • 2:44 - 2:46
    Je! ninataka kuzingatia nini?
  • 2:46 - 2:51
    Ninataka kufikia nini katika kazi yangu, maisha ya kibinafsi, biashara, fedha?
  • 2:51 - 2:53
    Ninataka kufanya nini?'
  • 2:53 - 3:01
    Unapopanga mipango, lazima ufanye hivyo
    kwa utambuzi wa mambo matatu.
  • 3:01 - 3:04
    Na mimi nataka uandike.
    Tafadhali andika hii.
  • 3:04 - 3:07
    Ujumbe huu utakusaidia kwa mwaka huu.
  • 3:07 - 3:16
    1. Maisha hayana uhakika
  • 3:16 - 3:27
    2. Mungu ni mwenye enzi kuu
  • 3:27 - 3:36
    3. Kila siku ina riziki yake
  • 3:36 - 3:39
    Nitawaambia tena, watu wa Mungu.
  • 3:39 - 3:44
    Unapopanga mipango, unapopanga juu ya siku zijazo,
  • 3:44 - 3:50
    lazima ufanye hivyo ukiwa na utambuzi huu,
    ufahamu huu -
  • 3:50 - 3:56
    1. Maisha hayana uhakika
  • 3:56 - 4:04
    Wakati fulani tutakabili hali
    zilizo nje ya uwezo wetu.
  • 4:04 - 4:10
    Kwa nini unapanga mipango
    kana kwamba unaudhibiti?
  • 4:10 - 4:23
    Wakati mwingine kama mtoto wa Mungu, unaweza
    kukutana na matukio yasiyobadilika -
  • 4:23 - 4:34
    hakuna kiasi cha maombi, kufunga au
    kukomaa kiroho kutabadili.
  • 4:34 - 4:39
    Maisha hayana uhakika.
  • 4:39 - 4:45
    2. Mungu ni mwenye enzi kuu
  • 4:45 - 4:53
    Maisha kukosa uhakika hakubadili
    enzi kuu ya Mungu.
  • 4:53 - 4:56
    Ndiyo, maisha yamejawa na kutokuwa na uhakika.
  • 4:56 - 5:07
    Lakini jambo moja unaweza kuwa na uhakika nalo - wema wa Mungu, nguvu za Mungu, upendo wa Mungu.
  • 5:07 - 5:13
    Hata katikati ya
    wazimu wa dunia hii,
  • 5:13 - 5:17
    tunaweza kuwa na uhakika juu ya
    wema wa Mungu.
  • 5:17 - 5:19
    Yeye ni mwenye enzi.
  • 5:19 - 5:33
    Na kama Wakristo, lazima tutambue maisha yetu, nyakati zetu ziko mikononi mwake.
  • 5:33 - 5:35
    Mungu ni mwenye enzi.
  • 5:35 - 5:40
    3. Kila siku ina riziki yake
  • 5:40 - 5:46
    Utupe leo mkate wetu wa kila siku.
  • 5:46 - 5:49
    Mana kwa hitaji la wakati huu.
  • 5:49 - 5:58
    Kila siku ina riziki yake -
    Mungu hutoa neema kwa kila siku.
  • 5:58 - 6:05
    Ujumbe ninaopaswa kushiriki
    nawe, kwa ufupi ni huu:
  • 6:05 - 6:10
    'Mipango yako Mikononi mwa Mungu'.
  • 6:10 - 6:15
    Unaweza kusema hivyo sasa hivi. Ikiwa uko na mtu nyumbani, mwambie tu,
  • 6:15 - 6:21
    "Mipango yako mikononi mwa Mungu."
  • 6:21 - 6:26
    Ikiwa uko peke yako, unaweza kujiambia
    au unaweza kuniambia,
  • 6:26 - 6:32
    "Mipango yangu iko mikononi mwa Mungu."
  • 6:32 - 6:37
    Mwanadamu hupanga; Mungu hutekeleza.
  • 6:37 - 6:44
    Mwanadamu anapendekeza; Mungu huamuru.
  • 6:44 - 6:50
    Kama Mkristo, tazama, sikwambii tena kwamba usifanye mpango,
  • 6:50 - 6:58
    bali panga mipango huku ukifahamu
    kuwa maisha yako yako mikononi mwa Mungu.
  • 6:58 - 7:08
    Fanya mipango kutoka katika nafasi ya
    kujitiisha kwa Mpangaji Mkuu
  • 7:08 - 7:16
    ambaye njia zake ni za juu kuliko zetu,
    ambaye mipango yake ni mikubwa kuliko yetu.
  • 7:16 - 7:26
    Wale wanaoshindwa kuweka
    mipango yao mikononi mwa Mungu
  • 7:26 - 7:32
    wanajiweka kwenye
    njia ya kushindwa.
  • 7:32 - 7:35
    Hata nitarahisisha. Nitasema hivi -
  • 7:35 - 7:46
    ukishindwa kumjumuisha Mungu katika mipango yako,
    unapanga kushindwa.
  • 7:46 - 7:52
    Hebu tuyaangazie Maandiko makini katika Yakobo 4.
  • 7:52 - 7:59
    Ninataka kuangazia ukweli huu ili wakati tunapanga mipango ya kesho,
  • 7:59 - 8:07
    tunafanya hivyo tukiwa na ufahamu sahihi wa
    nafasi ya Mungu na nafasi yetu.
  • 8:07 - 8:13
    Unapopanga juu ya siku zijazo,
    kumbuka ni nani aliye Mkuu.
  • 8:13 - 8:20
    Hebu tusome pamoja - Yakobo 4:13.
  • 8:20 - 8:29
    “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutakwenda katika mji fulani;
  • 8:29 - 8:34
    tutakaa huko mwaka mzima, tutanunua na kuuza
    na kujipatia faida...”
  • 8:34 - 8:40
    'Mnamo 2025, nitaenda huko.
    Nitafanya hivi katika biashara yangu.
  • 8:40 - 8:44
    Hakika hili litatokea.'
  • 8:44 - 8:53
    “... kumbe hujui kitakachotokea kesho. Kwani maisha yako ni nini?
  • 8:53 - 9:08
    Bali ni mvuke unaoonekana kwa muda mfupi na kisha kutoweka.
  • 9:08 - 9:20
    Badala yake mnapaswa kusema, Bwana akipenda, tutaishi na kufanya hili au lile.
  • 9:20 - 9:25
    "Bwana akipenda, hili litatokea mwaka wa 2025.
  • 9:25 - 9:33
    Bwana akipenda, mpango huu utatimia.'
  • 9:33 - 9:44
    Yakobo 4:16 BHN - Lakini sasa mnajivunia majivuno yenu. Majivuno yote kama hayo ni mabaya.”
  • 9:44 - 9:52
    Maandiko hapa, nataka kusisitiza,
    hayasemi kamwe usifanye mpango,
  • 9:52 - 10:00
    lakini yanakuonya usiichukue nafasi ya Mungu inapokuja kwenye mpango wako.
  • 10:00 - 10:08
    Kama nilivyosema hapo awali, unapotazama mbele, kumbuka ni nani aliye Kichwa - Yesu.
  • 10:08 - 10:15
    Hakuna kitu hatari zaidi kama kuchukua nafasi ya Mungu katika mpango wako.
  • 10:15 - 10:28
    Kuchukua nafasi ya Mungu katika mpango wako ndiyo njia ya uhakika ya kuanguka kwa mpango huo - hatimaye.
  • 10:28 - 10:31
    Sasa, unaweza kunitazama na kusema,
    'Unasema nini Ndugu Chris?
  • 10:31 - 10:39
    Sichukui nafasi ya Mungu katika mpango wangu. Ningewezaje kuwa Mungu? Mimi si Mungu!'
  • 10:39 - 10:46
    Lakini wengi wetu, kwa jinsi tunavofanya
    mipango yetu ya kesho,
  • 10:46 - 10:52
    tunafanya hivyo kwa njia inayochukua
    umiliki wa kesho.
  • 10:52 - 10:55
    Na unajua hatari ya hii?
  • 10:55 - 10:59
    Unapochukua umiliki wa kesho,
  • 10:59 - 11:02
    unabeba uzito ambao hukukusudiwa
    kubeba,
  • 11:02 - 11:11
    ndiyo maana bila shaka huishia
    katika wasiwasi, woga na mashaka.
  • 11:11 - 11:15
    'Nini kitatokea? Itakuwaje juu ya hiki?
    Vipi kuhusu lile?'
  • 11:15 - 11:20
    Wasiwasi ni mwizi wa furaha.
  • 11:20 - 11:25
    Wasiwasi ni mwizi wa amani.
  • 11:25 - 11:30
    Wasiwasi ni mwizi wa hukumu halali,
  • 11:30 - 11:36
    ambayo ni muhimu katika kuwa msimamizi mzuri
    wa kile kilicho mikononi mwako leo.
  • 11:36 - 11:47
    Ngoja nikukumbushe maneno mazuri ya Bwana wetu Yesu Kristo katika Mathayo 6:34.
  • 11:47 - 11:54
    Yesu alisema, “Basi, msisumbukie
    ya kesho;
  • 11:54 - 12:02
    maana kesho itajisumbukia na mambo yake. Yatosha kwa siku taabu yake yenyewe.”
  • 12:02 - 12:05
    Kila siku ina riziki yake.
  • 12:05 - 12:07
    Kila siku ina baraka zake.
  • 12:07 - 12:08
    Kila siku ina shida zake.
  • 12:08 - 12:10
    Tazama Yesu anachosema hapa.
  • 12:10 - 12:18
    Lakini kwa nini ni jambo la kawaida kwetu leo ​​kuanguka katika mtego wa kuhangaikia kesho?
  • 12:18 - 12:23
    Kwa sababu tunaanguka katika mtego
    wa kujivunia kesho,
  • 12:23 - 12:32
    Tunafanya kana kwamba kesho ni yetu,
    ilihali leo tu ndio yetu.
  • 12:32 - 12:34
    Kesho ni ya Mungu.
  • 12:34 - 12:39
    Sasa ni yako; kinachofuata ni cha Mungu.
  • 12:39 - 12:45
    Ngoja nisome Andiko lingine
    kutoka Mithali 27,
  • 12:45 - 12:49
    tukirudia maneno ya
    Yakobo ambayo tumesoma hivi punde.
  • 12:49 - 12:53
    Katika Mithali 27:1, mwenye hekima anasema hivi,
  • 12:53 - 13:12
    "Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa maana hujui yatakayoletwa na siku moja."
  • 13:12 - 13:17
    Ninasisitiza nini kwa kunukuu Maandiko haya, watu wa Mungu,
  • 13:17 - 13:20
    kuzungumza juu ya mada hii?
    Kwa sababu ni mwaka mpya.
  • 13:20 - 13:23
    Ni wakati tunafikiria mbele, tunapanga mipango.
  • 13:23 - 13:25
    Lengo ni lipi? Tutafanya nini?
  • 13:25 - 13:28
    Sipingani na mipango hiyo, narudia.
  • 13:28 - 13:33
    Mimi sihimizi uvivu.
    Mimi sihimizi uzembe.
  • 13:33 - 13:36
    Sikuhimii
    kukaa tu, kukunja mikono yako
  • 13:36 - 13:39
    na kutarajia mambo kushuka kutoka
    Mbinguni hadi mapajani mwako.
  • 13:39 - 13:51
    Ni vizuri kufanya mipango, lakini ni lazima tufanye hivyo kwa kutambua nafasi ya Mungu.
  • 13:51 - 14:00
    Ikiwa sivyo, unaweza kuanguka katika mtego wa kuwa na wasiwasi juu ya kesho au kujisifu kuhusu kesho.
  • 14:00 - 14:02
    Unaweza hata usijue,
  • 14:02 - 14:09
    lakini jinsi unavyoitikia
    mpango wako unapokatizwa itaonyesha hivyo.
  • 14:09 - 14:13
    Hii ni hatua ya kujichunguza,
    watu wa Mungu.
  • 14:13 - 14:18
    Umefanya mpango - 'Nataka kwenda hapa wakati huu; Nataka kufanya hivi katika biashara yangu.'
  • 14:18 - 14:24
    Je, unaitikiaje
    mpango huo unapokatizwa?
  • 14:24 - 14:34
    Mwitikio wako kwa kukatizwa kwa mpango wako unaonyesha ni mpango wa yupi unauamini hakika.
  • 14:34 - 14:37
    Je, unaanguka pale mipango yako inapoanguka?
  • 14:37 - 14:43
    Unaanza kunung'unika, kulalamika,
    kujilinganisha na wengine
  • 14:43 - 14:47
    na kujipima kwa
    viwango vilivyotengenezwa na mwanadamu.
  • 14:47 - 14:52
    Je, furaha yako huanguka pale
    mipango yako inapovunjika?
  • 14:52 - 14:57
    Je, amani yako husambaratika
    pale mpango wako unaposambaratika?
  • 14:57 - 15:01
    Inaonyesha hujaweka
    mpango wako mikononi mwa Mungu.
  • 15:01 - 15:06
    Kwa sababu kile unachokiona kama
    usumbufu katika mpango wako
  • 15:06 - 15:11
    kinaweza kuwa hatua kuelekea
    utimilifu wa mpango wa Mungu.
  • 15:11 - 15:15
    Mungu ni mkuu!
  • 15:15 - 15:19
    Anawatunza watoto wake.
  • 15:19 - 15:27
    Wakati mwingine kile unachokiona kama usumbufu kinaweza kuwa uingiliaji kati wa Mungu
  • 15:27 - 15:36
    kukuhifadhi, kukutayarisha, kukuimarisha, kukurekebisha, kukujenga kiroho.
  • 15:36 - 15:40
    Unachokiona kama
    usumbufu katika mpango wako
  • 15:40 - 15:46
    kinaweza kuwa hatua ya kutimiza mpango wa Mungu.
  • 15:46 - 15:56
    Lakini mara nyingi, mipango yetu inapoingiliwa, inapodukizwa,
  • 15:56 - 16:01
    tunaitikiaje? Je, tunajibuje?
  • 16:01 - 16:05
    Unajibu kwa imani au hofu?
  • 16:05 - 16:10
    Je, unajibu kwa
    utulivu au kulalamika?
  • 16:10 - 16:14
    Je, unatendaje
    mpango wako unapoingiliwa?
  • 16:14 - 16:16
    Umefanya kila
    linalowezekana kibinadamu.
  • 16:16 - 16:20
    Umetekeleza sehemu yako, lakini
    mambo yaliyo nje ya uwezo wako
  • 16:20 - 16:25
    yakaja na kuusambaratisha huo mpango.
    Je, unaitikiaje?
  • 16:25 - 16:32
    Ndiyo maana nilisema watu wa Mungu,
    mnapopanga mipango ya kesho,
  • 16:32 - 16:42
    fanya hivyo ukitambua maisha hayana uhakika, Mungu ni mwenye enzi na kila siku ina riziki yake.
  • 16:42 - 16:49
    Unapaswa kufanya nini?
    Zingatia neema ya leo.
  • 16:49 - 16:55
    Wengine tunahangaika sana kuhusu kesho, tunajishughulisha sana kufikiria kesho
  • 16:55 - 17:03
    kiasi kwamba hatusimamii ipasavyo, kukifanyia kazi kile kilicho mikononi mwetu leo.
  • 17:03 - 17:08
    Usitarajie tu
  • 17:08 - 17:13
    kwamba neema uliyo nayo leo itapatikana kwako kesho.
  • 17:13 - 17:24
    Usifikirie kuwa unachoweza kufikia leo, utaweza kukifikia kesho.
  • 17:24 - 17:29
    Mungu hutupa neema kwa kila siku.
  • 17:29 - 17:33
    Ndiyo maana ni lazima umwamini Yeye kila siku.
  • 17:33 - 17:37
    Ndiyo maana unahitaji kuwa na
    uhusiano naye.
  • 17:37 - 17:42
    Ndio, unapanga mipango yako. Ndiyo, unafanya kazi kwa bidii kuelekea utimizo huo.
  • 17:42 - 17:47
    Ndio, unatoa ubora wako ukiwa na
    ufahamu:
  • 17:47 - 17:52
    Nani mwenye kauli ya mwisho?
    Yehova ndiye mwenye kauli ya mwisho.
  • 17:52 - 17:54
    Unakumbuka wimbo huo!
  • 17:54 - 18:03
    Nani mwenye usemi wa mwisho
    Yehova ndiye mwenye usemi wa mwisho
  • 18:03 - 18:06
    Mungu ndiye mwenye neno la mwisho katika maisha yetu.
  • 18:06 - 18:10
    Mipango yetu si kuchukua nafasi yake.
  • 18:10 - 18:16
    Ukifanya mpango, uweke mikononi Mwake.
  • 18:16 - 18:21
    Hili ni neno langu la kutia moyo
    kwenu leo ​​watu wa Mungu.
  • 18:21 - 18:24
    Narudia, sikukatishi tamaa
    kufanya mpango huo.
  • 18:24 - 18:26
    Kwa kweli, ninahimiza!
  • 18:26 - 18:31
    Ukiwa Mkristo, tafakari kwa makini na kwa sala mwaka ujao.
  • 18:31 - 18:36
    Fanya mpango. Utafuteni uso wa Mungu kwa ajili yake. Ni nzuri!
  • 18:36 - 18:39
    Wakati mwingine watu huenda
    mbali sana kwa njia nyingine.
  • 18:39 - 18:44
    Wanasema, ‘Vema, kama Mungu
    ameniahidi hilo, basi
  • 18:44 - 18:48
    Yeye ndiye atakayeileta
    kwangu.' - kama hivyo.
  • 18:48 - 18:49
    Wacha niiweke kama hii:
  • 18:49 - 18:56
    Kumngoja Bwana si kisingizio
    cha kutokufanya sehemu yako.
  • 18:56 - 18:59
    'Namngoja Bwana kwa baraka hii.
  • 18:59 - 19:01
    Namngoja Bwana
    kwa ajili ya mafanikio hayo.
  • 19:01 - 19:05
    Ninamngojea Bwana
    ahadi hiyo itimie.' Nzuri!
  • 19:05 - 19:07
    Je, unamngojeaje Bwana kwa ufanisi?
  • 19:07 - 19:10
    Unatumia kile kilicho
    mikononi mwako leo.
  • 19:10 - 19:12
    Kumngoja Bwana si
    kisingizio cha uvivu.
  • 19:12 - 19:16
    Tusisingizie mambo ya kiroho juu ya usimamizi mbaya .
  • 19:16 - 19:25
    Mungu hatabariki uwakili usiowajibika kwa mafanikio.
  • 19:25 - 19:28
    Unaomba, 'Mungu, ibariki biashara yangu'
  • 19:28 - 19:32
    lakini unasimamia vibaya kile
    kilicho mikononi mwako leo.
  • 19:32 - 19:35
    Sala hiyo inawezaje kutimia?
  • 19:35 - 19:38
    Natumaini mtafuata ninachosema
    , watu wa Mungu.
  • 19:38 - 19:43
    Tumia kile kilicho mikononi mwako leo
    kwa neema ya leo.
  • 19:43 - 19:45
    Wacha niiweke kama hii:
  • 19:45 - 19:51
    Changanya kazi ngumu na
    imani tulivu kwa Mungu kwa siku zijazo.
  • 19:51 - 19:56
    Fanya bidii kuelekea ndoto yako. Ndoto yako haitafanya kazi kwa niaba yako.
  • 19:56 - 20:03
    Fanya bidii kuelekea mpango wako. Mpango wako
    hautapanda mbegu kwa ajili yako.
  • 20:03 - 20:10
    Lakini unapofanya kazi kwa bidii, unapotoa ubora wako, unafanya hivyo ukiwa na ufahamu -
  • 20:10 - 20:16
    maisha yangu yako mikononi mwa Mungu;
    nyakati zangu ziko mikononi mwa Mungu.
  • 20:16 - 20:22
    Acha nikusomee methali moja zaidi,
    wakati huu kutoka Mithali 16.
  • 20:22 - 20:29
    Mwenye hekima anaiweka wazi.
    Mithali 16:9 inasema hivi,
  • 20:29 - 20:36
    "Moyo wa mtu huifikiri njia yake,
    bali Bwana huziongoza hatua zake."
  • 20:36 - 20:42
    Mipango yako mikononi mwa Mungu.
  • 20:42 - 20:49
    Wana wa Mungu, liwekeni neno hili moyoni.
  • 20:49 - 20:57
    Unapoweka kila kitu mikononi mwa Mungu,
  • 20:57 - 21:03
    muda si mrefu utaiona
    mikono ya Mungu katika kila kitu.
  • 21:03 - 21:11
    Lazima uamini kwamba mkono Wake unafanya kazi
  • 21:11 - 21:19
    hata wakati huwezi
    kuyaona maandishi ya mkono Wake.
  • 21:19 - 21:26
    Labda sijui mwisho wa simulizi,
  • 21:26 - 21:32
    Lakini ninamwamini Mwandishi wa simulizi.
  • 21:32 - 21:37
    Naweza nisione taswira kamili.
  • 21:37 - 21:41
    Lakini ninamwamini Mpangaji Mkuu.
  • 21:41 - 21:44
    Naweza nisione bidhaa iliyokamilishwa.
  • 21:44 - 21:49
    Lakini ninamwamini Mbunifu wa Kimungu.
  • 21:49 - 21:53
    Huu ndio msimamo wetu kama Wakristo.
  • 21:53 - 21:58
    Ngoja ninukuu kitu
    alichosema Nabii TB Joshua
  • 21:58 - 22:01
    kufikisha ujumbe huu kwenye hitimisho.
  • 22:01 - 22:09
    Baada ya kufanya
    kila linalowezekana kibinadamu,
  • 22:09 - 22:15
    mwachie Mungu suala hilo ili aisahishe kazi yako.
  • 22:15 - 22:21
    Hivi ndivyo unavyoweka
    mipango yako mikononi mwa Mungu.
  • 22:21 - 22:27
    Shetani anataka tukazie fikira kile ambacho hatuna, na kukazia fikira kile ambacho hatujui.
  • 22:27 - 22:33
    Kwa sababu hii husababisha wasiwasi,
    malalamiko, usimamizi mbaya.
  • 22:33 - 22:37
    Lakini kama Mkristo, unajua nini?
    Mungu ni mwenye enzi. Mungu ni mwema.
  • 22:37 - 22:41
    Anaona picha kubwa zaidi.
  • 22:41 - 22:44
    Una nini? Neema kwa leo.
  • 22:44 - 22:53
    Tumia kile kilicho mikononi mwako leo na acha kila kitu mikononi mwake kwa ajili ya kesho.
  • 22:53 - 23:01
    Mungu abariki neno hili la kutia moyo katikati ya mioyo yetu.
Title:
MIPANGO YAKO MIKONONI MWA MUNGU! | Mahubiri ya Ndugu Chris
Description:

Je, tujipange vipi kwa ajili ya kesho bila kuingia katika mtego wa kujisifu kuhusu kesho au kuhangaikia kesho? Je, unapangaje mipango, kama Mkristo? Katika mahubiri haya halisia na Ndugu Chris yenye kichwa, 'Mipango Yako Mikononi mwa Mungu' - gundua jinsi ya kupanga mapema huku ukikumbuka ni nani aliye Mkuu - Yesu Kristo!

"Unapopanga mipango, lazima ufanye hivyo ukiwa na ufahamu wa mambo matatu:
1. Maisha hayana uhakika.
2. Mungu ni mwenye enzi kuu.
3. Kila siku ina riziki yake.

➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi Shirikishi - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
23:32

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions