< Return to Video

UPONYAJI kutoka kwa ARTHRITIS YA MAKALIO! | Ushuhuda wa Maombi ya Pamoja

  • 0:00 - 0:05
    Mungu alijidhihirisha kwa njia ya ajabu sana katika maisha yangu.
  • 0:05 - 0:08
    Baada ya maombi, nililala kama mtoto mchanga.
  • 0:08 - 0:15
    Sikuweza kuelewa ni nini kilikuwa kikiendelea. Usiku huo sikuchukua dawa zangu za kutuliza maumivu.
  • 0:15 - 0:18
    Ndipo asubuhi iliyofuata nilipoamka...
  • 0:25 - 0:39
    Hivi sasa, kwa kila dalili za ugonjwa ndani au nje,
  • 0:39 - 0:44
    uondolewe kwa jina la Yesu Kristo!
  • 0:44 - 0:51
    Uoshwei! Uoshwe leo!
  • 0:52 - 0:57
    Jina langu ni Eunice.
    Ninajiunga kutoka Afrika Kusini.
  • 0:57 - 1:06
    Nilikuwa na maumivu makali ya nyonga
    kwa takriban miaka mitatu.
  • 1:06 - 1:14
    Na kisha mbali na hayo, nilikuwa na pumu, shinikizo la damu, na tatizo la moyo.
  • 1:14 - 1:20
    Nilipowasiliana na madaktari kutokana na maumivu hayo,
    walisema nilikuwa na arthritis ya nyonga.
  • 1:20 - 1:24
    Na kisha, kama muuguzi,
    ilikuwa ngumu sana kwangu.
  • 1:24 - 1:28
    Iliniathiri vibaya sana kazini.
  • 1:28 - 1:32
    Kwa sababu mimi ni nesi, mara nyingi
    kazi yangu inanihitaji
  • 1:32 - 1:35
    kuwa ama amesimama au umeketi.
  • 1:35 - 1:40
    Na kutokana na maumivu hayo, kwa mimi kusimama kwa muda mrefu, ilikuwa shida.
  • 1:40 - 1:44
    Kukaa chini kwa muda mrefu ilikuwa shida.
  • 1:44 - 1:49
    Halafu hata hapa nyumbani, sikuweza kufanya kazi yoyote ngumu niliyozoea kufanya.
  • 1:49 - 1:52
    Ilikuwa ni kitu cha maumivu sana.
  • 1:52 - 1:56
    Wakati wa usiku, nyakati fulani nililazimika kuamka na kuketi.
  • 1:56 - 2:00
    Vinginevyo, ningelazimika
    kuchukua vidonge vya kulala.
  • 2:00 - 2:06
    Na kisha nikatumia dawa nyingi za kutuliza maumivu
    ili nipate usingizi.
  • 2:06 - 2:10
    Iliniathiri vibaya sana,
    haswa kazini kama nesi.
  • 2:10 - 2:14
    Maumivu hayakuvumilika;
    maumivu hayo yalikuwa mengi sana -
  • 2:14 - 2:16
    kiasi kwamba nilipoenda kushauriana na madaktari,
  • 2:16 - 2:21
    walinishauri kwamba itabidi
    nibadilishe makalio.
  • 2:21 - 2:28
    Na kisha, kama muuguzi, niliweza kuona kwamba
    singeweza kwenda kwa upasuaji kama huo.
  • 2:28 - 2:33
    Pia, nikitazama umri wangu, nilisema,
    'Hapana, sitafanya hivyo.
  • 2:33 - 2:38
    Ninamwamini Mungu kwa uponyaji wangu.
    Ninamwamini Mungu kwa muujiza.'
  • 2:38 - 2:42
    Mnamo Septemba 7, nilijiunga na
    Huduma ya Maombi ya Pamoja
  • 2:42 - 2:47
    baada ya kutuma ombi la maombi
    kwenye TV ya Moyo wa Mungu.
  • 2:47 - 2:51
    Ombi langu la maombi lilikuwa juu ya
    mafanikio yangu ya kifedha
  • 2:51 - 2:55
    na kisha mafanikio ya
    biashara ya wanangu wawili.
  • 2:55 - 3:00
    Sikuandika chochote kuhusu ugonjwa wangu katika ombi hilo la maombi,
  • 3:00 - 3:07
    lakini Mungu alijidhihirisha kwa namna ya ajabu sana katika maisha yangu.
  • 3:07 - 3:11
    Nilipojiunga na mkutano, Ndugu Chris alikuja na kutuombea.
  • 3:11 - 3:14
    Baada ya maombi, nililala kama mtoto mchanga.
  • 3:14 - 3:21
    Sikuweza kuelewa ni nini kilikuwa kikiendelea. Usiku huo sikuchukua dawa zangu za kutuliza maumivu.
  • 3:21 - 3:27
    Kisha asubuhi iliyofuata, nilipoamka - kwa sababu kuamka ilikuwa ngumu.
  • 3:27 - 3:32
    Nilipoamka, ilinilazimu kuketi kitandani kwa takribani dakika kumi kabla ya kusimama.
  • 3:32 - 3:35
    Asubuhi iliyofuata niliamka tu.
  • 3:35 - 3:38
    Nilikwenda bafuni.
  • 3:38 - 3:41
    Mwanzoni nilipuuza kisha nikajitayarisha kwenda kazini.
  • 3:41 - 3:46
    Siku hiyo, nilifanya kazi kama zamani.
  • 3:46 - 3:52
    Kwa hiyo niliporudi nyumbani, nilisema, 'Sawa, jana nilihudhuria Maombi ya Pamoja.
  • 3:52 - 3:56
    Nini kinatokea? Nimepona au vipi?'
  • 3:56 - 4:02
    Nilijaribu kuangalia maumivu kwani
    nilipogusa hapa niliweza kusikia uchungu.
  • 4:02 - 4:11
    Lakini wakati nikirudi kutoka kazini, nilikuwa nikitembea kwa madaha. Nilikuwa na nguvu sana.
  • 4:11 - 4:14
    Siku iliyofuata, nilikuwa na nguvu sana.
  • 4:14 - 4:16
    Maumivu hayakuwepo tena.
  • 4:16 - 4:20
    Mpaka leo, sina maumivu.
  • 4:20 - 4:29
    Sina dalili za pumu, matatizo ya moyo au shinikizo la damu - mpaka leo!
  • 4:29 - 4:37
    Kwa hiyo nataka kumpa Mungu utukufu wote
    kwa yale ambayo amefanya katika maisha yangu.
  • 4:37 - 4:41
    Hiyo inanionyesha kwamba Mungu
    anajua zaidi kuliko mimi.
  • 4:41 - 4:45
    Alinipa kile alichoona bora kwangu.
  • 4:45 - 4:52
    Nataka kumshukuru Ndugu Chris kwa kumruhusu Mungu amtumie kutuombea.
  • 4:52 - 4:57
    Na hapo nimeona kuwa hakika
    umbali sio kizuizi.
  • 4:57 - 5:03
    Kati ya Afrika Kusini na Uingereza, sijui ni maili ngapi - lakini maombi hayo...
  • 5:03 - 5:07
    sikujidhihirisha. sikuanguka.
    Sikufanya chochote.
  • 5:07 - 5:13
    Lakini baada ya maombi, nililala tu kama mtoto mchanga hadi asubuhi iliyofuata.
  • 5:13 - 5:18
    Kwa hiyo namshukuru sana Mungu kwa yale
    aliyonitendea katika maisha yangu.
  • 5:18 - 5:20
    Hakuna maumivu zaidi - hakuna kitu!
  • 5:20 - 5:30
    Naweza kupinda. Naweza kuchuchumaa. Naweza kuruka.
    Hakuna maumivu tena!
  • 5:30 - 5:33
    Baada ya kujiunga na Huduma ya Maombi ya Pamoja na Ndugu Chris,
  • 5:33 - 5:39
    Nina hiyo amani ya akili,
    amani ya Mungu - amani ya ndani.
  • 5:39 - 5:44
    Ninahisi utulivu huo;
    Nina amani katika kila kitu.
  • 5:44 - 5:48
    Neno langu la ushauri ni -
    tumwamini Mungu
  • 5:48 - 5:51
    kwa maana hakuna ugonjwa
    ambao Mungu hawezi kuuponya.
  • 5:51 - 5:56
    Na wakati wa Mungu ni bora zaidi. Haijalishi ni changamoto gani unapitia,
  • 5:56 - 5:58
    Mungu amefanya kwa ajili yangu na
  • 5:58 - 6:03
    Ninaamini ya kwamba atafanya hivyo kwa mtu ye yote aliyejiunga leo.
  • 6:03 - 6:09
    Haijalishi ugonjwa au chochote ambacho mtu yeyote anaweza kuwa anapitia leo,
  • 6:09 - 6:15
    mwamini Mungu tu kwa muujiza na utaupokea kwa jina kuu la Yesu.
  • 6:15 - 6:19
    Ninajua kuwa mazuri hayatoshi. Yaliyo bora zaidi bado yanakuja.
Title:
UPONYAJI kutoka kwa ARTHRITIS YA MAKALIO! | Ushuhuda wa Maombi ya Pamoja
Description:

Eunice, nesi kutoka Afrika Kusini, hata hakutaja ugonjwa wake katika ombi la maombi alilotuma kwa God's Heart TV - lakini baada ya kujiunga na Ibada ya Pamoja ya Maombi na Ndugu Chris, alipata muujiza wa ajabu! Tunaomba ushuhuda wake ukachochee imani yako kwa Mungu, kwa maana hakuna ugonjwa asioweza kuuponya!

Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom

➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Mwingiliano - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
06:49

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions