Ishi kama unakufa? Kutenda katika mashaka | Ariel Dempsey | TEDxMSU
-
0:04 - 0:36(Muziki unacheza:"A Million Dreams")
-
2:31 - 2:33(Makofi)
-
2:39 - 2:41Ngoja nivute pumzi kidogo ...
-
2:44 - 2:47lakini nitakuambia kipi ni, kinafurahisha sana,
-
2:47 - 2:48Ni kweli
-
2:50 - 2:54wimbo nilioucheza unaitwa
"Ndoto Millioni Moja" -
2:54 - 2:57Unatoka katika muvi
ninayoipenda, iitwayo " -
2:58 - 3:00Wakati mwingine tunaweza
kuziona ndoto zetu dhahiri, -
3:01 - 3:04lakini wakati mwingine mambo
hayako wazi sana, -
3:05 - 3:07Je naweza kuamini katika hii?
-
3:08 - 3:11Najuaje kuwa uthubutu huu una faida?
-
3:11 - 3:13Inakuwaje kama siko sahihi?
-
3:14 - 3:17Kwangu , haya si maswali ya kufikirika tu.
-
3:17 - 3:19Ni maswali ninayoishi nayo.
-
3:20 - 3:22Ngoja niwashirikishe kidogo
kuhusu chimbuko langu. -
3:23 - 3:24Jina langu ni Ariel,
-
3:24 - 3:27Ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa
udaktari katika chuo cha Jimbo la Michigan, -
3:27 - 3:29Ninakaribia kuhitimu na shahada ya Udaktari
-
3:29 - 3:33na ninafanya Shahada ya Udaktari
wa Falsafa ya sayansi na dini katika chuo cha Oxford. -
3:34 - 3:37Ninataka kuwa daktari wa kuondoa
maumivu ya mwili -
3:37 - 3:40na kuwa pamoja na watu katika
mwisho wa maisha yao. -
3:40 - 3:43na pia nataka kuwa mawanazuoni wa theolojia
-
3:43 - 3:46na kuchukua rasilimali za tamaduni zetu za kidini
-
3:46 - 3:48katika huduma za afya.
-
3:49 - 3:53kwa hiyo kama mwanafunzi wa
utabibu na theolojia -
3:53 - 3:56Nimekuwa na muda wa kutafakari
kuhusu tasnia hizi mbili -
3:56 - 4:00ambazo zinakutana na tashwishi nyingi.
-
4:00 - 4:02katika utabibu na dini,
-
4:02 - 4:04Kuna nyakati ambazo tunatenda,
-
4:04 - 4:07hata pale ambapo hatuwezi kuona.
-
4:08 - 4:10Nitakueleza kitu usiku huu wa leo
-
4:10 - 4:15Kuwa nimetunza siri mbali na
marafiki zangu wa karibu - -
4:16 - 4:18hata wale marafiki ambao
nimewaalika hapa usiku huu. -
4:19 - 4:21Ingawa ni ngumu kuongelea
habari zake, -
4:21 - 4:23Nitawaeleza habari yangu.
-
4:24 - 4:26(Anavuta pumzi kubwa)
-
4:29 - 4:31Januari, 2015
-
4:31 - 4:33Nilikuwa nasafiri kwa ndege
kwenda Uingereza. -
4:33 - 4:36Nilikuwa nimetoka kufanya usaili wa
chuo cha udaktari katika chuo cha Jimbo la Michigan -
4:36 - 4:39nilikuwa narudi katika chuo cha Oxford
kwa ajili ya masomo ya theolojia. -
4:40 - 4:43Ghafla, maumivu makali yakanipata kichwani,
-
4:43 - 4:45nikaanza kutapika sana,
-
4:45 - 4:48mapigo ya moyo na shinikizo la damu vikashuka sana,
-
4:48 - 4:52na nikaanza kupoteza na kurudiwa na fahamu.
-
4:52 - 4:55Ndege ilipotua, nilikimbizwa hospitalini,
-
4:55 - 5:01na wiki kadhaa, sikuwa na nguvu ya kusimama,
kuwaza,au hata ya kuwa macho. -
5:02 - 5:04Kwa miezi minne,
-
5:04 - 5:07nililala kitandani katika chumba chenye giza cha Uingereza.
-
5:08 - 5:09Mapazia yalifungwa,
-
5:09 - 5:11taa zikazimwa,
-
5:11 - 5:16na nikavaa miwani ya giza kwa kuwa sikuweza kuvumilia mwanga wowote.
-
5:17 - 5:20Chochote kilichotokea katika ndege
-
5:20 - 5:22kiliniacha katika mshtuko,
-
5:22 - 5:26lakini matokeo yangu ya MRI yalinishangaza
kwa namna ya nyingine. -
5:27 - 5:30Mama yangu, ambaye alisafiri kuja
Uingereza kuniuguza -
5:30 - 5:31alikuwa pembeni yangu
-
5:31 - 5:34wakati daktar alipokuwa anafafanua
matokeo ya picha ya ubongo, -
5:36 - 5:39Akaonyesha alama nyeusi inayotoa damu katikati,
-
5:39 - 5:41na akasema,
-
5:41 - 5:43"Ariel,
-
5:43 - 5:45Una shida ya cavernoma
-
5:45 - 5:48au tatizo katika mishipa ya damu ya ubongo.
-
5:48 - 5:50inavuja
-
5:50 - 5:52na mara ikianza kutoa damu
-
5:52 - 5:54itaendelea mara kwa mara kuta damu.
-
5:54 - 5:58na kila damu inapoanza kutoka
kunaweza kusababisha ulemavu. -
5:59 - 6:00pia inawezekana
-
6:00 - 6:03mishipa yako ikapasuka ghafla,
-
6:04 - 6:05na kama hii ikitokea,
-
6:05 - 6:07unaweza kufa mara moja,"
-
6:09 - 6:11Na akanipa takwimu mbaya,
-
6:11 - 6:15nikauliza nina muda gani umebaki wa kuishi.
-
6:15 - 6:17Akasema hajui.
-
6:19 - 6:20Usiku ule, katika giza,
-
6:20 - 6:21mama yangu na mimi tukalala kitandani,
-
6:21 - 6:22tukalia
-
6:22 - 6:25na tukacheka ubaya wa yote hayo.
-
6:26 - 6:28Kupoteza kumbukumbu na nguvu ya viungo
-
6:28 - 6:30au kifo cha ghafla.
-
6:30 - 6:33Kama vile , kitu gani kingine kibaya kinaweza kutokea?
-
6:34 - 6:35ninakumbuka
-
6:35 - 6:37nikiwa nimelala katika giza
-
6:37 - 6:39huku chumba kikiwa kinazunguka na nikiwa na miwani yangu,
-
6:40 - 6:42na sikuweza kuona
-
6:43 - 6:45sikuweza kuona maisha yangu yajayo
-
6:46 - 6:49maisha niliyokuwa nikiyaota yaliondoka
-
6:51 - 6:53niliamka asubuhi iliyofuata nikiwa na huzuni,
-
6:54 - 6:56na nilipokuwa ninaomba,
-
6:56 - 6:58nikagundua kitu kilichobadilisha maisha yangu
-
7:00 - 7:01niligundua kuwa
-
7:02 - 7:05sina tofauti na mtu yeyote mwingine.
-
7:06 - 7:08yoyote anayeishi maisha marefu
-
7:08 - 7:12anapoteza uwezo wa kumbukumbu na viungo.
-
7:12 - 7:14Kila mtu atakufa siku moja,
-
7:14 - 7:16na hakuna ajuaye siku hiyo.
-
7:17 - 7:22maisha yetu yote ni mateke na yamejaa mashaka
-
7:24 - 7:25ninogopa
-
7:26 - 7:29lakini sina mashaka zaidi ya mtu yeyote mwingine
-
7:31 - 7:33kwa hiyo nikakubaliwa kujiunga na chuo cha udaktari,
-
7:33 - 7:36lakini kama nitakufa ndani ya mwaka,
-
7:36 - 7:38kwa kujisumbua kwenda?
-
7:39 - 7:41Rafiki yangu wa karibu alikuja kunitembelea,
-
7:41 - 7:44nikamuuliza nifanye nini.
-
7:45 - 7:46Akasema,
-
7:47 - 7:48"Ariel,
-
7:48 - 7:50ishi kama vile unaenda kufa,
-
7:50 - 7:52Jaribu kujifunza vitu vingi kadiri iwezekanavyo
-
7:52 - 7:55na raha nyingi kadiri iwezekanavyo,"
-
7:56 - 8:00Lakini nilijua , "kuishi kama ninakufa"
-
8:00 - 8:02haitakuwa njia yangu.
-
8:03 - 8:04nisingekuwa na furaha kikamilifu.
-
8:05 - 8:07nikafunga macho yangu nisione majibu ya vipimo,
-
8:07 - 8:10nikijisahaulisha na jambo moja hadi jingine,
-
8:10 - 8:13nikijaribu kujipatia raha maishani.
-
8:14 - 8:15Pamoja na hayo,
-
8:16 - 8:19umejaribu kuishi kama vile unaenda kufa?
-
8:20 - 8:22Inachosha
-
8:23 - 8:26ningependa kuishi kama ...
-
8:26 - 8:28ninaishi.
-
8:30 - 8:32Mchungaji wangu alikuja kunipaka mafuta,
-
8:32 - 8:34Nikamuuliza natakiwa kufanya nini.
-
8:34 - 8:36Akasema,
-
8:36 - 8:38"Ariel,
-
8:38 - 8:40sitakwambia nini cha kufanya,
-
8:40 - 8:42lakini nitakwambia hivi,
-
8:42 - 8:44Mungu anajitosheleza,
-
8:44 - 8:48Usiache majibu haya yakutoe katika mstari."
-
8:50 - 8:51Wakati huo,
-
8:51 - 8:55nikaamua kuendelea na njia ambayo nilihisi kuitiwa.
-
8:56 - 8:58nikaamua kufanya kile ambacho ningefanya
-
8:58 - 9:00kama nisingepata majibu haya.
-
9:01 - 9:03kama maisha yangu ni igizo
-
9:03 - 9:05na najiandaa kupanda kuigiza
-
9:05 - 9:07pazia linaweza kufunguliwa muda wowote
-
9:07 - 9:10na nitakutwa nikicheza sehemu yangu vizuri.
-
9:11 - 9:13nikapata ujasiri wa kuchukua hatua.
-
9:15 - 9:18Lakini mwili wangu ukawa unaenda
taratibu kuliko nilivyotaka. -
9:18 - 9:20nilikuwa mwanamichezo maisha yangu yote -
-
9:20 - 9:22Nilikuwa mwanariadha katika
Chuo kikuu cha Michigan; -
9:22 - 9:24Nikacheza kandanda nikiwa chuo kikuu cha Oxford
-
9:24 - 9:28Lakini sasa, nikahisi mwili wangu ukinisaliti,
-
9:28 - 9:30kama vile sikuweza kuuamini kufanya kazi.
-
9:32 - 9:33Ingawa nilikuwa nimechoka,
nilijifanya kama nina nguvu kuliko hali halisi -
9:33 - 9:34Kwa hiyo,
-
9:34 - 9:37Nikafanya mazoezi ya yoga ya bibi kizee -
-
9:37 - 9:38kama hivi -
-
9:38 - 9:40na nikafanya hivi kila siku,
-
9:40 - 9:42hata kama itakuwa kwa dakika chache,
-
9:43 - 9:45sikuweza kufanya vitu vingi,
-
9:45 - 9:46lakini niliweza kulala sakafuni
na kujinyoosha mara moja, -
9:48 - 9:49ningeweza kusoma ukurasa huo mmoja,
-
9:49 - 9:53Ningeweza kupata wakati mmoja wa furaha.
-
9:53 - 9:55na kuna wakati nilifanya zaidi.
-
9:55 - 9:59Taratibu, nikaweza kujinyoosha
-
9:59 - 10:02na kucheka kwa nguvu
-
10:02 - 10:06na kupenda zaidi.
-
10:06 - 10:07nikashikilia tafakari kutoka katika
kitabu cha Common Prayer -
10:08 - 10:09Kinasema,
-
10:11 - 10:14"Leo ni siku nyingine, ee Bwana,
-
10:14 - 10:16Sijui kipi kitatokea,
-
10:17 - 10:19Lakini nifanye niwe tayari, Bwana,
-
10:20 - 10:22Kwa chochote kitakachotokea,
-
10:22 - 10:24Kama nitaweza kusimama
-
10:24 - 10:26niwezeshe kusimama kishujaa.
-
10:26 - 10:28Kama nitakaa,
-
10:28 - 10:30nisaidie kukaa kimya,
-
10:31 - 10:32Kama nitakaa kimya,
-
10:32 - 10:34nisaidie kuwa na uvumilivu
-
10:35 - 10:36Na kama sitakiwi kufanya chochote
-
10:36 - 10:38nisaidie kutofanya kitu kwa ujasiri.
-
10:39 - 10:41Fanya maneno haya kuwa zaidi ya maneno,
-
10:41 - 10:44na naomba roho ya Yesu.
-
10:44 - 10:47Amen,"
-
10:47 - 10:49Kwa neema ya Mungu,
-
10:49 - 10:50Nikaanza masomo ya udaktari
wakati wa vuli. -
10:51 - 10:53Masomo ya udaktari hayakuwa rahisi.
-
10:53 - 10:56Siku ya kwanza,
-
10:57 - 10:59Rafiki yangu kipenzi kutoka shule
ya Sekondari aliniendesha kwena chuoni -
10:59 - 11:00kwa sababu nilikuwa bado
siwezi kuendesha -
11:00 - 11:02nikaingia katika usaili
-
11:02 - 11:04nikiwa nimevaa miwani.
-
11:04 - 11:06kwa sababu ya jeraha katika ubongo,
-
11:06 - 11:08kusoma ilikuwa shida
-
11:08 - 11:10na sikuweza kufikiri vizuri
au kujisomea kama zamani. -
11:10 - 11:11Katika siku nilizohisi kuwa naumwa
-
11:11 - 11:14na kuchoka kujisomea,
-
11:15 - 11:17Kwa nini, " ninafanya hili
kama nitakufa kesho"? -
11:17 - 11:18Je unajua,
-
11:19 - 11:23ni mwanafunzi gani wa udaktari aiyeuliza swali
hilo katika wakati fulani? -
11:24 - 11:25(Vicheko)
-
11:25 - 11:28Masomo ya udaktari yalinikumbusha
kuhusu mashaka. -
11:28 - 11:29Kutokea MRI mpaka maabara
ya cadaver. -
11:29 - 11:33Katika chumba cha wagonjwa mahututi,
-
11:34 - 11:37nilimuhudumia binti wa rika langu
ambaye alikuwa anatoka damu katika uvimbe. -
11:37 - 11:38Alikuwa amepooza
na kiufahamu kama mtoto wa miaka mitano -
11:38 - 11:42majibu yangu niliyafanya kuwa siri kwa
watu wengi -
11:43 - 11:46Kwa sababu sikutaka watu wanitambulishe nayo
-
11:47 - 11:50Lakini kuna nyakati,
-
11:50 - 11:53siri yangu ilikuwa ni upweke
-
11:53 - 11:55na mashaka yalijaa giza.
-
11:55 - 11:57Lakini taratibu, nikatiwa nguvu.
-
11:57 - 12:00Unifikirie vibaya, haikuwa rahisi.
-
12:01 - 12:03kulikuwa na nyakati nyingi za kushuka na kupanda.
-
12:03 - 12:06Lakini kwa wakati, yoga ya bibi kizee
-
12:06 - 12:08ikabadilika na kuwa yoga kamili
-
12:08 - 12:13na acroyoga
-
12:13 - 12:15na yoga ya juu
-
12:15 - 12:17na hariri ya juu.
-
12:17 - 12:18Dansi la juu kwangu likawa ni alama
ua uzuri kutoka majonzi yangu. -
12:19 - 12:20ikawa ni kikumbusho
-
12:23 - 12:28ya furaha na shukrani
-
12:29 - 12:31ambayo inaangaza maisha yangu,
-
12:31 - 12:33na kama taswira ya ufufuko.
-
12:33 - 12:34kwa hiyo, kitabibu, niko wapi kwa sasa?
-
12:35 - 12:38Sijui.
-
12:39 - 12:42Ninajua nina uvimbe wa cavernoma.
-
12:44 - 12:46najua ulitoa damu hapo kabla.
-
12:47 - 12:49sijui kama utatoa damu tena.
-
12:49 - 12:51labda nitaishi miaka 80,
-
12:52 - 12:53nikiwa na maisha kamili ya afya.
-
12:55 - 12:57labda haitawezekana.
-
12:57 - 12:59Lakinibado nashikilia tafakari ile
kutoka kitabu cha maombi cha Common Prayer, -
13:00 - 13:01na kuishi katika mashaka.
-
13:03 - 13:07ninakumbuka kwa undani
-
13:07 - 13:09kuhusu ushauri wa Sir William Osler, Baba
Utabibu wa Kisasa, -
13:10 - 13:12ambao aliutoa kwa wanafunzi wake wa udaktari.
-
13:12 - 13:16Akasema,
-
13:16 - 13:18"Kazi yetu si kuangalia kipi kipo gizani kwa mbali
-
13:18 - 13:20lakini kufanya kilicho sahihi hapa karibu."
-
13:21 - 13:25Je kufanya kilicho sahihi sasa
-
13:25 - 13:28na kuona wakti ujao kwa mbali
-
13:29 - 13:32kunakuwaje?
-
13:32 - 13:34Nahisi inaonekana kama kudansi
na hariri ukiwa na kitambaa usoni, -
13:34 - 13:35kama kuzunguka angani,
-
13:36 - 13:39bila kujua uko wapi,
-
13:39 - 13:41Kipi kinachokuwa nawe mkononi?
-
13:41 - 13:44naweza kuzungusha hivi,
-
13:44 - 13:46naweza kufunga hivi.
-
13:46 - 13:48naweza kuachia kama hivi.
-
13:48 - 13:50siwezi kuona,
-
13:50 - 13:52lakini naweza kufanya -
-
13:53 - 13:54nikidansi katika mashaka
-
13:55 - 13:56bila kujali tunazungumzia utabibu au dini
-
13:57 - 14:00au mahusiano au shule au kazi
-
14:02 - 14:06au ndoto zetu
-
14:06 - 14:10au hata muda wa kifo chetu chenyewe
-
14:10 - 14:11wote tunaishi katika mashaka
-
14:11 - 14:14majibu yangu ya vipimo yananikumbusha kuwa
maisha hayana uhakika. -
14:15 - 14:18Lakini labda,
-
14:20 - 14:24maisha hayahitaji hakika
-
14:25 - 14:26ili kuyaishi
-
14:26 - 14:28wote tunaona lakini kwa hafifu
-
14:28 - 14:30Na kama vile daktari mzuri
Osler anavyotukumbusha, -
14:32 - 14:34wote tunaweza kufanya kile kilicho dhahiri.
-
14:35 - 14:38labda
-
14:38 - 14:42tunaweza kufanya,
-
14:44 - 14:45hata
-
14:45 - 14:47pale tusipoona.
-
14:48 - 14:49(Muziki wa: "A Million Dreams")
-
14:49 - 14:51(Cheers)
-
15:17 - 15:20(Makofi)
- Title:
- Ishi kama unakufa? Kutenda katika mashaka | Ariel Dempsey | TEDxMSU
- Description:
-
Linapokuja suala la kufuatilia maono yetu, ni rahisi kuhisi kushindwa kufanya kitu kutokana na mashaa; tunawezaje kupata ujasiri wa kutenda, hata pale tusipoweza kuona?
Ariel Dempsey shares a story she has kept secret from many: her story of receiving a terminal diagnosis and recovering from traumatic brain injury. As a medical student at Michigan State and a PhD student in science and religion at Oxford, she draws on both medicine and spirituality to reflect on living with uncertainty. She embodies her message in a beautiful and inspiring performance danced in aerial silks.
Ariel Dempsey ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa udaktari ambaye anakaribia kuhitimu kutoka chuo kikuu cha Jimbo la Michigan akiwa na shahada ya Udaktari na akielekea kukamilisha shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) katika sayansi na dini katika chuo kikuu cha Oxford. Anatazamia kuwa daktari wa kuhudumia watu wasiojiweza akihusisha elimu ya udaktari na ya dini. Ukiacha masomo yake, Ariel anapenda dansi la kuzunguka angani na sanaa ya sarakasi. Ni sehemu ya kikundi huko Grand Rapids kiitwacho Bangarang Circus na amesafiri pwani ya California akitumbuiza mitaani kuchangisha pesa kwa ajili ya kusaidia shirika la WorldVision na kuchangisha pesa kwa ajili ya huduma za Afya.
Mazungumzo haya yalifanyika katika tukio la TEDx kwa kutumia muundo wa mkutano wa TED lakini likiandaliwa na jamii ya watu wa eneo husika. Jifunze zaidi hapa https://www.ted.com/tedx
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDxTalks
- Duration:
- 17:36
![]() |
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for Live like you're dying? Acting in uncertainty | Ariel Dempsey | TEDxMSU | |
![]() |
Joyce Nyakale accepted Swahili subtitles for Live like you're dying? Acting in uncertainty | Ariel Dempsey | TEDxMSU | |
![]() |
Joyce Nyakale edited Swahili subtitles for Live like you're dying? Acting in uncertainty | Ariel Dempsey | TEDxMSU | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Live like you're dying? Acting in uncertainty | Ariel Dempsey | TEDxMSU | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Live like you're dying? Acting in uncertainty | Ariel Dempsey | TEDxMSU | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Live like you're dying? Acting in uncertainty | Ariel Dempsey | TEDxMSU | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Live like you're dying? Acting in uncertainty | Ariel Dempsey | TEDxMSU | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Live like you're dying? Acting in uncertainty | Ariel Dempsey | TEDxMSU |