< Return to Video

INATOSHA KABISA kuwa na huduma ya midomo bila ya huduma ya maisha!

  • 0:00 - 0:03
    Kipindi cha Mwaka Mpya ni kipindi muhimu sana,
  • 0:03 - 0:07
    sio kusherehekea tu, mshukuru Mungu na kufurahi.
  • 0:07 - 0:10
    Pia ni fursa ya kutafakari
  • 0:10 - 0:12
    katika mwaka unaotoka
  • 0:12 - 0:15
    na maandalizi ya mwaka ujao,
  • 0:15 - 0:19
    kwa sababu kutathmini maisha yetu ni jambo jema.
  • 0:19 - 0:24
    Mambo machache ni hatari zaidi kuliko mtu
  • 0:24 - 0:28
    mwenye maisha yasiyo na tathmini.
  • 0:28 - 0:31
    Matokeo ya kujitathmini kwetu yataamua sisi ni watu wa aina gani.
  • 0:31 - 0:34
    itaamua sisi ni watu wa aina gani.
  • 0:34 - 0:39
    ikiwa tunjitathmini wenyewe kwa dhati,
  • 0:39 - 0:44
    Ninaamini kuwa matokeo ya tafakari yetu
  • 0:44 - 0:47
    yatatuongoza kwenye hitimisho
  • 0:47 - 0:52
    kwamba inatosha.
  • 0:52 - 0:58
    Ukitaka kuwa Mkristo, uwe Mkristo.
  • 0:58 - 1:03
    Inatosha kuhudhuria kanisani
  • 1:03 - 1:06
    bila toba ya kweli.
  • 1:06 - 1:07
    Inatosha
  • 1:07 - 1:10
    kwa neno la maombi katika vinywa vyetu
  • 1:10 - 1:14
    bila Neno la Mungu mioyoni mwetu.
  • 1:14 - 1:19
    Inatosha kutoa huduma ya mdomo
  • 1:19 - 1:21
    bila huduma ya maisha.
  • 1:21 - 1:23
    Watu wa Mungu, inatosha
  • 1:23 - 1:26
    kwa dini ya maneno bila
  • 1:26 - 1:28
    hatua inayolingana
  • 1:28 - 1:30
    kutoka katika uhusiano.
  • 1:30 - 1:32
    Inatosha sisi kuja kanisani
  • 1:32 - 1:36
    Jumapili na kuhamasishwa, kupewa motisha, kupata msukumo
  • 1:36 - 1:38
    katika huduma, katika mahubiri lakini
  • 1:38 - 1:41
    kisha turudi katika tabia zetu mbaya siku ya Jumatatu,
  • 1:41 - 1:43
    tushindwe na fikra zetu Jumanne,
  • 1:43 - 1:46
    kuzama katika udhaifu wetu siku ya Jumatano.
  • 1:46 - 1:47
    Inatosha.
  • 1:47 - 1:50
    Hatuwezi kuendelea hivi.
  • 1:50 - 1:55
    Inatosha kwa sisi kumridhisha mtu
  • 1:55 - 1:56
    na wakati huo huo kudai
  • 1:56 - 1:58
    kwamba tunajaribu kumpendeza Mungu.
  • 1:58 - 2:00
    Tutaendelea mpaka lini kupasha joto
  • 2:00 - 2:02
    viti katika makanisa yetu?
  • 2:02 - 2:04
    Kwa muda gani?
  • 2:04 - 2:08
    Kuja kanisani kukaa tu kuonekana,
  • 2:08 - 2:11
    kuzungumza ili kusikilizwa, kutembea ili kutambuliwa,
  • 2:11 - 2:13
    kutoa ili kusifiwa.
  • 2:13 - 2:17
    Wakati Yesu, Mkuu wa kanisa,
  • 2:17 - 2:21
    anaangalia nia nyuma ya matendo yako.
  • 2:21 - 2:25
    Mwambie jirani yako, "Inatosha!"
Title:
INATOSHA KABISA kuwa na huduma ya midomo bila ya huduma ya maisha!
Description:

“Kipindi cha Mwaka Mpya ni kipindi muhimu sana, si kusherehekea tu, kumshukuru Mungu na kushangilia. Pia ni fursa ya kutafakari mwaka unaoisha na maandalizi ya mwaka ujao, kwa sababu kutathmini maisha yetu ni jambo jema. Vitu vichache ni hatari zaidi kuliko mtu aliye na maisha yasiyo na tathmini. Matokeo ya kujitathmini kwetu yataamua sisi ni watu wa aina gani. Tukijitathmini kwa dhati, naamini kuwa matokeo ya tafakari yetu yatatufikisha kwenye hitimisho kwamba inatosha. Ukitaka kuwa Mkristo, uwe Mkristo. Inatosha kuhudhuria kanisa bila toba ya kweli. Inatosha kwa neno la maombi katika vinywa vyetu bila Neno la Mungu mioyoni mwetu. Inatosha kutoa huduma ya mdomo bila ya huduma ya maisha. Enyi watu wa Mungu, inatosha kwa dini ya maneno bila matendo yanayolingana yanayotokana na uhusiano. Inatosha kwetu kuja kanisani siku ya Jumapili ili kuhawihika, kutiwa motisha, kuhamasishwa katika ibada, katika mahubiri lakini kisha turudi kwenye tabia zetu mbaya siku ya Jumatatu, tushindwe na hisi zetu siku ya Jumanne, kuzama katika udhaifu wetu siku ya Jumatano. Inatosha. Hatuwezi kuendelea hivi. Inatosha sisi kumfurahisha mwanadamu na wakati huo huo kudai kwamba tunajaribu kumpendeza Mungu. Je, tutaendelea kupasha joto viti katika makanisa yetu hadi lini? Kwa muda gani - kuja kanisani ili tu kuketi ili kuonekana, kuzungumza ili kusikilizwa, kutembea ili kutazamwa, kutoa ili kusifiwa - wakati Yesu, Mkuu wa kanisa, hutazama nia iliyo nyuma ya matendo yako.

Unaweza kutazama ujumbe kamili kutoka kwa Kaka Chris hapa - https://www.youtube.com/watch?v=Xy7_JSK6tdQ

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
02:26

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions