RACINE & RUTH: UNGANA NASI KATIKA CHUO KIKUU CHA MUNGU!
-
0:00 - 0:07[muziki]
-
0:08 - 0:12Je! unajua kuwa wewe ni kazi ya sanaa?
-
0:12 - 0:14Mwanadamu ndiye zao kuu la Mungu.
-
0:14 - 0:16Ninamaanisha, mtu aliyeundwa kufikiria,
-
0:16 - 0:20kuzungumza na kutenda pamoja na Mungu.
-
0:20 - 0:22Je, unaishi sambamba na Mungu?
-
0:22 - 0:25Je, hali yako ikoje mbele za Mungu leo?
-
0:25 - 0:28Bila neema ya Roho Mtakatifu inayokaa ndani yake,
-
0:28 - 0:33mwanadamu ni kivuli tu cha yule aliyeumbwa na Mungu!
-
0:33 - 0:35Mwanadamu ambaye Mungu alimuumba
-
0:35 - 0:37hakuwa mtu wa kimwili tu
-
0:37 - 0:40anayetawaliwa na hisi zake
-
0:40 - 0:42bali ni mjumbe kati ya ulimwengu
-
0:42 - 0:45unaoonekana na usioonekana.
-
0:45 - 0:48Mungu na mwanadamu walikuwa wakizungumza
-
0:48 - 0:50pamoja kama marafiki.
-
0:50 - 0:52Lakini siku moja, mwanadamu
-
0:52 - 0:56alivunja uhusiano kwa kutokutii
-
0:56 - 0:58na akaenda mbali na Mungu.
-
0:58 - 1:01Kisha akaenda mbali zaidi hadi,
-
1:01 - 1:03mwishowe akaondoka nyumbani.
-
1:03 - 1:05Aliiacha nchi yake ya asili, Edeni,
-
1:05 - 1:07ambako aliishi na Mungu.
-
1:07 - 1:12Alihama kutoka kwenye uwepo wa Mungu.
-
1:12 - 1:14Tangu wakati huo, Mungu amekuwa
-
1:14 - 1:16na shauku ya kuweza
kuzungumza tena -
1:16 - 1:19na rafiki yake wa zamani
-
1:19 - 1:20lakini mwanadamu,
-
1:20 - 1:23kwa kuondoka katika uwepo wa Muumba wake,
-
1:23 - 1:25alipoteza lugha yake mama.
-
1:25 - 1:29Namaanisha, alipoteza lugha yake
ya asili na Mungu. -
1:29 - 1:34Na akawa hawezi kuwasiliana na
Muumba wake katika roho na kweli. -
1:34 - 1:38Mwanadamu wa kawaida hawezi kusikia
au kuzungumza na Mungu; -
1:38 - 1:43hii ndiyo changamoto tunayokabiliana
nayo leo. -
1:43 - 1:46Ingawa Mungu huzungumza tena na tena,
-
1:46 - 1:49wengi sana hawapo makini kusikia
kile Anachosema (Ayubu 33:14). -
1:49 - 1:52Ukimya ni mgumu kwa Mungu.
-
1:52 - 1:56Kama vile baba wa mwana mpotevu
-
1:56 - 1:58alivyokuwa na shauku ya kumwona
mwanawe akirudi nyumbani, -
1:58 - 2:02Mungu ana shauku ya kuwa na uhusiano
wa karibu tena na mwanadamu, -
2:02 - 2:04Rafiki yake wa zamani.
-
2:04 - 2:07Ndiyo maana ilimbidi achague lugha
-
2:07 - 2:09ambayo mwanadamu angeelewa.
-
2:09 - 2:13Kwa hivyo alimtuma Mwanawe,
Yesu Kristo duniani kumrudisha mwanadamu, -
2:13 - 2:18Rafiki Yake wa zamani, arudi Kwake tena.
-
2:18 - 2:22Mungu aliheshimu lugha ya mwanadamu
kwa kumwita Yesu Neno. -
2:22 - 2:26Neno alifanyika mwili na akaingia
ulimwenguni. -
2:26 - 2:29Yesu ni Mungu akijieleza Mwenyewe
-
2:29 - 2:33kwa lugha ambayo mwanadamu
anaweza kuelewa, -
2:33 - 2:36lugha ya roho na uzima (Yohana 6:63).
-
2:36 - 2:39Je, ni kwa muda gani tutaendelea kuwaza,
-
2:39 - 2:41kuzungumza na kuishi katika hali
ya kimwili -
2:41 - 2:45ilihali Yesu anakungoja katika mahala
pa Roho Wake? -
2:45 - 2:48Ni wasaa wa kurudi tena katika chuo
cha Mungu -
2:48 - 2:52Na kuanza kumtafuta Roho.
-
2:52 - 2:56Kutoka kwenye miaka mingi ya kujifunza
chini ya, na kutembea -
2:56 - 2:59pamoja na Jenerali wa Mungu, Nabii
TB Joshua, -
2:59 - 3:01hadi alipoitwa Nyumbani Mbinguni,
-
3:01 - 3:07shauku imewashwa mioyoni mwetu
kutoa hazina tuliyopewa na Mungu; -
3:07 - 3:10Neno lililo hai katika nguvu za
Roho Mtakatifu! -
3:10 - 3:12Maandishi ya Neno hayawezi kusonga,
-
3:12 - 3:15hayawezi kufanya kazi bila
uhai wa Mungu (Yohana 6:63). -
3:15 - 3:18Kila Neno la Mungu ni Roho na uzima.
-
3:18 - 3:20Na ni uzima halisi wa Mungu
-
3:20 - 3:24katika Neno hilo unaotia nguvu,
nishati katika Neno. -
3:24 - 3:27Hili ndilo Neno linaloponya, kuokoa,
kukomboa -
3:27 - 3:30na kumwezesha mwamini kuishi maisha
ya ushindi katika Kristo. -
3:30 - 3:35Kama vile Simoni Petro katika Yohana 6:68,
-
3:35 - 3:38tumegundua kwamba hakuna mbadala wa Yesu
-
3:38 - 3:42kwa sababu Yeye peke yake ndiye mwenye
Maneno ya uzima wa milele. -
3:42 - 3:47Baada ya mshauri wetu kuitwa Nyumbani
tarehe 5 Juni 2021, -
3:47 - 3:51kama wanafunzi wa zamani,
Yesu alipopaa Mbinguni, -
3:51 - 3:55tumekuwa tukingoja katika imani.
-
3:55 - 4:00Na katika tarehe 8 ya Desemba 2021,
nilipokea ufunuo toka kwa Mungu. -
4:00 - 4:05Na nikapewa jina la
'Chuo Kikuu Cha Mungu'. -
4:05 - 4:16[muziki]
-
4:16 - 4:20Nilijikuata katika chumba cha glasi
ndani ya pango -
4:20 - 4:23lisilokuwa na sehemu ya kutokea
-
4:23 - 4:28Ghafla mwamba wenye nguvu ukaja
kutoka Mbinguni -
4:28 - 4:31na kugonga mlima wa mawe.
-
4:31 - 4:33ulitoboa lile pango.
-
4:33 - 4:38Mlima ulitikisika, lakini nilibaki
thabiti ndani ya chumba cha kioo. -
4:38 - 4:48Jiwe lilitoboa kwenye mlima wa mawe.
-
4:48 - 4:52Niliangalia.
-
4:52 - 4:54Kisha nikatoka na kutembea.
-
4:54 - 4:58Nilisimama na kushtuka pale nilipoona
-
4:58 - 5:06mwamba ulikuwa umechimba handaki zuri kabisa
iliyotengenezwa kwa dhahabu! -
5:06 - 5:12Nilijiambia, lazima kuwe na maji
mwishoni mwa handaki hili. -
5:12 - 5:14Nilianza kutembea.
-
5:14 - 5:18Ghafla sauti ikasikika kutoka juu:
-
5:18 - 5:25“Baki hapo ulipo. Usiingie!
Maji yanakujia.” -
5:25 - 5:29Nilisimama na kubaki pale nilipokuwa.
-
5:29 - 5:33Niliposimama tuli, ghafla niliona maji
-
5:33 - 5:36yakitiririka kutoka mwishoni mwa handaki
kuelekea kwangu. -
5:36 - 5:40Maji yalikuwa safi, yakimeta kwa uhai.
-
5:40 - 5:43Yalitiririka karibu zaidi
-
5:43 - 5:45mpaka yakafika kwenye vidole vyangu
-
5:45 - 5:53na kunawisha miguu yangu kama wimbi
kwenye ufuo wa bahari. -
5:53 - 5:56Nilipokuwa nikitafakari juu ya ono hilo,
-
5:56 - 6:03moyo wangu ulinisukuma kwenye
Kitabu cha Danieli 2:44. Nitasoma; -
6:03 - 6:08Na katika siku za wafalme hao Mungu
wa mbinguni atausimamisha ufalme -
6:08 - 6:13ambao hautaangamizwa milele, wala watu
wengine hawataachiwa enzi yake; -
6:13 - 6:18bali utavunja falme hizi zote
vipande vipande na kuzikomesha, -
6:18 - 6:22nao utasimama milele na milele.
-
6:22 - 6:29Hii ndiyo maana ya maono ya mwamba
uliochongwa kutoka mlimani, -
6:29 - 6:32lakini si kwa mikono ya binadamu
— mwamba uliovunja -
6:32 - 6:41chuma, shaba, udongo, fedha na dhahabu
vipande vipande. -
6:41 - 6:44Kusudi la mwamba ni nini?
-
6:44 - 6:49Kama inavyosema katika kitabu cha
Yeremia 1:10, nitasoma; -
6:49 - 6:57angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa
na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, -
6:57 - 7:02na kuharibu, na kuangamiza;
ili kujenga na kupanda. -
7:03 - 7:10Kusudi la mwamba ni kuondoa kizuizi
kati ya mioyo yetu na Mungu. -
7:10 - 7:16Muda ambapo mtu anapokabidhi moyo wake
kwa Roho Mtakatifu, pazia huondolewa. -
7:16 - 7:20Neno la Mungu ni mbegu ya maisha ya
kiungu -
7:20 - 7:25ambayo huja ndani ya mioyo yetu
na kusababisha imani kukua. -
7:25 - 7:31Maono hayo ni kwa wakati ulioamriwa
(Habakuki 2:3). -
7:31 - 7:34Sasa, muda umewadia
-
7:34 - 7:38Maono ni kwa ajiri kumuunganisha mwanadamu
kwa Mungu tena. -
7:38 - 7:44kupitia Neno Lake, kwa Roho Wake,
ili kuujenga Mwili wa Kristo. -
7:44 - 7:49na kushirikiana na mtandao wa makanisa
kote ulimwenguni. -
7:49 - 7:54Maono haya yanaendana na wito na
zawadi ya Mungu katika maisha yetu. -
7:54 - 7:59Mwamba ulioanguka kutoka Mbinguni
ni Neno la Ufalme -
7:59 - 8:04kama Yesu alivyosema katika Mathayo 13:19.
-
8:04 - 8:07Maono yetu ni kusaidia kuingiza Neno
katika mioyo ya watu - -
8:07 - 8:11kwa sababu ni pale tu ndipo linafanya kazi
kwa ufanisi. -
8:11 - 8:16Kama Biblia inavyosema Katika kitabu cha
2 Wakorintho 3:3 - Wacha nikusomee; -
8:17 - 8:21Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua
iliyoandikwa na Kristo, -
8:21 - 8:22matokeo ya kazi yetu.
-
8:22 - 8:26Barua hii haikuandikwa kwa wino bali kwa
Roho wa Mungu aliye hai, -
8:26 - 8:32si juu ya vibao vya mawe, bali juu ya
vibao vya mioyo ya wanadamu. -
8:32 - 8:36Katika miongo miwili iliyopita chini ya
ushauri wa Nabii TB Joshua, -
8:36 - 8:40mwingiliano wetu na maelfu ya waumini na
viongozi wa makanisa ulimwenguni kote -
8:40 - 8:44na maswali ya mara kwa mara yaliyoulizwa
na wengi wakati wa mihadhara -
8:44 - 8:48yamevuta mtazamo wetu kwenye upande
wa vitendo wa Ukristo, -
8:48 - 8:53Namaanisha, matembezi yetu
ya kila siku na Roho Mtakatifu: -
8:53 - 8:57jinsi ya kukuza ufahamu wa kiroho,
jinsi ya kusikia kutoka kwa Mungu, -
8:57 - 9:01jinsi ya kujenga imani ya mtu katika
hali ya kutokuwa na uhakika wa maisha. -
9:01 - 9:04Masuala haya ya msingi na mengine
yatashughulikiwa -
9:04 - 9:06chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu
-
9:06 - 9:11kupitia vipindi vya ufundishaji wa kina
na muda wa maswali shirikishi na majibu. -
9:11 - 9:16Maono yetu pia yanakumbatia
makanisa ya mtaani. -
9:16 - 9:21Tunataka kushirikiana na mtandao wa
huduma mbalimbali -
9:21 - 9:28ili kutoa ujuzi wetu, uzoefu, na karama
za kiroho kama Roho anavyoongoza. -
9:28 - 9:35Hadi kanisa la leo linatambua kwamba
roho ya mwanadamu ni chemchemi ya imani, -
9:35 - 9:39hapo ndipo Roho Mtakatifu atakapohusika
katika mambo yetu. -
9:39 - 9:42Jiunge nasi katika Chuo Kikuu cha Mungu
-
9:42 - 9:46Maarifa ya kimwili hukoma,
mara ufunuo unapowadia. -
9:46 - 9:48Kama mshauri wetu, Nabii TB Joshua
alitufundisha, -
9:48 - 9:55“Katika Chuo Kikuu cha Mungu, hata uwe
na kipaji gani, hutapandishwa maradufu, -
9:55 - 10:00lazima usome kila kozi kwani
kila kozi ina kusudi lake.” -
10:00 - 10:02Kwa hiyo, unahitaji nini?
-
10:02 - 10:04Moyo wazi.
-
10:04 - 10:09Ni nyenzo gani zinazohitajika kuchukua
kila kozi - kutokukata tamaa, -
10:09 - 10:11kutafuta njia mbadala au kukata tamaa
-
10:11 - 10:14kwa vipigo vya kikatili vya maisha
vya mara kwa mara? -
10:14 - 10:23Unyenyekevu, imani, uvumilivu, saburi,
msamaha na upendo bila kutarajia. -
10:23 - 10:25Nani anasahihisha kazi zetu?
-
10:25 - 10:27Roho Mtakatifu.
-
10:27 - 10:34Mungu anakungojea mahala pa Roho wake.
-
Not Synced
- Title:
- RACINE & RUTH: UNGANA NASI KATIKA CHUO KIKUU CHA MUNGU!
- Description:
-
Kutoka kwenye miaka mingi ya kujifunza chini ya na kutembea na Jenerali wa Mungu, Nabii TB Joshua, hadi siku alipoitwa Nyumbani, shauku imewaka mioyoni mwetu ya kutoa hazina ambayo Mungu ametupa - Neno lililo hai kwa nguvu ya Mungu. Roho takatifu!
- Video Language:
- English
- Team:
The University of God
- Duration:
- 10:41
![]() |
fatinakatisha edited Swahili subtitles for RACINE & RUTH: JOIN US IN THE UNIVERSITY OF GOD! | |
![]() |
fatinakatisha edited Swahili subtitles for RACINE & RUTH: JOIN US IN THE UNIVERSITY OF GOD! | |
![]() |
fatinakatisha edited Swahili subtitles for RACINE & RUTH: JOIN US IN THE UNIVERSITY OF GOD! | |
![]() |
fatinakatisha edited Swahili subtitles for RACINE & RUTH: JOIN US IN THE UNIVERSITY OF GOD! | |
![]() |
fatinakatisha edited Swahili subtitles for RACINE & RUTH: JOIN US IN THE UNIVERSITY OF GOD! | |
![]() |
fatinakatisha edited Swahili subtitles for RACINE & RUTH: JOIN US IN THE UNIVERSITY OF GOD! | |
![]() |
fatinakatisha edited Swahili subtitles for RACINE & RUTH: JOIN US IN THE UNIVERSITY OF GOD! | |
![]() |
fatinakatisha edited Swahili subtitles for RACINE & RUTH: JOIN US IN THE UNIVERSITY OF GOD! |