UPONYAJI dhidi ya UGONJWA WA TUMBO(GASTRITIS) nchini Marekani! | Ushuhuda wa Maombi ya Mtandaoni
-
0:01 - 0:06Baada ya maombi, nilienda na kula chakula cha aina hiyo ambacho kawaida kinaweza kunisababishia maumivu.
-
0:06 - 0:10na sikuhisi maumivu tena - hadi leo!
-
0:14 - 0:20USHUHUDA
-
0:21 - 0:27Kwa mamlaka katika jina la Yesu Kristo, pokea uhuru wako!
-
0:27 - 0:30Pokea uponyaji wako!
-
0:30 - 0:32Pokea mafanikio yako!
-
0:32 - 0:35Pokea marejesho!
-
0:35 - 0:41Pokea! Pokea leo!
-
0:42 - 0:52Jina langu ni Merick, na ninapatikana Knoxville, Tennessee, Marekani.
-
0:52 - 1:03Ninatoka Afrika Mashariki, Tanzania,
na nilikuja hapa mwaka wa 2007. -
1:03 - 1:13Tangu wakati huo, baada ya miaka mitano hivi kupita, nilianza kuona mabadiliko fulani.
-
1:13 - 1:18Nilikuwa nikipata maumivu ndani ya
tumbo langu, maumivu mengi, -
1:18 - 1:24hasa nilipokula maharagwe,
nyanya au maji ya limao. -
1:24 - 1:31Nilikuwa nikipata maumivu mengi,
kwa hiyo niliishi nayo kwa muda. -
1:31 - 1:37Ndipo nikaamua kwenda kumwona daktari na wakapanga miadi.
-
1:37 - 1:44Siku ya matibabu,
ambapo waliniwekea kamera, -
1:44 - 1:51matokeo yalikuja kuwa nilikuwa na gesi -
kulikuwa na gesi nyingi ndani yangu. -
1:51 - 1:56Waliutaugonjwa wa tumb( gastritis),
ambao ulisababisha maumivu mengi. -
1:56 - 1:59Hata wakati fulani nilihisi maumivu ya moyo.
-
1:59 - 2:05Hapo awali, nilikuwa nikifikiria ni suala la moyo - kana kwamba nilikuwa karibu kupata mshtuko wa moyo.
-
2:05 - 2:08Kisha, nilikuwa nikipata maumivu mengi ya kichwa.
-
2:08 - 2:14Kwa hiyo waliniwekea dawa
na nilikuwa natumia dawa -
2:14 - 2:20kupunguza gesi kwa sababu hakuna dawa ya kuponya hali hiyo.
-
2:20 - 2:25Niliendelea kunywa dawa.
-
2:25 - 2:30Mwishoni mwa siku, nilifikiri, 'Nitaendelea kutumia dawa sikuzote.'
-
2:30 - 2:41Kisha nikasema, 'Hapana, ninaweza kumwamini Mungu kwa sababu najua Mungu anaweza kuleta mabadiliko ndani yangu.'
-
2:41 - 2:48Na niliendelea kuomba - lakini bado nilikuwa nikipata maumivu ndani yangu.
-
2:48 - 2:53Niliacha kutumia dawa, hivyo kila
nilipokula vyakula hivyo... -
2:53 - 2:57Kwa sababu sikuweza kuacha kula chakula walichoniambia niache,
-
2:57 - 3:03ambacho nilikuwa nakula tangu nikiwa Afrika.
-
3:03 - 3:07Nilipata maumivu hayo
kwa karibu miaka minane. -
3:07 - 3:16Siku moja nilikuwa kwenye mitandao ya kijamii - na nilimfahamu Ndugu Chris tangu alipokuwa SCOAN.
-
3:16 - 3:23Niligundua alirudi UK,
na niliendelea kumfuatilia. -
3:23 - 3:26Ninajua yeye ni mtu mzuri, mnyenyekevu wa Mungu.
-
3:26 - 3:31Na niliona jinsi watu walivyoungana naye na jinsi alivyokuwa akiwatia moyo.
-
3:31 - 3:36Kwa hiyo nilibarikiwa sana na
motisha yake. -
3:36 - 3:41Niliendelea kujipa moyo kwa kila alichonitia moyo.
-
3:41 - 3:44Niliendelea kuungana na
kujipa moyo kwa hilo. -
3:44 - 3:49Na kisha nikaona kiungo cha mtandao kuhusu
jinsi ya kuunganishwa kwa maombi. -
3:49 - 3:59Najua Roho wa Mungu alikuwa akinielekeza kufuata kiungo hicho na kuwasilisha ombi langu la maombi.
-
3:59 - 4:05Nilipotuma ombi langu, nilialikwa kujiunga na Maombi ya Pamoja mnamo Mei 4, 2024.
-
4:05 - 4:09Niliunganisha kwenye ibada,
nikingoja Ndugu Chris aje. -
4:09 - 4:14Kwa hiyo nilipokuwa nimeunganishwa,
ulikuwa ni wakati wa shuhuda. -
4:14 - 4:24Niliunganishwa, nikisikiliza watu wakishuhudia kile ambacho Mungu alikuwa amefanya katika maisha yao.
-
4:24 - 4:28Mtu wa mwisho, mwanamke kutoka Afrika Kusini,
-
4:28 - 4:35alikuwa akishuhudia kuhusu tatizo lilelile
nililokuwa nikipitia wakati huo. -
4:35 - 4:37Hivyo ndivyo alivyokuwa akishuhudia.
-
4:37 - 4:44Nilijua kwamba ilikuwa ni miadi ya kiungu, na nilijua nilikuwa nikipokea uponyaji wangu
-
4:44 - 4:51pale pale baada ya kuamini kuwa Mungu akimponya, angeniponya mimi pia.
-
4:51 - 4:59Kwa hiyo niliendelea na maombi, nikiamini ‘leo ni siku yangu’ na ningepokea uponyaji wangu.
-
4:59 - 5:06Ndugu Chris alipokuja, tuliungana katika maombi. Tuliomba na kuomba.
-
5:06 - 5:13Na tangu wakati huo,
nilianza kuhisi mabadiliko ndani yangu. -
5:13 - 5:18Nilianza kuhisi amani.
Sikuhisi maumivu ya aina yoyote. -
5:18 - 5:25Na baada ya maombi, nilienda na kula chakula cha aina hiyo ambacho kawaida kingeniletea maumivu.
-
5:25 - 5:28na kamwe sikuhisi maumivu tena - hadi leo!
-
5:28 - 5:32Mungu anaweza na amenitendea.
-
5:32 - 5:40Ninapokula maharagwe au aina yoyote ya chakula kilicho na limao, nyanya au vitu kama hivyo,
-
5:40 - 5:41Sijisikii maumivu tena.
-
5:41 - 5:50Au nikinywa matunda ya mpasheni au juisi ya machungwa,
siumii tena. -
5:50 - 5:52Kwa hivyo hakuna maumivu tena.
-
5:52 - 5:56Na kwa kweli, nilikuwa na
wakati mgumu kulala. -
5:56 - 6:00Nilipokula, nililazimika
kulala upande mmoja. -
6:00 - 6:05Kwa sababu wakati mwingine nilihisi
kujaa gesi tumboni wakati nimelala. -
6:05 - 6:12Ningelazimika kutumia mto
kuinua kichwa changu wakati nimelala. -
6:12 - 6:14Lakini Mungu alifanya hivyo kwa ajili yangu.
-
6:14 - 6:20Ninataka kuwaambia watu - Mungu wetu ni wa ajabu
na Yeye ni Baba mwenye upendo. -
6:20 - 6:26Anajua tunachohisi.
Anajua uchungu wetu. Anajua kilio chetu. -
6:26 - 6:31Na daima hutuwekea miadi mitakatifu.
-
6:31 - 6:34Yeye daima anahisi kile tunachohisi.
-
6:34 - 6:38Hakuna mtu anayeweza kuhisi jinsi tunavyohisi - kama Mungu.
-
6:38 - 6:43Hakuna anayeweza kuona machozi yetu - kama Mungu.
-
6:43 - 6:48Kwa hiyo Mungu anatuhurumia siku zote.
-
6:48 - 6:51Kama mtoto wa Mungu, lazima pia uamini.
-
6:51 - 6:57Ikiwa Mungu alinifanyia mimi, atakufanyia wewe pia. Yeye ni Mungu mwema!
- Title:
- UPONYAJI dhidi ya UGONJWA WA TUMBO(GASTRITIS) nchini Marekani! | Ushuhuda wa Maombi ya Mtandaoni
- Description:
-
Wakati Merick, Mtanzania anayeishi Marekani, akisikiliza ushuhuda wa TV Ya Moyo Wa Mungu kutoka kwa mwanamke mmoja wa Afrika Kusini, imani yake ilichochewa - kwani Mungu alimponya kutoka katika hali ile ile aliyokuwa nayo. Unaposikiliza ushuhuda wake, tunaomba imani yako mwenyewe itachochewa kumwamini Mungu kwa muujiza wako mwenyewe!
Ili kupokea kwa uhuru Maombi ya Pamoja kutoka kwa Ndugu Chris kwenye Zoom, tafadhali wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom
➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Mwingiliano - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live - Video Language:
- English
- Team:
God's Heart TV
- Duration:
- 07:27
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for HEALING from GASTRITIS in USA! | Online Prayer Testimony | |
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for HEALING from GASTRITIS in USA! | Online Prayer Testimony |