< Return to Video

Roho Mtakatifu HUFANYA KAZI APENDAVYO!

  • 0:00 - 0:02
    Kupitia safari hiyo ya uponyaji wangu,
  • 0:02 - 0:07
    Nilitambua kwamba niliongezeka zaidi katika imani
    na nikamkaribia Mungu zaidi,
  • 0:07 - 0:11
    na uhusiano wangu na Bwana na Mwokozi wangu Yesu Kristo kwa kweli uliboreka.
  • 0:18 - 0:21
    Sawa, ndugu yetu wa Zambia - tuombe.
  • 0:21 - 0:27
    Katika jina la Yesu Kristo!
  • 0:27 - 0:36
    Sasa hivi kila uharibifu kwenye misuli yako, kwenye mifupa yako – urejeshwe kwa jina la Yesu!
  • 0:36 - 0:41
    Urejeshwe kwa jina la Yesu.
  • 0:41 - 0:46
    Ndugu, unaweza kuniinua mguu wako?
  • 0:46 - 0:53
    Katika jina la Yesu Kristo,
    uwe mzima sasa hivi.
  • 0:53 - 1:04
    Kila maumivu - toka kwake,
    kwa jina la Yesu Kristo.
  • 1:04 - 1:05
    Asante, Roho Mtakatifu.
  • 1:05 - 1:09
    Ndugu, uko huru kwa utukufu wa Mungu.
  • 1:09 - 1:12
    Unaweza kujiangalia sasa hivi.
  • 1:12 - 1:16
    Najua hutaweza
    kuiondoa piopi kwa sasa,
  • 1:16 - 1:19
    lakini unaweza kujua kwamba
    Mungu amekugusa.
  • 1:19 - 1:22
    Jiangalie tu na umshukuru
    Mungu kwa uponyaji wako.
  • 1:22 - 1:23
    Asante, Bwana.
  • 1:25 - 1:31
    Jina langu ni Francis na
    ninatoka Zambia, Afrika.
  • 1:31 - 1:39
    Mwaka jana mwezi wa Machi, nilivunjika kigoko(fibula) nilipokuwa nikicheza soka.
  • 1:39 - 1:49
    Lakini hali ya jeraha na mambo ambayo yalisababisha hayakuwa ya asili.
  • 1:49 - 1:53
    Kwa hivyo ilikuwa suala ambalo mahali pa kazi yangu,
  • 1:53 - 1:59
    Nilikuwa katika nafasi ya kaimu
    mkuu wa idara.
  • 1:59 - 2:05
    Kwa hiyo kwa fursa hiyo, nilileta kipengele cha kuwa na Maandiko na sala
  • 2:05 - 2:09
    mahali pangu pa kazi,
    ambayo ni taasisi ya kujifunza.
  • 2:09 - 2:12
    Kwa hivyo siku ya Ijumaa, tulikuwa na maombi na wanafunzi.
  • 2:12 - 2:17
    Tulimsifu Bwana, tukashiriki Neno la Mungu, na nilijua hivi ndivyo inavyopaswa kuwa.
  • 2:17 - 2:26
    Siku iliyofuata, Jumamosi, nilienda kucheza mpira wa miguu na marafiki zangu, kama nilivyokuwa nikifanya siku zote.
  • 2:26 - 2:31
    Kabla sijaenda kucheza mechi ya mpira wa miguu,
    nilipokea ujumbe mfupi wa maandishi
  • 2:31 - 2:37
    kutoka kwa mmoja wa wanafunzi waliokuwa kwenye mkutano wa maombi tuliokuwa nao siku iliyotangulia.
  • 2:37 - 2:41
    Alikuwa na ndoto ambapo aliona
    ninashambuliwa -
  • 2:41 - 2:44
    kulikuwa na shambulio la karibu
    kwenye maisha yangu.
  • 2:44 - 2:48
    Kwa hivyo katika siku hiyo ya kutisha,
    Jumamosi hiyo hiyo, moyo wangu ...
  • 2:48 - 2:53
    Unajua, moyo unajua wakati kitu kibaya lakini nilipuuzia tu
  • 2:53 - 2:56
    nikasema, Baba, mapenzi yako yatimizwe;
  • 2:56 - 2:59
    kwa sababu sikujua jinsi
    shambulio hilo lingekuja.
  • 2:59 - 3:02
    Nilimshukuru Mungu kwa kila jambo
    na kuendelea kucheza soka.
  • 3:02 - 3:13
    Kwa hivyo mechi ilianza karibu saa 11 jioni. Ardhi ilikuwa na unyevu kwa sababu ilikuwa imetoka tu kunyesha.
  • 3:13 - 3:16
    Kwa hivyo katika siku hiyo jaala, kufupisha hadithi hii ndefu, nilipokuwa nikicheza,
  • 3:16 - 3:20
    Niliteleza kwenye makabiliano nikijaribu kucheza mpira.
  • 3:20 - 3:24
    Sikuwa na mawasiliano na mchezaji yeyote, wala sikupiga chochote kigumu.
  • 3:24 - 3:27
    Lakini baada ya kuteleza tu kwenye chenga rahisi,
  • 3:27 - 3:30
    nilipokuwa chini,
    niliweza kuhisi kwamba kigoko(fibula) yangu ilivunjika.
  • 3:30 - 3:35
    Kwa hivyo mara moja, wenzangu wengi walidhani ninacheza au nikijifanya kuanguka tu,
  • 3:35 - 3:37
    kwa hivyo labda nisingeweza
    kushiriki katika mchezo.
  • 3:37 - 3:43
    Lakini hapohapo, niliweza kuhisi mfupa wangu ukisonga; Niliweza kuhisi maumivu makali.
  • 3:43 - 3:46
    Na mara moja hili lilipotokea,
  • 3:46 - 3:49
    ilinikumbusha ujumbe
    nilioupokea siku hiyo ya maafa.
  • 3:49 - 3:54
    Baada ya hapo, nilikimbizwa hospitali
    na kisha wakanifanyia X-ray.
  • 3:54 - 3:59
    Baada ya kunifanyia X-ray, ndivyo walivyogundua kuwa mfupa wangu wa kigoko(fibula) ulikuwa umevunjika.
  • 3:59 - 4:03
    na mvunjiko wa mfupa ulikuwa kana
    kwamba nilipigwa na kitu
  • 4:03 - 4:07
    hiyo ilipelekea mifupa kutengana kabisa.
  • 4:07 - 4:11
    Kwa hiyo, kilichofanyika nilipewa piopi.
  • 4:11 - 4:18
    Hiyo piopi niliyopewa ndiyo inayoonyeshwa kwenye video uliyoiona.
  • 4:18 - 4:23
    Na kisha, bila shaka, niliweka dawa za kutuliza maumivu na pia dawa zingine.
  • 4:23 - 4:27
    Lakini nilikuwa na maumivu makali
    na nilipewa magongo.
  • 4:27 - 4:32
    Kwa hiyo siku hiyohiyo niliwasiliana na Timu ya TV ya Moyo wa Mungu na kueleza hali yangu yote.
  • 4:32 - 4:37
    Na mara nikatuma ujumbe wangu,
    Timu ya TV ya Moyo wa Mungu ikajibu.
  • 4:37 - 4:44
    Katika siku hiyo ya mahsusi, kwakweli, Ndugu Chris alihubiri Neno la Mungu kwetu
  • 4:44 - 4:45
    kabla ya kutuombea.
  • 4:45 - 4:48
    Alisema kitu ambacho sijawahi
    kusahau hadi leo.
  • 4:48 - 4:53
    Alisema jambo muhimu, na
    ninaamini aliongozwa na Roho Mtakatifu,
  • 4:53 - 4:56
    juu ya nini kitatokea, haswa kuhusu hali yangu.
  • 4:56 - 5:00
    Kwa hivyo katika hali nyingi,
    ninapotazama TV ya Moyo wa Mungu,
  • 5:00 - 5:03
    Ningeona watu wakiombewa ungeona uponyaji mara moja.
  • 5:03 - 5:05
    Watu wangehisi kitu.
  • 5:05 - 5:08
    Wengine wangehisi umeme.
    Kwa wengine, itakuwa joto.
  • 5:08 - 5:10
    Wangehisi mambo mengi.
  • 5:10 - 5:14
    Lakini kabla Ndugu Chris hajasali kwa ajili ya yeyote kati yetu siku hiyo, alitaja jambo fulani.
  • 5:14 - 5:21
    Alisema, “Unapoombewa, Roho Mtakatifu hufanya kazi apendavyo yeye.”
  • 5:21 - 5:26
    Kwa hivyo hiyo inamaanisha ni kwamba sio lazima uhisi kitu,
  • 5:26 - 5:29
    au nilazima uanguke, au nilazima ujidhihirishe au kwa namna yeyote,
  • 5:29 - 5:33
    kwa sababu tunapokuja kwenye maombi,
    tunakuja tukiwa na matarajio mengi.
  • 5:33 - 5:35
    Labda utafikiri kwamba
    wanapokuombea,
  • 5:35 - 5:38
    ili ujue kuwa umepona,
    lazima uhisi aina fulani ya umeme.
  • 5:38 - 5:40
    Lazima uhisi kitu.
  • 5:40 - 5:45
    Wakati mwingine Roho Mtakatifu - hata hutahisi chochote, lakini Mungu atakuponya.
  • 5:45 - 5:50
    Kwa hiyo Ndugu Chris alivyonifanyia maombi, ilipofika zamu yangu ya maombi,
  • 5:50 - 5:55
    jambo moja ninalokumbuka ni kwamba, nililoweza kuhisi ni kwamba -
    nilikuwa na amani ya moyo.
  • 5:55 - 5:56
    Hilo ndilo lilikuwa jambo la kwanza nililokuwa nalo.
  • 5:56 - 5:58
    Bila shaka, kulikuwa na mambo mengi
    ambayo nilikuwa nikipitia.
  • 5:58 - 6:00
    Mvunjiko wa mfupa ulikuwa ni kitu kimoja tu kati ya hayo.
  • 6:00 - 6:05
    Lakini nilikuwa na amani ya moyo na jambo moja ambalo lilikuwa dhahiri kimwili lilikuwa
  • 6:05 - 6:08
    kwamba, maumivu yaliyokuwa kwenye mguu wangu yalipungua.
  • 6:08 - 6:12
    Zaidi ya hayo, sikuhisi aina yoyote ya ...
  • 6:12 - 6:15
    Sikuhisi chochote zaidi
    ya maumivu kupungua
  • 6:15 - 6:21
    na amani ya moyo ambayo niliipata siku ile ya maafa niliombewa.
  • 6:21 - 6:23
    Na niliweza kupata
    nguvu kwenye mguu wangu
  • 6:23 - 6:27
    kwa sababu, wakati huo, nilikuwa na maumivu makali.
  • 6:27 - 6:32
    Kwangu mimi, maombi na uzoefu wote ilikuwa ni zaidi ya kuvunjika mguu tu,
  • 6:32 - 6:35
    kwa sababu ninaamini nilikuwa na
    mpasuko katika imani yangu.
  • 6:35 - 6:42
    Kwa hivyo kupitia uzoefu, uponyaji wangu
    ulikuwa maalum kabisa. Ninauchukua kama maalum.
  • 6:42 - 6:46
    Baada ya Ndugu Chris kusali,
    jambo alilotaja lilikuwa
  • 6:46 - 6:51
    kwamba kipengele chochote cha kiroho
    kilichosababisha mpasuko
  • 6:51 - 6:54
    na kilichoweza kusababisha
    matatizo kiondolewe.
  • 6:54 - 6:58
    Kwa hivyo katika kisa changu, uponyaji wangu
    ulichukua 'zamu ya asili' katika hilo
  • 6:58 - 7:02
    Sikupokea
    muunganiko wa mfupa mara moja.
  • 7:02 - 7:07
    Ilichukua muda na kupitia
    safari hiyo ya uponyaji wangu,
  • 7:07 - 7:11
    Nilitambua kwamba niliongezeka zaidi katika imani
    na nikamkaribia Mungu zaidi,
  • 7:11 - 7:15
    na uhusiano wangu na Bwana na Mwokozi wangu Yesu Kristo kwa kweli uliboreka.
  • 7:15 - 7:19
    Sawa, kwa hivyo nina uhakika watu wanaweza
    kuona X-rays mbili.
  • 7:19 - 7:23
    Ile ya kushoto ni kabla ya maombi.
  • 7:23 - 7:30
    Ile iliyo upande wa kulia ni baada ya maombi,
    ambayo niliyapata takriban wiki mbili zilizopita.
  • 7:30 - 7:34
    Kwa hivyo hiyo ndiyo ambayo sasa inaonyesha uponyaji wangu kwa sasa.
  • 7:34 - 7:37
    Na utukufu ni kwa Mungu - mifupa yangu imeunganishwa.
  • 7:37 - 7:43
    Yote kwa yote, jeraha langu limepona
    na Mungu ameponya maisha yangu.
  • 7:43 - 7:47
    Kwa hivyo ikiwa uliona kwenye video,
    sikuweza kusimama peke yangu.
  • 7:47 - 7:49
    Kwa hiyo kusimama lilikuwa tatizo.
  • 7:49 - 7:55
    Lakini sasa, ninaweza kusimama kwa
    miguu yangu miwili kama watu wanavyoona.
  • 7:55 - 8:00
    Na, naweza pia kujisawazisha. Kwa hivyo huu ndio mguu
    ambao uliathiriwa - mguu wa kushoto.
  • 8:00 - 8:03
    Unaweza kuona ninaweza kujisawazisha
    na kuwa na nguvu kwenye mguu wangu.
  • 8:03 - 8:11
    Ninaweza kujongea kwa uhuru, naweza kutembea kwa uhuru, naweza kuruka na kufanya shughuli nyingi za kimwili
  • 8:11 - 8:15
    ambazo sikuweza kufanya wakati huo.
    Hakuna maumivu katika mfupa!
  • 8:15 - 8:20
    Unaweza hata kuona jinsi mguu wangu unavyoonekana -
    wengine hawawezi hata kusema kuwa nimevunjika.
  • 8:20 - 8:23
    Imepona vizuri na
    hakuna ulemavu kwenye mguu wangu.
  • 8:24 - 8:30
    Napenda kuwashauri tu
    ndugu zangu -
  • 8:30 - 8:32
    unapokaribia kupokea maombi,
  • 8:32 - 8:39
    moja ya mambo ya kukumbuka ni kwamba huwezi kumpendeza Mungu bila imani (Waebrania 11:6).
  • 8:39 - 8:43
    Kwa hiyo naamini, kwa kadiri tunavyotaka kupokea uponyaji wa kimwili
  • 8:43 - 8:45
    au maombi kwa aina yoyote ya shida tuliyo nayo,
  • 8:45 - 8:49
    kwanza tunapaswa kuamini kwamba Mungu
    atatuponya matatizo yetu.
  • 8:49 - 8:54
    Na kisha Mungu anapotuponya,
    Mungu anataka wokovu kwa ajili yetu.
  • 8:54 - 8:58
    Kwa hiyo inampasa kwanza kujenga
    uhusiano huo ndani yetu pamoja naye
  • 8:58 - 9:01
    hiyo itatuwezesha kudumisha uponyaji.
  • 9:01 - 9:05
    Kwa sababu ninaweza kupokea uponyaji leo,
    lakini ikiwa sitadumisha uhusiano wangu
  • 9:05 - 9:08
    pamoja na Bwana na Mwokozi wangu Yesu Kristo,
    ninaweza kupoteza baraka hiyo.
  • 9:08 - 9:11
    Najua wengine wanaomba
    kupandishwa vyeo, ​​ajira -
  • 9:11 - 9:13
    kuna mambo mengi sana ambayo
    watu wanaomba.
  • 9:13 - 9:17
    Lakini jambo la muhimu zaidi ni - utadumishaje baraka?
  • 9:17 - 9:21
    Na katika kisa changu, Mungu alinionyesha uvumilivu na pia ustahamilifu.
  • 9:21 - 9:23
    na jinsi ya kudumisha baraka yangu.
  • 9:23 - 9:28
    Na hadi leo, ninashukuru kwa zawadi nyingi ambazo Mungu ameonyesha maishani mwangu.
Title:
Roho Mtakatifu HUFANYA KAZI APENDAVYO!
Description:

Francis alivunjika kigoko(fibula) alipokuwa akicheza soka na marafiki zake nchini Zambia - lakini hali iliyopelekea kuumia kwake haikuwa ya kawaida.

Baada ya kupokea maombi katika jina la Yesu Kristo kutoka kwa Ndugu Chris, maumivu yaliondoka mara moja na amani ikaja papo hapo. Kilichofuata ni safari ya pekee ya kupona, ambayo hatimaye ilimtia nguvu kiroho. Tunaomba utiwe moyo na ushuhuda wake, tukijua kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kama apendavyo na inapokuja suala la kuingilia kati kwa Mungu, hatuwezi kutenganisha suluhisho na wokovu!

Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom

➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Pamoja - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
09:59

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions