Miguel Nicolelis: Nyani anayethibiti roboti akitumia fikra. Ukweli mtupu.
-
0:00 - 0:03Hii sayansi ya ubongo ninayofanya na wenzangu
-
0:03 - 0:05ni kama mtabiri wa hali ya hewa.
-
0:05 - 0:09Tunakimbizana na dhoruba kila wakati.
-
0:09 - 0:14Tunataka kuona na kupima dhoruba--namaanisha dhoruba za ubongo.
-
0:14 - 0:17Sisi sote huongea kuhusu dhoruba za ubongo maishani mwetu
-
0:17 - 0:20lakini ni nadra kuona au kuisikia mojawapo.
-
0:20 - 0:22Hivyo basi mimi hupenda kuanza mazungumzo haya
-
0:22 - 0:25kwa kuwatambulisheni kwa mojawapo.
-
0:25 - 0:28Kusema kweli, mara yetu ya kwanza kupima zaidi ya neuron moja--
-
0:28 - 0:30seli za ubongo mia moja kwa wakati mmoja--
-
0:30 - 0:33tungeweza pima cheche za umeme
-
0:33 - 0:35za seli mia moja kutoka kwa mnyama mmoja,
-
0:35 - 0:37hii ndio picha ya kwanza tuliyopata,
-
0:37 - 0:39sekunde kumi za kwanza za rekodi hii.
-
0:39 - 0:43Sasa tukajaribu kufikiria,
-
0:43 - 0:46na tukaweza kuiona mbele yetu.
-
0:46 - 0:47mimi huwaambia wanafunzi
-
0:47 - 0:51kuwa tunaweza waita wanasayansi wa ubongo kama pia wataalam wa anga,
-
0:51 - 0:52kwa sababu tunakabiliana na mfumo
-
0:52 - 0:55ambao unalingana kwa ncha ya nambari ya viini
-
0:55 - 0:58na nambari za galaksi tulizo nazo ulimwenguni.
-
0:58 - 1:01Kwa hivyo hapa ndipo tulipo, katika mabilioni ya neuroni,
-
1:01 - 1:04tukirekodi tu, miaka kumi iliyopita, alafu mia moja.
-
1:04 - 1:06Sasa hivi tunarekodi hadi miaka elfu moja.
-
1:06 - 1:11Na tunatumai kuelewa cha msingi kuhusu asili yetu ya kibinadamu.
-
1:11 - 1:13Kwa sababu, kama bado hujui,
-
1:13 - 1:18kila kitu tunachotumia kutambua asili ya binadamu kimetoka katika dhoruba hizi,
-
1:18 - 1:23katika dhoruba zishukazo kutoka milima na mabonde ya akili zetu
-
1:23 - 1:27na ambazo zinaeleza kumbukumbu zetu, imani zetu,
-
1:27 - 1:30hisia zetu, mipango yetu ya siku za usoni.
-
1:30 - 1:32Kila kitu tunachofanya,
-
1:32 - 1:37kila kitu ambacho binadamu amekifanya, anakifanya ama atakifanya,
-
1:37 - 1:42kinahitaji bidii ya idadi kubwa ya neuroni zinazozalisha dhoruba hizi.
-
1:42 - 1:45Na sauti ya dhoruba ya ubongo, kama hujawaisikia moja,
-
1:45 - 1:48huwa hivi.
-
1:48 - 1:51Unaweza ongeza sauti kama waweza.
-
1:51 - 1:58Mwanangu huiita "kutengeneza popcorn huku ukiskiza kituo cha redio kilichoegezwa vibaya."
-
1:58 - 1:59Huu ni ubongo.
-
1:59 - 2:03Haya ndiyo yanayotokea unapoelekeza dhoruba hizi za umeme kwenye kipaza sauti
-
2:03 - 2:06na usikie seli mia moja vya ubongo vikirushwa,
-
2:06 - 2:10haya ndiyo yatakayosikika katika ubongo wako--ubongo wangu, na ubongo wowote.
-
2:10 - 2:14Kile tunachotaka kufanya kama wanasayansi ya ubongo katika wakati huu
-
2:14 - 2:19ni kuskiza kwa makini sauti hizi, sauti hizi za ubongo,
-
2:19 - 2:23na kujaribu kudondoa zile jumbe zinazobeba
-
2:23 - 2:26Haswa, takriban miaka kumi na mbili iliyopita
-
2:26 - 2:29tulitengeneza muundo tuliouita mashine ya akili.
-
2:29 - 2:31Na hapa una mpango unaoeleza vile inavyotumika.
-
2:31 - 2:37Lengo ni, tuwe na vitega hisia vinavyosikiza dhoruba hizi, vile umeme unavyozalishwa,
-
2:37 - 2:40na kuona kama inawezekana, kwa wakati huo huo wakati unaopita
-
2:40 - 2:45kabla ya dhoruba hii kutoka kwa akili na kufika kwenye miguu ama mikono ya mnyama
-
2:45 - 2:48kama nusu sekunde--
-
2:48 - 2:50wacha tuone kama tunaweza kusoma ishara hizi,
-
2:50 - 2:54kudondoa jumbe za ubongo inazobeba,
-
2:54 - 2:56kuitafsiri iwe amri za kikompyuta
-
2:56 - 2:58na kuituma hadi kwenye kifaa kilichoundwa na binadamu
-
2:58 - 3:04kitakachozalisha ule mzunguko hiari wa akili wakati ule ule.
-
3:04 - 3:08tuone kama tunaweza kupima ni vipi tunaweza tafsiri ujumbe huo vyema zaidi
-
3:08 - 3:11wakati tunapolinganisha na vile mwili unavyofanya kazi hio.
-
3:11 - 3:14Wakati tunapotoa maoni,
-
3:14 - 3:20viashiria hisia
-
3:20 - 3:22sasa iliyo chini ya udhibiti wa ubongo,
-
3:22 - 3:23hadi tena kwa ubongo,
-
3:23 - 3:25vile ubongo unavyokabiliana na kazi hiyo,
-
3:25 - 3:30ya kupokea jumbe kutoka mashine zilizoundwa na binadamu
-
3:30 - 3:33Na ndivyo haswa tulivyofanya miaka kumi iliyopita.
-
3:33 - 3:36Tulianza na nyani nyota kwa jina Aurora
-
3:36 - 3:38aliyekuwa nyota kwenye eneo hili.
-
3:38 - 3:40Na Aurora alipenda kucheza michezo ya kompyuta.
-
3:40 - 3:42Mnavyoona hapa,
-
3:42 - 3:47anapenda kutumia kijiti, kama vile kila mmoja wetu, na watoto wetu, kucheza mchezo huu.
-
3:47 - 3:51Kama mnyama mwerevu, anajaribu kudanganya kabla afikie jibu sahihi.
-
3:51 - 3:56Kwa hivyo kabla ya hatua anayopaswa kupita
-
3:56 - 3:58akitumia mshale anaodhibiti kwa kijiti,
-
3:58 - 4:02Aurora anajaribu kufikia hatua, popote ilipo.
-
4:02 - 4:04Na anapofanya hivyo,
-
4:04 - 4:07kwa sababu kila wakati anapovuka hatua akitumia ule mshale mdogo,
-
4:07 - 4:10anapata tone la juisi ya machungwa.
-
4:10 - 4:13nakuambia, nyani yeyote atakufanyia chochote
-
4:13 - 4:16kama utampa tone la juisi ya machungwa.
-
4:16 - 4:19Kwa kweli mnyama yeyote anaweza kufanya hivyo.
-
4:19 - 4:20Hebu tafakari hayo.
-
4:20 - 4:24Hivyo basi, wakati Aurora alikuwa akicheza mchezo huu, vile mlivyoona,
-
4:24 - 4:26na kufanya majaribio elfu moja kwa siku
-
4:26 - 4:30na kupata asilimia tisini na saba sahihi na milimita mia tatu na hamsini za juisi ya machungwa,
-
4:30 - 4:33tunarekodi dhorubaza ubongo zitokazo kichwani mwake
-
4:33 - 4:35na kuzituma kwenye mkanda wa mashine
-
4:35 - 4:39unaotoa zile dhoruba haswa Aurora alikuwa akitoa.
-
4:39 - 4:43Kwa sababu wazo lilikuwa ni kuwasha hii mashine ya ubongo
-
4:43 - 4:47na kuona Aurora akicheza mchezo ule kwa kufikiria tu,
-
4:47 - 4:50bila mwili wake kuingilia kati.
-
4:50 - 4:53Dhoruba zake za akili zitadhibiti mkono
-
4:53 - 4:56utakaosogeza ule mshale na kuvuka hatua.
-
4:56 - 4:59Na kwa mshangao wetu, hivyo haswa ndivyo Aurora alifanya.
-
4:59 - 5:03Alicheza mchezo huo bila kusogeza mwili wake.
-
5:03 - 5:05Hivyo basi kila msogezo unaoona sasa kwenye kijiti
-
5:05 - 5:08hivyo ndivyo haswa alivyofanya mara ya kwanza.
-
5:08 - 5:10Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza
-
5:10 - 5:17nia kwenye ubongo ilitolewa kutoka kwenye mwili wa nyani
-
5:17 - 5:21na iliweza kufanya kazi nje ya mwili, hapa ulimwengu wa nje,
-
5:21 - 5:24kwa kudhibiti mashine.
-
5:24 - 5:29Na Aurora aliendelea kucheza mchezo huo, aliendelea kufikia ile hatua
-
5:29 - 5:32na kupata juisi ya machungwa aliyotaka, aliyotamani.
-
5:32 - 5:39Kwa kweli, alifanya hivyo kwa sababu, wakati ule, yeye alipata mkono mpya.
-
5:39 - 5:42Mkono ule wa roboti unaoona ukitembea hapa siku thelathini baadaye,
-
5:42 - 5:45baada ya ile video ya kwanza niliyowaonyesheni,
-
5:45 - 5:47uko chini ya udhibiti wa ubongo ya Aurora
-
5:47 - 5:51na unasongeza mshale ule ili kufikia ile hatua.
-
5:51 - 5:55Na Aurora sana anajua kuwa anaweza kucheza mchezo huu akitumia mkono mashine,
-
5:55 - 6:00lakini hajapoteza uwezo wa kutumia mkono wake asili kwa chochote angependa kufanya.
-
6:00 - 6:04Anaweza kujikuna mgongo, anaweza kukuna mmoja wetu, anaweza kucheza mchezo wowote mwingine.
-
6:04 - 6:06Kwa nia zote na madhumuni,
-
6:06 - 6:10akili ya Aurora imehusisha kile kifaa bandia
-
6:10 - 6:13kama muendelezo wa mwili wake.
-
6:13 - 6:16Huu mfano wa ubinafsi ambao Aurora alikuwa nao kwa akili yake
-
6:16 - 6:20umepanuliwa kupata mkono mmoja zaidi.
-
6:20 - 6:23Tulifanya hivyo miaka kumi iliyopita.
-
6:23 - 6:26Sasa songea mbele miaka kumi.
-
6:26 - 6:31Mwaka uliopita tu tuligundua kuwa huhutaji kuwa na kifaa cha mashine.
-
6:31 - 6:36Unaweza tu kutengeneza kifaa cha kompyuta.
-
6:36 - 6:40Na unaweza kuitumia kwa nyani zetu kuleta uhusiano kati yao
-
6:40 - 6:45ama unaweza wafunza kudhania ulimwengu gushi
-
6:45 - 6:48maono ya mtu kuhusiana na mashine ile
-
6:48 - 6:53na kutumia msisimko wa akili yake kudhibiti matembezi ya mikono na miguu ya mashine.
-
6:53 - 6:56Na cha msingi tulichofanya kilikuwa kufunza hawa wanyama
-
6:56 - 6:59njia ya kudhiiti mashine hizi
-
6:59 - 7:03na kuchunguza vidude vinavyojitokeza katika ulimwengu gushi.
-
7:03 - 7:05Na vidude hivi vimefanana
-
7:05 - 7:09lakini wakati mashine inapovuka mbele ya vidude hivi,
-
7:09 - 7:16zinatuma ujumbe wa umeme uliyosawia na uso wa kile kidude
-
7:16 - 7:20ambao unaenda moja kwa moja hadi kwenye ubongo wa nyani,
-
7:20 - 7:25ukieleza ubongo kile hasa machine ile inagusa.
-
7:25 - 7:30Na kwa muda wa wiki nne tu, akili inajifunza kuhisi hii hisia mpya
-
7:30 - 7:36na inapata njia mpya ya hisia--kama hisia mpya.
-
7:36 - 7:38Sasa unaiacha akili iwe huru
-
7:38 - 7:43kwa sababu unaikubali akili kutuma jumbe ili kuthibiti mashine hii.
-
7:43 - 7:48Na maoni yanayotoka kwenye mashine yanachanganuliwa kwenye ubongo moja kwa moja
-
7:48 - 7:50bila ya ngozi kuingilia kati.
-
7:50 - 7:53Kwa hivyo kile mnachoona hapa ni ule ubunifu wa kazi ile.
-
7:53 - 7:57Mtaweza kuona mnyama akigusa sehemu au hatua hizi tatu.
-
7:57 - 8:01Lazima achague moja kwa vile ni moja pekee inayoelekea palipo na zawadi,
-
8:01 - 8:03ile juisi ya machungwa ambayo wanayoitaka.
-
8:03 - 8:09Na inambidi aichague kwa mguso akitumia mkono gushi, mkono amao haupo.
-
8:09 - 8:11Na hivyo ndivyo hasa wanavyofanya.
-
8:11 - 8:14Huu ni uhuru kamili wa akili
-
8:14 - 8:19kutokana na vikwazo vya kimwili na kazi ya akili ya kuona.
-
8:19 - 8:23Yule mnyama anathibiti mashine ile kugusa malengo hayo.
-
8:23 - 8:28Na anahisi vile ilivyo kwa kupokea ujumbe umeme moja kwa moja kwenye ubongo.
-
8:28 - 8:32Na huo ubongo unaamua ni hisia ipi inayoashiria ile zawadi.
-
8:32 - 8:36Wale wakongwe uwaonao kwenye filamu hawawakilishi nyani huyu.
-
8:36 - 8:39Na kusema kweli, hata hawawezi kusoma Kiingereza,
-
8:39 - 8:44kwa hivyo wako hapa kuwaonyesheni ya kwamba lengo sahihi linabadilika badilika.
-
8:44 - 8:48Hata hivyo, wanawezazipata kwa kubagua,
-
8:48 - 8:51na wanawezazibonyeza na kuzichagua.
-
8:51 - 8:54Hivyo basi tunapoangalia bongo za wanyama hawa,
-
8:54 - 8:57katika sehemu ya juu mtaona mpangilio wa viini mia na ishirini na tano
-
8:57 - 9:02vikionyesha kile kinachotokea kwenye ubongo, zile dhoruba umeme,
-
9:02 - 9:04za sampuli hii ya neuron kwenye ubongo
-
9:04 - 9:06wakati mnyama huyo anatumia kijiti.
-
9:06 - 9:08Na hiyo ndio picha kila mwanafiziolojia ayoinajua.
-
9:08 - 9:13Mpangilio wa kimsingi unaonyesha kuwa viini hivi vinafuata kila mwelekeo.
-
9:13 - 9:19Picha iliyo chini inaonyesha kinachotokea wakati mwili uachapo kusongea
-
9:19 - 9:25na yule mnyama aanzapo kuthibiti kidude cha roboti ama mashine ya kikompyuta.
-
9:25 - 9:28Kwa kasi ile ile tunayoweza kubadilisha kompyuta zetu,
-
9:28 - 9:34kazi inayoendelea akilini hubadilika ili kuwakilisha kifaa hiki kipya,
-
9:34 - 9:39kana kwamba ilikuwa sehemu ya mwili wa mnyama huyo.
-
9:39 - 9:44Akili inaichanganua pia, kwa kasi ile ile tunayopima nayo.
-
9:44 - 9:48Hiyo inatuashiria kuwa hisia za kibinafsi
-
9:48 - 9:52haziishi kwenye safu ya mwisho ya ngozi ya miili yetu,
-
9:52 - 9:58bali inaisha kwenye safu ya mwisho ya electroni za vifaa tunavyotumia akili zetu kuvithibiti.
-
9:58 - 10:02Vayolini zetu, magari yetu, baiskeli zetu, mipira yetu ya kandanda, nguo zetu
-
10:02 - 10:09zote zinabadilishwa na hiki chombo thabiti, huu mfumo badilifu unaoitwa ubongo.
-
10:09 - 10:11Ni umbali upi tunaoweza kuipeleka?
-
10:11 - 10:15Katika jaribio tulilofanya miaka chache iliyopita, tuliipeleka hadi kikomo.
-
10:15 - 10:18Tulikuwa na mnyama aliyekimbia kwenye baiskeli zoezi
-
10:18 - 10:20katika chuo kikuu cha Duke katika mashariki ya pwani ya Marekani,
-
10:20 - 10:23ikizalisha dhoruba bongo zinazohitajika kusonga.
-
10:23 - 10:27Na tukawa na chombo cha roboti, roboti ya kibinadamu,
-
10:27 - 10:29huko Kyoto, Ujapani katika maabara ya ATR
-
10:29 - 10:35iliyopanga maisha yake yote kuthibitiwa na ubongo,
-
10:35 - 10:38akili ya binadamu, ama ya mnyama.
-
10:38 - 10:43Kile kinachotokea hapa ni kwamba shighuli katika ubongo uliozalisha msongeo katika nyani huyo
-
10:43 - 10:47ulisambazwa hadi Ujapani na ukafanya roboti kutembea
-
10:47 - 10:51na ukanda ya matembezi haya ukapelekwa hadi Duke,
-
10:51 - 10:56ili nyani huyo aone miguu ya yule roboti ikitembea mbele yake.
-
10:56 - 11:00Ilmradi azawadiwe, sio kwa kile mwili wake ulikuwa ukifanya
-
11:00 - 11:05bali kwa kila hatua sahihi iliyochukuliwa na roboti aliyekuwa sehemu ya pili ya ulimwengu
-
11:05 - 11:07ikithibitiwa na shughuli ya akili yake.
-
11:07 - 11:15Cha kuchekesha ni kwamba, safari hiyo ilichukua milisekunde ishirini chini
-
11:15 - 11:19ya wakati dhoruba bongo inayochukua kutoka kichwani mwake, kichwa cha nyani,
-
11:19 - 11:23hadi kwenye msuli wake.
-
11:23 - 11:29Nyani alikuwa akisongeza roboti iliyokuwa na ukubwa mara sita wake yeye, kutoka sehemu moja ya ulimwengu hadi nyengine.
-
11:29 - 11:35Hii ni moja wapo ya majaribio ambapo roboti iliweza kutembea bila usaidizi.
-
11:35 - 11:40Hii ni CB1 ikitimiza ndoto yake Ujapani
-
11:40 - 11:44chini ya uthibiti wa shughuli ya ubongo wa mnyama.
-
11:44 - 11:46Kwa hivyo ni wapi tunapopeleka haya yote?
-
11:46 - 11:48Ni wapi tunapoenda na huu utafiti,
-
11:48 - 11:54kando na kusomea tabia za ulimwengu huu badilifu tulionao katikati ya masikio yetu?
-
11:54 - 11:59Nia yetu ni kutumia usomi huu na teknolojia hii
-
11:59 - 12:04na duniani.kujaribu kurekebisha mojawapo ya shida kubwa zaidi katika ufahamu wa ubongo tulizonazo hapa ulimwenguni.
-
12:04 - 12:09Mamilioni ya watu wamepoteza uwezo wakutafsiri hizi dhoruba za ubongo
-
12:09 - 12:11ziwe hatua, au harakati.
-
12:11 - 12:16Ingawaje akili zao zinazidi kuzaa dhoruba hizo na matembezi,
-
12:16 - 12:21haziwezi kilichoundwa kwa lesheni kwenye uti wa mgongo.kupita kizuizi
-
12:21 - 12:24Kwa hivyo lengo letu ni kutengeneza njia,
-
12:24 - 12:28tukitumia hizi mashine za ubongo kutafsiri viashiria hivi,
-
12:28 - 12:32dhoruba kubwa akilini zilizo na hamu ya kutembea tena,
-
12:32 - 12:36kupita ile lesheni tukitumia uhandisi wa kikompyuta
-
12:36 - 12:43na kuituma hadi kwenye mwili mpya, mwili mpya kabisa unaoitwa eksoskeletoni,
-
12:43 - 12:49suti mpya ya kiroboti inatakayokuwa mwili mpya wa wagonjwa hawa.
-
12:49 - 12:53Na unaweza kuona picha inayojitokeza kutokana na muungano huu.
-
12:53 - 12:57Huu ni muungano uitwao Walk Again Project
-
12:57 - 13:00unaoleta pamoja wanasayansi kutoka Uropa,
-
13:00 - 13:01kutoka hapa Marekani, na Brazili
-
13:01 - 13:06kufanya kazi ili kutengeneza mwili huu mpya—
-
13:06 - 13:09mwili tunaoamini, katika mfumo plastiki ule ule
-
13:09 - 13:15uliowezesha Aurora na nyani wengine kutumia hivi vifaa kupitia kwa mashine ya ubongo
-
13:15 - 13:21na ambayo ilituwezesha kuingiza vifaa tunavyoweza kutengeneza na kutumia katika maisha yetu, siku baada ya siku.
-
13:21 - 13:24Mfumo huu huu, tunatumai, utawezesha wagonjwa hawa,
-
13:24 - 13:28Mfumo huu huu, tunatumai, utawezesha wagonjwa hawa,
-
13:28 - 13:31bali pia kutafsiri mafikira hayo kuwa matembezi ya mwili huu mpya,
-
13:31 - 13:38lakini kwa mwili huu kubadilika kama ule mwili mpya unaothibitiwa na ubongo.
-
13:38 - 13:42Niliambiwa miaka kumi iliyopita
-
13:42 - 13:47kuwa haya yote hayatatokea, ati hii ilikuwa haiwezekani.
-
13:47 - 13:49Na naweza kuwaamia kama mwanasayansi,
-
13:49 - 13:52nilikua huko Brazili ya kusini katika miaka ya sitini
-
13:52 - 13:58nikiangalia wale wenye maono wakituambia kuwa wataenda Mwezini.
-
13:58 - 13:59Na nilikuwa na umri wa miaka mitano,
-
13:59 - 14:03na sikuwahi kuelewa sababu gani NASA haikuwaajiri manahodha Kirk na Spock kufanya kazi hiyo;
-
14:03 - 14:06kwani, si walikuwa na ustadi wa hali ya juu—
-
14:06 - 14:09lakini kuona tu kama mtoto
-
14:09 - 14:12ilinifanya kuamini, kama nyanyangu alivyokuwa akiniambia,
-
14:12 - 14:14kwamba "kisichowezekana ni kile tu kinachowezekana
-
14:14 - 14:18lakini mtu hajatia bidii ya kutosha kukitimiza."
-
14:18 - 14:22Kwa hivyo waliniambia kuwa haiwezekani kufanya mtu atembee.
-
14:22 - 14:25Nafikiri nitafuata wasia wa nyanyangu.
-
14:25 - 14:26Asanteni.
-
14:26 - 14:34(Makofi)
- Title:
- Miguel Nicolelis: Nyani anayethibiti roboti akitumia fikra. Ukweli mtupu.
- Speaker:
- Miguel Nicolelis
- Description:
-
Tunaweza kutumia akili zetu kuthibiti mashine--bila kutumia mwili kama kiegezo? Miguel Nicolelis anazungumza kuhusu jaribio la kushangaza, ambalo nyani mwerevu huko Marekani alijifunza kuthibiti mashine, na pia mkono wa roboti huko Ujapani, kwa njia ya fikra tu. Jaribio hili lina athari kubwa kwa walemavu--na labda kwa sisi sote. (Filamu ilitengenezwa TEDMED 2012.)
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 14:55
![]() |
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for A monkey that controls a robot with its thoughts. No, really. | |
![]() |
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for A monkey that controls a robot with its thoughts. No, really. | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for A monkey that controls a robot with its thoughts. No, really. | |
![]() |
David Mvoi edited Swahili subtitles for A monkey that controls a robot with its thoughts. No, really. | |
![]() |
David Mvoi edited Swahili subtitles for A monkey that controls a robot with its thoughts. No, really. | |
![]() |
David Mvoi edited Swahili subtitles for A monkey that controls a robot with its thoughts. No, really. | |
![]() |
David Mvoi added a translation |