< Return to Video

RACINE & RUTH: UNGANA NASI KATIKA CHUO KIKUU CHA MUNGU!

  • 0:08 - 0:12
    Je! unajua kuwa wewe ni kazi ya sanaa?
  • 0:12 - 0:14
    Mwanadamu ndiye bidhaa kuu ya Mungu.
  • 0:14 - 0:20
    Ninamaanisha, mtu aliyeundwa kufikiria, kuzungumza na kutenda na Mungu.
  • 0:20 - 0:22
    Je, unaishi pamoja na Mungu?
  • 0:22 - 0:25
    Je, hadhi yako ikoje mbele za Mungu leo?
  • 0:25 - 0:33
    Bila neema ya Roho Mtakatifu inayokaa ndani yake,
    mwanadamu ni kivuli tu cha yule aliyeumbwa na Mungu!
  • 0:33 - 0:39
    Mwanadamu ambaye Mungu alimuumba hakuwa mtu wa kimwili tu
    anayetawaliwa na hisia zake
  • 0:39 - 0:45
    bali ni mjumbe kati ya ulimwengu unaoonekana na usioonekana.
  • 0:45 - 0:50
    Mungu na mwanadamu walikuwa wakizungumza pamoja kama marafiki.
  • 0:50 - 0:57
    Lakini siku moja mwanadamu alivunja uhusiano kwa kutotii
    na akaenda mbali na Mungu.
  • 0:57 - 1:03
    Kisha akaenda mbali zaidi hadi mwishowe akaondoka nyumbani.
  • 1:03 - 1:06
    Aliiacha nchi yake ya asili, Edeni, ambako aliishi na Mungu.
  • 1:06 - 1:12
    Alihama kutoka kwenye uwepo wa Mungu.
  • 1:12 - 1:18
    Tangu wakati huo, Mungu amekuwa na shauku ya kuweza
    kuzungumza tena na rafiki yake wa zamani
  • 1:18 - 1:25
    lakini mwanadamu, kwa kuacha uwepo wa Muumba wake,
    alikuwa amepoteza lugha yake mama.
  • 1:25 - 1:29
    Namaanisha, alipoteza lugha yake ya asili na Mungu
  • 1:29 - 1:34
    na hakuweza kuwasiliana na Muumba wake katika roho na kweli.
  • 1:34 - 1:42
    Mwanadamu wa kawaida hawezi kusikia au kuzungumza na Mungu;
    hii ndiyo changamoto tunayokabiliana nayo leo.
  • 1:43 - 1:46
    Ingawa Mungu huzungumza tena na tena,
  • 1:46 - 1:49
    wengi sana hawapo makini kusikia
    kile Anachosema (Ayubu 33:14).
  • 1:49 - 1:52
    Ukimya ni mgumu kwa Mungu.
  • 1:52 - 1:56
    Kama vile baba wa mwana mpotevu
  • 1:56 - 1:58
    alivyokuwa na shauku ya kumwona
    mwanawe akirudi nyumbani,
  • 1:58 - 2:02
    Mungu ana shauku ya kuwa na uhusiano
    wa karibu tena na mwanadamu,
  • 2:02 - 2:04
    Rafiki yake wa zamani.
  • 2:04 - 2:07
    Ndiyo maana ilimbidi achague lugha
  • 2:07 - 2:09
    ambayo mwanadamu angeelewa.
  • 2:09 - 2:13
    Kwa hivyo alimtuma Mwanawe,
    Yesu Kristo duniani kumrudisha mwanadamu,
  • 2:13 - 2:18
    Rafiki Yake wa zamani, arudi Kwake tena.
  • 2:18 - 2:22
    Mungu aliheshimu lugha ya mwanadamu
    kwa kumwita Yesu Neno.
  • 2:22 - 2:26
    Neno alifanyika mwili na akaingia
    ulimwenguni.
  • 2:26 - 2:29
    Yesu ni Mungu akijieleza Mwenyewe
  • 2:29 - 2:33
    kwa lugha ambayo mwanadamu
    anaweza kuelewa,
  • 2:33 - 2:36
    lugha ya roho na uzima (Yohana 6:63).
  • 2:36 - 2:39
    Je, ni kwa muda gani tutaendelea kuwaza,
  • 2:39 - 2:41
    kuzungumza na kuishi katika hali
    ya kimwili
  • 2:41 - 2:45
    ilhali Yesu anakungoja katika mahala
    pa Roho Wake?
  • 2:45 - 2:48
    Ni wasaa wa kurudi tena katika Chuo Kikuu
    cha Mungu
  • 2:48 - 2:52
    Na kuanza kumtafuta Roho.
  • 2:52 - 2:56
    Kutoka kwenye miaka mingi ya kujifunza
    chini ya, na kutembea
  • 2:56 - 2:59
    pamoja na Jenerali wa Mungu, Nabii
    TB Joshua,
  • 2:59 - 3:01
    hadi alipoitwa Nyumbani Mbinguni,
  • 3:01 - 3:07
    shauku imewaka mioyoni mwetu
    kutoa hazina tuliyopewa na Mungu;
  • 3:07 - 3:10
    Neno lililo hai katika nguvu za
    Roho Mtakatifu!
  • 3:10 - 3:12
    Maandishi ya Neno hayawezi kusonga,
  • 3:12 - 3:15
    hayawezi kufanya kazi bila
    uhai wa Mungu (Yohana 6:63).
  • 3:15 - 3:18
    Kila Neno la Mungu ni Roho na uzima.
  • 3:18 - 3:20
    Na ni uzima halisi wa Mungu
  • 3:21 - 3:24
    katika Neno hilo unaotia nguvu,
    nishati katika Neno.
  • 3:24 - 3:27
    Hili ndilo Neno linaloponya, kuokoa,
    kukomboa
  • 3:27 - 3:30
    na kumwezesha mwamini kuishi maisha
    ya ushindi katika Kristo.
  • 3:30 - 3:35
    Kama vile Simoni Petro katika Yohana 6:68,
  • 3:35 - 3:38
    tumegundua kwamba hakuna mbadala wa Yesu
  • 3:38 - 3:42
    kwa sababu Yeye peke yake ndiye mwenye
    Maneno ya uzima wa milele.
  • 3:42 - 3:47
    Baada ya mshauri wetu kuitwa Nyumbani
    tarehe 5 Juni 2021,
  • 3:47 - 3:51
    kama wanafunzi wa zamani,
    Yesu alipopaa Mbinguni,
  • 3:51 - 3:55
    tumekuwa tukingoja katika imani.
  • 3:55 - 4:00
    Na tarehe 8 ya Desemba 2021,
    nilipokea ufunuo toka kwa Mungu.
  • 4:00 - 4:05
    Na nikapewa jina la
    'Chuo Kikuu Cha Mungu'.
  • 4:05 - 4:16
    [muziki]
  • 4:16 - 4:20
    Nilijikuta katika chumba cha glasi
    ndani ya pango
  • 4:20 - 4:23
    lisilokuwa na sehemu ya kutokea
  • 4:23 - 4:28
    Ghafla mwamba wenye nguvu ukaja
    kutoka Mbinguni
  • 4:28 - 4:31
    na kugonga mlima wa mawe.
  • 4:31 - 4:33
    ulitoboa lile pango.
  • 4:33 - 4:38
    Mlima ulitikisika, lakini nilibaki
    thabiti ndani ya chumba cha kioo.
  • 4:38 - 4:48
    Jiwe lilitoboa kwenye mlima wa mawe.
  • 4:48 - 4:52
    Niliangalia.
  • 4:52 - 4:54
    Kisha nikatoka na kutembea.
  • 4:54 - 4:58
    Nilisimama na kushtuka pale nilipoona
  • 4:58 - 5:06
    mwamba ulikuwa umechimba handaki zuri kabisa
    iliyotengenezwa kwa dhahabu!
  • 5:06 - 5:12
    Nilijiambia, lazima kuwe na maji
    mwishoni mwa handaki hili.
  • 5:12 - 5:14
    Nilianza kutembea.
  • 5:14 - 5:18
    Ghafla sauti ikasikika kutoka juu:
  • 5:18 - 5:25
    “Baki hapo ulipo. Usiingie!
    Maji yanakujia.”
  • 5:25 - 5:29
    Nilisimama na kubaki pale nilipokuwa.
  • 5:29 - 5:33
    Niliposimama tuli, ghafla niliona maji
  • 5:33 - 5:36
    yakitiririka kutoka mwishoni mwa handaki
    kuelekea kwangu.
  • 5:36 - 5:40
    Maji yalikuwa safi, yakimeta kwa uhai.
  • 5:40 - 5:43
    Yalitiririka karibu zaidi
  • 5:43 - 5:45
    mpaka yakafika kwenye vidole vyangu
  • 5:45 - 5:53
    na kunawisha miguu yangu kama wimbi
    kwenye ufuo wa bahari.
  • 5:53 - 5:56
    Nilipokuwa nikitafakari juu ya ono hilo,
  • 5:56 - 6:03
    moyo wangu ulinisukuma kwenye
    Kitabu cha Danieli 2:44. Nitasoma;
  • 6:03 - 6:08
    Na katika siku za wafalme hao Mungu
    wa mbinguni atausimamisha ufalme
  • 6:08 - 6:13
    ambao hautaangamizwa milele, wala watu
    wengine hawataachiwa enzi yake;
  • 6:13 - 6:18
    bali utavunja falme hizi zote
    vipande vipande na kuzikomesha,
  • 6:18 - 6:22
    nao utasimama milele na milele.
  • 6:22 - 6:29
    Hii ndiyo maana ya maono ya mwamba
    uliochongwa kutoka mlimani,
  • 6:29 - 6:32
    lakini si kwa mikono ya binadamu
    — mwamba uliovunja
  • 6:32 - 6:41
    chuma, shaba, udongo, fedha na dhahabu
    vipande vipande.
  • 6:41 - 6:44
    Kusudi la mwamba ni nini?
  • 6:44 - 6:49
    Kama inavyosema katika kitabu cha
    Yeremia 1:10, nitasoma;
  • 6:49 - 6:57
    angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa
    na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa,
  • 6:57 - 7:02
    na kuharibu, na kuangamiza;
    ili kujenga na kupanda.
  • 7:03 - 7:10
    Kusudi la mwamba ni kuondoa kizuizi
    kati ya mioyo yetu na Mungu.
  • 7:10 - 7:16
    Muda ambapo mtu anapokabidhi moyo wake
    kwa Roho Mtakatifu, pazia huondolewa.
  • 7:16 - 7:20
    Neno la Mungu ni mbegu ya maisha ya
    kiungu
  • 7:20 - 7:25
    ambayo huja ndani ya mioyo yetu
    na kusababisha imani kukua.
  • 7:25 - 7:31
    Maono hayo ni kwa wakati ulioamriwa
    (Habakuki 2:3).
  • 7:31 - 7:34
    Sasa, muda umewadia
  • 7:34 - 7:38
    Maono ni kwa ajili kumuunganisha mwanadamu
    kwa Mungu tena.
  • 7:38 - 7:44
    kupitia Neno Lake, kwa Roho Wake,
    ili kuujenga Mwili wa Kristo.
  • 7:44 - 7:49
    na kushirikiana na mtandao wa makanisa
    kote ulimwenguni.
  • 7:49 - 7:54
    Maono haya yanaendana na wito na
    zawadi ya Mungu katika maisha yetu.
  • 7:54 - 7:59
    Mwamba ulioanguka kutoka Mbinguni
    ni Neno la Ufalme
  • 7:59 - 8:04
    kama Yesu alivyosema katika Mathayo 13:19.
  • 8:04 - 8:07
    Maono yetu ni kusaidia kuingiza Neno
    katika mioyo ya watu -
  • 8:07 - 8:11
    kwa sababu ni pale tu ndipo linafanya kazi
    kwa ufanisi.
  • 8:11 - 8:16
    Kama Biblia inavyosema Katika kitabu cha
    2 Wakorintho 3:3 - Wacha nikusomee;
  • 8:17 - 8:21
    Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua
    iliyoandikwa na Kristo,
  • 8:21 - 8:22
    matokeo ya kazi yetu.
  • 8:22 - 8:26
    Barua hii haikuandikwa kwa wino bali kwa
    Roho wa Mungu aliye hai,
  • 8:26 - 8:32
    si juu ya vibao vya mawe, bali juu ya
    vibao vya mioyo ya wanadamu.
  • 8:32 - 8:36
    Katika miongo miwili iliyopita chini ya
    ushauri wa Nabii TB Joshua,
  • 8:36 - 8:40
    mwingiliano wetu na maelfu ya waumini na
    viongozi wa makanisa ulimwenguni kote
  • 8:40 - 8:44
    na maswali ya mara kwa mara yaliyoulizwa
    na wengi wakati wa mihadhara
  • 8:44 - 8:48
    yamevuta mtazamo wetu kwenye upande
    wa vitendo wa Ukristo,
  • 8:48 - 8:53
    Namaanisha, matembezi yetu
    ya kila siku na Roho Mtakatifu:
  • 8:53 - 8:57
    jinsi ya kukuza ufahamu wa kiroho,
    jinsi ya kusikia kutoka kwa Mungu,
  • 8:57 - 9:01
    jinsi ya kujenga imani ya mtu katika
    hali ya kutokuwa na uhakika wa maisha.
  • 9:01 - 9:04
    Masuala haya ya msingi na mengine
    yatashughulikiwa
  • 9:04 - 9:06
    chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu
  • 9:06 - 9:11
    kupitia vipindi vya ufundishaji wa kina
    na muda wa maswali shirikishi na majibu.
  • 9:11 - 9:16
    Maono yetu pia yanakumbatia
    makanisa ya mtaani.
  • 9:16 - 9:21
    Tunataka kushirikiana na mtandao wa
    huduma mbalimbali
  • 9:21 - 9:28
    ili kutoa ujuzi wetu, uzoefu, na karama
    za kiroho kama Roho anavyoongoza.
  • 9:28 - 9:35
    Hadi kanisa la leo linatambua kwamba
    roho ya mwanadamu ni chemchemi ya imani,
  • 9:35 - 9:39
    hapo ndipo Roho Mtakatifu atakapohusika
    katika mambo yetu.
  • 9:39 - 9:42
    Jiunge nasi katika Chuo Kikuu cha Mungu
  • 9:42 - 9:46
    Maarifa ya kimwili hukoma,
    mara ufunuo unapowadia.
  • 9:46 - 9:48
    Kama mshauri wetu, Nabii TB Joshua
    alivyotufundisha,
  • 9:48 - 9:55
    “Katika Chuo Kikuu cha Mungu, hata uwe
    na kipaji gani, hutapandishwa maradufu,
  • 9:55 - 10:00
    lazima usome kila kozi kwani
    kila kozi ina kusudi lake.”
  • 10:00 - 10:02
    Kwa hiyo, unahitaji nini?
  • 10:02 - 10:04
    Moyo wazi.
  • 10:04 - 10:09
    Ni nyenzo gani zinazohitajika kuchukua
    kila kozi - kutokukata tamaa,
  • 10:09 - 10:11
    kutafuta njia mbadala au kutokukata tamaa
  • 10:11 - 10:14
    kwa vipigo vya kikatili vya maisha
    vya mara kwa mara?
  • 10:14 - 10:23
    Unyenyekevu, imani, uvumilivu, saburi,
    msamaha na upendo bila kutarajia.
  • 10:23 - 10:25
    Nani anasahihisha kazi zetu?
  • 10:25 - 10:27
    Roho Mtakatifu.
  • 10:27 - 10:34
    Mungu anakungojea mahala pa Roho wake.
Title:
RACINE & RUTH: UNGANA NASI KATIKA CHUO KIKUU CHA MUNGU!
Description:

Kutoka kwenye miaka mingi ya kujifunza chini ya na kutembea na Jenerali wa Mungu, Nabii TB Joshua, hadi siku alipoitwa Nyumbani, shauku imewaka mioyoni mwetu ya kutoa hazina ambayo Mungu ametupa - Neno lililo hai kwa nguvu ya Mungu. Roho takatifu!

more » « less
Video Language:
English
Team:
The University of God
Duration:
10:41

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions