-
Je! unajua kuwa wewe ni kazi ya sanaa?
-
Mwanadamu ndiye zao kuu la Mungu.
-
Ninamaanisha, mtu aliyeundwa kufikiria,
-
kuzungumza na kutenda pamoja na Mungu.
-
Je, unaishi sambamba na Mungu?
-
Je, hali yako ikoje mbele za Mungu leo?
-
Bila neema ya Roho Mtakatifu inayokaa ndani yake,
-
mwanadamu ni kivuli tu cha yule aliyeumbwa na Mungu!
-
Mwanadamu ambaye Mungu alimuumba
-
hakuwa mtu wa kimwili tu
-
anayetawaliwa na hisi zake
-
bali ni mjumbe kati ya ulimwengu
-
unaoonekana na usioonekana.
-
Mungu na mwanadamu walikuwa wakizungumza
-
pamoja kama marafiki.
-
Lakini siku moja, mwanadamu
-
alivunja uhusiano kwa kutokutii
-
na akaenda mbali na Mungu.
-
Kisha akaenda mbali zaidi hadi,
-
mwishowe akaondoka nyumbani.
-
Aliiacha nchi yake ya asili, Edeni,
-
ambako aliishi na Mungu.
-
Alihama kutoka kwenye uwepo wa Mungu.
-
Tangu wakati huo, Mungu amekuwa
-
na shauku ya kuweza
kuzungumza tena
-
na rafiki yake wa zamani
-
lakini mwanadamu,
-
kwa kuondoka katika uwepo wa Muumba wake,
-
alipoteza lugha yake mama.
-
Namaanisha, alipoteza lugha yake
ya asili na Mungu.
-
Na akawa hawezi kuwasiliana na
Muumba wake katika roho na kweli.
-
Mwanadamu wa kawaida hawezi kusikia
au kuzungumza na Mungu;
-
hii ndiyo changamoto tunayokabiliana
nayo leo.
-
Ingawa Mungu huzungumza tena na tena,
-
wengi sana hawapo makini kusikia
kile Anachosema (Ayubu 33:14).
-
Ukimya ni mgumu kwa Mungu.
-
Kama vile baba wa mwana mpotevu
-
alivyokuwa na shauku ya kumwona
mwanawe akirudi nyumbani,
-
Mungu ana shauku ya kuwa na uhusiano
wa karibu tena na mwanadamu,
-
Rafiki yake wa zamani.
-
Ndiyo maana ilimbidi achague lugha
-
ambayo mwanadamu angeelewa.
-
Kwa hivyo alimtuma Mwanawe,
Yesu Kristo duniani kumrudisha mwanadamu,
-
Rafiki Yake wa zamani, arudi Kwake tena.
-
Mungu aliheshimu lugha ya mwanadamu
kwa kumwita Yesu Neno.
-
Neno alifanyika mwili na akaingia
ulimwenguni.
-
Yesu ni Mungu akijieleza Mwenyewe
-
kwa lugha ambayo mwanadamu
anaweza kuelewa,
-
lugha ya roho na uzima (Yohana 6:63).
-
Je, ni kwa muda gani tutaendelea kuwaza,
-
kuzungumza na kuishi katika hali
ya kimwili
-
ilihali Yesu anakungoja katika mahala
pa Roho Wake?
-
Ni wasaa wa kurudi tena katika chuo
cha Mungu
-
Na kuanza kumtafuta Roho.
-
Kutoka kwenye miaka mingi ya kujifunza
chini ya, na kutembea
-
pamoja na Jenerali wa Mungu, Nabii
TB Joshua,
-
hadi alipoitwa Nyumbani Mbinguni,
-
shauku imewasha mioyoni mwetu
kutoa hazina tuliyopewa na Mungu;
-
Neno lililo hai katika nguvu za
Roho Mtakatifu!
-
Maandishi ya Neno hayawezi kusonga,
-
haiwezi kufanya kazi bila
uhai wa Mungu (Yohana 6:63).
-
Kila Neno la Mungu ni Roho na uzima.
-
Na ni uzima halisi wa Mungu
-
katika Neno hilo unaotia nguvu,
nishati katika Neno.
-
Hili ndilo Neno linaloponya, kuokoa,
kukomboa
-
na kumwezesha mwamini kuishi maisha
ya ushindi katika Kristo.
-
Kama vile Simoni Petro katika Yohana 6:68,
-
tumegundua kwamba hakuna mbadala wa Yesu
-
kwa sababu Yeye peke yake ndiye mwenye
Maneno ya uzima wa milele.
-
Baada ya mshauri wetu kuitwa Nyumbani
tarehe 5 Juni 2021,
-
kama wanafunzi wa zamani,
Yesu alipopaa Mbinguni,
-
tumekuwa tukingoja katika imani.
-
Na katika tarehe 8 ya Desemba 2021,
nilipokea ufunuo toka kwa Mungu.
-
Na nikapewa jina la
'Chuo Kikuu Cha Mungu'.
-
[muziki]
-
Nilijikuata katika chumba cha glasi
ndani ya pango
-
lisilokuwa na sehemu ya kutokea
-
Ghafla mwamba wenye nguvu ukaja
kutoka Mbinguni
-
na kugonga mlima wa mawe.
-
ulitoboa lile pango.
-
Mlima ulitikisika, lakini nilibaki
thabiti ndani ya chumba cha kioo.
-
Jiwe lilitoboa kwenye mlima wa mawe.
-
Niliangalia.
-
Kisha nikatoka na kutembea.
-
Nilisimama na kushtuka pale nilipoona
-
mwamba ulikuwa umechimba handaki zuri kabisa
iliyotengenezwa kwa dhahabu!
-
Nilijiambia, lazima kuwe na maji
mwishoni mwa handaki hili.
-
Nilianza kutembea.
-
Ghafla sauti ikasikika kutoka juu:
-
“Baki hapo ulipo. Usiingie!
Maji yanakujia.”
-
Nilisimama na kubaki pale nilipokuwa.
-
Niliposimama tuli, ghafla niliona maji
-
yakitiririka kutoka mwishoni mwa handaki
kuelekea kwangu.
-
Maji yalikuwa safi, yakimeta kwa uhai.
-
Yalitiririka karibu zaidi
-
mpaka yakafika kwenye vidole vyangu
-
na kunawisha miguu yangu kama wimbi
kwenye ufuo wa bahari.
-
Nilipokuwa nikitafakari juu ya ono hilo,
-
moyo wangu ulinisukuma kwenye
Kitabu cha Danieli 2:44. Nitasoma;
-
Na katika siku za wafalme hao Mungu
wa mbinguni atausimamisha ufalme
-
ambao hautaangamizwa milele, wala watu
wengine hawataachiwa enzi yake;
-
bali utavunja falme hizi zote
vipande vipande na kuzikomesha,
-
nao utasimama milele na milele.
-
Hii ndiyo maana ya maono ya mwamba
uliochongwa kutoka mlimani,
-
lakini si kwa mikono ya binadamu
— mwamba uliovunja
-
chuma, shaba, udongo, fedha na dhahabu
vipande vipande.
-
Kusudi la mwamba ni nini?
-
Kama inavyosema katika kitabu cha
Yeremia 1:10, nitasoma;
-
angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa
na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa,
-
na kuharibu, na kuangamiza;
ili kujenga na kupanda.
-
Kusudi la mwamba ni kuondoa kizuizi kati ya
moyo wetu na Mungu.
-
Wakati mtu anapokabidhi moyo wake kwa
Roho Mtakatifu, pazia huondolewa.
-
Neno la Mungu ni mbegu ya uzima wa kiungu
-
ambayo huja ndani ya mioyo yetu
na kusababisha imani kukua.
-
Maono hayo ni ya wakati uliowekwa (Habakuki 2:3).
-
Maono ni kuunganisha mwanadamu na Mungu
-
kupitia Neno Lake, kwa Roho Wake,
ili kuujenga Mwili wa Kristo.
-
na kushirikiana na mtandao wa makanisa
kote ulimwenguni.
-
Maono hayo yanaendana na wito na
zawadi ya Mungu katika maisha yetu.
-
Mwamba ulioanguka kutoka Mbinguni
ni Neno la Ufalme
-
kama Yesu alivyosema katika Mathayo 13:19.
-
Maono yetu ni kusaidia kuingiza Neno
katika mioyo ya watu -
-
kwa sababu ni pale tu ndipo linafanya kazi
kwa ufanisi.
-
Katika miongo miwili iliyopita chini ya ushauri
wa Nabii TB Joshua,
-
mwingiliano wetu na maelfu ya waumini na
viongozi wa kanisa ulimwenguni kote
-
na maswali ya mara kwa mara yaliyoulizwa
na wengi wakati wa mihadhara
-
yamevuta mtazamo wetu kwa upande
wa vitendo wa Ukristo,
-
Namaanisha, matembezi yetu
ya kila siku na Roho Mtakatifu:
-
jinsi ya kukuza ufahamu wa kiroho,
jinsi ya kusikia kutoka kwa Mungu,
-
jinsi ya kujenga imani ya mtu katika
uso wa kutokuwa na uhakika wa maisha.
-
Masuala haya ya msingi na mengine
yatashughulikiwa
-
chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu
-
kupitia vipindi vya ufundishaji wa kina
na muda wa maswali shirikishi na majibu.
-
Maono yetu pia yanakumbatia
makanisa ya mtaa.
-
Tunataka kushirikiana na mtandao wa
huduma ili kutoa ujuzi wetu, uzoefu,
-
na karama za kiroho kama Roho anavyoongoza.
-
Hadi kanisa la leo linatambua kwamba
roho ya mwanadamu ni chemchemi ya imani,
-
hapo ndipo Roho Mtakatifu atakapohusika
katika mambo yetu.
-
Kama mshauri wetu, Nabii TB Joshua
alitufundisha,
-
“Katika Chuo Kikuu cha Mungu, hata uwe
na kipaji gani, hutapewa vyeo maradufu,
-
lazima usome kila kozi kwa
kila kozi ina kusudi lake.”
-
Kwa hiyo, unahitaji nini?
-
Moyo wazi.
-
Ni nyenzo gani zinazohitajika kuchukua
kila kozi - kutokukata tamaa,
-
kutafuta njia mbadala au kukata tamaa kwa
vipigo vya kikatili vya maisha mara nyingi?
-
Unyenyekevu, imani, saburi, saburi,
msamaha na upendo bila kutarajia.
-
Nani anaashiria kazi yetu?
-
Roho Mtakatifu.