Je dini yangu inasema nini hasa kuhusu wanawake?
-
0:01 - 0:04Njiani kufika hapa,
-
0:04 - 0:08nilikuwa na mazungumzo mazuri na
mtu aliyekuwa anakaa pembeni yangu kwenye -
0:08 - 0:11ndege. Alinambia
-
0:11 - 0:14"Hamna kazi tena USA,
-
0:14 - 0:16yaani sasa wamebuni kazi mpya:
-
0:16 - 0:21mwanasaikolojia wa paka,
mzungumzaji wa mbwa,msasi wa kimbunga." -
0:21 - 0:24Punde, aliniuliza,
-
0:24 - 0:27"Kwani wewe unafanya kazi gani?"
-
0:27 - 0:30Nikamjibu, "Mjenzi wa usalama?"
-
0:30 - 0:33(Vicheko)
-
0:34 - 0:39Kila siku, nafanya bidii
kuwazidishia wanawake sauti -
0:39 - 0:43na kuoneysha maisha yao na michango yao
-
0:43 - 0:46katika hatua za kutafuta usalama
na kutatua migogoro, -
0:48 - 0:53na kwa sababu ya kazi zangu,
natambua kwamba njia ya pekee -
0:53 - 0:55kwa kuhakikisha ushirikiano kamili
-
0:55 - 0:59wa wanawake duniani
ni kuchukua tena dini mikononi mwetu. -
0:59 - 1:03Sasa, jambo hilo ni muhimu sana kwangu.
-
1:03 - 1:07Kama muislamu na mwanamke kijana,
ninaijali dini yangu sana. -
1:08 - 1:12Inanipa nguvu na msimamo katika
kazi zangu kila siku. -
1:12 - 1:15Ndiyo sababu inayoniwezesha
kusimama hapa leo mbele yenu. -
1:16 - 1:20Lakini siwezi kutojali hasara kubwa
zilizofanyika kwa kutumia jina la dini, -
1:21 - 1:25si dini yangu tu, lakini
dini zote kubwa za dunia. -
1:25 - 1:30Kuyatumia vibaya na
kuyageuza maandiko ya kidini -
1:31 - 1:34kumebadilisha desturi zetu
za kijamii na kitamaduni, -
1:34 - 1:37sheria zetu, kila siku zetu,
-
1:37 - 1:40hadi kumefikia tusipoweza
kupagundua. -
1:40 - 1:45Wazazi wangu walihama Libya,
Afrika ya Kaskazini kwenda Kanada -
1:45 - 1:47mwanzoni mwa miaka 1980,
-
1:47 - 1:51na mimi niko katikati ya watoto 11.
-
1:51 - 1:53Ehee, 11.
-
1:54 - 1:55Lakini katika kukulia kwangu,
-
1:55 - 2:00niliwaona wazazi wangu, wote wacha Mungu
na waumini wa Akhera, wakisali na -
2:00 - 2:02kumshukuru kwa baraka zao,
-
2:02 - 2:06kama mimi, lakini zinginezo pia.
(Vicheko) -
2:07 - 2:10Walikuwa na huruma, wenye kuchekesha,
na wenye subira, -
2:10 - 2:15subira kubwa, aina inayofunzwa
kwa kuwalea watoto 11. -
2:16 - 2:18Pia walifanya haki.
-
2:18 - 2:22Sikuwahi kupaswa kuijua dini kwa
mtazamo wa kitamaduni tu. -
2:23 - 2:25Nilitendewa sawasawa na kaka zangu,
na sisi sote -
2:25 - 2:27tulikuwa tunatarijiwa
kufanya sawasawa. -
2:27 - 2:32Sikuwahi kuambiwa kwamba Mungu
huhukumu tofauti kwa jinsia. -
2:33 - 2:40Wazazi wangu walimwona Mungu kuwa
Mwingi wa Rehema, Fadhila na rizki -
2:40 - 2:42na mimi nilichukulia
msimamo wao. -
2:43 - 2:46Kwa uhakika, malezi yangu yalikuwa
na faida zake. -
2:47 - 2:51kuwa katikati ya watoto 11
ni kama Diplomasia 101. (Vicheko) -
2:52 - 2:55Mpaka leo, watu huniuliza wapi
nilipokwenda skule, -
2:55 - 2:58kama, “Ulienda Skule ya
Kennedy ya Serikali?" -
2:58 - 2:59na mimi huwatazama na
kuwambia, “Hapana, -
2:59 - 3:03Nimeenda Skule ya Murabit ya
Mambo ya Kimataifa.” -
3:03 - 3:08Ni maalum sana. Ungeongea na
Mamangu kwa kujipatia nafasi -
3:08 - 3:11Lakini kwa bahati yenu, yupo leo.
-
3:12 - 3:16Lakini kuwa miongoni wa watoto 11,
na kuwa na ndugu 10, -
3:16 - 3:20kunafundisha mengi kama
mifumo ya mamlaka na muungano. -
3:20 - 3:23Kama kuzingatia lengo;
useme haraka au -
3:23 - 3:26usiseme sana, kwa sababu
utadakiwa mazungumzo kila mara. -
3:26 - 3:28Kunafundisha umuhimu wa kuwa
mjumbe mzuri. -
3:29 - 3:33Uyaulize maswali kwa mpango kwa
kupata jibu unalolitaka, na -
3:33 - 3:36ujue kusema 'la' kwa mpango pia
kwa kufuliza usalama. -
3:37 - 3:41Lakini funzo muhimu sana
nililolipata kutoka utoto wangu -
3:41 - 3:44lilikuwa umuhimu wa kuwa na nafasi kwenye
meza. -
3:45 - 3:48Taa yake ndogo mamangu ilipovunjika,
alivyoipenda sana, ilinilazimu niwepo -
3:48 - 3:53wakati alipochunguza ilikuwaje,
ili nijitetee, -
3:54 - 3:57kwa sababu kama hupo,
lawama inakuangukia kwako, -
3:57 - 4:00na kabla hujagundua, utakuwa umeadhibiwa.
-
4:00 - 4:03Kwa uhahika, sijapewa
adhabu mimi mwenyewe. -
4:04 - 4:09Nilipokuwa na miaka 15 mwakani 2005,
nikatimiza skule ya sekondari nikahamia -
4:09 - 4:11Kanada-- Saskatoon --
-
4:12 - 4:16Ila Zawiya, Libya,
mji wa nyumbani wa wazazi wangu, -
4:16 - 4:18mji wa kidesturi sana.
-
4:18 - 4:23Fikiri, muda huo niliwahi kufika
Libya kwa ajili ya matembezi tu, -
4:23 - 4:28na kama msichana wa miaka 7,
ilipendeza sana. -
4:28 - 4:32Ilikuwa aiskrimu na pwani na jamaa
wenye furaha. -
4:34 - 4:38niligundua haiko vilevile kama
msichana wa miaka 15. -
4:38 - 4:44Nikakutana upesi na mambo ya dini ya
kiutamaduni. -
4:45 - 4:49Maneno ya "haramu" --
lenye maana ya kukatazwa kidini -- -
4:49 - 4:52na "aibu" -- lenye maana ya kutofaa
kimaadili -- -
4:52 - 4:55yalibadilishanwa bila mpango.
-
4:55 - 4:59kama yalikuwa na maana moja na
adhabu moja vilevile. -
5:00 - 5:04Nikajikuta sana katika mazungumzo na
wenzangu wa skule -
5:04 - 5:08na wa kazi, profesa, rafiki zangu na hata
jamaa zangu, -
5:08 - 5:12nikaanza kujiuliza kuhusu desturi zangu
na malengo yangu. -
5:12 - 5:16Na hata na msingi mzuri niliopokea
kutoka wazazi wangu, -
5:16 - 5:20Nilijikuta nikajiuliza kuhusu nafasi
ya mwanamke katika dini yangu. -
5:22 - 5:24Kule kwenye Skule ya Murabit ya Mambo
ya Kimataifa, -
5:24 - 5:27tunapenda sana kufanya mjadala,
-
5:27 - 5:33na sheria ya kwanza ni fanya utafiti wako,
na hivyo ndivyo nilivyofanya mimi, -
5:33 - 5:36Ikanishangaza sana vipi ilikuwa rahisi
-
5:36 - 5:40kuwagundua wanawake katika Uislamu
waliokuwa viongozi, -
5:40 - 5:44wavumbuzi, wenye nguvu --
-
5:44 - 5:47za kisiasa, za kiuchumi hata za kijeshi.
-
5:47 - 5:51Khadija aliziendesha fedha za
harakati za Kiislamu -
5:51 - 5:53katika siku zake za mwanzo.
-
5:53 - 5:55Tusingekuwepo hapa leo bila michango yake.
-
5:56 - 5:58Kwa nini tusifundishwe kisa chake?
-
5:58 - 6:01Kwa nini tusifundishwe
visa vya hao wanawake? -
6:01 - 6:04Kwa nini wanawake wapewe vyeo
vilivyotoka -
6:04 - 6:07zama zilizotangulia mafunzo ya dini yetu?
-
6:07 - 6:09Na kwa nini, kama sisi sote tuko sawasawa
machoni mwa Mungu, -
6:09 - 6:12hatuko sawasawa machoni mwa binadamu?
-
6:13 - 6:17Hayo yalinipeleka kufikiria mafunzo
yangu ya utotoni. -
6:18 - 6:22Anayeamua, na kuwa na mamlaka
juu ya ujumbe, -
6:22 - 6:25anayo nafasi kwenye meza,
-
6:25 - 6:29na kwa bahati mbaya, katika dini zote
za kidunia, -
6:29 - 6:31hao si wanawake.
-
6:32 - 6:35Taasisi za kidini
zinatawaliwa na wanaume -
6:35 - 6:37na kuendeshwa na viongozi vya kiume,
-
6:37 - 6:41na wanabuni sera zinazowafaa wanaume tu,
-
6:41 - 6:45na ila tunaweza kubadilisha mfumo huo
kabisa, kwa kweli hatuwezi -
6:45 - 6:48kutarajia wanawake kushiriki
kwa ukamilifu -
6:48 - 6:50katika uchumi au siasa.
-
6:52 - 6:54Msingi wetu umevunjika.
-
6:56 - 7:00Mamangu husema, "huwezi kujenga nyumba
nzima juu ya msingi mbovu". -
7:03 - 7:09Mwakani 2011, Mapinduzi ya Libya yaliripuka
na aila yangu walikuwepo mistari ya mbele. -
7:10 - 7:13Kuna jambo moja la kushangaza
linalojitokeza katika vita, -
7:13 - 7:15kama mageuzo ya kiutamaduni,
kwa muda mfupi tu. -
7:16 - 7:19Kwa mara ya kwanza nilijisikia
ilikubaliwa, au hata -
7:19 - 7:22ilisisitizwa kwa mimi kujihusisha
na mambo. -
7:22 - 7:24Ilihitajika.
-
7:25 - 7:27Mimi na wanawake wengine walipewa nafasi
kwenye meza. -
7:27 - 7:31Hatukuwa wasaidizi wa wanaume tu.
-
7:31 - 7:32Tulichangia katika uamuzi.
-
7:32 - 7:36Tulichangia katika kutoa taarifa.
Tulikuwa muhimu sana. -
7:36 - 7:40Na mimi nilitaka, nilihitaji mageuzo hayo
kutoondoka. -
7:43 - 7:45Lakini niligundua si rahisi
kuwa nilivyotaka. -
7:45 - 7:49Ilichukua wiki chache tu kabla hao
wanawake niliowafanya nao kazi -
7:49 - 7:52walikuwa wanarejea katika kazi zao za
zamani, -
7:52 - 7:56na wengi walipewa maneno ya
kusisitizwa -
7:56 - 7:59kutoka kwa viongozi wa kidini na
vya kisiasa, wengi wao -
7:59 - 8:02walijaribu kuthibitisha hoja
zao kwa maandishi ya kidini. -
8:02 - 8:06Ndivyo walivyojipatia mikono ya
watu katika hoja zao. -
8:07 - 8:12Mwanzoni, nilizingatia kuwapa
wanawake nguvu katika siasa na uchumi. -
8:12 - 8:15Nikafikiri ingeliongoza
mabadiliko ya kiutamaduni na kijamii. -
8:16 - 8:20Niligundua, ilifanikiwa kidogo tu, lakini
sio sana. -
8:20 - 8:24Nikaamua kuitumia njia yao wale
viongozi wa kidini -
8:24 - 8:28nikaanza kuthibitisha hoja zangu kwa
maandishi ya kiislamu pia. -
8:29 - 8:33Katika miaka 2012 na 2013, shirika langu
liliongoza kampeni ya pekee iliyokuwa -
8:33 - 8:36kubwa na pana kuliko zote Libya.
-
8:37 - 8:40Tulipenyeza nyumbani, skuleni na
vyuoni, hata misikitni. -
8:41 - 8:44Tulizungumza na watu 50,000
uso kwa uso, na mamia ya maelfu zaidi -
8:45 - 8:47kwa njia za
matangazo ya kubandika, -
8:47 - 8:49matangazo kwenye tv na kwenye radio.
-
8:51 - 8:53Labda mnajiuliza, shirika la
haki za wanawake -
8:53 - 8:57waliweza kufanya hivyo vipi katika jamii
ilyopingana na sisi -
8:57 - 8:58kabisa mwanzoni.
-
8:59 - 9:02Niliyatumia maandishi ya kiislamu.
-
9:02 - 9:06Nilitumia aya za Korani na misemo ya
Mtume Mohammed, -
9:07 - 9:11Hadithi zake, misemo yake ambayo ni,
kwa mfano, -
9:12 - 9:15"Mtu bora ndiye anayefanya
wema kwa familia yake." -
9:15 - 9:18"Usimruhusu mtu kumdhulumu mwingine."
-
9:19 - 9:24Kwa mara ya kwanza, hotuba za Ijumaa
kutoka kwa imamu wa kienyeji -
9:24 - 9:26zilitangaza haki za wanawake.
-
9:26 - 9:30zilizungumzia masuala yasiyo kawaida, kama
vurugu ya nyumbani. -
9:31 - 9:33Sera zilibadilishwa.
-
9:34 - 9:39Katika jamii fulani, ilitubidi
kusema lile Azimio -
9:39 - 9:42la Kimataifa la Haki ya Wanadamu
mlilopingana nayo -
9:42 - 9:45kwa sababu haikuandikwi na watalaamu
wa kidini, -
9:45 - 9:49eti, misingi yote ile imo kitabu chetu.
-
9:50 - 9:53Yaani, Shirika la Umoja wa Mataifa
lilituiga tu. -
9:56 - 9:59Kwa kuubadilisha ujumbe wenyewe,
tuliweza kuitoa -
9:59 - 10:03sura mpya iliyotangaza haki za wanawake
Libya. -
10:03 - 10:06Ni jambo ambalo sasa limeigwa duniani,
-
10:09 - 10:12na sisemi ni rahisi--- niamini,
si rahisi kabisa. -
10:13 - 10:17'Liberals' watasema unaitumia dini
na kukuita 'conservative' mbaya. -
10:17 - 10:20na 'conservatives' watakupa
matusi mengi. -
10:20 - 10:24Mimi mwenyewe nimeyapata mengi, kama
"Wazazi wako hawaaibiki na wewe?" -- -
10:24 - 10:26sio kweli;
wao wananipenda kuliko wote -- -
10:26 - 10:29au "Hutoishi kuona siku
yako ya kuzaliwa tena" -- -
10:29 - 10:31tena sio kweli, nimeshaiona.
-
10:33 - 10:37Na bado, ninaamini kabisa
-
10:37 - 10:40kwamba haki za wanawake
na dini zinaweza kuendana. -
10:42 - 10:46Lakini lazima tupewe nafasi kwenye meza.
-
10:46 - 10:49Tusiache kupigania
nafasi yetu, kwa sababu -
10:49 - 10:55kwa kukaa kimya, tunaruhusu mateso na
dhuluma za wanawake duniani kuendelea. -
10:56 - 10:59Kwa kudai tutapigania haki za wanawake
-
10:59 - 11:02na kupigania ugaidi kwa kutumia
mabomu na vita, -
11:03 - 11:07tunaharibu jamii za kienyeji zinazohitaji
kuyashughulikia masuala hayo -
11:08 - 11:11ili yawezekane kuendelea.
-
11:12 - 11:16Sio rahisi, kushindana na taarifa za dini
za kupotosha. -
11:17 - 11:22Utapata vyako vya matusi na dhihaka na
vitisho. -
11:22 - 11:24Lakini ni lazima ifanyike.
-
11:24 - 11:29Hatuna budi ila kuuchukua tena
ujumbe wa haki za binadamu, -
11:29 - 11:33maadili ya dini yetu, si kwa ajili yetu,
-
11:33 - 11:35na si kwa ajili ya
wanawake wenu tu, -
11:35 - 11:36si kwa ajili ya
wanawake humu leo, -
11:36 - 11:39hata si kwa ajili ya
wanawake kule nje, -
11:40 - 11:43bali kwa ajili ya jamii ambazo
zingebadilika kuwa nzuri -
11:43 - 11:46kwa mashirikiano ya wanawake.
-
11:46 - 11:49Na jinsi ya pekee sisi tunavyoweza
kufanya hivyo, -
11:49 - 11:50njia yetu moja tu,
-
11:50 - 11:53ni kupata nafasi na kukaa daima,
kwenye meza. -
11:54 - 11:55Asante.
-
11:55 - 11:58(Makofi)
- Title:
- Je dini yangu inasema nini hasa kuhusu wanawake?
- Speaker:
- Alaa Murabit
- Description:
-
Familia ya Alaa Murabit ilihamia Canada kutoka Libya alipokuwa na miaka 15. Kabala alijiona yuko sawa na kaka zake, lakini katika mazingira haya mapya alihisi vizuizi kuhusu yale mafanikio anayoweza kuyapata. Kama mwanamke wa Kiislam , alijiuliza kama haya kweli ni mafundisho ya dini? Kwa namna ya kuchangamsha anatushirikisha ugunduzi wa mifano ya viongozi wanawake katika historia ya imani yake - Na jinsi alivyoanzisha kampeni ya kupigania haki za wanawake kwa kutumia mistari ya Korani.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 12:13
![]() |
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for What my religion really says about women | |
![]() |
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for What my religion really says about women | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for What my religion really says about women | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for What my religion really says about women | |
![]() |
Hope Crick edited Swahili subtitles for What my religion really says about women | |
![]() |
Hope Crick edited Swahili subtitles for What my religion really says about women | |
![]() |
Hope Crick edited Swahili subtitles for What my religion really says about women | |
![]() |
Hope Crick edited Swahili subtitles for What my religion really says about women |