UKOMBOZI Kutokana na Kupooza Usingizi; UPONYAJI Kutoka kwenye Maumivu ya Mgongo!
-
0:00 - 0:05Ndugu Chris alipoomba,
niliweka mkono wangu kwenye mgongo wangu wa chini -
0:05 - 0:12na ghafla nilihisi joto kwenye sehemu ya chini ya mgongo wangu
na nilihisi vuguvugu kwenye mwili wangu. -
0:12 - 0:16Kuanzia siku iliyofuata,
nilijihisi mwepesi na utulivu. -
0:18 - 0:27Maumivu hayo yanayopinga matibabu -
aponywe sasa hivi! -
0:27 - 0:37Taabu hiyo inayoonekana kukaidi
suluhisho la matibabu - iponywe leo! -
0:37 - 0:40Pokea uponyaji kwa jina kuu la Yesu!
-
0:42 - 0:47Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi hii.
-
0:47 - 0:50Jina langu ni Evelyn. Ninatoka Manipur, India.
-
0:50 - 0:54Nimekuwa nikisumbuliwa na
maumivu ya kiuno kwa karibu miaka kumi, -
0:54 - 0:58na iliathiri sana kila eneo la maisha yangu.
-
0:58 - 1:04Kwa mfano, sikuweza kuketi kwa zaidi ya saa mbili au kufanya kazi za nyumbani.
-
1:04 - 1:06Na sikuweza kubeba vitu vizito.
-
1:06 - 1:13Na iliniathiri sana kimwili, kiakili, kiroho, kihisia na kisaikolojia.
-
1:13 - 1:20Kwa kuwa mwanafunzi wa uuguzi, ilikuwa vigumu sana kwangu kuendelea na uuguzi wangu.
-
1:20 - 1:23Ilibidi niketi kwa muda mrefu.
-
1:23 - 1:29Na maumivu yangu ya mgongo yalianza kuwa mbaya zaidi.
-
1:29 - 1:32Nilipata nafuu
pale tu nilipojilaza. -
1:32 - 1:39Mara nyingi, nilikuwa nikilala chini na ilikuwa ikiathiri sana masomo yangu pia.
-
1:39 - 1:47Kila nilipojaribu kuteremka kutoka kitandani, nilihisi michirizi ya maumivu.
-
1:47 - 1:52Niliifahamu TV ya Moyo wa Mungu kupitia kwa rafiki wa kaka yangu.
-
1:52 - 1:57Nilikuja kujua Septemba 6, na
nikajiunga na huduma Septemba 7. -
1:57 - 2:03Nilituma ombi la maombi siku yenyewe, na nikapata jibu la kujiunga mnamo Septemba 7.
-
2:03 - 2:07Lakini wakati huo, nilikuwa na masuala mengi sana.
-
2:07 - 2:10Kwa sababu nilikuwa katika mji wangu,
nilikuwa na masuala mengi na mtandao wangu -
2:10 - 2:14Niliweza tu kujiunga kwa dakika 10-20
wakati Ndugu Chris aliomba, -
2:14 - 2:16lakini sikuweza kujiunga hadi mwisho.
-
2:16 - 2:18Na nilikuwa na huzuni sana wakati huo.
-
2:18 - 2:22Wiki hiyo, nilituma
ombi lingine la maombi na nikapata jibu -
2:22 - 2:25ili kujiunga na Ibada ya Maombi Shirikishi ya moja kwa moja mnamo Oktoba 5.
-
2:25 - 2:31Ndugu Chris alipoomba,
niliweka mkono wangu kwenye mgongo wangu wa chini -
2:31 - 2:37na ghafla nilihisi joto kwenye sehemu ya chini ya mgongo wangu
na nilihisi vuguvugu kwenye mwili wangu. -
2:37 - 2:44Kuanzia siku iliyofuata,
nilihisi mwepesi na mtulivu. -
2:44 - 2:49Nilihisi uhuru mkubwa kutoka kwenye
uzito na maumivu yote. -
2:49 - 2:53Lazima niandikie
maelezo yangu ya uuguzi na kukaa kwa muda mrefu. -
2:53 - 2:58Na baadaye, nilikaa kwa zaidi ya masaa matatu - lakini hakuna kilichotokea.
-
2:58 - 3:03Hakukuwa na kitu kama maumivu makali
au uzito katika mwili wangu. -
3:03 - 3:04Maumivu yameisha kabisa!
-
3:04 - 3:09Ninaweza kusonga, kufanya
kazi zangu zote za nyumbani na kukaa kwa muda mrefu. -
3:09 - 3:15Kama mwanafunzi wa uuguzi, taaluma hiyo ina shughuli nyingi lakini sasa ninaweza kusimamia vizuri sana.
-
3:15 - 3:21Ninaweza kuona mabadiliko makubwa kimwili, kiroho na kihisia.
-
3:21 - 3:25Ingawa wakati mwingine mimi huhisi huzuni,
sio kama hapo awali. -
3:25 - 3:30Hata kama nina mawazo mabaya au kukatishwa tamaa, si kama hapo awali
-
3:30 - 3:34Ninayakemea na kuomba. Ninahisi maendeleo kama haya katika maisha yangu ya kiroho!
-
3:34 - 3:40Jambo moja ambalo nilisahau kutaja ni kwamba
nilikuwa na ugonjwa huu wa kupooza. -
3:40 - 3:44Ningekabiliwa na shambulio katika ndoto zangu usiku.
-
3:44 - 3:50Kwa karibu miaka mitatu hadi minne,
nilikuwa na tatizo hili la kupooza usingizi. -
3:50 - 3:53Lakini sasa ninaweza kulala kwa amani sana!
-
3:53 - 3:59Ningependa kusema - haijalishi ni hali gani unapitia,
-
3:59 - 4:04haijalishi umetenda dhambi ngapi, mtegemee Mungu na umkimbilie Mungu.
-
4:04 - 4:08Badala ya kukata tamaa kwa Mungu na
kumkimbia, mkimbilie. -
4:08 - 4:11Suluhisho lako kuu liko kwa Mungu pekee.
-
4:11 - 4:17Na ningependa kusema kwamba hutatengwa kamwe na upendo wa Mungu,
-
4:17 - 4:19haijalishi unapitia nini
sasa hivi. -
4:19 - 4:22Ikiwa Mungu anaweza kufanya kwa ajili yangu,
anaweza kukufanyia wewe pia. -
4:22 - 4:27Mungu anatawala na anafanya kazi
katika kila eneo la maisha yetu. -
4:27 - 4:31Ningependa kumalizia na Maandiko haya - Yeremia 33:3.
-
4:31 - 4:36“Niite nami nitakuitikia na kukuambia mambo makubwa na yasiyochunguzika usiyoyajua.
- Title:
- UKOMBOZI Kutokana na Kupooza Usingizi; UPONYAJI Kutoka kwenye Maumivu ya Mgongo!
- Description:
-
"Ikiwa Mungu anaweza kunifanyia mimi, anaweza kukufanyia wewe pia!" Evelyn, mwanafunzi wa uuguzi kutoka India, alipokea uponyaji kutoka kwenye maumivu ya mgongo yaliyodumu na uhuru kutoka kwenye mashambulizi ya mapepo katika usingizi wake - baada ya kujiunga na Ibada Shirikishi ya Maombi pamoja na Ndugu Chris kwenye TV ya Moyo wa Mungu.
Ili kupokea maombi bila malipo kupitia Zoom kutoka kwa Ndugu Chris, wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom - na Timu ya God's Heart TV itawasiliana nawe hivi karibuni kupitia barua pepe kwa info@godsheart.tv
➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi Shirikishi - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live - Video Language:
- English
- Team:
God's Heart TV
- Duration:
- 05:07
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for DELIVERANCE From Sleep Paralysis; HEALING From Back Pain! | |
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for DELIVERANCE From Sleep Paralysis; HEALING From Back Pain! | |
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for DELIVERANCE From Sleep Paralysis; HEALING From Back Pain! | |
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for DELIVERANCE From Sleep Paralysis; HEALING From Back Pain! |