"MAUMIVU YAMETOWEKA!!!" | UPONYAJI wa Papo hapo Baada ya Maombi ya Mtandaoni!
-
0:01 - 0:05Ninashukuru sana!
Ninahisi kama mwanadamu sasa. -
0:05 - 0:09Ninaweza kula chochote
ninachotaka kula. niko huru sana. -
0:09 - 0:14Sina hata maumivu. Ninaweza kufanya mazoezi kama hivi. Ninaweza kufanya mazoezi kama hayo.
-
0:14 - 0:16Sijisikii maumivu yoyote.
-
0:19 - 0:21Sijisikii maumivu yoyote.
-
0:28 - 0:34Jeraha hilo la ndani - liponywe sasa hivi!
-
0:34 - 0:42Jeraha hilo la ndani - upone sasa hivi!
-
0:42 - 0:46Uwe mzima, katika jina la Yesu Kristo.
-
0:46 - 0:55Kila chanzo cha ugonjwa katika mfumo wako - safishwa leo!
-
0:55 - 0:58Oshelewa nje sasa hivi!
-
1:00 - 1:04Mimi ni Sylvia, ninajiunga kutoka Afrika Kusini.
-
1:04 - 1:12Nilijiunga na TV ya Moyo wa Mungu kwa ajili ya mafanikio katika nyanja zote za maisha yangu.
-
1:12 - 1:16Nilihisi kwamba kulikuwa na udumavu katika maisha yangu.
-
1:16 - 1:24Lakini kabla ya hapo, nilikuwa na hali ambayo haikuwa sehemu ya maombi yangu.
-
1:24 - 1:32Hali niliyokuwa nayo ilikuwa
ugonjwa wa uvimbe wa tumbo kwa muda wa mwaka mmoja. -
1:32 - 1:40Niligunduliwa na daktari na kwa sababu ya ugonjwa huo, nilikuwa kwenye dozi ya dawa.
-
1:40 - 1:45Nilikuwa nikisikia
maumivu makali sana ya kifua. -
1:45 - 1:53Na mara nyingi, ningehisi kichefuchefu na kupelekea kutapika.
-
1:53 - 2:04Pia, ningehisi maumivu kwenye tumbo la juu chini ya mbavu za kulia.
-
2:04 - 2:14Usiku, ningekuwa na tatizo ambalo
ningekuwa na hofu ya kulala -
2:14 - 2:23kwa sababu ya msukumo wa asidi ambayo ingekuja katika usingizi wangu wakati wa usiku.
-
2:23 - 2:29Lakini pia nilishauriwa na daktari kwamba
lazima nilale upande wangu wa kushoto. -
2:29 - 2:39Niliwekwa kwenye lishe na daktari na kulikuwa na chakula kingi ambacho sikuweza kula
-
2:39 - 2:45na vinywaji vingi, kama vile vinywaji baridi
na juisi, ambavyo sikuweza kunywa. -
2:45 - 2:50Ilinipa wakati mgumu sana,
kama mama pia - -
2:50 - 2:55kuandaa chakula cha familia ambacho unajua huwezi kula.
-
2:55 - 3:03Kwa hivyo nilituma ombi la maombi
katikati ya Machi 2024. -
3:03 - 3:13Nilipokea mwaliko wa kujiunga na Huduma ya Maombi ya Pamoja tarehe 6 Aprili 2024.
-
3:13 - 3:19Lakini kabla ya hapo, wiki hiyo
baada ya kupokea mwaliko, -
3:19 - 3:25Niliamka asubuhi na
kuhisi maumivu makali sana -
3:25 - 3:29kuanzia tumbo la chini hadi mgongoni.
-
3:29 - 3:35Na kilikuwa kitu kipya ambacho sikuwa nacho kabla ya kutuma ombi langu la maombi.
-
3:35 - 3:39Niliamua kwamba sitaenda
kumuona daktari -
3:39 - 3:45kwa sababu tayari nilikuwa nimepokea mwaliko wa Ibada ya Pamoja ya Maombi.
-
3:45 - 3:52Kwa hiyo niliweza tu kuyashighulikia yale maumivu makali
ya tumbo kwa kutumia dawa za kutuliza maumivu -
3:52 - 3:59kwa sababu nilimwamini Mungu kwamba kwa vile ningekuwa sehemu ya maombi, ningepata uponyaji wangu.
-
3:59 - 4:06Wakati wa maombi pamoja na Ndugu Chris, kwanza nilihisi joto fulani katika mwili wangu
-
4:06 - 4:12Nilihisi kama kulikuwa na mijongeo ndani yangu - kitu ambacho kilikuwa kikitokea.
-
4:12 - 4:17Nilihisi mijongeo, kutoka
nyuma hadi kwenye tumbo langu. -
4:17 - 4:22Nilihisi kutapika alipokuwa akiomba
kisha, nikatapika. -
4:22 - 4:26Baada ya Ibada ya Pamoja ya Maombi
kukamilika, -
4:26 - 4:30Nilihisi mwili wangu ulikuwa mwepesi sana.
-
4:30 - 4:39Kifua ambacho kwa kawaida kilikuwa kizito sana na chenye maumivu makali - maumivu yote yalikuwa yamekwisha.
-
4:39 - 4:45Maumivu ya tumbo ambayo nilikuwa nayo kwa wiki moja ambayo niliyashughulikia tu na dawa za kutuliza maumivu -
-
4:45 - 4:48nayo yalikwisha.
-
4:48 - 4:54Ninahisi wepesi sana na tangu wakati huo,
baada ya maombi, -
4:54 - 4:59Ninaweza kula kila kitu ambacho ninahisi kula.
-
4:59 - 5:05Vitu vyote ambavyo sikuwa nikila,
haikuwezekana kwangu kula - -
5:05 - 5:09sasa naweza kula kila kitu kwa utukufu wa Mungu.
-
5:09 - 5:16Ninalala vizuri sana, kama mtoto mchanga, na ninaweza kubadilisha pande kitu ambacho ni kizuri sana.
-
5:16 - 5:20Siku ya kwanza baada ya maombi, nililala vizuri sana
-
5:20 - 5:25kwa sababu hapo awali, wakati wote, ilibidi nilale tu upande huu wa kushoto wa mwili wangu.
-
5:25 - 5:30Kwa hiyo siku ya kwanza nililala upande
wa pili, nililala vizuri sana. -
5:30 - 5:36Ninashukuru sana!
Ninajihisi kama mwanadamu sasa. -
5:36 - 5:40Ninaweza kula chochote
ninachotaka kula. niko huru sana. -
5:40 - 5:48Mgongo wangu ni mzima kabisa. Kama unavyoona,
naweza kuzunguka. -
5:48 - 5:52Naweza kuinama. Mgongo wangu uko vizuri sana.
-
5:52 - 5:58Sina hata maumivu. Ninaweza kufanya mazoezi kama hivi. Ninaweza kufanya mazoezi kama hayo.
-
5:58 - 6:00Sijisikii maumivu yoyote.
-
6:00 - 6:05Ushauri wangu kwa watazamaji ni kwamba kuamini
ndio muunganisho wako. -
6:05 - 6:09Unapounganishwa leo,
fungua moyo wako -
6:09 - 6:14na utapata kile
ulichomwamini Mungu.
- Title:
- "MAUMIVU YAMETOWEKA!!!" | UPONYAJI wa Papo hapo Baada ya Maombi ya Mtandaoni!
- Description:
-
Sylvia kutoka Afrika Kusini alijiunga na Ibada ya Pamoja ya Maombi akiwa na masuala mengi ya kiafya - ingawa hakuyajumuisha katika ombi la maombi alilowasilisha kwa God's Heart TV. Wakati wa maombi na Ndugu Chris, Roho Mtakatifu - ambaye anajua YOTE kuhusu sisi - alimgusa kwa namna kuu, na kusababisha ushuhuda wa utukufu. Asante, Yesu Kristo!
Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom
➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Mwingiliano - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live - Video Language:
- English
- Team:
God's Heart TV
- Duration:
- 06:34
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for "THE PAIN HAS GONE!!!" | Instant HEALING After Online Prayer! | |
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for "THE PAIN HAS GONE!!!" | Instant HEALING After Online Prayer! | |
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for "THE PAIN HAS GONE!!!" | Instant HEALING After Online Prayer! |