< Return to Video

Jinsi nilivyopata KAZI iliyo sambamba na HATIMA yangu!! | Ushuhuda Wenye Motisha

  • 0:00 - 0:04
    Ingawa bado niliipata ofa ya kazi hiyo,
    bado nilimtafuta Mungu.
  • 0:04 - 0:09
    Kwa sababu nilielewa Alikuwa amenipa ndoto kuhusu kampuni ya awali, Kampuni A.
  • 0:09 - 0:13
    Na sasa fursa hii na
    Kampuni B ilikuwa imepatikana.
  • 0:13 - 0:16
    Kwa hiyo wakati huo nilitafuta uso wa Mungu.
  • 0:16 - 0:22
    USHUHUDA
    YV YA MOYO WA MUNGU
  • 0:23 - 0:33
    Ndiyo, watu wa Mungu, sasa hivi,
    ninazungumza na kila eneo la maisha yenu
  • 0:33 - 0:39
    ambapo umekuwa ukipata msongo wa mawazo.
  • 0:39 - 0:47
    Sasa hivi, pokea pumziko la Kimbingu
    kwa jina la Yesu Kristo!
  • 0:47 - 0:53
    Pumzika katika kazi yako! Pumzika katika biashara yako! Pumzika kwenye ndoa yako! Pumzika katika familia yako!
  • 0:53 - 0:56
    Pokea pumziko kutoka juu leo!
  • 0:58 - 1:01
    Jina langu ni Dumisani kutoka Zambia.
  • 1:01 - 1:05
    Ushuhuda wangu unahusu mafanikio ya kazi mwaka huu, 2024.
  • 1:05 - 1:12
    Yote ilianza 2022 nilipomaliza shule, na wakati huo nilikuwa nikitafuta kazi.
  • 1:12 - 1:18
    Nilikuwa nimehitimu kutoka China. Nimekuwa nikisoma nje ya nchi kwa zaidi ya miaka minne.
  • 1:18 - 1:23
    Na nilipokea digrii yangu ya kwanza
    kufikia mwisho wa mwaka wa 2022.
  • 1:23 - 1:26
    Kwa hiyo nilikuwa nimerudi Zambia,
    na kipindi hicho,
  • 1:26 - 1:31
    baada ya shahada yangu ndipo nilipolazimika
    kuanza kutafuta kazi.
  • 1:31 - 1:38
    Na katika hali hiyo, haikuwa rahisi hata kidogo kwa sababu ya ushindani wa soko la ajira.
  • 1:38 - 1:45
    Tunao wahitimu wengi ambao wana uwezo wa kupata kazi yoyote ile.
  • 1:45 - 1:49
    Lakini kwa upande wangu, nilikuwa pia nikijaribu kushindana katika soko hilohilo la ajira.
  • 1:49 - 1:52
    Nilisomea uhandisi wa umeme na elektroniki nchini China.
  • 1:52 - 2:03
    Ilinibidi nichukue hatua hiyo mbele ili kupata kazi inayolingana na taaluma yangu
  • 2:03 - 2:04
    na katika kisa hiki, ilikuwa ngumu sana.
  • 2:04 - 2:11
    Kufikia wakati huo, sikujua ni kazi gani ningeweza hata kuomba - iwe mafunzo au kujishikiza.
  • 2:11 - 2:15
    Kwa sababu wakati wa kukaa kwangu nchini Uchina,
    ambao ulikuwa wakati wa COVID,
  • 2:15 - 2:21
    ilikuwa ngumu sana kwangu kuwa na
    aina yoyote ya kujishikiza kikazi
  • 2:21 - 2:29
    au kupata uzoefu wowote wakati wa masomo yangu ambao unaweza kutumika katika kutuma maombi ya kazi kwa urahisi zaidi.
  • 2:29 - 2:33
    Kwanza kabisa, sina budi kusema kwamba
    Mungu amenisaidia sana.
  • 2:33 - 2:37
    Wakati huo nilikuwa nimeomba na kumtafuta Mungu juu ya kazi gani naweza kuomba.
  • 2:37 - 2:41
    Naweza kufanya nini? Je, ni aina gani ya nafasi ya kazi ninayopaswa kutafuta?
  • 2:41 - 2:43
    Na katika hali hiyo, Mungu aliniongoza kweli,
  • 2:43 - 2:49
    na kwa usadikisho huo, ilinisaidia kuanza kuangalia nafasi ya mwanafunzi aliyehitimu.
  • 2:49 - 2:55
    Na wakati huo, iligusa sana
    moyo wangu na kunihukumu.
  • 2:55 - 2:59
    Nilikuwa nimemshirikisha wazo mama yangu,
    na hivyo ndivyo nilianza kufanya utafiti zaidi.
  • 2:59 - 3:03
    Niliomba kwa Mungu na kutafuta mwongozo wake kwa sababu ya usadikisho huo huo -
  • 3:03 - 3:06
    kujua nini cha kufanya baadaye.
  • 3:06 - 3:12
    Kwa hiyo, wakati huo, nilijaribu kutuma ombi kwenye kampuni fulani ya uchimbaji madini katika nchi yangu.
  • 3:12 - 3:16
    Sikujua hata kuandika CV.
  • 3:16 - 3:23
    Sikujua jinsi ya kuangazia uzoefu niliokuwa nao nchini Uchina na mara nyingi,
  • 3:23 - 3:28
    watu wangeniambia ninahitaji uzoefu kupitia kujishikiza au aina fulani ya uzoefu wa kazi
  • 3:28 - 3:32
    ili upate kazi kwa urahisi.
  • 3:32 - 3:39
    Kwa hivyo nilihisi kukatishwa tamaa na ilionekana kana kwamba hakuna tumaini kwangu.
  • 3:39 - 3:43
    Lakini nilitiwa moyo na usadikisho huo wa kufuata mafunzo ya wahitimu.
  • 3:43 - 3:48
    Wakati huo, mama yangu alikuwa amenitia moyo kujaribu kutuma ombi mahali tofauti.
  • 3:48 - 3:52
    Nilisema ningejaribu ingawa
    nilikuwa nikihisi kukata tamaa.
  • 3:52 - 3:59
    Nilikuwa nikimfuata Ndugu Chris
    tangu mapema mwaka wa 2022.
  • 3:59 - 4:04
    Kwa sababu wakati huo, alikuwa ameonekana
    kwenye muhtasari wa taarifa zangu kwenye Facebook.
  • 4:04 - 4:09
    Na kisha nikatiwa moyo na maneno yake katika mahubiri fulani niliyotazama.
  • 4:09 - 4:15
    Nilitiwa moyo kuanza kumfuata na kusikiliza mahubiri yake.
  • 4:15 - 4:20
    Na kwa neema ya Mungu, nilianza kufuatilia kwa jumbe
  • 4:20 - 4:23
    na klipu fupi za kutia moyo
    hapa na pale.
  • 4:23 - 4:28
    Kwa hivyo wakati huo, nilipokuwa nikituma maombi,
    mama yangu aliota ndoto
  • 4:28 - 4:35
    ambapo alipewa jina la 'Nishati'.
  • 4:35 - 4:37
    Nikasema, ‘Nishati. Unamaanisha nini?'
  • 4:37 - 4:44
    Alisema, 'Dumisani, nimeota jambo hili, na wewe ndiye pekee katika familia yetu
  • 4:44 - 4:49
    ambaye najua amefanya jambo linalohusiana na uhandisi, kwa hiyo inapaswa kuwa yako.'
  • 4:49 - 4:54
    Nilifikiri, 'Sawa, nishati. Ni kampuni gani
    inayohusiana na nishati?' Nami nikaitazama.
  • 4:54 - 5:00
    Kwa hivyo nilikuwa na imani ya kutafiti
    zaidi kuhusu kampuni hii.
  • 5:00 - 5:06
    Nilikuwa nimetafuta maoni ya Mungu kwa sababu kama si Yeye, hata nisingeweza
  • 5:06 - 5:12
    kujua la kufanya, jinsi ya kuandika wasifu wa kazi(curriculum vitae) au kitu kama hicho.
  • 5:12 - 5:20
    Wakati wa utafiti, niligundua kuwa walikuwa na programu ya mafunzo kwa wahitimu.
  • 5:20 - 5:32
    Ili kutoa muktadha zaidi, mara tu nilipoanza kufikiria zaidi juu ya mafunzo kwa wahitimu,
  • 5:32 - 5:36
    pia kulikuwa na fursa ambayo
    ilikuja katika kampuni nyingine.
  • 5:36 - 5:39
    Kwa hivyo katika kisa hiki, sina budi kuelezea
    kampuni hizi mbili
  • 5:39 - 5:42
    kama Kampuni A na Kampuni B,
    kwa ajili ya uwazi.
  • 5:42 - 5:45
    Kwa hivyo Kampuni A ndiyo ambayo
    mama yangu aliniambia kuihusu,
  • 5:45 - 5:49
    basi Kampuni B ilikuwa fursa hii ya baadaye ambayo ilikuwa imetokea.
  • 5:49 - 5:53
    Kwa hivyo kufikia wakati huo nilisema, 'Hey, nitajaribu tu
    na kutuma maombi.'
  • 5:53 - 5:59
    Na kwa neema ya Mungu, niliitwa kwenye mahojiano ambayo nilihudhuria.
  • 5:59 - 6:03
    Niliwaza, 'Acha nijiweke pale na niende kwenye mahojiano haya.'
  • 6:03 - 6:09
    Sikufikiri kwamba nilifanya vyema
    katika mahojiano na Kampuni B.
  • 6:09 - 6:14
    Lakini kwa neema ya Mungu, nilihojiwa
    na niliitwa kwa ajili ya ofa ya kazi.
  • 6:14 - 6:20
    Kwa hiyo, ingawa bado nilipokea kazi hiyo, bado nilimtafuta Mungu.
  • 6:20 - 6:25
    Kwa sababu nilielewa Alikuwa amenipa ndoto kuhusu Kampuni A.
  • 6:25 - 6:29
    Na sasa fursa hii na
    Kampuni B ilikuwa imepatikana.
  • 6:29 - 6:32
    Kwa hiyo wakati huo nilitafuta uso wa Mungu.
  • 6:32 - 6:37
    Na kwa neema ya Mungu, alikuwa amempa mama yangu ndoto tena.
  • 6:37 - 6:41
    Alikuwa ameniona katika ndoto yake
    nikisaini mikataba miwili.
  • 6:41 - 6:44
    Kwa hiyo kulikuwa na karatasi ndogo na kisha kulikuwa na karatasi kubwa zaidi.
  • 6:44 - 6:52
    Karatasi ndogo iliwakilisha ofa ya kazi niliyokuwa nimepata kwanza, ambayo aliniona nikitia sahihi.
  • 6:52 - 6:56
    Baada ya kuzinduka kutoka kwenye ndoto hiyo, alinitia moyo,
  • 6:56 - 6:59
    'Utapata kazi hii na Kampuni B - ifanyie kazi.
  • 6:59 - 7:06
    Lakini baadaye, utajiunga na Kampuni A - kampuni ile ile niliyokuambia juu yake hapo awali.'
  • 7:06 - 7:10
    Kwa hiyo, kwa neema ya Mungu, nilianza
    kufanya kazi katika Kampuni B
  • 7:10 - 7:16
    lakini bado nilikuwa nikitafuta mwongozo na uwazi kwa Kampuni A, kujua wakati wa Mungu ndio bora zaidi.
  • 7:16 - 7:22
    Kwa hivyo, mapema mwaka huu, kulikuwa na fursa ambayo ilikuja na Kampuni A
  • 7:22 - 7:26
    chini ya nafasi hiyo hiyo ya mkufunzi wa wahitimu, na nilisitasita kidogo
  • 7:26 - 7:31
    kwa sababu ya ndoto hizo hizo na sikutaka kumwasi Mungu kwa njia yoyote ile.
  • 7:31 - 7:40
    Kwa hiyo mnamo Februari 2024, Ndugu Chris alikuwa na Huduma ya Maombi ya Pamoja.
  • 7:40 - 7:44
    Kufikia wakati huo, nilikuwa nikiitazama kwenye
    YouTube na nilisali naye.
  • 7:44 - 7:47
    Na kwa usadikisho uliokuja
    moyoni mwangu wakati wa sala,
  • 7:47 - 7:52
    Niliamua kuweka ombi
    la kazi katika Kampuni A.
  • 7:52 - 7:57
    Maombi yalifunguliwa Januari,
    lakini nilipata fursa tu
  • 7:57 - 8:01
    kufanya mtihani wa kupima uwezo(aptitude test) mwezi Mei.
  • 8:01 - 8:08
    Kufikia wakati huo, watu wengi pia walikuwa wametuma maombi, wakijaribu kupata fursa hiyo pia.
  • 8:08 - 8:13
    Lakini kwa neema ya Mungu, katika mwezi wa
    Agosti 2024, nilipokea simu
  • 8:13 - 8:16
    kusema nihudhurie mahojiano.
  • 8:16 - 8:23
    Kufikia wakati huo, nilikuwa nimeomba. Na kati ya mwezi wa Februari na Agosti,
  • 8:23 - 8:31
    Nilikuwa bado nikiomba pamoja na Ndugu Chris kuhusu usadikisho wangu na fursa hii.
  • 8:31 - 8:38
    Na kwa usadikisho huo, nilisikia sauti ya Mungu moyoni mwangu - ni vizuri!
  • 8:38 - 8:42
    Nilijua nilihitaji tu kuendelea kumtegemea, kujua wakati wa Mungu ndio bora zaidi.
  • 8:42 - 8:47
    Kwa hiyo Agosti ilikuja na nilikuwa
    nimehudhuria mahojiano hayo.
  • 8:47 - 8:51
    Ninahitaji kuelezea kuwa
    haikuwa wakati rahisi
  • 8:51 - 8:54
    kwa sababu wakati huo, nilikuwa nikivunjika moyo pia.
  • 8:54 - 8:59
    Watu walikuwa wakisema, 'Hapana, kampuni hii ni ngumu sana kuingia.
  • 8:59 - 9:00
    Labda unahitaji kujuana na mtu
  • 9:00 - 9:04
    ili upate fursa hapo ya kupata kazi hiyo.'
  • 9:04 - 9:06
    Na watu pia walikuwa wakitoa malalamiko.
  • 9:06 - 9:09
    Lakini kwa ujumbe kutoka kwa Ndugu Chris,
  • 9:09 - 9:14
    Nilitiwa moyo kuendelea kudumisha imani yangu
    na kumtumaini Mungu, nikijua hilo
  • 9:14 - 9:20
    Alikuwa ametoa ndoto na mwongozo kwamba
    ningeenda kwenye kampuni hii,
  • 9:20 - 9:22
    na kwamba kwa wakati Wake mwenyewe, ningeenda huko.
  • 9:22 - 9:27
    Kwa hiyo, ingawa nyakati za kuvunjika moyo zilikuwa zimefika, Neno la Mungu lilikuwa likinitia moyo
  • 9:27 - 9:31
    na pia jumbe na Huduma shirikishi za Maombi pamoja na Ndugu Chris.
  • 9:31 - 9:34
    Zilikuwa zikinitia moyo sana
    kwa kila namna.
  • 9:34 - 9:39
    Kwa hivyo baada ya mahojiano mnamo Agosti,
    nilisubiri hadi Oktoba
  • 9:39 - 9:44
    na kwa neema ya Mungu, nilipokea simu kwamba nimepata ofa ya kazi katika Kampuni A,
  • 9:44 - 9:47
    kampuni ambayo ninafanya kazi kwa sasa.
  • 9:47 - 9:50
    Na unaionaje
    kazi hapo kwenye jukumu hilo jipya?
  • 9:50 - 9:54
    Inasisimua kabisa.
    Ninafurahia sana kazi hiyo.
  • 9:54 - 9:57
    Kwa sababu ni kitu ambacho
    siku zote nilitaka kufanya.
  • 9:57 - 10:01
    Kwa neema ya Mungu nikifaulu vizuri
    kupandishwa cheo (promotion) kupo mezani.
  • 10:01 - 10:04
    Neno langu la ushauri naloweza kumpa mtu yeyote,
  • 10:04 - 10:09
    awe kijana au mtu yeyote ambaye bado yuko shuleni na labda anatazamia kupata kazi,
  • 10:09 - 10:12
    ni kwamba tunapaswa daima kumtafuta Mungu kwanza.
  • 10:12 - 10:14
    Tunapaswa kuanza naye
    na kumaliza naye.
  • 10:14 - 10:18
    Yeye ndiye Mwanzilishi na Mkamilishaji wa imani yetu.
  • 10:18 - 10:21
    Naye yuko pale akitutunza
    katika kila eneo.
  • 10:21 - 10:24
    Tunaanza maisha yetu naye na tunapaswa kuhitimisha maisha yetu pamoja Naye.
  • 10:24 - 10:29
    Wakati huo, hatupaswi kukatishwa tamaa, haswa na sauti zilizo nje.
  • 10:29 - 10:33
    Na pia tunapaswa kuweka mioyo yetu
    sambamba na Neno la Mungu.
  • 10:33 - 10:41
    Kama vile inavyosema katika Kitabu cha Yeremia 29:11 kuhusu mipango yake ya ajabu kwa ajili yetu.
  • 10:41 - 10:44
    kutufanikisha, tufanikiwe,
    na sio kutuangamiza.
  • 10:44 - 10:48
    Kwa njia hiyo hiyo, tunapaswa pia kuweka mioyo yetu sambamba na Neno hilo,
  • 10:48 - 10:52
    na pia kwa maneno mengi ya hekima yaliyomo katika Biblia,
  • 10:52 - 10:58
    ili tusipoteze mwelekeo wetu na kuchukuliwa na matamanio ya muda mfupi -
  • 10:58 - 11:00
    'Hapana, nahitaji pesa tu, hiki na kile...'
  • 11:00 - 11:05
    Kwa sababu zaidi ya yote, tunapaswa kutafuta kumtukuza Mungu katika kila jambo tunalofanya,
  • 11:05 - 11:09
    ikiwa ni pamoja na kazi au kazi
    ambazo tunaomba au kuingia.
  • 11:09 - 11:13
    Hivyo nakushauri usikate tamaa, endelea kutuma maombi lakini umtumaini Mungu kwa kila jambo.
  • 11:13 - 11:16
    badala ya kuingia katika uasi.
Title:
Jinsi nilivyopata KAZI iliyo sambamba na HATIMA yangu!! | Ushuhuda Wenye Motisha
Description:

Dumisani, kijana kutoka Zambia ambaye alisoma nchini China, anashirikisha ushuhuda wa kutia moyo - hasa kwa vijana - kuhusu jinsi alivyotafuta mwelekeo wa kimungu kwa kazi yake. Mungu alizungumza naye kupitia ndoto za mama yake pamoja na usadikisho wa moyo kutoka kwa Roho Mtakatifu - baada ya kujiunga na Ibada Shirikishi ya Maombi pamoja na Ndugu Chris. Leo, anafanya kazi iliyo sambamba na hatima yake. Utukufu ni kwa Mungu!

Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom

➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Pamoja - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
11:47

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions