< Return to Video

YESU ndiye kipengele kimoja katika mlingano unaobadilisha KILA KITU!

  • 0:00 - 0:03
    Tunamhitaji Yesu.
  • 0:03 - 0:12
    Yeye ndiye sababu moja katika mlinganyo ambao unabadilisha kila kitu.
  • 0:12 - 0:19
    Kwa kweli, tunahitaji nguvu zake ili kushinda.
  • 0:19 - 0:24
    Tunahitaji neema yake ili kudhibiti chochote kile kinacholetwa na maisha.
  • 0:24 - 0:29
    Na unapomzingatia Yeye,
  • 0:29 - 0:35
    inabadilisha mtazamo wako kwa kila kitu kingine maishani.
  • 0:35 - 0:39
    Namaanisha, nichukue mfano wa sherehe za msimu huu wa sikukuu.
  • 0:39 - 0:45
    Kuzingatia Yesu kutabadilisha mtazamo wako wa jinsi ya kusherehekea msimu.
  • 0:45 - 0:52
    Ndio, kwa kweli, Krismasi ni wakati mzuri wa sherehe, furaha, kubadilishana zawadi,
  • 0:52 - 0:57
    wakati wa kuwa na marafiki na familia. Ajabu!
  • 0:57 - 1:06
    Lakini nataka uangalie zaidi ya maana ya kidesturi ya sherehe.
  • 1:06 - 1:13
    Kwa sababu katika Yohana 13:34, Yesu aliwaambia wanafunzi wake,
  • 1:13 - 1:20
    "Amri mpya nawapa - pendaneni."
  • 1:20 - 1:28
    Hakuna njia kuu zaidi ya kumheshimu Yesu Krismasi hii
  • 1:28 - 1:36
    kuliko kushiriki na kuonyesha upendo wake kwa wengine.
  • 1:36 - 1:45
    Ikiwa ni neno la fadhili kwa jirani huyo aliyekata tamaa au
  • 1:45 - 1:50
    tabasamu la kutia moyo kwa mgeni huyo mwenye upweke.
  • 1:50 - 1:56
    Iwe ni kupiga simu kwa mtu ambaye umetengana naye kwa miaka mingi
  • 1:56 - 2:03
    au kumtembelea mtu ambaye kikawaida hutawahi kwenda kumuona.
  • 2:03 - 2:09
    Ikiwa ni kutoa tu zawadi kwa mtu
  • 2:09 - 2:15
    ambaye hana ushirika wa marafiki na familia
  • 2:15 - 2:20
    kutokana na mazingira yaliyo nje ya uwezo wao.
  • 2:20 - 2:27
    Shiriki na uonyeshe upendo wa Yesu Krismasi hii.
  • 2:27 - 2:37
    Na ninataka kukuhimiza uangalie zaidi ya mduara wa marafiki na familia yako tu.
  • 2:37 - 2:46
    Sherehekea Yesu Krismasi hii kwa kuufikisha upendo wake
  • 2:46 - 2:47
    kwa aliye mdogo katika hawa (Mathayo 25:40).
Title:
YESU ndiye kipengele kimoja katika mlingano unaobadilisha KILA KITU!
Description:

“Tunamhitaji Yesu. Yeye ndiye sababu moja katika mlinganyi ambayo inabadilisha kila kitu. Kwa kweli, tunahitaji nguvu zake ili kushinda. Tunahitaji neema yake ili kudhibiti chochote kile kinacholetwa na maisha. Na unapomzingatia Yeye, inabadilisha mtazamo wako juu ya kila kitu kingine maishani. Namaanisha, nichukue mfano wa sherehe za msimu huu wa sikukuu. Kumzingatia Yesu kutabadilisha mtazamo wako wa jinsi ya kusherehekea msimu. Ndiyo, bila shaka, Krismasi ni wakati mzuri wa sikukuu, furaha, kubadilishana zawadi, wakati wa kuwa na marafiki na familia. Ajabu! Lakini nataka uangalie zaidi ya maana ya kidesturi ya sherehe. Kwa sababu katika Yohana 13:34 , Yesu aliwaambia wanafunzi wake, ‘Amri mpya ninawapa ninyi – mpendane.’ Hakuna njia kuu ya kumheshimu Yesu Krismasi hii kuliko kushiriki na kuonyesha upendo Wake kwa wengine. Iwe ni neno la fadhili kwa jirani huyo aliyevunjika moyo au tabasamu la kutia moyo kwa mgeni huyo mwenye upweke. Iwe ni kupiga simu kwa mtu ambaye umetengana naye kwa miaka mingi au kumtembelea mtu ambaye kwa kawaida hungewahi kwenda kumuona. Iwe ni kutoa tu zawadi kwa mtu ambaye hana ushirika wa marafiki na familia kutokana na hali zilizo nje ya uwezo wao. Shiriki na uonyeshe upendo wa Yesu Krismasi hii. Na ninataka kukuhimiza uangalie zaidi ya mduara wa marafiki na familia yako tu. Sherehekea Yesu Krismasi hii kwa kufikisha upendo Wake kwa walio wadogo zaidi kati ya hawa (Mathayo 25:40). - Ndugu Chris

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
02:48

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions