< Return to Video

UPONYAJI dhidi ya BEGA LILILOKUFA GANZI!!! | "Mungu alijibu haja ya moyo wangu!"

  • 0:00 - 0:06
    Ninaweza kuutumia mkono wangu wa kulia kwa uhuru,
  • 0:06 - 0:10
    na ninaweza kulala vizuri kama mtoto
    wakati wowote ninapotaka.
  • 0:10 - 0:15
    Sio lazima ninywe
    tena dawa hizo za usingizi na za kutuliza maumivu.
  • 0:15 - 0:21
    Ninaweza kufanya kazi zangu zote bila
    shida kwenye bega langu.
  • 0:21 - 0:27
    USHUHUDA WA
    TV YA MOYO WA MUNGU
  • 0:28 - 0:36
    Maumivu hayo yasiyoelezeka katika kichwa chako,
    moyo, mgongo, magoti, mapafu,
  • 0:36 - 0:41
    popote pale ambapo maumivu hayo yasiyoelezeka
    yapo katika mwili wako,
  • 0:41 - 0:47
    Ninatangaza uponyaji sasa hivi!
    Upone kwa jina kuu la Yesu!
  • 0:47 - 0:51
    Uponywe kwa
    Damu ya thamani ya Yesu Kristo.
  • 0:53 - 0:59
    Jina langu ni Janet. Ninatoka Ufilipino na ninafanya kazi Hong Kong.
  • 0:59 - 1:09
    Tatizo lililonileta kwenye TV ya Moyo wa Mungu ni maumivu ya bega la kulia.
  • 1:09 - 1:14
    Sababu ya maumivu ya bega niliyokuwa nayo
  • 1:14 - 1:21
    ilikuwa ajali ya pikipiki
    iliyotokea miaka minne iliyopita.
  • 1:21 - 1:29
    Kwa hiyo nilienda kwa daktari na kuchukua dawa za aina mbalimbali.
  • 1:29 - 1:38
    Nilipata matibabu ya mwili,
    hata tiba vitobo na kuchua.
  • 1:38 - 1:46
    Na pia niliweka dawa za kutuliza maumivu, haswa usiku,
  • 1:46 - 1:50
    ili kunipunguzia maumivu ili nilale.
  • 1:50 - 1:56
    Lakini basi, maumivu yangekuja tu na kwenda.
  • 1:56 - 2:02
    Na iliniletea shida nyingi
    kwa sababu sikuweza kulala vizuri.
  • 2:02 - 2:08
    Kwa hivyo, ilibidi nitumie
    dawa za kutuliza maumivu kila wakati,
  • 2:08 - 2:14
    na pia kunywa dawa za usingizi
    ili tu kulala na kupumzika.
  • 2:14 - 2:21
    Lakini basi, ilichukua muda mrefu -
    lakini maumivu yalirudi kila wakati.
  • 2:21 - 2:27
    Ikiwa ningeenda kwenye matibabu, maumivu
    yangerudi tu.
  • 2:27 - 2:34
    Ilinipa shida katika eneo langu la kazi kwa sababu mkono wa kulia ulikuwa unauma sana.
  • 2:34 - 2:40
    Ningehisi kufa ganzi wakati wote,
    kwa hiyo nilitumia mkono wangu wa kushoto kufanya kazi.
  • 2:40 - 2:48
    Kwa sababu hiyo, nilikuwa nikimwachia mwajiri wangu vitu na ilileta shida kwa sababu
  • 2:48 - 2:54
    ikiwa vitu nilivyoangusha vilikuwa vya bei ghali,
    ilibidi nivifidie kwa pesa zangu.
  • 2:54 - 3:04
    Kwa hivyo nilikutana na God's Heart TV kwenye YouTube tarehe 5 Agosti 2024,
  • 3:04 - 3:11
    na kisha nikatuma ombi langu la maombi na kujiunga na Huduma ya Maombi ya Pamoja.
  • 3:11 - 3:18
    Na baada ya hapo, niliona kwamba
    sikuwa na maumivu tena.
  • 3:18 - 3:23
    Na haikunilazimu nitumie dawa za usingizi.
  • 3:23 - 3:33
    Ninalala kila ninapopenda na sihitaji
    tena kutumia dawa za kutuliza maumivu.
  • 3:33 - 3:39
    Bega langu limeponywa kwa nguvu ya uponyaji ya Yesu Kristo.
  • 3:39 - 3:44
    Ninaweza kutumia mkono wangu wa kulia kwa uhuru,
  • 3:44 - 3:49
    na ninaweza kulala vizuri kama mtoto
    wakati wowote ninapotaka.
  • 3:49 - 3:53
    Sio lazima ninywe
    tena dawa hizo za usingizi na za kutuliza maumivu.
  • 3:53 - 3:59
    Ninaweza kufanya kazi zangu zote bila
    shida kwenye bega langu.
  • 3:59 - 4:07
    Na pia shida niliyokuwa nikipata hapo awali katika sehemu yangu ya kazi ilikuwa
  • 4:07 - 4:11
    uhusiano na wafanyakazi wenzangu.
  • 4:11 - 4:18
    Ombi moja la maombi nililotuma ni Mungu anisaidie kutafuta kazi nyingine.
  • 4:18 - 4:22
    Lakini basi baada ya
    Ibada ya Pamoja ya Maombi,
  • 4:22 - 4:28
    Niliona tofauti kubwa katika jinsi
    mfanyakazi mwenzangu anavyonitendea.
  • 4:28 - 4:36
    Ananiheshimu, na anazungumza nami kwa adabu, tofauti na hapo awali.
  • 4:36 - 4:42
    Na tunashiriki chakula; tunashiriki
    kila kitu ndani ya nyumba.
  • 4:42 - 4:50
    Sehemu ya kazi niliyo nayo
    sasa ni ya amani sana.
  • 4:50 - 4:54
    Sihitaji kutafuta mwajiri mwingine
    kwa sababu moyoni mwangu,
  • 4:54 - 5:01
    Sikutaka kwenda ikiwa kulikuwa na
    amani mahali pa kazi.
  • 5:01 - 5:06
    Na Mungu akajibu haja ya moyo wangu.
  • 5:06 - 5:09
    Kwa hiyo nampa Mungu utukufu wote.
  • 5:09 - 5:14
    Mwanzoni ulisema kwamba pia ulikuwa unasumbuliwa na ganzi kwenye mkono wako
  • 5:14 - 5:19
    kutokana na maumivu ya bega - bado unapata ganzi hiyo?
  • 5:19 - 5:27
    Hakuna tena! Pako huru. niko huru katika jina la Yesu.
  • 5:27 - 5:35
    Neno langu la kutia moyo kwa kila mtu ni - ikiwa unahisi maumivu au unajua
  • 5:35 - 5:42
    una tatizo lolote kama vile
    masuala ya afya au kitu chochote - kimbilia tu kwa Mungu.
  • 5:42 - 5:50
    Tafuta tu nguvu za Mungu maana Yesu Kristo ndilo jina lipitalo majina yote.
  • 5:50 - 5:54
    Kwa kupigwa kwake, tumeponywa
    katika jina la Yesu.
Title:
UPONYAJI dhidi ya BEGA LILILOKUFA GANZI!!! | "Mungu alijibu haja ya moyo wangu!"
Description:

Janet kutoka Ufilipino, akifanya kazi Hong Kong, alizoea kuishi na dawa za kutuliza maumivu na tembe za usingizi kutokana na miaka minne ya maumivu makali ya bega. Baada ya kujiunga na Huduma ya Maombi ya Pamoja na Ndugu Chris, alipokea uponyaji wa papo hapo pamoja na mafanikio katika eneo lake la kazi. Utiwe moyo na ushuhuda wake wa ajabu katika jina la Yesu!

Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom

➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Mwingiliano - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
06:24

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions