"Niliomba Kazi Zaidi ya 100..." | USHUHUDA wa Mafanikio ya Ajira!
-
0:00 - 0:06Nilituma maombi kwa karibu nafasi 100.
-
0:06 - 0:15Nilipata majibu ya kuhudhuria mahojiano zaidi ya 40 lakini bila mafanikio.
-
0:15 - 0:18Ilikuwa ni majuto kila wakati.
-
0:18 - 0:24USHUHUDA
TV YA MOYO WA MUNGU (GOD’S HEART TV) -
0:25 - 0:39Je, unakabiliwa na vikwazo katika kazi yako, biashara, fedha, kupanda cheo?
-
0:39 - 0:46Leo ni siku yako ya kuinuliwa
kwa kiwango kipya! -
0:46 - 0:54Kila ngome ya kipepo ya
kizuizi katika familia yako, -
0:54 - 1:02ngome hiyo ya vilio,
kurudi nyuma katika familia yako - -
1:02 - 1:09sasa hivi, ivunjwe!
-
1:09 - 1:12Jikomboe kutoka kwenye
ngome hiyo ya kizuizi. -
1:12 - 1:16Jikomboe kutoka kwenye ngome hiyo
ya vikwazo hivi sasa. -
1:17 - 1:24Mimi ni Joseph, ninaishi Sudan lakini
asili yangu ni kutoka Zimbabwe. -
1:24 - 1:31Mnamo 2021, nilipoteza kazi yangu kwa sababu ya COVID.
-
1:31 - 1:35Ikabidi nirudi Zimbabwe.
-
1:35 - 1:44Nilikaa hapo na baada ya miezi miwili hadi mitatu, hali ya COVID ilipokuwa ikiimarika,
-
1:44 - 1:52Nilianza kujaribu kutuma ombi tena kwenye kampuni na sikuweza kupata nafasi.
-
1:52 - 2:02Nilipumzika kidogo lakini niliendelea kujaribu kutuma maombi, hata kwa mashirika na makampuni mengine.
-
2:02 - 2:122021 ilipita. 2022 ilipita.
Na 2023 pia ilikuja na kwenda. -
2:12 - 2:19Wakati huo, nilikuwa nikikabiliwa na
changamoto za rasilimali za kifedha. -
2:19 - 2:26Na ilikuwa ni ada ya mwanangu
ambaye yuko shule ya bweni - -
2:26 - 2:29Sikuweza tena kuimudu hilo.
-
2:29 - 2:31Kwa sababu yuko katika shule ya binafsi.
-
2:31 - 2:36Kwa hivyo, niliendelea kujaribu kutafuta suluhisho.
-
2:36 - 2:42Nilikwenda kwa watalaamu wa kiroho.
Nilikwenda kwa waganga wa mitishamba. -
2:42 - 2:48Na katika mchakato huo, nilianza
kupoteza pesa zaidi -
2:48 - 2:55kwani nilikuwa nikiombwa pesa nyingi ili kupata dawa ya kazi nilizokuwa naomba.
-
2:55 - 3:00Nilituma maombi kwa karibu nafasi 100.
-
3:00 - 3:06Nilikuwa nafanya hesabu ya
kazi nilizoomba. -
3:06 - 3:13Lakini baadhi, nilituma maombi moja kwa moja kwenye tovuti yao, na sikuweza kuzihesabu.
-
3:13 - 3:23Nilipata majibu ya kuhudhuria mahojiano zaidi ya 40 lakini hakuna nilichoambulia.
-
3:23 - 3:26Ilikuwa ni majuto kila wakati.
-
3:26 - 3:30'Tutaendelea kukujuza ;
tutawasiliana nawe.' -
3:30 - 3:36Na wengine, unaweza kuona kwamba
'nimepitia haya; Nimefanikiwa'. -
3:36 - 3:40Lakini katika dakika ya mwisho, ungesikia tu,
-
3:40 - 3:47'Samahani, tunajuta kukushauri kwamba hujafanikiwa. Tafadhali endelea kujaribu.'
-
3:47 - 3:55Ni mahojiano matano tu kati ya yale 40 ambayo
nilifanya yalikaribia kufanikiwa. -
3:55 - 4:02Lakini ilikuwa ngumu sana -
hiyo ilikuwa sehemu ya 2023 na 2024. -
4:02 - 4:09Pia kulikuwa na shida na mabishano katika familia yangu na mke wangu.
-
4:09 - 4:16Kwa sababu nilikuwa nimeanzisha mradi wa ufugaji wa wanyama na kuku.
-
4:16 - 4:23Na kupitia hilo, nilipoteza pesa kwa sababu watu walikuwa wakisema,
-
4:23 - 4:31'Tuwekee kuku na tutawasiliana kwa namba yako watakapokuwa tayari.'
-
4:31 - 4:35Wakati ulipofika na walikuwa
tayari, watu wangesema, -
4:35 - 4:40'Hapana, tumepata mkandarasi mwingine ambaye ametupatia. Pole.'
-
4:40 - 4:48Kwa hiyo umekwama na bidhaa na unaziuza kwa hasara. Kwa hivyo hiyo ilinimaliza.
-
4:48 - 4:57Na wakati huohuo, nilipokuwa nikienda kwa wataalamu wa kiroho, hali ilizidi kuwa mbaya zaidi.
-
4:57 - 5:01Kulikuwa na ugomvi wa mara kwa mara nyumbani.
-
5:01 - 5:07Hata jamaa hawakuzungumza nami.
-
5:07 - 5:08Ilikuwa tu hali ngumu.
-
5:08 - 5:14Na nilipoona akaunti yangu ya benki
ikishuka na kushuka na -
5:14 - 5:21kutokuwa na pesa za ada ya shule kwa mwaka huu kwa mwanangu, ilizidi kuwa mbaya.
-
5:21 - 5:29Kisha mke wangu akanitia moyo kuwasilisha ombi la maombi kwa TV ya Moyo wa Mungu.
-
5:29 - 5:36Nilisita kidogo, lakini baada ya kuona kwamba hali haikuwa sawa,
-
5:36 - 5:42Niliwasilisha ombi la maombi -
hiyo ilikuwa katikati ya Aprili 2024. -
5:42 - 5:50Nilijibiwa na mnamo Mei 4,
nilialikwa kwenye Maombi ya Pamoja. -
5:50 - 6:00Mnamo Mei 13, nilipata mahojiano kutoka kwenye shirika ninalofanya kazi nalo,
-
6:00 - 6:02ambalo nilikuwa nakilifanyia kazi.
-
6:02 - 6:08Nilipitia mahojiano.
Sikufikiri nilikuwa na nimefaulu. -
6:08 - 6:13Kwa sababu maswali yalikuwa magumu sana na sababu zilikuwa -
-
6:13 - 6:20kwa nini nilikaa nje kwa muda mrefu bila kurudi kwenye shirika?
-
6:20 - 6:24Hiyo ilikuwa Mei 13.
-
6:24 - 6:31Mnamo Juni 14, nilipata jibu kwamba
nilikuwa nimefaulu mahojiano. -
6:31 - 6:39Nilitia saini mkataba na ndiyo
maana sasa niko Sudan pia. -
6:39 - 6:47Na ninamshukuru Mungu kwa yote aliyofanya kupitia TV ya Moyo wa Mungu na maombi ya Ndugu Chris.
-
6:47 - 6:58Sasa ninaweza kulipia karo ya shule ya mwanangu kwa 2024 na 2025.
-
6:58 - 7:03Tangu kusali na Kaka Chris, uhusiano na mke wako ukoje?
-
7:03 - 7:16Ni mnzuri sana. Hata nikiwa hapa, kila usiku, tunasali pamoja kupitia WhatsApp au video.
-
7:16 - 7:20Pia tunasali pamoja kama familia
wakati mwanangu pia yupo. -
7:20 - 7:25Na vipi kuhusu hali ya
wataalamu wa kiroho, mganga wa mitishamba? -
7:25 - 7:28Je, bado una mwelekeo wa kuwatembelea?
-
7:28 - 7:33Hapana, sitaki tena. Nilipoteza sana.
-
7:33 - 7:37Sikutaja kuwa hata nilipoteza
gari kupitia mchakato huo, -
7:37 - 7:41kwa hivyo sina mwelekeo wa kufikiria juu ya hilo tena,
-
7:41 - 7:49zaidi ya kusoma Biblia yangu na kuomba - na hicho ndichu tu ninachokifikiria.
-
7:49 - 7:53Je, kuna ushauri wowote ambao ungependa kuwapa watazamaji wanaotazama sasa hivi?
-
7:53 - 7:59Sisi sote tunakabiliwa na hali ngumu katika maisha yetu,
-
7:59 - 8:05na wakati mwingine tunafikiri ni mwisho wa dunia, na hakuna mtu atakayetusikiliza.
-
8:05 - 8:10Na hasa unapopoteza kipato, inakuwa ngumu sana.
-
8:10 - 8:13Unakuwa kama mzigo kwa watu.
-
8:13 - 8:19Kwa hivyo ningependa kuwaambia wengine ambao wanakabiliwa na hali kama hiyo
-
8:19 - 8:22na hawajapata suluhisho -
-
8:22 - 8:28angalau kwa Mungu, kuna suluhisho,
ingawa inaweza kuchukua muda. -
8:28 - 8:35Wakati tunapomkimbilia Mungu, atatukumbuka kwa hakika katika saa yetu ya uhitaji.
- Title:
- "Niliomba Kazi Zaidi ya 100..." | USHUHUDA wa Mafanikio ya Ajira!
- Description:
-
Joseph kutoka Zimbabwe alikabiliwa na changamoto za kifedha zinazoongezeka kutokana na ukosefu wa ajira kwa miaka mitatu. Licha ya jitihada zake nyingi, na kutembelea wataalamu wengi wa kiroho, utafutaji wa kazi ulionekana kutozaa matunda - hadi alipojiunga na Huduma ya Maombi ya Pamoja na Ndugu Chris mnamo Mei 2024. Mwezi huo huo mafanikio yake yalikuja!
Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom
➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Pamoja - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live - Video Language:
- English
- Team:
God's Heart TV
- Duration:
- 09:05
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for "I Applied For Over 100 Jobs..." | Employment Breakthrough TESTIMONY! | |
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for "I Applied For Over 100 Jobs..." | Employment Breakthrough TESTIMONY! |