< Return to Video

"Niliomba Kazi Zaidi ya 100..." | USHUHUDA wa Mafanikio ya Ajira!

  • 0:00 - 0:06
    Nilituma maombi kwa karibu nafasi 100.
  • 0:06 - 0:15
    Nilipata majibu ya kuhudhuria mahojiano zaidi ya 40 lakini bila mafanikio.
  • 0:15 - 0:18
    Ilikuwa ni majuto kila wakati.
  • 0:18 - 0:24
    USHUHUDA
    TV YA MOYO WA MUNGU (GOD’S HEART TV)
  • 0:25 - 0:39
    Je, unakabiliwa na vikwazo katika kazi yako, biashara, fedha, kupanda cheo?
  • 0:39 - 0:46
    Leo ni siku yako ya kuinuliwa
    kwa kiwango kipya!
  • 0:46 - 0:54
    Kila ngome ya kipepo ya
    kizuizi katika familia yako,
  • 0:54 - 1:02
    ngome hiyo ya vilio,
    kurudi nyuma katika familia yako -
  • 1:02 - 1:09
    sasa hivi, ivunjwe!
  • 1:09 - 1:12
    Jikomboe kutoka kwenye
    ngome hiyo ya kizuizi.
  • 1:12 - 1:16
    Jikomboe kutoka kwenye ngome hiyo
    ya vikwazo hivi sasa.
  • 1:17 - 1:24
    Mimi ni Joseph, ninaishi Sudan lakini
    asili yangu ni kutoka Zimbabwe.
  • 1:24 - 1:31
    Mnamo 2021, nilipoteza kazi yangu kwa sababu ya COVID.
  • 1:31 - 1:35
    Ikabidi nirudi Zimbabwe.
  • 1:35 - 1:44
    Nilikaa hapo na baada ya miezi miwili hadi mitatu, hali ya COVID ilipokuwa ikiimarika,
  • 1:44 - 1:52
    Nilianza kujaribu kutuma ombi tena kwenye kampuni na sikuweza kupata nafasi.
  • 1:52 - 2:02
    Nilipumzika kidogo lakini niliendelea kujaribu kutuma maombi, hata kwa mashirika na makampuni mengine.
  • 2:02 - 2:12
    2021 ilipita. 2022 ilipita.
    Na 2023 pia ilikuja na kwenda.
  • 2:12 - 2:19
    Wakati huo, nilikuwa nikikabiliwa na
    changamoto za rasilimali za kifedha.
  • 2:19 - 2:26
    Na ilikuwa ni ada ya mwanangu
    ambaye yuko shule ya bweni -
  • 2:26 - 2:29
    Sikuweza tena kuimudu hilo.
  • 2:29 - 2:31
    Kwa sababu yuko katika shule ya binafsi.
  • 2:31 - 2:36
    Kwa hivyo, niliendelea kujaribu kutafuta suluhisho.
  • 2:36 - 2:42
    Nilikwenda kwa watalaamu wa kiroho.
    Nilikwenda kwa waganga wa mitishamba.
  • 2:42 - 2:48
    Na katika mchakato huo, nilianza
    kupoteza pesa zaidi
  • 2:48 - 2:55
    kwani nilikuwa nikiombwa pesa nyingi ili kupata dawa ya kazi nilizokuwa naomba.
  • 2:55 - 3:00
    Nilituma maombi kwa karibu nafasi 100.
  • 3:00 - 3:06
    Nilikuwa nafanya hesabu ya
    kazi nilizoomba.
  • 3:06 - 3:13
    Lakini baadhi, nilituma maombi moja kwa moja kwenye tovuti yao, na sikuweza kuzihesabu.
  • 3:13 - 3:23
    Nilipata majibu ya kuhudhuria mahojiano zaidi ya 40 lakini hakuna nilichoambulia.
  • 3:23 - 3:26
    Ilikuwa ni majuto kila wakati.
  • 3:26 - 3:30
    'Tutaendelea kukujuza ;
    tutawasiliana nawe.'
  • 3:30 - 3:36
    Na wengine, unaweza kuona kwamba
    'nimepitia haya; Nimefanikiwa'.
  • 3:36 - 3:40
    Lakini katika dakika ya mwisho, ungesikia tu,
  • 3:40 - 3:47
    'Samahani, tunajuta kukushauri kwamba hujafanikiwa. Tafadhali endelea kujaribu.'
  • 3:47 - 3:55
    Ni mahojiano matano tu kati ya yale 40 ambayo
    nilifanya yalikaribia kufanikiwa.
  • 3:55 - 4:02
    Lakini ilikuwa ngumu sana -
    hiyo ilikuwa sehemu ya 2023 na 2024.
  • 4:02 - 4:09
    Pia kulikuwa na shida na mabishano katika familia yangu na mke wangu.
  • 4:09 - 4:16
    Kwa sababu nilikuwa nimeanzisha mradi wa ufugaji wa wanyama na kuku.
  • 4:16 - 4:23
    Na kupitia hilo, nilipoteza pesa kwa sababu watu walikuwa wakisema,
  • 4:23 - 4:31
    'Tuwekee kuku na tutawasiliana kwa namba yako watakapokuwa tayari.'
  • 4:31 - 4:35
    Wakati ulipofika na walikuwa
    tayari, watu wangesema,
  • 4:35 - 4:40
    'Hapana, tumepata mkandarasi mwingine ambaye ametupatia. Pole.'
  • 4:40 - 4:48
    Kwa hiyo umekwama na bidhaa na unaziuza kwa hasara. Kwa hivyo hiyo ilinimaliza.
  • 4:48 - 4:57
    Na wakati huohuo, nilipokuwa nikienda kwa wataalamu wa kiroho, hali ilizidi kuwa mbaya zaidi.
  • 4:57 - 5:01
    Kulikuwa na ugomvi wa mara kwa mara nyumbani.
  • 5:01 - 5:07
    Hata jamaa hawakuzungumza nami.
  • 5:07 - 5:08
    Ilikuwa tu hali ngumu.
  • 5:08 - 5:14
    Na nilipoona akaunti yangu ya benki
    ikishuka na kushuka na
  • 5:14 - 5:21
    kutokuwa na pesa za ada ya shule kwa mwaka huu kwa mwanangu, ilizidi kuwa mbaya.
  • 5:21 - 5:29
    Kisha mke wangu akanitia moyo kuwasilisha ombi la maombi kwa TV ya Moyo wa Mungu.
  • 5:29 - 5:36
    Nilisita kidogo, lakini baada ya kuona kwamba hali haikuwa sawa,
  • 5:36 - 5:42
    Niliwasilisha ombi la maombi -
    hiyo ilikuwa katikati ya Aprili 2024.
  • 5:42 - 5:50
    Nilijibiwa na mnamo Mei 4,
    nilialikwa kwenye Maombi ya Pamoja.
  • 5:50 - 6:00
    Mnamo Mei 13, nilipata mahojiano kutoka kwenye shirika ninalofanya kazi nalo,
  • 6:00 - 6:02
    ambalo nilikuwa nakilifanyia kazi.
  • 6:02 - 6:08
    Nilipitia mahojiano.
    Sikufikiri nilikuwa na nimefaulu.
  • 6:08 - 6:13
    Kwa sababu maswali yalikuwa magumu sana na sababu zilikuwa -
  • 6:13 - 6:20
    kwa nini nilikaa nje kwa muda mrefu bila kurudi kwenye shirika?
  • 6:20 - 6:24
    Hiyo ilikuwa Mei 13.
  • 6:24 - 6:31
    Mnamo Juni 14, nilipata jibu kwamba
    nilikuwa nimefaulu mahojiano.
  • 6:31 - 6:39
    Nilitia saini mkataba na ndiyo
    maana sasa niko Sudan pia.
  • 6:39 - 6:47
    Na ninamshukuru Mungu kwa yote aliyofanya kupitia TV ya Moyo wa Mungu na maombi ya Ndugu Chris.
  • 6:47 - 6:58
    Sasa ninaweza kulipia karo ya shule ya mwanangu kwa 2024 na 2025.
  • 6:58 - 7:03
    Tangu kusali na Kaka Chris, uhusiano na mke wako ukoje?
  • 7:03 - 7:16
    Ni mnzuri sana. Hata nikiwa hapa, kila usiku, tunasali pamoja kupitia WhatsApp au video.
  • 7:16 - 7:20
    Pia tunasali pamoja kama familia
    wakati mwanangu pia yupo.
  • 7:20 - 7:25
    Na vipi kuhusu hali ya
    wataalamu wa kiroho, mganga wa mitishamba?
  • 7:25 - 7:28
    Je, bado una mwelekeo wa kuwatembelea?
  • 7:28 - 7:33
    Hapana, sitaki tena. Nilipoteza sana.
  • 7:33 - 7:37
    Sikutaja kuwa hata nilipoteza
    gari kupitia mchakato huo,
  • 7:37 - 7:41
    kwa hivyo sina mwelekeo wa kufikiria juu ya hilo tena,
  • 7:41 - 7:49
    zaidi ya kusoma Biblia yangu na kuomba - na hicho ndichu tu ninachokifikiria.
  • 7:49 - 7:53
    Je, kuna ushauri wowote ambao ungependa kuwapa watazamaji wanaotazama sasa hivi?
  • 7:53 - 7:59
    Sisi sote tunakabiliwa na hali ngumu katika maisha yetu,
  • 7:59 - 8:05
    na wakati mwingine tunafikiri ni mwisho wa dunia, na hakuna mtu atakayetusikiliza.
  • 8:05 - 8:10
    Na hasa unapopoteza kipato, inakuwa ngumu sana.
  • 8:10 - 8:13
    Unakuwa kama mzigo kwa watu.
  • 8:13 - 8:19
    Kwa hivyo ningependa kuwaambia wengine ambao wanakabiliwa na hali kama hiyo
  • 8:19 - 8:22
    na hawajapata suluhisho -
  • 8:22 - 8:28
    angalau kwa Mungu, kuna suluhisho,
    ingawa inaweza kuchukua muda.
  • 8:28 - 8:35
    Wakati tunapomkimbilia Mungu, atatukumbuka kwa hakika katika saa yetu ya uhitaji.
Title:
"Niliomba Kazi Zaidi ya 100..." | USHUHUDA wa Mafanikio ya Ajira!
Description:

Joseph kutoka Zimbabwe alikabiliwa na changamoto za kifedha zinazoongezeka kutokana na ukosefu wa ajira kwa miaka mitatu. Licha ya jitihada zake nyingi, na kutembelea wataalamu wengi wa kiroho, utafutaji wa kazi ulionekana kutozaa matunda - hadi alipojiunga na Huduma ya Maombi ya Pamoja na Ndugu Chris mnamo Mei 2024. Mwezi huo huo mafanikio yake yalikuja!

Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom

➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Pamoja - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
09:05

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions